Wednesday, 1 June 2016

[wanabidii] AHADI YA RAIS MAGUFULI KWA WAFANYABIASHARA WAKUBWA YAANZA KUTIMIA

Na Mwandishi wetu


Nia serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuanza kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa nchini ili kuweza kufanya kazi kwa pamoja na kusaidia kuinua uchumi wa nchi lakini pia kutoa ajira kwa watanzania katika viwanda vinavyoilikiwa na matajiri hao.


Hilo limenza kuonekana siku moja baada ya Rais Magufuli kuweka wazi nia yake hiyo ambapo Mo Blog ilifanikiwa kupata picha ambayo ilimwonesha Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akizungumza mambo mbalimbali na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Taznzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi mara baada ya kumalizika kwa halfa ya utoaji wa Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda (PMAYA) zilizoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).


Kutokana na muonekano wa viongozi hao wawili wa serikali na sekta binafsi ni wazi kuwa serikali ya Rais Magufuli imejipanga kushirikiana na wafanyabiashara ili kufanya kazi kwa pamoja na kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya viwanda jambo ambalo litachangia ukuaji wa kasi wa uchumi na upatikanaji wa ajira kwa Watanzania.



CAPTIONS:


Reginald Mengi and Sospeter Muhongo: Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akisalimiana kwa furaha na  Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto) wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda 2015 (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana.


Sospeter Muhongo: Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda  (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana.


Dk. Mengi na Muhongo: Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akifurahi jambo na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto) wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda  (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana.

 

Rais Magufuli na Wafanyabiashara: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda 2015 (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment