Friday 31 July 2015

Re: [wanabidii] TULIOMWITA LOWASSA FISADI TUMUOMBE RADHI

Mike Zunzu: wote huo ulikuwa ni mwendelezo wa uzandiki na uzushi wa hao mnawaabudu kwamba ni malaika. Baba wa watu EL alikuwa hajawahi hata siku moja kuongea nasi kuhusu kuja ACT lakini ukatungwa uwongo mwingi juu ya uhusiano wa EL na ACT. Ukweli hukwea ngazi polepole na hatimaye hufika na sasa umefika. Hili jibu pia linamhusu Emmanuel Muganda. Kiongozi wetu aliposema tungemkaribisha yes kwa utaratibu wetu wala hilo hakuna shaka. Na ndiyo maana tumewapongeza wenzetu CDM kwa kupata mwanasiasa mwenye nguvu. 

Paul Lawala: Msimamo wangu ni uleule uliousikia juzi katika BBC. Ni kwamba Lowassa ni jasiri kwa maamuzi aliyochukua. Ni mwanasiasa aliyeshinda majaribu mengi. Amepitia kila aina ya mateso ya kisiasa kwa mwanasiasa wa aina yake. Na sasa amefanya maamuzi sahihi kuondoka CCM. Na hapa tulipo hakuna sehemu sahihi kwake katika opposition zaidi ya CDM. Angeenda chama kingine chochote angepata shida sana kwa sababu viongozi wa CDM wangejitenga nacho. Ilikuwa lazima aende kwenye chama chao hichohicho hata kama imani zao haziendani aslani. Maslahi yamekutana. Kwa kitendo chake hiki cha kishujaa, amebadilisha kabisa siasa za Tanzania na ana uwezo wa kuishinda CCM kuliko mwana siasa mwingine yeyote ndani ya upinzani na hili CCM wanalijua, hakuna shaka. Tunawapongeza pia CDM kwa kufanikiwa kumpata mwanasiasa huyu. 

Lakini ninaenda mbele na kusema kwamba hao viongozi wa CDM ndiyo waliomchafua Lowassa na ndio haohao watakaolazimika kumsafisha. Hao akina Kubenea wameandika miaka kadhaa mfululizo wakimnanga Lowassa kwa mambo ya kutunga lakini ghafla jana wanatoa makala za kumsifia.  Kiswahili rahisi katika hilo ni UNAFIKI, nothing less, nothing more. Ndiyo maana mzee wa watu Dk Slaa amejifungia kwa sababu amejaliwa uso wa soni na aibu! 

Nasema tena siasa za maji taka hazina mwisho mwema. Viongozi wa CDM lazima wale matapishi yao.Hawana muda wa kuhubiri sera zao, wao ni kutukana watu barabarani mchana na usiku.Na kitendo hiki ni chema sana kwa sababu hawa wandugu wameumiza watu wengi sana kwa uzushi, vendeta na uwongo wao. Na tunaamini kuna watanzania wengi waliojaliwa ufahamu ambao wataanza kuhoji mambo mengi waliyoyasema huko nyuma ili wajue yapi ni kweli na yapi si kweli. Ndio tukasema mwiba hutokea ulipoingilia. 

So my position about this fracas has consistently been clear from day go, which is that: there is no doubt that CCM is a casualty for loosing such an enigmatic politician, and they lost him for hatred and political stupidity. But we shouldn't forget that CDM are also a casualty as much as they are a beneficiary. They have a surmountable task to explain this level of hypocrisy, dithering and flip-flopping that is clearly unprecedented at a global scale. In short, with what they have done, CDM leaders can no longer conceal their malice, spitefulness and malevolence! 

Kitila





2015-07-31 12:19 GMT+03:00 mayrosekm <mayrosekm@gmail.com>:
Ndugu Herment Mrema,
Naunga mkono maelezo yako juu ya ufisadi ndani ya Taifa kwani huo ndio ukweli wa hali halisi.
Daima nimekuwa natamani nisikie watu wanagusa penye dawa ya maisha ya mtanzania.
 Hatuwezi, hatuwezi katu hatuwezi kuwa na maisha ya uhakika ikiwa hatuna siasa safi. Hata matumaini ya kupata katiba inayowafaa watanzania, itawezekana tu tutakapokuwa na siasa safi. Maana siasa safi zinazingatia maisha safi yenye tija kwa watu wote. 
Pale ulipogusa siasa safi, yaani umeugusa moyo wangu. Siasa safi ndio chemchem ya maisha bora.
Suala hili la siasa safi ni muhimili mkuu wa dira ya Taifa ni vema tulitafutie wakati maalum wa kulijadili. Wakati ambapo watu wametulia hawana ushabiki wala joto la nani atakuwa nani serikali ijayo.
Kwa hali ilipofikia ni busara tuendelee kujadili na kutafakari namna ya kufanikisha kwa usalama na amani uchaguzi mkuu.
Binafsi kama mwanaharakati wa maendeleo ya watu nipo katika tafakari nzito ya kutafuta namna gani tutaweza kujenga tunu ya uadilifu katika taifa letu. Tutasikiana juu ya hilo mara tu nitakapokuwa nimemaliza tafakari yangu ya muda mrefu.
Tujaliwe amani na utulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
Nakushukuru sana na kukupongeza ndugu yangu Herment.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Mayrose Kavura Majinge,
Mwanaharakati wa Maendeleo ya Watu,






Sent from Samsung tablet

Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com> wrote:
Kwa mfumo tuliokuwa nao tangu tupate uhuru asili mia 80% ya watanzania ni mafisadi kila mmoja kwa nafasi yao.  Mkulima ataongeza maji na mawe na takataka ili kilo ziongezeke, mnunuzi atachakachua mizani ili kilo zipunguwe na afisa ugani atabariki uuzaji wa mbolea na madawa feki ali mradi kapata mshiko.  Muuza duka atapanga bei ya ulanguzi.  Mfanyakazi ambaye ana kipata cha Shs 500,000 kwa mwezi atajenga nyumba ya zaidi ya Shs150 million - 1 billion bila mkopo na wote tunaona.  Utakumbuka tulikotoka kulikuwa hakuna mikopo ya nyumba na wengi wetu tumejenga kwa njia za ajabu.

Kwa sasa hivi mshahara wa mfanyakazi hautoshi kuishi zaidi ya wiki mbili lakini unaona wanaishi kwa mwezi mzima na ukiuliza anaishi je anakujibu kwa kubangaiza.

Kinachotakiwa ni kujipanga na kuanza upya kurudi huko nyuma hakutamsaidia mtu yeyote.  Tuanze na katiba ambayo itatoa fursa kwa kila mtanzania kupata kipato halali kutokana na jasho lake.  Tuanze na mkulima mdogo kuzalisha, kusindika na kuuza mazao yaliyoongezewa thamani ili kumwezesha kushiriki kupanga bei badala ya kupangiwa bei.  Kwa mfano tuuwe soko la mpunga na kuuza mchele uliopangwa kwenye madaraja, wakulima wawezeshwe wauze unga wa mahindi badala ya kuuza mahindi, na wauze pamba iliyochambuliwa badala ya kuuza pamba mbegu.

Nchi hii bila umaskini ule uliokithiri inawezekana na ndio mwanzo wa siasa safi na demokrasia ya kweli.

Herment A. Mrema

> Date: Fri, 31 Jul 2015 02:38:17 +0300
> Subject: Re: [wanabidii] TULIOMWITA LOWASSA FISADI TUMUOMBE RADHI
> From: wanabidii@googlegroups.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> Report ili bias bana
> Lesian
>
> 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> >Ukikumbuka sana ripoti aliyoitoa Mwakyembe bungeni ni wazi kuwa tume iliacha kumshitaki Lowasa maana baada ya hapo boss wake ndiye angeambiwa apime mazingira achukue hatua. badala yake tume ilikomea kwa kumwambia Lowasa apime mwenenyewe. Hii ilikuwa wazi kuwa boss wa Lowasa ana kosa ila tume imemstahi labda kwa kuzingatia ushauri wa Nyerere kuwa waziri mkuu kujiuzulku si tatizo sana kama rais kujiuzulu.
> >Hata hivyo ripoti hiyo haikuacha mashaka kuwa Lowasa alikuwa na maslahi katika sakata la Richmond. kwa hiyo kumuomba msamaha Lowasa inabidi uwe huyakumbuki yote na ripoti hatunayo hadharani. Pia kama mtu ukianzia na kuishia kwenye YouTube ambayo nitaisikiliza baadaye unaweza kuishia kumuomba Lowasa msamaba. lakini ukianzia nyuma. ukaja mazindira ya sakata la Richmond ukapima mazingira ya uchunguzi wa TAKUKURU kuhusu richmond na ripoti yake kukataliwa ba watu ikiwa ni bunge pia. Ukakumbuka picha z\ bunge na ukamkumbuka Lowasa baada ya bunge kuamua kuunda tume. Ukikumbuka zawaqdi alizokuwa akitoa siku za karibuni. Michango makanisani na misikitini. Ukikumbuka jinsi alivyobanwa akasema ni marafikizake wanampa lakini hakusema wanatarajia nini kwake. ukimumbuka mateso ya mtandao tuliyoyapata Huwezi kumuomba msamaha maana hapo utakuwa unapalilia njia yake kuelekea Ikulu na kulitumbukiza taifa kuongozwa na mtandao uliotutesa mia\ka hiiyote 10. Utakuwa
> > unaelekea kukivunja chama kikuu cha upinzani kilichomkaribisha maana baada ya yeye kwenda Ili;u kitabaki jina. Hii itakuwa jinai kwa vizazi vijavyo na nadhni tusione aibu kuepuka hilo
> >--------------------------------------------
> >On Thu, 7/30/15, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
> >
> > Subject: [wanabidii] TULIOMWITA LOWASSA FISADI TUMUOMBE RADHI
> > To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
> > Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
> > Date: Thursday, July 30, 2015, 2:43 AM

> >
> >
> > Nimemsikiliza Edward  Lowassa  kwenye you tube
> > tuliyowekewa humu jukwaani akiulizwa maswali na wanahabari
> > kuhusu kashfa ya Richmond iliyotokea alipokuwa Waziri Mkuu
> > miaka minane iliyopita. Kulingana na  majibu aliyoyatoa
> > hata mimi kama mwanahabari niliwahi kumwita fisadi kwa
> > sababu ya  kashfa hiyo. Lakini kulingana na maelezo
> > aliyoyatoa ninakiri nilifanya dhambi maana kumsingizia mtu
> > uongo ni dhambi na binafsi baada ya kusikia upande wake mimi
> > kwa upande wangu namuomba radhi.
> >  
> > Kumbe kinara wa  kashfa ya Richmond alikuwa bosi wake.
> > Lo!  Sasa inaingia akilini ni kwa nini TOR za Mwakyembe
> > hakikumuweka Lowassa kama sample ya kuhojiwa kashfa ya
> > Richmond ilipotokea. Lakini kwa unyenyekevu Lowassa
> > alijiuzulu kuinusuru serikali nzima  isianguke. Mungu
> > mwema miaka minane  baadaye ukweli kamili wa Richmond
> > unajulikana. Kama ulichokisema ni kweli Lowassa, Mungu
> > atakupigania kwa sababu ni wewe  na Mzee Mwinyi peke
> > yenu mna rekodi ya kujiuzulu kuonyesha uwajibikaji kutokana
> > na nafasi zenu na siyo kosa mlilolitenda  ninyi
> > wenyewe. Viongozi wengine mpaka umma upige kelele sana ndipo
> > wajibaraguze kujiuzulu mfano kashfa ya escrow 2014. Sasa
> > ninaelewa ni kwa nini baadhi ya watu wana hofu baada ya
> > LOwassa  kukubaliwa na UKAWA kuwa mgombea Urais.
> >
> > Namshukuru sana aliyetuwekea hii you-tube huku jukwaani
> > maana baadhi yetu ambao hatuko site tungeweza kuendelea
> > kufanya uchambuzi wetu kwa kutumia habari nusu nusu
> > tulizopewa miaka iliyopita kuhusu kashfa ya Richmond.
> >
> > Ananilea Nkya
> >  E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
> >
> > --
> > Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
> >
> > Kujiondoa Tuma Email kwenda
> > wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
> > Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
> >
> > Disclaimer:
> > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> > for any legal consequences of his or her postings, and hence
> > statements and facts must be presented responsibly. Your
> > continued membership signifies that you agree to this
> > disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> > ---
> > You received this message because you are subscribed to the
> > Google Groups "Wanabidii" group.
> > To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> > from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> > For more options, visit
> > https://groups.google.com/d/optout.
> >
> >--
> >Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
> >
> >Kujiondoa Tuma Email kwenda
> >wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
> >
> >Disclaimer:
> >Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> >---
> >You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> >To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> >For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment