|
Tuesday, 1 April 2014
[wanabidii] New content updates
Re: [wanabidii] BARUA YA WAZI KWA JK KUTOKA KWA CHAMA CHA WAZANZIBARI UINGEREZA
Rais yupo UK si wamalizane naye hukohuko
--Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
Ikulu
P O Box 9120
Dar es SalaamYah: Hotuba Yako ya Kuwagawa Watanzania
Mheshimiwa Rais,
Tumelazimika kuandika barua hii kwako kama kiongozi wa juu wa taifa letu ili kukuonesha namna ambavyo tumesikitishwa na matamshi yako wakati wa ufunguzi wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Tukiwa sehemu ya jamii kubwa ya Kizanzibari tuishio nje ya nchi yetu, hotuba yako imetutia khofu kubwa kulenga kwake zaidi kwenye kuvunja na sio kujenga mustakbali mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hotuba yako Mheshimiwa Rais, haikuzingatia maslahi ya Muungano wetu kwa misingi ya umoja unaonendana na matakwa ya wananchi walio wengi.
Tunakuandikia barua hii kukuzindua kile ambacho tumekiona kinakwenda tafauti na akhlaki zako. Ukweli ni kwamba kwa muda wote wa kipindi chako cha utawala tumekuwa tukikutazama kama ni tarajio jipya lililojengeka kwa misingi ya haki, insaaf na kioo cha uadilifu kwa pande mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano.
Tunazungumza nawe moja kwa moja sio tu kama kiongozi wa taifa, bali pia kama mtu tuliyempa matumaini hayo. Wewe ni mtu wa mwisho kwetu kuamini kuwa anaweza kujenga khofu badala ya matumaini, batili badala ya halali, kitisho badala ya nasaha na mgawanyiko badala ya utangamano.
Mheshimiwa Rais,
Ulichokifanya siku ya tarehe 21 Machi 2013 ni kuzua taharuki kwa raia wa Jamhuri ya Muungano hasa kwa ndugu zetu wa Kizanzibari waishio upande wa pili wa Muungano huo. Ulichofanya ni kulihusisha jeshi letu linalothaminiwa dunia nzima kwa misingi ya heshima kwa kusaidia pakubwa kuifanya Jamhuri yetu kuwa ndio kisiwa cha amani kwa takribani miaka yote 50 ya Muungano wetu. Hakujawahi katika historia ya Tanzania kwa rais kuzuwa hisia za mapinduzi ya kijeshi kama hoja mbadala ya kuviza maoni ya walio wengi katika kiwango ambacho wewe umefanya.
Mheshimiwa Rais,
Ulikuwa umejizolea sifa kwa kuwa mmoja wa viongozi wachache wa Tanzania ambao hawakuonea haya mtafaruku wa kisiasa visiwani Zanzibar na ukaamua kuuvalia njuga ili kuhakikisha kuwa unatulizwa kwa amani. Kwa Wazanzibari wengi walio ndani na nje ya nchi, matarajio yao yalikuwa ni kwamba wewe ungelisimimia haki yao ndani ya Muungano kwa uadilifu mkubwa haidhuru maoni waliyonayo kuhusu muundo wa Muungano yanatafautiana na yako.
Tulikutegemea kuwa msimamizi wa haki uliyejizatiti kuhakikisha chembechembe za ubaguzi zinakufa katika kipindi chako cha utawala. Tulikutegemea usimame imara kusimamia hilo maana ndiyo misingi ya kiuongozi. Hatukutegemea hata kidogo uyumbe na uyumbishwe na kundi la wahafidhina ndani na nje ya Chama chako cha Mapinduzi (CCM), kwani maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni muhimu zaidi kuliko maslahi finyu ya makundi hayo ya kihafidhina. Lakini leo hii umekwenda kinyume hata na imani yako kwa kuwabeza Wazanzibari waishio Tanganyika bila ya kuthamini mchango wao mkubwa katika ukuwaji wa uchumi katika Muungano huu.Tukukumbushe Mheshimiwa Rais, ikiwa umesahau, kuwa ni Zanzibar ndiyo iliyoungana na Tanganyika. Si Wapemba wala Waunguja. Sawa na sisi kusema kwamba hatukuungana na Wadengereko au Wanyamwezi waishio visiwani Zanzibar, bali ni Tanganyika kwa jumla kama nchi iliyo na makabila zaidi ya 100 ambayo tokea awali tumekuwa pamoja kwa misingi ya udugu kabla hata ya Muungano wa nchi zetu.
Pili tukukumbushe Mheshimiwa Rais kwamba suala la kuuvunja Muungano halijawahi kuwa sehemu ya mjadala mkuu kwenye Rasimu ya Katiba. Ni wewe na wenzako ndio ambao munalizusha kila mara kwa mintarafu hiyo hiyo ya kutisha. Lakini hata kama hayo yatakuwa ndio matokeo ya munayoyataka, basi tukukumbushe kuwa Waunguja na Wapemba waishio Tanganyika wataathirika sawa sawa na mtetemeko wa Muungano kama ilivyo kwa Watanganyika waishio visiwani. Si walima vitunguu tu ambao husaidia katika ulipaji wa kodi inayotumika kuijenga Tanganyika watakaoathirika na uvunjwaji wa Muungano, bali kila mmoja wetu.
Inashutsha sana kwa rais wa nchi mwenye heshima duniani kukiuka misingi ya usawa kwa kuwalenga jamii ya watu anaowaongoza kwa vitisho badala ya kuwahakikishia ulinzi hasa kwa vile ndie jemedari mkuu wa jeshi aliyeapa kuwalinda wananchi wote wa Muungano huu kwa nguvu zote alizopewa kikatiba.
Hatukuzuii kutetea na kulinda mfumo wa serikali mbili hasa ukiwa mwenyekiti wa chama chako kilichojizatiti katika mfumo huu wa sasa. Lakini ukiwa kama ni rais wa nchi inakupasa kuzitafautisha sehemu hizi mbili za kimamlaka ili kuwe na ufanisi wa demokrasia iliyokuchaguwa na kukupa hadhi ya rais wa Muungano huu.
Hivi kweli hakukuwa na hoja nzito za kuulinda mfumo wa sasa bila ya kuwaingiza wananchi katika mzozo mkubwa utaoleta nyufa katika taasisi tunayotarajia kuilinda na kuiimarisha? Umeamsha hisia kwamba ni Wapemba pekee – kama ulivyotuita – tunaofaidika na Muungano huu na kuendeleza kampeni ya chuki juu yetu, badala ya kuwazindua wananchi michango ya pande zote mbili katika ukuwaji wa uchumi na pia misingi ya amani tunayojivunia. Umekiuka maadili ya uongozi uliotukuka ulioapa kuitekeleza ukiwa ni mkuu wa Muungano huu na kudharau michango yetu Wazanzibari katika sekta zote za maendeleo ya Tanganyika.
Tukukumbushe tena Mheshimiwa Rais kwamba huna uhalali wa kuunganisha mfumo wa Serikali Tatu na uwezekano wa kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi. Umekuwa mmoja wa wapatanishi wa mzozo wa Madagascar, kwa mfano, na unajuwa kwamba mapinduzi ni zao la wapenda madaraka, wasiopenda kuwasikiliza wananchi walio wengi pamoja na uendeshwaji wa nchi kwa misingi isiyoendana na haki, uadilifu na ihsani.
Mfumo wa muungano unahitaji ithibati nzito kutoka kwa wananchi wa pande zote mbili. Haiwi sawa kuendeleza hamasa za kisiasa kwa kuzidharau hisia na matakwa ya walio wengi kwa kisingizio cha kuendeleza siasa za kuwaridhisha Wazanzibari pekee. Hiyo ni sawa na rushwa ya upande mmoja, na ulaghai wa hali ya juu kwa upande mwengine, kwa vile kero za Muungano hazipo kwa Wazanzibari pekee. Tunahitaji mfumo utaokuwa na nguvu ya matakwa ya pande zote mbili, utakaoweza kudumu na kuwa tunu kwa Afrika nzima.
Miaka 50 ya Muungano huu wetu mbali ya kwamba hakuna aliyejaribu kujiunga nasi kwa kutokuwa na manufaa, bali hata wengine walioungana hawakuwahi kuutazama huu wetu kama kigezo cha kuungana. Kwa kuendeleza mfumo wa sasa katika jitihada za kutiatia viraka, zipo ishara nzito kwamba sio tu kwamba Muungano hautadumu, bali pia utazua machafuko makubwa na kuzitia nchi zetu katika giza la historia chafu na dowa litaanza kwako kwa kuogopa kivuli chako mwenyewe. Ni vigumu kwa wakuu wa nchi kupima hali halisi ya nchi kwa kusikiliza wapambe waliojipenyeza kwa fitna na kukisema kile ambacho wakuu hupenda kukisikia. Kwa sasa angalizo kwako ni kuangalia mazingira yalivyo hasa katika Muungano na muamko wa wananchi katika mabadiliko waliyoyategemea zaidi kutoka kwako.
Mheshimiwa Rais,
Tunakuusia tena kama tunavyoziusia nafsi zetu, wasikilize wananchi walio wengi na matakwa yao katika ujenzi wa Muungano mpya utakaokuwa madhubuti na utakaoacha jina lako kuwa kwenye kumbukumbu njema kwa vizazi vijavyo. Haki, usawa na heshima baina ya pande hizi mbili ndio ziwe dira kwako katika kuleta mustakbali wa mabadiliko yatayotuweka katika Muungano utakaothaminiwa na kutunzwa na kila mdau. Matarajio yetu katika kipindi chako ni mageuzi ya kweli yanayoendana na wakati, yatakayoangalia matakwa ya wananchi na kuhakikisha hekima zako na busara zitaweza kuzaa matunda makubwa yatayoweza kuwa neema kwa vizazi vijavyo.
Mheshimiwa Rais,
Khofu ni adui mkubwa wa mabadiliko ya kweli na yaliyo thabiti. Ulichaguliwa kwa matarajio makubwa kwa vile ulionyesha wazi kuwa miongoni mwa wachache walio na dira ya mapatano, ukuwaji wa amani na mapambazuko ya demokrasia nchini. Tanzania iliweza kubadili mfumo wa vyama vingi na kubeza waliokuwa na khofu ya mabadiliko. Zanzibar iliweza kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo kwa upande mkubwa imerejesha imani kwa wananchi na hata wawekezaji na kuwa ni chombezo kwa wengine majirani kufuatia. Na kwa hili la mabadiliko ya mfumo wa Muungano tuna hakika ndio nafasi pekee ya Muungano mpya utakaobeba haki, usawa na heshima kwa kila mwananchi wa nchi zetu hizi.
Mheshimiwa Rais,
Tumekuandikia haya yote kwa kuwa tunaamini kuwa ukitaka unaweza kurekebisha pale ulipoteleza. Wewe ni mwanaadamu licha ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Una nafasi ya kufanya makosa, lakini una nafasi kubwa zaidi ya kusahihisha makosa yako, maana makosa yako yana uzito mkubwa na wa kipekee kwa hatima ya taifa. Tunakunasihi uipitie tena hotuba yako, weka sawa ulimopinda, safisha ulimochafua. Nchi inataka uongozi wako kukwamuka na kusonga mbele. Haitaki vitisho wala khofu zako. Ukihisi ni maamuzi magumu zaidi, rudi kwa wananchi na uwaulize tena kwa uwazi matakwa yao juu ya mfumo wa Muungano wa nchi zetu. Sote tunataka Tanzania kwanza pia hapana shaka, lakini kwa maana gani ya Tanzania kwanza?
Tanzania kwanza isiyobebwa na shengesha za mfumo butu wa sasa.
Tanzania kwanza isiyoviza ukweli wa kuwepo kwa Zanzibar na Tanganyika zinazojiendesha kwa ufanisi.
Tanzania kwanza iliyojidhatiti katika Muungano wa heshima, usawa na haki.
Tanzania kwanza iliyobebwa na matashi na matakwa ya wananchi.
Tanzania kwanza ya Serikali Tatu sio moja ya kuimeza Zanzibar na isiyotenda haki kwa Tanganyika.Ahsante.
Hassan M Khamis
Mwenyekiti ZAWA UK
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Re: [wanabidii] CCM NDIO CHAMA TAWALA NI LAZIMA KIONGOZE KATIBA MPYA
I know that guy (not personaly) wanaomjua hawawezi kuhangaika kujibu maneno yake. Aligombea ubunge wa Africa Mashariki pia ila akapigwa chini.
"i have never fail trying"
--Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Re: [wanabidii] CCM NDIO CHAMA TAWALA NI LAZIMA KIONGOZE KATIBA MPYA
--CCM NDIO CHAMA TAWALA NI LAZIMA KIONGOZE KATIBA MPYA.Hatimaye mpaka leo Tarehe 30/3/2014 Bunge la Katiba Dodoma sasa limetimiza siku 40 toka lianze rasmi Tarehe 18/2/2014, na katika muda wote kwa mahesabu ya haraka haraka Taifa letu limekwisha tumia Shillingi Bilioni 85.6 kwa ajili ya marekebisho ya Katiba kwa ujumla. Shillingi Billioni 70 zilitumika na Kamati ya Tume ya Rasimu ya Warioba, Shillingi Billioni 8.2 zilitumika kukarabati bunge la sasa na Shillingi Billioni 7.6 zimeshatumika mpaka sasa kwa ajili ya posho tu za Wabunge hao 640 wa bunge hilo huko Dodoma mahesabu ambayo hayajumlishi matumizi mengine ya kiofisi ya bunge hilo. Pesa zote hizo zilozkwisha tumika ni sawa na Dola za Kimarekani Millioni 540 na ukweli bado upo pale pale kwamba wananchi wengi haturidhiki na matokeo tunayoyaona huko Bungeni Dodoma, ambako bunge jipya limetawaliwa na malumbano ya kitoto na yasiyo na tija kabisa kwa Wananchi wala Taifa kinyume na wananchi wengi tulivyotegemea baada ya kuongozwa kwa Miaka 52 na Katiba ambayo kimsingi ilitengenezwa kukidhi matakwa ya utawala wa Serikali ya chama kimoja tu CCM. Pesa zilkizokwisha tumika mpaka sasa ambapo Taifa limeambulia kujionea uwezo mdogo wa kufikiri wa Wabunge wengi wa Bunge hilo, zingeweza kuimaliza kabisa barabara mpya ya Iringa mpaka Dodoma ya Kilmoita 260, ambayo inahita dola 140 tu za Kimarekani toka mwanzo wake mpaka mwisho na bado zingeweza kubaki za kutosha Bajeti nzima ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka huu ambayo ni jumla ya Dola za Kimarekani 153 na bado zingeweza kubaki hela za kutosha kutengeneza barabara zote za Tanzania ili ziweze kufikia viwango vya kisasa Mwaka 2025 ambapo zinahitajika jumla ya Dola za Kimarekani Millioni 222 tu ambapo kwa ujumla wake hapa zingetumika jumla ya Dola za Kimarekani 514 Millioni, na bado ukabaki na chenji ya Dola Millioni 26 kwa hela zilizotumika mpaka sasa na Katiba mpya ambayo bado haipo hata dalili ya theluthi moja tu! Tume ya Rasimu ya Katiba imezichoma wee pesa za wananchi Billioni 70 na kuishia kutupatia Rasimu ambayo imekuwa ni utata mtupu kutokana na Tume hiyo kujiingiza kwenye kutenengeza maoni ya Rasimu badala ya kusikiliza tu na kukusanya maoni ya wananchi kama ilivyotakiwa na Jamhuri. Zikaja tena zikatumika Billioni 8.2 kukarabati bunge liweze kuwahudumu Wabunge wote 640, na sasa Billioni 7.6 tayari zimeshachomwa kwa ajili ya posho za Wabunge hao kwa siku 40 ambapo kila siku Wabunge hao hulipwa jumla ya Shillingi 300,000.Wanachi wengi tunajiuliza maswali mengi makubwa na mazito kuliko majibu kwamba kulikoni huko Dodoma na suala zima la marekebisho ya Katiba?Wananchi wengi tulitegemea kwamba Wabunge wetu wanakwenda Dodoma wakiwa wanajua mapema wanachokitaka na wasichokitaka kuhusiana na mapungufu ya Katiba yetu ambayo imekuwa ikililiwa kwa miaka nenda rudi na Wanasiasa wetu wa pande zote mbili, yaani Chama tawala na Wapinzani na hasa wananchi wengi wasomi wa Taifa hili ambao wanawakilishwa vizuri sana na kundi la wajumbe wapya 201 walioteuliwa na Rais kutokana na mapendekezo ya Taasisi mbali mbali za Taifa letu. Badala yake tunajionea vituko vya ajabu kila kukicha ndani ya bunge hilo, kwa siku 10 mfululizo bunge hilo limelumbana kushoto na kulia kwa hoja moja ndogo sana ya namna ya kupiga kura kama iwe ya siri au ya wazi. Na hata pale Kamati maalum ya maridhiano ya bunge ilipotoa hoja ya namna ya kupiga kura hizo, bado Wabunge wetu wameendeleza malumbano ya kitoto na ya aibu sana yasiyo na tija kabisa kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.Wabunge tuliowategemea waturekebishie Katiba sasa wamefikia mahali pa wananchi wengi kujiuliza kujiuliza Taifa letu limekubwa na nani cha ajabu maana sio siri wanaotuwakilisha huko Dodoma ndio sisi wenyewe Wananchi wa Tanzania hii ya sasa. Kila siku Wabunge hawa na hasa wasiokuwa wa CCM wanapochangia hoja za Bunge hilo kuna neno moja wengi wao wanalirudia rudia kila wakati wakiwashambulia Wabunge wa CCM na wale wote wanaounga mkono hoja za msimamo wa chama hicho kwamba wasijione kwa vile ni wengi basi wakadhani kwamba watapitisha mambo yao wanavyotaka, wengine wameeenda mbali hata kutishia kuondoka Bungeni hapo iwapo hoja zinazoungwa mkono na CCM zitalazimishwa kupitishwa bila ridhaa zao. Hoja hizi na zingine za namna hii zimerudiwa bungeni mara kwa mara na hata kuwahoji Wabunge wa CCM wanaotaka kura za wazi kwamba wanaogopa nini kupiga kura za siri kama wao wanajiamini ni wengi? Halafu kuna Wabunge ambao kazi yao ni kuzomea zomea wengine wasiokubaliana na mawazo kama yao, haya yote yamelifanya Bunge kutonyesha sura halisi ya Taifa letu kwamba bado tuna kazi kubwa sana ya kubadilika kimawazo kwa vile sio siri kwamba bado tupo katika usingizi mzito sana kutoelewa maana ya matumizi ya muda, na hasa mazingira ya kisiasa tuliyomo sasa hivi ambayo ndio hoja yangu hasa ya msingi ya waraka wangu huu wa leo.Mataifa yote yalioyendelea Duniani utakuta wananchi wake wana msemo mmoja mzito wa "Muda ni Pesa", ikiwa na maana kwamba ni makosa makubwa sana kwa Binadam kuchezea muda kwa sababu historia ya maisha Duniani ipo wazi kwamba mchezea muda siku zote huwa anazichezea Pesa ambazo aidha angezitengeneza kwa kutumia muda aliouchezea au kupoteza pesa ambazo tayari anazo lakini kwa kuchezea muda anaishia kutoongeza zaidi.Kwa mfano, umekata tiketi ya ndege ya kuondoka Saa Tisa wewe ukafika Saa tisa na dakika mbili maana yake ni kwamba hutaondoka kwa sababu ndege zote zinafunga milango saa ile ile uliyoambiwa kwenye tiketi sasa kwa sababu umechelewa ili uitumie tena ile tiketi basi ni lazima utalazimika kuongeza pesa ili uweze kuitumia kusafiria ama sivyo ile tiketi itakuwa haina kazi tena.Kwa hiyo utakuwa umepoteza muda na pesa kama msemo huu unavyosema na sio siri kwamba dhana zote hizo mbili zimefanyika na Mchakato mzima wa hii Katiba sio tu na hili bunge tu bali ni kuanzia mwanzo wa Tume hii ya Rasimu mpaka hapo ulipofikia sasa hivi Taifa hili tumepoteza muda mwingi sana wa Taifa na pia tumepoteza pesa nyingi za Taifa.Halafu ni dhana muhimu na ya msingi haswa wa waraka wangu huu wa leo nayo ni nafasi ya chama tawala CCM katika mchakato huu mzima wa kurekebisha Katiba, Wabunge wengi wasiokuwa wa CCM wanaonekana kutoelewa kabisa umuhimu wao ndani ya suala hili. Ni muhimu sana tukawekana sawa kwenye hili tena kuambiana ukweli usio mzuri sana lakini ni ukweli wa mambo wa mazingira ya kisiasa tuliona Taifa hili la Tanzania, ni kwamba Chama Cha Mapinduzi ndio chama chenye ridhaa ya wananchi wa Tanzania kutawala kutokana na kura walizowapa kwenye chaguzi karibu zote kuanzia Kata, Wilaya, Mikoa mpaka Taifa. Chama hicho ndicho chenye Viongozi wengi waliochaguliwa na wananchi kwenye kila kona za chaguzi za Taifa hili kwa hiyo kama Sheria inavyosema wao ndio wenye nafasi kubwa ya kufanya maamuzi mengi sana ndani ya mchakato huu kwa sababu nyingi sana mojawapo ikiwa ni pamoja na wingi wao ndani ya bunge hili la Katiba kwa mujibu wa Sheria. Sheria ya Bunge la Jamhuri ipo wazi kwamba ni Theluthi mbili kwa Tatu ndio inayotawala ndani ya jengo hilo la Taifa, kwa maana ya kwamba wengi ndio wenye nafasi kubwa ya kushinda maamuzi mengi kutokana na dhana muhimu sana ya wengi ndio wenye hoja ndani ya Demokrasia yoyote Duniani. Na ni ukweli usiopingika kuwa ni Serikali ya chama hicho hicho Tawala iliyoamua kuruhusu mchakato huu kwa hiyo, haiwekzekani kwamba Chama hicho hakikujua kwamba kwenye mbio hizi za mchakato kungetokea ambayo yanatokea sasa hivi, halafu baada ya kutawala miwa miaka 52 mfululizo chama hicho sasa hivi ndio chama pekee kikongwe kilichomo kwenye madaraka katika Afrika nzima ni kwa sababu kimepitia madharuba mengi sana ndio kipo hapo kilipo yaani bado kwenye madaraka. Wale wabunge wote wasiotaka kuelewa ukweli ni kwamba CCM ndio wengi ndani ya Bunge sio kwa bahati mbaya ila kwa mujibu wa sheria kwa hiyo ni lazima Wabunge hao waelewe hilo katika kazi zao zote humo Bungeni.Demokrasia ipo wazi katika Dunia nzima inapotumika kwamba siku zote wengi wape, kwa hiyo CCM ndio wanaotakiwa kuwa na mkono wa juu katika maamuzi mengi na wala hawana sababu ya kuogopa au kujisikia vibaya au kuanza siasa za huruma. Kwa wale wasiotaka kuelewa hilo ni muhimu wakajitoa huko Bungeni sasa hivi kuliko kupoteza muda bure wa Taifa kubishania hoja zisizo na mashiko za kuilaumu CCM kwa wingi wao bungeni ni ujuha wa hali ya juu sana ambao usingetegemea kuonekana Bunge la Taifa. Wabunge wakubali ukweli kwamba wananchi wengi wa Tanzania wanaridhika na CCM na ndio maana wapo madarakani kwa miaka 52 toka tupate Uhuru mpaka leo, huu ni ukweli usiopingika kwamba hata wanayoyasimamia ndio yanayoungwa mkono na wananchi wengi wa Taifa hili. Sasa tunakubali kwamba kutakuwa na misuguano ndani ya mchakato huu ni muhimu sana wabunge wasio wa CCM wakalielewa na kulikubali hili kwamba CCM ndio wenye mkono mrefu kutokana na wingi wao unaotokana na kukubalika zaidi na wananchi wengi wa Taifa hili. Kwenye waraka wa leo nimeshindwa kwa makusudi kabisa kutumia mifano ya Demokrasia zingine ni kwa sababu ya kuelewa sana kwamba katika suala la mchakato kama huu huwezi kutumia mifano ya mataifa mengine kwa sababu mazingira ya kila Taifa lililohusika na michakato ya namna hii hayafanani kabisa.Kwa kumaliza ninapenda kuwakumbusha Wabunge wa bunge hili la Katiba kwamba wafike mahali wajiridhishe na ukweli wa mazingira ya kisiasa tuliyonayo kwamba CCM ndio chama Tawala na ndio kwa mujibu wa Sheria na kwamba pamoja na Demokrasia kuwapa nafasi ya kushiriki kwa kutoa mawazo yao, bado inapofikia mahali pa kushindana sana basi zitapigwa kura za wanaotaka na wasiotaka na sio siri kwamba kwenye kura za namna hiyo CCM watakuwa ndio wenye mkono mrefu kuliko wengine. Wakubali kwamba uamuzi wa kufanyika marekebisho ya Katiba umefanyika kutokana na kilio cha wananchi wengi wa Taifa hili na ni kilio kilichosikilizwa na Chama Tawala CCM, tunategemea wabunge wote wafanye kazi pamoja na kutuletea Katiba mpya yenye tija kwa wananchi na Taifa. Wafike pahali waachane na malumbano ya kitoto yasiyo na tija kabisa kama yalikuwa yakifanyika jana juzi Tarehe 27/3/2014, ilikuwa ni moja ya siku ya aibu sana kwa Taifa hili na hasa watoto wetu na wajukuu wetu, ninaomba kuwakumbusha wabunge wetu kwamba Taifa limekwisha tumia Shiilingi Billioni 85.6 na mpaka leo siku ya 40 bado hatujaona la maana walilokwisha lifanya kuelekea kutuaminisdha kwamba tutapata Katiba mpya na bora kwa Taifa. Tumewasikia kwamba wengi wao ni wasemaji wazuri sana, wengi wao ni wasemaji wazuri sana, lakini mwisho wa yote CCM ndio wengi ndani ya bunge na ndio wenye nafasi ya kuamua maamuzi mengi iwapo kutatokea utata au msuguano kwenye hoja, na wajaribu sana kuweka Tanzania kwanza.MUNGU AIBARIKI TANZANIA
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
[wanabidii] BARUA YA WAZI KWA JK KUTOKA KWA CHAMA CHA WAZANZIBARI UINGEREZA
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
Ikulu
P O Box 9120
Dar es Salaam
Yah: Hotuba Yako ya Kuwagawa Watanzania
Mheshimiwa Rais,
Tumelazimika kuandika barua hii kwako kama kiongozi wa juu wa taifa letu ili kukuonesha namna ambavyo tumesikitishwa na matamshi yako wakati wa ufunguzi wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Tukiwa sehemu ya jamii kubwa ya Kizanzibari tuishio nje ya nchi yetu, hotuba yako imetutia khofu kubwa kulenga kwake zaidi kwenye kuvunja na sio kujenga mustakbali mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hotuba yako Mheshimiwa Rais, haikuzingatia maslahi ya Muungano wetu kwa misingi ya umoja unaonendana na matakwa ya wananchi walio wengi.
Tunakuandikia barua hii kukuzindua kile ambacho tumekiona kinakwenda tafauti na akhlaki zako. Ukweli ni kwamba kwa muda wote wa kipindi chako cha utawala tumekuwa tukikutazama kama ni tarajio jipya lililojengeka kwa misingi ya haki, insaaf na kioo cha uadilifu kwa pande mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano.
Tunazungumza nawe moja kwa moja sio tu kama kiongozi wa taifa, bali pia kama mtu tuliyempa matumaini hayo. Wewe ni mtu wa mwisho kwetu kuamini kuwa anaweza kujenga khofu badala ya matumaini, batili badala ya halali, kitisho badala ya nasaha na mgawanyiko badala ya utangamano.
Mheshimiwa Rais,
Ulichokifanya siku ya tarehe 21 Machi 2013 ni kuzua taharuki kwa raia wa Jamhuri ya Muungano hasa kwa ndugu zetu wa Kizanzibari waishio upande wa pili wa Muungano huo. Ulichofanya ni kulihusisha jeshi letu linalothaminiwa dunia nzima kwa misingi ya heshima kwa kusaidia pakubwa kuifanya Jamhuri yetu kuwa ndio kisiwa cha amani kwa takribani miaka yote 50 ya Muungano wetu. Hakujawahi katika historia ya Tanzania kwa rais kuzuwa hisia za mapinduzi ya kijeshi kama hoja mbadala ya kuviza maoni ya walio wengi katika kiwango ambacho wewe umefanya.
Mheshimiwa Rais,
Ulikuwa umejizolea sifa kwa kuwa mmoja wa viongozi wachache wa Tanzania ambao hawakuonea haya mtafaruku wa kisiasa visiwani Zanzibar na ukaamua kuuvalia njuga ili kuhakikisha kuwa unatulizwa kwa amani. Kwa Wazanzibari wengi walio ndani na nje ya nchi, matarajio yao yalikuwa ni kwamba wewe ungelisimimia haki yao ndani ya Muungano kwa uadilifu mkubwa haidhuru maoni waliyonayo kuhusu muundo wa Muungano yanatafautiana na yako.
Tulikutegemea kuwa msimamizi wa haki uliyejizatiti kuhakikisha chembechembe za ubaguzi zinakufa katika kipindi chako cha utawala. Tulikutegemea usimame imara kusimamia hilo maana ndiyo misingi ya kiuongozi. Hatukutegemea hata kidogo uyumbe na uyumbishwe na kundi la wahafidhina ndani na nje ya Chama chako cha Mapinduzi (CCM), kwani maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni muhimu zaidi kuliko maslahi finyu ya makundi hayo ya kihafidhina. Lakini leo hii umekwenda kinyume hata na imani yako kwa kuwabeza Wazanzibari waishio Tanganyika bila ya kuthamini mchango wao mkubwa katika ukuwaji wa uchumi katika Muungano huu.
Tukukumbushe Mheshimiwa Rais, ikiwa umesahau, kuwa ni Zanzibar ndiyo iliyoungana na Tanganyika. Si Wapemba wala Waunguja. Sawa na sisi kusema kwamba hatukuungana na Wadengereko au Wanyamwezi waishio visiwani Zanzibar, bali ni Tanganyika kwa jumla kama nchi iliyo na makabila zaidi ya 100 ambayo tokea awali tumekuwa pamoja kwa misingi ya udugu kabla hata ya Muungano wa nchi zetu.
Pili tukukumbushe Mheshimiwa Rais kwamba suala la kuuvunja Muungano halijawahi kuwa sehemu ya mjadala mkuu kwenye Rasimu ya Katiba. Ni wewe na wenzako ndio ambao munalizusha kila mara kwa mintarafu hiyo hiyo ya kutisha. Lakini hata kama hayo yatakuwa ndio matokeo ya munayoyataka, basi tukukumbushe kuwa Waunguja na Wapemba waishio Tanganyika wataathirika sawa sawa na mtetemeko wa Muungano kama ilivyo kwa Watanganyika waishio visiwani. Si walima vitunguu tu ambao husaidia katika ulipaji wa kodi inayotumika kuijenga Tanganyika watakaoathirika na uvunjwaji wa Muungano, bali kila mmoja wetu.
Inashutsha sana kwa rais wa nchi mwenye heshima duniani kukiuka misingi ya usawa kwa kuwalenga jamii ya watu anaowaongoza kwa vitisho badala ya kuwahakikishia ulinzi hasa kwa vile ndie jemedari mkuu wa jeshi aliyeapa kuwalinda wananchi wote wa Muungano huu kwa nguvu zote alizopewa kikatiba.
Hatukuzuii kutetea na kulinda mfumo wa serikali mbili hasa ukiwa mwenyekiti wa chama chako kilichojizatiti katika mfumo huu wa sasa. Lakini ukiwa kama ni rais wa nchi inakupasa kuzitafautisha sehemu hizi mbili za kimamlaka ili kuwe na ufanisi wa demokrasia iliyokuchaguwa na kukupa hadhi ya rais wa Muungano huu.
Hivi kweli hakukuwa na hoja nzito za kuulinda mfumo wa sasa bila ya kuwaingiza wananchi katika mzozo mkubwa utaoleta nyufa katika taasisi tunayotarajia kuilinda na kuiimarisha? Umeamsha hisia kwamba ni Wapemba pekee – kama ulivyotuita – tunaofaidika na Muungano huu na kuendeleza kampeni ya chuki juu yetu, badala ya kuwazindua wananchi michango ya pande zote mbili katika ukuwaji wa uchumi na pia misingi ya amani tunayojivunia. Umekiuka maadili ya uongozi uliotukuka ulioapa kuitekeleza ukiwa ni mkuu wa Muungano huu na kudharau michango yetu Wazanzibari katika sekta zote za maendeleo ya Tanganyika.
Tukukumbushe tena Mheshimiwa Rais kwamba huna uhalali wa kuunganisha mfumo wa Serikali Tatu na uwezekano wa kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi. Umekuwa mmoja wa wapatanishi wa mzozo wa Madagascar, kwa mfano, na unajuwa kwamba mapinduzi ni zao la wapenda madaraka, wasiopenda kuwasikiliza wananchi walio wengi pamoja na uendeshwaji wa nchi kwa misingi isiyoendana na haki, uadilifu na ihsani.
Mfumo wa muungano unahitaji ithibati nzito kutoka kwa wananchi wa pande zote mbili. Haiwi sawa kuendeleza hamasa za kisiasa kwa kuzidharau hisia na matakwa ya walio wengi kwa kisingizio cha kuendeleza siasa za kuwaridhisha Wazanzibari pekee. Hiyo ni sawa na rushwa ya upande mmoja, na ulaghai wa hali ya juu kwa upande mwengine, kwa vile kero za Muungano hazipo kwa Wazanzibari pekee. Tunahitaji mfumo utaokuwa na nguvu ya matakwa ya pande zote mbili, utakaoweza kudumu na kuwa tunu kwa Afrika nzima.
Miaka 50 ya Muungano huu wetu mbali ya kwamba hakuna aliyejaribu kujiunga nasi kwa kutokuwa na manufaa, bali hata wengine walioungana hawakuwahi kuutazama huu wetu kama kigezo cha kuungana. Kwa kuendeleza mfumo wa sasa katika jitihada za kutiatia viraka, zipo ishara nzito kwamba sio tu kwamba Muungano hautadumu, bali pia utazua machafuko makubwa na kuzitia nchi zetu katika giza la historia chafu na dowa litaanza kwako kwa kuogopa kivuli chako mwenyewe. Ni vigumu kwa wakuu wa nchi kupima hali halisi ya nchi kwa kusikiliza wapambe waliojipenyeza kwa fitna na kukisema kile ambacho wakuu hupenda kukisikia. Kwa sasa angalizo kwako ni kuangalia mazingira yalivyo hasa katika Muungano na muamko wa wananchi katika mabadiliko waliyoyategemea zaidi kutoka kwako.
Mheshimiwa Rais,
Tunakuusia tena kama tunavyoziusia nafsi zetu, wasikilize wananchi walio wengi na matakwa yao katika ujenzi wa Muungano mpya utakaokuwa madhubuti na utakaoacha jina lako kuwa kwenye kumbukumbu njema kwa vizazi vijavyo. Haki, usawa na heshima baina ya pande hizi mbili ndio ziwe dira kwako katika kuleta mustakbali wa mabadiliko yatayotuweka katika Muungano utakaothaminiwa na kutunzwa na kila mdau. Matarajio yetu katika kipindi chako ni mageuzi ya kweli yanayoendana na wakati, yatakayoangalia matakwa ya wananchi na kuhakikisha hekima zako na busara zitaweza kuzaa matunda makubwa yatayoweza kuwa neema kwa vizazi vijavyo.
Mheshimiwa Rais,
Khofu ni adui mkubwa wa mabadiliko ya kweli na yaliyo thabiti. Ulichaguliwa kwa matarajio makubwa kwa vile ulionyesha wazi kuwa miongoni mwa wachache walio na dira ya mapatano, ukuwaji wa amani na mapambazuko ya demokrasia nchini. Tanzania iliweza kubadili mfumo wa vyama vingi na kubeza waliokuwa na khofu ya mabadiliko. Zanzibar iliweza kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo kwa upande mkubwa imerejesha imani kwa wananchi na hata wawekezaji na kuwa ni chombezo kwa wengine majirani kufuatia. Na kwa hili la mabadiliko ya mfumo wa Muungano tuna hakika ndio nafasi pekee ya Muungano mpya utakaobeba haki, usawa na heshima kwa kila mwananchi wa nchi zetu hizi.
Mheshimiwa Rais,
Tumekuandikia haya yote kwa kuwa tunaamini kuwa ukitaka unaweza kurekebisha pale ulipoteleza. Wewe ni mwanaadamu licha ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Una nafasi ya kufanya makosa, lakini una nafasi kubwa zaidi ya kusahihisha makosa yako, maana makosa yako yana uzito mkubwa na wa kipekee kwa hatima ya taifa. Tunakunasihi uipitie tena hotuba yako, weka sawa ulimopinda, safisha ulimochafua. Nchi inataka uongozi wako kukwamuka na kusonga mbele. Haitaki vitisho wala khofu zako. Ukihisi ni maamuzi magumu zaidi, rudi kwa wananchi na uwaulize tena kwa uwazi matakwa yao juu ya mfumo wa Muungano wa nchi zetu. Sote tunataka Tanzania kwanza pia hapana shaka, lakini kwa maana gani ya Tanzania kwanza?
Tanzania kwanza isiyobebwa na shengesha za mfumo butu wa sasa.
Tanzania kwanza isiyoviza ukweli wa kuwepo kwa Zanzibar na Tanganyika zinazojiendesha kwa ufanisi.
Tanzania kwanza iliyojidhatiti katika Muungano wa heshima, usawa na haki.
Tanzania kwanza iliyobebwa na matashi na matakwa ya wananchi.
Tanzania kwanza ya Serikali Tatu sio moja ya kuimeza Zanzibar na isiyotenda haki kwa Tanganyika.
Ahsante.
Hassan M Khamis
Mwenyekiti ZAWA UK
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
[wanabidii] Tujali mazingira yetu
Kuwa na afya bora ni jambo muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Kama una matatizo ya afya hutaweza kutimiza majukumu yako ya kila siku, hivyo maisha yako hayatakuwa katika hali nzuri.
Sote tunajua huwezi kufanya chochote pale unapokuwa mgonjwa na masuala ya afya yanahusisha zaidi mazingira yanayotuzunguka. Ni ukweli kwamba mazingira yetu yakiwa machafu basi afya zetu zitakuwa katika hatari kubwa, kwani uchafu ndiyo mahali mwafaka kwa wadudu wasababishao magonjwa kuzaliana na kustawi.
Ni jambo la kusikitisha kuwa Watanzania wengi hatujali mazingira yanayotuzunguka. Elimu ya kutosha imetolewa kwa njia za mikutano ya kijamii, vyombo vya habari na njia nyinginezo, lakini haieleweki kinachotokea kama ni kutojali au ni kweli kutoelewa. Hebu tuzitafakari tabia hizi.
Unaweza kukuta mtu amevaa vizuri, anapendeza lakini ukienda kuangalia mahali anapotoka yaani nyumbani kwake, utashangaa. Kumejaa uchafu usiofanana na kupendeza kwa mtu huyo. Mtu mtanashati ndiye utakuta anakula ndizi barabarani na maganda akayatupa hapo barabarani bila kujali kwamba atavutia inzi waletao maradhi.
Mtu huyu mtanashati ndiye anayetupa uchafu barabarani akiwa ndani ya daladala bila kujali nani atauokota, kama kweli utaokotwa. Usafi ni tabia, kama ni tabia ina maana mtu atakuwa msafi katika nyendo zake zote, iweje sasa mtu awe msafi katika nguo alizovaa halafu akatupa taka ovyo, kwa nini asijimwagie takataka mwenewe.
Bila shaka mtu huyu ni mnafiki, hata mavazi hayo masafi ni kwa ajili ya kujionyesha tu. Kama kungekuwa hakuna mtu wa kumwangalia, bila shaka hata nguo zake zingekuwa chafu.
Utakuta watu na akili zao wanauza chakula pembeni mwa mifereji ya maji machafu. Wakati mwingine utakuta mtu anafanya usafi sehemu anayofanyia biashara na kuzisukuma takataka pembeni au upande wa pili wa barabara. Watu wa namna hii wanafikiria inzi nao wanaijua mipaka yao.
Bila kujali, utakuta mtu anaukaribisha ugonjwa wa kipindupindu kwa kufanya vitendo vya kinyama kabisa; kwani ni vitendo vya uuaji. Utakuta katika kipindi cha mvua mtu anatumia mwanya wa kunyesha mvua kwa kuzibua choo chake na kuelekeza uchafu wote barabarani.
Watoto wanatembea pekupeku, wadudu wanazaliana na magonjwa nje nje. Cha kushangaza uchafu huo unaelekezwa kwenye barabara ambayo hata yeye na familia yake wanapita. akati mwingine ni watoto wake ndiyo wanaoetembea pekupeku. Wakipata maradhi, ataishia kulalamika kwamba wanawe wamerogwa. Hakumbuki vitendo vichafu alivyofanya. Ukiuliza ni kwa nini watu wanaishi na uchafu watakwambia kwamba Serikali imeshindwa kutoa takataka hizo; sababu ya kawaida kwa Watanzania wasiotaka kutimiza wajibu wao.
Kama nilivyosema hapo mwanzo usafi ni tabia, hivyo hauendeani na usomi, utajiri au sifa nyingine. Wapo watu wenye uwezo ambao nao wana tabia zinazochangia kufanya mazingira yawe machafu. Hawa unakuta wanajenga ukuta kuzuia njia ya maji, hivyo kusababisha kero na madhara ya kiafya kwa watu wananowazunguka.
Kwa kutumia uwezo wa kifedha wanaziba kabisa njia za maji machafu, hivyo kulazimisha maji hayo kuishia kwenye nyumba za watu wanaowazunguka na wenyewe wanaona ni sawa kabisa.
Wengine ni wasomi wazuri lakini usomi wao unashindwa kuwafafanulia kwamba kipindupindu kitakapofumuka, hata wao wapo hatarini kwani hawaruki kwa helikopta kwenda majumbani kwao.
Yaani utakuta maji yenye kemikali hatari yanatiririka kuelekea kwenye makazi ya watu na kusababisha harufu kali na hatari ya magonjwa kama vile saratani na mengineyo. Utaona maji machafu yenye rangi za ajabu na harufu kali yakitiririka kwenye makazi ya watu.
Watu hawa wanatumia fedha nyingi kuhonga wenye mamlaka ili wasiwachukulie hatua, badala ya kutumia fedha hizo kutengeneza miundombinu itakayosaidia kusafirisha majitaka kwa usalama zaidi. Ni tabia za uchafu ndiyo zinazowasumbua na kuwafanya watenda vitendo vya kuchafua mazingira
Tunaweza kufikiri ni gharama kuweka mazingira yetu safi, lakini ukweli ni kwamba ni gharama kubwa zaidi kutibu madhara yanayosababishwa na mazingira machafu. Ukipata magonjwa kwanza shughuli zako zinasimama, pili unatumia muda na fedha nyingi kujitibia, hii yote ni hasara kubwa kwako.
Lakini hasara kubwa kuliko zote ni kwamba, unaweza kupoteza maisha yako na hakuna gharama inayoweza kuifidia maisha. Kwani ungetumia gharama gani kushughulikia maji machafu ukilinganisha na kuharisha wiki nzima?
Mwisho utaona kile kidimbwi kinasababisha mlolongo wa hasara juu ya hasara. Na hapo bado tutaililia Serikali kweli ni sahihi hii?
Ni wakati sasa Watanzania tubadilike na kujali mazingira yanayotuzunguka kwani mazingira bora maana yake afya bora na hakuna maendeleo, bila afya bora. Huu ni wajibu wetu sote kama kweli tunataka kupiga hatua.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
[wanabidii] Programu ya kompyuta kuvuruga ATM wiki ijayo
Wiki moja kabla ya kusitishwa huduma za programu ya kompyuta (OS) ya Windows Xp, imefahamika kuwa waathirika wakubwa watakuwa ni benki na taasisi za fedha ambazo hutumia mfumo huo katika mashine za kutolea fedha (ATMs)
Shirika la Microsoft limethibitisha kuwa benki ni miongoni mwa taasisi nyingi zitakazoathirika na mabadiliko hayo.
Baadhi zimeanza kufanyia kazi tatizo hilo, ikiwamo benki moja ambayo jana alasiri ilituma ujumbe kwa wateja wake kuwa, "Ndugu mteja, kuanzia Jumamosi saa 2:00 usiku Aprili 5, mpaka Jumapili saa 12:00 asubuhi tutakuwa tunaboresha mashine zetu za ATM, hivyo kadi yako haitafanya kazi kwa kipindi hiki. Asante."
Kwa mujibu wa Microsoft asilimia kubwa ya benki katika nchi zinazoendelea zinatumia programu ya Windows XP katika kuendesha ATM, hivyo kuwa moja ya waathirika wa mpango huo.
Katikati ya Machi, Microsoft ilitangaza kusitisha huduma zote zinazohusiana na bidhaa zake za Windows Xp kufikia Aprili 8, mwaka huu. Pia shirika hilo litasitisha ufanisi wa programu ya kuzuia na kupambana na virusi ya Microsft Security Essentials katika mfumo wa Windows Xp, hivyo kufanya urahisi wa kompyuta zinazoitumia kukosa ulinzi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Twiga Hosting, Jacob Urassa alisema Watanzania hawatakiwi kupuuza onyo hilo kwa kuwa ikifika Aprili 9 usalama wa taarifa zao utakuwa hatarini.
"Windows XP ni dhaifu mara tano zaidi ya Windows 7 na 8, kwa hiyo Microsoft wameona ni bora wakaitoa sokoni. Kwa maana hiyo ATM na kompyuta zote zinazotumia programu hizo hazitakuwa na ulinzi wa uhakika," alisema Urassa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Teknolojia ya Mawasiliano (IT).
Alisema kuwa kuna idadi kubwa sana ya Watanzania wanaoendelea kutumia bidhaa hizo zikiwemo taasisi kubwa nchini hivyo kuna haja kubwa ya kuchukua hatua za kubadilika na teknolojia.
Naye, Ofisa Uhusiano wa Benki ya Posta, Noves Moses aliwatoa wasiwasi wateja wake kuwa licha ya kusitishwa kwa matumizi ya Windows XP, bado benki hiyo itaendelea kutoa huduma zenye kiwango kile kile.
http://www.mwananchi.co.tz/kitaifa/Programu-ya-kompyuta-kuvuruga-ATM-wiki-ijayo/-/1597568/2264804/-/mj380v/-/index.html