Mnaodhani kuwa Dr Makufuri ni mtetezi wa wanyonge (kama anvyojinukuuu mara kwa mara) mnapaswa kutafakari upya. Tangu Dr Makufuri alipoingia madarakani amefanikiwa kukanyaga haki mbalimbali za raia pamoja na kufanya maisha ya mamilioni ya watanzania wa kawaida yawe magumu zaidi kuliko ilivyokuwa katika utawala wa Dr JK. Kuna baadhi ya maamuzi ya kikandamizaji ninayoweza kuyakumbuka ambayo madhara yake yamewaumiza wananchi huku wanafiki na wachochezi wachache wakichekelea wakati wanajua haki za msingi za wananchi zimekanyagwa:
*
KUINGILIA MFUMO WA BIASHARA HURIA
Ni dhahiri mfumo wa uchumi wa sasa ni wa BIASHARA HURIA – kwamba upatikanaji wa bidhaa (supply) na na mahitaji (demand) ndio huamua bei (price). Kazi ya serikali sio kufanya biashara ila kazi yake ni kurahisisha mazingira ya biashara na kukusanya kodi. Lakini tumeshuhudia Dr Makufuri akizuia uagizaji wa sukari (intentional supply disruption) na kusababisha upungufu mkubwa wa sukari ambayo sasa huuzwa kati ya Tsh 6000 kwa kilo badala ya bei ya Tsh 1200 ya awali. Kwa lugha nyepesi naweza kusema uamuzi huu umekuza ugumu wa maisha ya wanyonge kwa 400% . Tazama sasa jinsi maamuzi ya mtu mmoja yanavyoweza kuathiri maisha ya mamilioni ya watanzania.
*
KODI YA MITUMBA, NYUMBA ZA KUPANGA, ATM NA MIAMALA YA SIMU
Kodi hizi zimelenga kuwaumiza wanyonge moja kwa moja. Viwanda vya nguo vya hapa ndani havijatosheleza mahitaji ya nguo kwa watanzania wote. Aidha, viwanda hivi bado havijawa na uwezo wa kutengeneza aina mbalimbali za nguo na imara kama za mitumba. Wananchi sio wajinga hadi wang'ang'anie kuvaa chupi na sidiria za mitumba. Ni kwa sababu hakuna nguo mbadala zilizo maridadi na imara kama mitumba ndio maana wanaona ni afadhali waendelee kuvaa chupi na sidiria za mitumba. Viatu vya mitumba vimekuwa ni mkombozi wa wanyonge kwa muda mrefu. Sasa inabidi wananchi tujiandae kuvaa YEBOYEBO nyeupe na njano zinazotengenezwa na makanjibai wa hapa nchini.
*
Utozaji wa kodi kwa wenye nyumba za kupanga ni msumali mwingine wa moto kwenye kidonda cha wanyonge. Asilimia 99% ya watanzania wanaishi kwenye nyumba za kupanga. Kodi hii itawaumiza watanzania wanyonge na ambao hawana uwezo wa kujenga nyumba zao za kuishi kwa sababu ya ugumu wa maisha unaowakabili. Tutarajie baba wenye nyumba kupandisha kodi za pango maradufu. Hivyo, wapangaji wengi watashindwa kumudu kodi za pango na kuishi chini ya miti huku wengine wakikimbilia mapangoni kujihifadhi. Naona kasi ya watanzania kuanza kuishi mapangoni kama ilivyokuwa zama za kwanza za mawe imewadia. Tunatolewa kwenye maisha ya utu na kurudishwa kwenye maisha ya kinyama!
*
Kana kwamba hili halitoshi, bado mwananchi huyo huyo amebebeshwa zigo la kodi ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu na kupitia ATM. Makampuni ya simu yote nchini Tanzania yameongeza gharama za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu na tayari marekebisho hayo yameishasambazwa kwa mawakala wote. Nimebahatika kuona nakala hiyo ila nilishindwa kuipiga picha na kuiattach humu kwa sababu simu yangu feki imefungiwa na TCRA. Naomba mdau yeyote atakayeipata nakala hiyo aipige picha na kuitupia humu ili kila mtanzania aangalie maumvivu atakayopata. Na bado.....mabenki nayo yataongeza gharama za kuchukua fedha na kuangalia salio very soon....stay tuned.....tuko pamoja katika maumivu haya hadi mwisho wa dahari! Tutarajie ukabaji na uporaji wa fedha majumbani kuongezeka kwa kuwa sasa wananchi wataamua kutunzia fedha zao kwenye michago na vibubu nyumbani badala ya kuzihifahi benki au kwenye simu.
*
KUVUNJA SHERIA YA KAZI
Kwa kisingizio cha kusaka wafanyakazi hewa, serikali ya Dr Makufuri imesema haitaongeza mishahara ya watumishi, imezuia upandaji wa vyeo na uhamisho wa watumishi kutoka kitengo kimoja hadi kingine (recategorization) au kutoka mwajili mmoja hadi mwajiri mwingine ambao atalipwa mshahara mkubwa kuliko ule wa sasa. Aidha, serikali imezuia ulipaji wa nauli kwa watumishi wanaoenda likizo au wanaostaafu. Kwa maana hiyo ni kwamba serikali imeaumua kuendesha nchi bila kuzingatia sheria za ajira. Hii ni hali ya hatari sana.
*
WAFANYAKAZI HEWA
Serikali imeanza kuwakamata baadhi ya watumishi wanaosadikiwa kuwa "wafanyakazi hewa" na kuwalazimisha kulipa fedha zilizongizwa (na mafisadi) kwenye akaunti zao. Inakuwaje mtumishi amestaafu lakini bado SERIKALI inaingiza fedha kwenye akaunti yake halafu leo serikali hiyo hiyo inakuja kumkamata na kumfungulia mashtaka? Na kibaya zaidi kuna baadhi ya watumishi ambao fedha zimeingizwa kwenye akaunti zao na kuchukuliwa na mafisadi walioziingiza pasipo mwenye akaunti kujua. Kwanini hao mafisadi waliongiza fedha kwenye akaunti hizo wasichuliwe hatua badala yake wananchi wanyonge wasiokuwa na hatia ndio wananyanyaswa? Na je, mbona hatujasikia wale mabingwa wa kuchomekea wafanyakazi hewa wakikamatwa mpaka leo hii wakati wameitia serikali hasara ya mabilioni ya shilingi? Kwanini wahusika wanaachwa lakini wasiohusika wanaandamwa kila kukicha?
*
UKOSEFU WA FEDHA MTAANI
Kufuatia "ubanaji wa matumizi" unaofanywa na serikali ya Makufuri, mzunguko wa fedha umepungua sana hapa mtaani na kupelekea mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa muhimu kwa wananchi. Ukosefu huu wa fedha umeongeza ughali wa maisha kwa wanyonge, hivyo kushindwa kumudu gharama za maisha. Wananchi wamekata tama kabisa ya maisha na wanajuta kuzaliwa katika nchi hii ya Tanganyika.
0 comments:
Post a Comment