BAADA ya kudumu kwa zaidi ya miaka 10, imebainika kuwa ndoa ya mwanamuziki mahiri wa muziki wa Injili Bongo, Flora na mumewe Emmanuel Mbasha ipo chali kwa maana ya kuanguka huku ikidaiwa kuwa, kusimama imara tena inawezekana lakini ni kazi kubwa, Amani limefukunyua mazito.
Hilo limejitokeza wiki moja baada ya madai ya mwanaume huyo kudaiwa kumbaka shemeji yake na kesi ipo polisi.
Imeelezwa Flora na mumewe ambao walifunga ndoa Agosti 22, 2002 wamepita katika migogoro mizito lakini wawili hao walikuwa wakiyamaliza kifamilia hadi kufikia hili la hivi karibuni ndilo lililoziba mataumaini ya wawili hao kuishi kama mume na mke.
Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimeeleza kuwa, mzizi wa wawili hao kugombana ulichochewa na mwanamke mmoja (jina tunalo) ambaye alikuwa akikinzana na ushauri wa Mbasha mara kwa mara.
"Kuna vitu Mbasha alikuwa akimshauri huyo mama lakini walikuwa wakipishana Kiswahili na hapo ndipo tatizo lilipokua hadi kufikia hatua ya kumwagana," kilisema chanzo.
TUJIUNGE NA MBASHA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Emmanuel alizungumza na mwandishi wetu ambapo alikiri ndoa yake haina uhai tena na si rahisi kurejea katika hali ya kawaida licha ya kudai kuwa bado anampenda mkewe.
"Tulikuwa tunagombana sana na Flora lakini tulikuwa tukipatana ila mama… (anamtaja jina) alichangia ugomvi,
Flora naye alikuwa na nyendo zake mbaya, kuna wakati alikuwa anatoka kwenda gym (sehemu ya mazoezi) anachelewa kurudi ikafika wakati na nguvu ya ndugu wa mke ikawa kubwa kiasi cha kunizidi mimi na hapo ndipo mambo yalipofikia pabaya kabisa."
FLORA ATIMKA NYUMBANI
Mbasha anaendelea: "Ugomvi ulizidi, ilifika wakati tulipishana kiasi cha yeye kuondoka nyumbani na kwenda kuishi katika nyumba ya wageni kwa miezi kadhaa wakati huo.
"Ndani ya ugomvi huo nilisikia mengi, baadhi ya watu wananiambia mke wangu anaonekana na Prado na mwanaume mwingine mwenye pesa, iliniuma sana ingawa sijawahi kumuona moja kwa moja," alisema Emmanuel.
Kuhusu ugomvi huo, hivi karibuni Flora alikaririwa katika vyombo vya habari akisema hana tatizo na mumewe na ameshasamehe na kusahau yote yaliyopita hivyo ajitokeze tu ili akajibu mashitaka ya kudaiwa kubaka binti wa miaka 17 yaliyofunguliwa.
"Mimi sina tatizo kabisa na mume wangu, nimeshasamehe yote yaliyopita, kuhusu mashitaka ningeweza kuyafuta kama ningekuwa mimi ndiye niliyemshitaki," alisema Flora.
FLORA ADAIWA KUHAMIA KWA GWAJIMA
Wakati gazeti hili likiendelea kusaka undani juu ya sakata hili, kuna chanzo kingine kilipenyeza data kuwa baada ya ugomvi kuwa mzito, Flora alihamia kwa Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar, Josephat Gwajima ambako ndiko alikuwa akisali kila Jumapili.
"Kwani nyinyi Global hamna habari? Flora amehamia kwa Gwajima Jumapili iliyopita, kwanza alihudhuria ibada jioni akaenda kuishi maana Gwajima ni mchungaji wake kwa sasa," kilisema chanzo.
GWAJIMA ACHOMOA
Ili kupata mizani ya madai hayo, juzi Amani lilimpigia simu Mchungaji Gwajima na kumuuliza kama kweli Flora amehamia kwake kufuatia ugomvi kati yake na mumewe ambapo alikataa katakata.
"Flora hayupo hapa…mnataka niwaambiwe yuko hapa halafu vyombo vya habari muanze kuandika vibaya? Hakuna kitu kama hicho," alisema Gwajima.
KWA NINI CHALI?
Ndoa kuwa chali ni ile ambayo imeanguka lakini inaweza kusimama tena tofauti na ndoa kuvunjika. Global iliwahi kuandika NDOA YA THEA CHALI baadaye ikasimama tena. Thea ni msanii wa filamu alifunga ndoa na Michael Sangu 'Mike' ambaye pia ni mwigizaji.
Wakati Emmanuel akizungumza na mwandishi wetu, alikiri kuwa Flora ameshamgeuka na nguvu kubwa imemuingia ndani ya moyo wake hivyo kuna ugumu sana wa kurudiana.
"Flora ambaye nilitegemea awe msaada katika hili lakini amefikia steji ya kuacha kunisikiliza, anasema haniamini, kwamba ninaweza kumfanyia lolote, sasa si bora kama anataka tuachane kwa heri kuliko kuniundia zengwe ambalo linataka kunipeleka mimi jela?" alihoji Mbasha.
Kutokana na mvutano huo pamoja na kesi hiyo ya kudaiwa kubaka inayomwandana Mbasha ni dhahiri kwamba kila mmoja hana imani na mwenzake tena hivyo suala la wawili hao kuishi kama zamani linakuwa gumu kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
Emmanuel Mbasha alishitakiwa katika Kituo cha Polisi cha Tabata Shule, Mei 30, mwaka huu kwa madai ya kumbaka shemejie.Uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea hadi sasa shitaka ambalo mwenyewe amelikanusha.
On Monday, June 2, 2014 9:42:46 PM UTC+3, paul lawala wrote:
Miaka 17 kisheria hawezi kuhiari kufanya ngono,Law of child act 20092014-06-02 19:33 GMT+03:00 Jovias Mwesiga <ngo...@gmail.com>:
Hivi ubakaji kwa sheria ya tazania unasomekaje? Kwa hili ni ngumu kuhukumu kwa kusoma yaliyoandikwa labda tusubiri likianza kushugulikiwa kisheria
2014-06-01 17:11 GMT-05:00 Nicomedes Kajungu <nicom...@gmail.com>:Hapa kuna maswali mengi kuliko majibi.
Wengine wanapenda kuharibiana tu.
On Jun 2, 2014 12:18 AM, "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wana...@googlegroups.com> wrote:--
--
Kwa nini alipotaka kumbaka kwa mara ya kwanza sebureni asikimbie kupiga kelele na kutoka ndani. Miaka kumi na saba ana nguvu ya kupambana naye. Pili tena ndani ya gari ana nafasi gani ya kukuzuia ukashindwa kupiga dirisha hata kupasua kioo na kitu. Gari ni mbanano mapaka akufuate kitini akubake na iwezekane umelala au upo macho. Mengine nayo ni ya kuuliza. Asiikamate hiyo dudu na kuivuta why-age 17???? ama kweli!On Thursday, 29 May 2014, 9:02, Emma Kaaya <emma...@gmail.com> wrote:
--JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na uvumba Emmanuel Mbasha (pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake mwenye miaka 17 (jina tunalo) ambaye ni yatima.Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu makini zinadai kwamba mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo Jumatatu iliyopita muda wa mchana na kufungua kesi yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi Na. TBT/IR/1865/2014 akidai kufanyiwa unyama huo kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili) wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar.Ilidaiwa kuwa, Ijumaa iliyopita mlalamikiwa alifanya kitendo hicho sebuleni nyumbani na Jumapili ilidaiwa alitekeleza ukatili wake huo ndani ya gari lake hali ambayo ilimfanya mlalamikaji kutoa taarifa Kituo cha Polisi, Tabara-Aroma jijini Dar.Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha anayetafutwa na polisi kwa kosa la ubakaji.Iliendelea kudaiwa kuwa, kufuatia maumivu makali aliyoyapata mlalamikaji huyo ilibidi aende Hospitali ya Amana na kugundulika kuwa aliingiliwa kimapenzi na kumsababishia michubuko sehemu za siri.HISTORIA YA MLALAMIKAJI
Mlalamikaji ni kati ya watoto mapacha waliozaliwa jijini Mwanza na mama ambaye jina lake halikupatikana mara moja.Mama wa mtoto huyo (kwa sasa ni marehemu pamoja na mume wake) akiwa muumini wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God (EAGT) aliamua kumtoa mtoto mmoja kwa mama mzazi wa Flora Mbasha kwa lengo la kumlea, wakati huo mtoto huyo alikuwa na miezi mitatu.Ikaelezwa kuwa, mama wa Flora alikaa na mtoto huyo akimsomesha hadi alipofika darasa la saba ambapo alimkabidhi kwa Flora na kuishi naye hadi alipofikwa na janga hilo.Maelezo zaidi yanasema Mbasha aliweza kufanya kitendo hicho kwa sababu mkewe (Flora) ameondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini kwa kile kilichodaiwa kwamba kuna ugomvi mkubwa ndani ya ndoa yao.Taarifa zaidi zinadai kwa sasa Mbasha naye hayupo nyumbani kwake huku mlalamikaji yuko Hospitali ya Amana akiendelea kufanyiwa uchunguzi wa kiafya ili kubaini kama ana maambukizi ya magonjwa ya zinaa au la!Kwa upande wake mlalamikaji huyo alipopigiwa simu juzi kwa lengo la kuthibitisha kuhusiana na sakata hilo alikiri na kusema amekwishatoa taarifa polisi kwa kitendo alichofanyiwa na mwenye nyumba huyo huyo.
Send Emails to wana...@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
Send Emails to wana...@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com .

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment