Wednesday, 4 June 2014

Re: [wanabidii] Majibu ya Dr. Slaa kwa mwanachama kuhusu kukwepa mazishi ya Mama Zitto

Pamoja na ndugu 'mabadiliko' kulenga kumchafulia Dr. Slaa mm imenisaidia kujua kuwa kumbe viongozi wa CHADEMA kuna kitu walifanya kwa mgonjwa. Ikumbukwe kuna wkt niliandika humu kuwa hawa viongozi wamtembelee mgonjwa huyu wkt wakimsulubu Zitto kuhusu fedha za tanapa. Pia kwa jibu la Dr. Slaa mambo ya magonjwa au vifo kwao sio jambo la vyombo vya habari. Kura zingetosha 2010 tungeona katiba mpya ya wa Tz bila mizengwe, Tungeona bei ya vifaa vya ujenzi ikishuka, Tungeona elimu bora bila malipo, etc. Lakini tusingemuona kwenye vilio. Mwana mabadiliko ulitaka tujue hivyo? Asante.

----------
Sent from my Nokia Phone

------Original message------
From: MABADILIKO CHADEMA <mabadilikochadema@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, June 4, 2014 12:53:36 PM GMT-0700
Subject: [wanabidii] Majibu ya Dr. Slaa kwa mwanachama kuhusu kukwepa mazishi ya Mama Zitto

Majibu ya Dr. Slaa kwa mwanachama kuhusu kukwepa mazishi ya Mama Zitto

Wadau,

Katika ufuatiliaji zaidi nimegundua kwambakuna mwanachama wa CHADEMA ambaye
aliguswa na kisa cha viongozi wakuu wa chamakususia mazishi ya Shida Salum
aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA. Mwanachamahuyo baada ya kuumizwa
na kitendo hicho cha viongozi wake, alimwandikia smsifuatayo Dr. Slaa.

Nimeihariri ili kuondoa vifupisho vya maneno alivyovitumia ili kila mmoja
aelewe:
"Kweli baba wewe na Mbowe mmeshindwa kabisa kushiriki mazishi ya mjumbe wa
kamati kuu!! Ninyi hamna kabisa utu hata chembe? Sababu za kisiasa
zimewafanya muwe na mioyo migumu kiasi hicho? Utadhani nyinyi hamtakaa mfe
milele?

Mmeshangaza ulimwengu, ubinadamu kwenu siyo kitu kwa ajili yasiasa? Hivi
wewe utakuwa mwanasiasa milele? Kweli hamna hata hata hofu ya Munguhata
kidogo, hata wewe ambaye ulikuwa mtumishi wa Mungu kweli baba? Hata kamani
ubabe, wa kwenu haujawahi kutokea.

Hata kama Zitto hayuko CDM mchango wakekatika kujenga chama mmeusahau
kabisa? Mmelipa kisasi kwa kususa hata maiti! Kwa ajili ya siasa tu! Duh!
Hongereni, fanyeni siasa milele. Watu wenye hekimawamepata somo toka kwenu.
Mungu awabariki sana".

Mwisho wa kunukuu.

Sasa soma majibu ya mtu anayeitwa Dr.Willibrod Slaa ambaye kama kura
zingetosha mwaka 2010, eti leo angekuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Sms yake imetoka kwenye namba yake ya 0783967519 na ili-deliver
kwenye simu ya huyo kijana saa 18:40:27 jana Jumanne tar 2/6/2014. Nainukuu
sms hiyo bila kuhariri chochote:

"Acha ushabiki usiokuhusu. Makamu Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA, mhe. Issa
Mohamed alifiwa na mama yake mzazi siku 7 zilizopita. Nani alihudhuria,
mbona hata wewe hukuhudhuria! Wala hukuandika sms kama hii, kumbe Utu wako
unapimwa kwa fulani tu! Upuuzi. Chadema haifanyi siasa ya misiba. Utu
unapimwa uliyomfanyia mgonjwa siyo kwenye mitandao na magazeti. Fanya
utafiti kabla ya kujifanya mjuaji. Dr Slaa"

Mwisho wa kunukuu. Huyo ndiye rais wa UKAWA.

Mohamedi Mtoi | Facebook
<https://www.google.co.tz/url?sa=t&rct=j&q=&esrc=s&source=web&cd=1&cad=rja&uact=8&ved=0CCEQFjAA&url=https%3A%2F%2Fwww.facebook.com%2Fmouddymtoi&ei=GXmPU8TsLafg4QTmvID4DQ&usg=AFQjCNGzi1WvNc69vPsECRWLWh_y4ZIyWQ&bvm=bv.68235269,d.bGE>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment