Mimi ninaomba, atakayekuwa Rais-awanyang'anye mashamba waliyojigawia yaliyokuwa ya mamlaka mbali mbali ya serikali, viwanda walivyojipa na kuwakata kodi yote kulingana na grace period katika mkataba ili pesa iingie serikalini. Wamejiuzia magari na nyumba za serikali badala ya kukaa na kutumia magari kupunguza gharama ya serikali majumba wamejenga matoteli wanalipwa kwa $ magari ni ya kitalii wao bado wanabebwa na magari ya sereikali na kwenda nayo kila kona. Mafao ya mbunge yapunguzwe na kila mbunge atathiminiwe kwa report ya evaluation ya majimbo kuonyesha maendeleo aliyofanikisha kutokana na strategic plan ya jimbo katika wilaya husika. Hii itawafanya wawajibike sio kununua kura na kutembea kwa magari ya thamani na kulala usingizi. Hata kijiji aishiko huko jimboni sio mfano kwa maendeleo yeye na madiwani wake. Diwani ndio kwanza ni mmiliki wa kilabu cha pombe na vigenge vya mama ntilie kawapangisha na wauza mitumba.
Tunataka kusonga mbele, mtu anayehamasisha wananchi wake na kuwashirikisha waone mbele wajitume kikamilifu na kulinda mazingira ya waishipo na wapatapo liveliihood zao ili tuwe na mazingira ya usafi na raslimali endelevu. Lele mama na lawama ziishe. Kuwajibika na kuacha uzembe ni budi sisi sote. Anayeiba hata ndugu na marafiki wasimtetee.
--------------------------------------------
On Wed, 2/9/15, 'Reuben Mwandumbya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [Mabadiliko] Re: [wanabidii] WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2O15
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, 2 September, 2015, 7:56
Mama
Anilea;Time will
tell and it is also a good don for almost all the
time.Tusubiri
tu,kwani kesi ya jinai haifi, hukaa hata miaka sitini (kwa
mujibu wa Mwakyembe) alipokuwa akiongea na wananchi wa Kyela
hapo majuzi.Mwisho wao
tutaujua tu,Magufuli katoa ahadi ya kuanzisha mahakama ya
mafisadi kama akiwa Presdo. Reuben
On Tuesday,
September 1, 2015 7:25 PM, 'ananilea nkya' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Ndugu Mokili Juma,
Reuben Mwandumbya, Omukunirwa Ireneus, na Wa Sembeye
Nanawashukuruniu sana kwa
kusoma hadi mwisho makala yangu niliyoposti jioni ya leo.
Ndugu Mokili Juma, nakushukuru zaidi
kwa kunishauri kwamba nipitie makala zangu kwa makini
kabla ya kuposti ili kuondoa makosa madogo madogo. Lakini
hilo la kumpa mtu mwingine anisomee bahati mbaya sina mtu
wa kumpa asome maana niko nje ya nchi—niko mwenyewe.
Kadhalika ninaamini kwamba kama ni makosa madogo madogo
yasiyo ya kimaudhui msomaji anaweza kusahihisha na kama ni
mtu anataka kuitumia kuchapisha gazetini au blog ni vema
kuyaondoa makosa hayo madogo madogo.
Nisema kuwa ninapoandika humu hoja zangu
ninachojaribu kufanya ni kutoa mchango wangu wa mawazo
ili sote tujadili hatma ya nchi yetu kwa kuzingatia ukweli
hata kama ukweli huo unaumiza.
Mokili kama
umesoma andiko langu vema nimeeleza sababu ya wananchi
kupiga kura ya hapana CCM. Kama huafikiani na sababu
nilizotoa nawe andika hoja yako tuzijadili hapa maana
tunachoshindanisha hapa ni hoja---hoja zilizojikita kwenye
ukweli bila woga.
Ndugu
Reuben Mwandumbya , Wa Sembeye na Omukunirwa Ireneus.
Kama mnakumbuka Profesa Lipumba awali alisema
amemkubali Lowassa baada ya kubaini ufisadi nchini
chanzo chake ni serikali CCM na kwamba hata baada ya
Lowassa kuachia Uwaziri Mkuu kumekuwa na ufisadi kibao na
alitolea mfano ufisadi wa Tegeta escrow. Lipumba
alipoachia uenyekiti wa CUF alisema tatizo lake nafsi
inamsuta kwa kumpa mtu aliyetoka CCM kugombea Urais
kupitia vyama vya upinzani. Lakini kumbuka hata Mwalimu
Nyerere alisema upinzani wa kweli utakaowaondolea wananchi
umaskini utapatikana pale CCM itakapopasuka. Je kuna ubaya
gani mtu aliyetoka CCM kugombea Urais vyama vya
upinzani?
Lakini mimi
wacha ya Lipumba au Dr Slaa kujiweka pembeni maana
hawa wawili nao walikuwa wanataka kugombea Urais kupitia
UKAWA.
Swali langu siku
zote limekuwa hili: Kama Edward Lowassa ndiye fisadi wa
Richmond na mtu hatari Tanzania kwa ufisadi na
serikali ya CCM haikuhusika na ufisadi huo wa Richmond
wala wa Tegeta escrow ni kwa nini serikali ya CCM
haikumpeleka mahakamani Lowassa kwa ufisadi wa Richmond
miaka minane imepita sasa?
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Tue, 9/1/15, Ireneus Kakuru Mushongi <ireneuskakurumushongi@gmail.com>
wrote:
Subject:
[Mabadiliko] Re: [wanabidii] WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE
UCHAGUZI 2O15
To: "wanabidii@googlegroups
com" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: "Wanazuoni@yahoogroups.com"
<Wanazuoni@yahoogroups.com>,
"mabadilikotanzania@googlegroups.com"
<mabadilikotanzania@googlegroups.com>,
"Paschally Mayega" <ngowe2006@yahoo.com>
Date: Tuesday, September 1, 2015, 4:21 PM
Mama
Nkya
Hebu weka vizuri hicho
kichwa hapo juu. Kwa kuwa una mahaba na UKAWA
sema ama
andika hivi WANAUKAWA TUFANYE NINI
ILI TUSHINDE
UCHAGUZI..Sio wananchi hapa
kila mtu ni mwananchi bila
kujali itikadi
ya chama chake. Unawaambia wananchi wote ama
wana UKAWA tu? Sijaelewa hapa nani mwananchi
na na nani sio
mwananchi and are the
wananchi against each other..are all
wananchi fighting the common enemy? Wagombea pia bila
kujali
vyama vyao na itikadi zao ni
wananchi tu!
Sema nani (Mwananchi
fulani)
kumshinda mwananchi wa chama
fulani... Usifumbe macho au
kufunika uso
huku ukidhani huonekani.
Kuwa wazi kama
ambavyo umekuwa wazi
baada ya mapinduzi (ya
wanaCCM) ndani ya CHADEMA... na
kubadilisha
kabisa dhana ya mabadiliko ambayo ndiyo kimsingi
iliijenga CDM na hatimaye kuendelea kuiua
dhana hii kadiri
muda unavyokwenda. Watu
wanaoijua spidi ya JPM hawatokaa
ndani ya
CCM sababu they will be next in a new reformed CCM
hasa baada ya shedding inayoendelea. So lazima
wacheze na
opportunities (Diversification).
UKAWA ikiwini then they
will safeguard
their interests sababu sasa dhana ya ufisadi
sio issue tena huko CDM, the moment
ukitumbukia, you are
automatically clean.
Hata hawa champions wa Radar, Escrow,
Kagoda, kesho wakifanya Shedding wakahamia UKAWA, they
are
auto-cleaned kadiri tunavyoona maana
mnajitahidi kuja na
kiLa aina ya strategy
za kuwanawisha.
.......na
lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa
limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani,
litakuwa limefunguliwa
mbinguni...... (Mt.16:19)
Kuwa
specific..
Omukunirwa
Ireneus
2015-09-01 17:51 GMT+03:00
'mokili juma' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Sawa dadangu Nkya.
Nimeisoma
makala yako ndefu kuhusu "Wananchi wafanye
nini washinde Uchaguzi 2015". Lakini
ajabu ukiingia
ndani unaongelea haja ya
Wananchi kuiondoa CCM kwa Kupiga
Kura mwaka
2025!!!!!Nakushauri tena,
Tulia
dadangu......... Acha jazba!!! Unapoandika makala
jaribu kumpa mtu mwingine mmoja ama hata
ikiwezekana, wawili
ili waisome na kufanya
masahihisho kabla ya
"kuipost"
kwa wasomaji. Badilika
Anna!
On
Tuesday,
September 1, 2015 5:26 PM,
'ananilea nkya' via
Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
WANANCHI WAFANYE NINI
WASHINDE UCHAGUZI
2015?
Na Ananilea Nkya
Mmoja
wa watu waliosoma
makala yangu Raymond
Mauki, makala niliyoandika kwamba
CCM
ilimtoa Edward Lowassa kafara kwa kumpakazia
ufisadi wa Richmond ili chama hicho
kidanganye
wananchi kwamba fisadi ni
Lowassa na CCM ni chama safi,
amenishukuru kwa mchango wangu kwa taifa kupitia ile
makala. Baada ya kuisoma ameniomba nijubu
maswali mawili.
Kwenye malaka hiyo
iiliandika kwa serikali ya CCM ndiyo fisadi wa fedha
za
umma na hivyo chanzo cha wananchi wengi
hapa nchini kuwa
maskini. Nilitoa mfano
wa serikali ya CCM kuwa fisadi
kusimamia wizi wa fedha za umma kwenye akaunti ya
Tegeta
Escrow shilingi bilioni 306 mwaka
jana 2014. Nilitoa pia
mfano wa ufisadi wa
Richmond kwamba ni serikali ya CCM
yenyewe ilihusika lakini walidanganya umma kwamba
muhusika
ni Edward Lowassa.
Uthibitisho ni kwamba kama
Lowassa ndiye
alikuwa fisadi wa Richmond
leo hii angekuwa yuko jela kama
Mramba na
Yona. Nilisema pia kwamba hivi sasa nchi
imejaa ufisadi unaofanywa na watawala wa
serikali ya CCM
kwa hiyo hata mgombea wa
CCM wa sasa John Pombe Magufuli
wanayejidai ni mtu msafi akichaguliwa yerikali yake
italazimika kufanya ufisadi penda
asipende. Na yeye
mwenyewe Magufuli
amekaririwa akisema kwamba ataika
mfano
marais waliomtangulia.
Kwa hiyo nikawashauri wananchi wapiga kura
wakiwepo wanaCCM kwamba kama wanataka nchi yetu
iondokane
na ufisadi wa fedha za umma na
jeuri ya watawala wa CCM
kujitajirisha huku
wananchi wengi wakiwa ni maskini wa
kutupa,
na tena watawala hadi kufikia kuwatukana wananchi
masikini kwamba ni malofa na wapumbavu ni
lazima
wananchi wafanye
mabadiliko—waiondoe CCM madarakani mwaka
huu 2025 kwa kutumia sanduku huru la kura hapo tarehe
25
Oktoba .
Maswali mawili
ambayo msomaji
wangu alitaka niyajibu ni haya
ifuatavyo:
Swali la kwanza: Nini mchango
wa
wanawake kwenye harakati hizi za
leo,unadhani wameamka
kiasi cha kutosha?
Mchango
wa
wanawake katika kuleta mabadiliko katika maisha yao
kupitia uchaguzi wa mwaka huu 2015 ni
mkubwa na muhimu
sana. Wanawake kwa wingi
wao wakijitokeza kusikiliza
kampeni za
uchaguzi kisha wakijitokeza kupiga kura na
wakaipigia kura UKAWA wataleta mabadiliko.
Hivyo kila
mwanamke aliyejiandikisha kupiga
kura, namshauri atunze
kitambulisho
chake cha kupiga kura(kichinjio).
Afanye hivyo kwa
kutokukubali kumuonyesha mtu yeyote kitambulisho chake.
Kitambulisho chako ni siri yako (ni silaha
yako) ya itunze
kama mboni ya jicho hakuna
mtu mwingine yeyote hata kama ni
kiongozi,
hata kama ni polisi au mgambo hapaswi kukiona
kitambulisho (kichinjio)n chako. Zaidi hata
kama huyo mtu
atakuwa amekuletea zawadi ya
kanga, kitende, fulana, sukari,
fedha au
chochote kile mwanamke USIDANGANYIKE.
Mimi sina chama chochote cha
siasa nimefungamana nacho lakini nasisitiza wanawake
waipigie kura UKAWA kwa sababu ilani
ya UKAWA ina
agenda kuu mbili muhimu
zinazogusa maisha ya wanawake moja
kwa
moja.
Kwanza UKAWA
wana agenda ya kutoa elimu bure hadi Chuo
Kikuu. Hili ni
muhimu kwa sababu elimu
ndiyo msingi wa maendeleo yote kwa
mtu
binafsi wakiwopo watoto wa kike, familia na taifa
zima.
Pili UKAWA wana
agenda ya kuandika
Katiba Mpya inayotokana na maoni ya
wananchi. Moja ya jambo muhimu katika Katiba ya
wananchi
ni kuweka uhusiano mpya kati ya
viongozi na wananchi.
Katiba Mpya itazuia
viongozi kujitajirisha kwa mali za
umma
huku mamilioni ya wananchi wakiwepo wanawake
wakitaabika kwa umaskini.
Fedha za nchi zinazotafunwa na
watawala
wachache zitatumika kwa mfano
kuboresha elimu, huduma
za afya,maji,
umeme, kujenga viwanda kuwapatia maelefu ya
watu ajira. Pili Katiba mpya itaweka
misingi imara ya
kuhakikisha uwakilishi
wa wanawake kwenye vyombo vya
maamuzi
unafikiwa asilimia 50/50.
Kashalika Katiba Mpya italeta usawa wa
kweli
wa kijinsia nchini na usawa huo
utaanza kuonekana dhahiri
uchaguzi wa
2020 kwa kutoa idadi sawa wanawake na
wanaume madiwani kwenye kata na idadi
sawa ya wabunge
wanawake na wanaume
majimboni. Kadhalika kwenye vijiji na
mitaa
mwanamke akiwa mwenyekiti mwanaume atakuwa Makamu
mwenyekiti.
Utaratibu
wa viti maaluma
utatumika kwa watu wenye ulemavu peke
yake. Kila aina ya ulemavu itakuwa mbunge mwanamke na
mwanaume. Hayo ndiyo mabadiliko kamili nay a
kweli kuhusu
usawa wa kijinsia unaotakiwa
Tanania ili nchi yetu na watu
wake
waondokane na umaskini.
Katika uchaguzi wa mwaka huu kuna vyama
vinajinasibu eti vimezingatia usawa wa
jinsia kwa kuweka
mwanamke mgombea mwenza
au mgombea wa Urais. Ni sawa
lakini hiyo
ni geresha ya danganya toto kwa sababu kwa
mfumo wa sasa ambapo usawa wa 50 kwa 50
haujawekewa
misingi kwenye Katiba
wanawake wanatumika tu kama
wanaume
kupitisha sheria na sera za maendeleo za
kunufaisha kikundi kidogo cha watawala wananchi wanaume
na
wanawake wakibaki mafukara wa kuputa.
Usawa wa jinsia wa
kweli na wa kudumu
hauwezi kufikiwa hapa
nchini bila Katiba Mpya ya wananchi
kuandikwa na kuweka misingi ya kutekeleza usawa wa
jinsia kwa vitendo—misingi inayowaondolea
wanawake vikwazo
vya kugombea na kushinda
sawa na wanaume majimboni na
kwenye kata na
siyo viti maalum vya upendeleo—miaka 50
baada ya nchi kupa uhuru.
Kwa hiyo
ushuri
wangu kwa wanawake na wale wote
wanaofanya kampeni UKAWA
ni kuwaeleza
wanawake na wananchi ukweli kwamba wakitaka
mabadiliko ya kweli katika maisha yao wachague
UKAWA ndio
waliobeba ajenga ya
ukombozi—agenda ya kuwaletea
Watanzania
mabadiliko ya kweli yatakayojengwa kwenye misingi
imara –Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya
wananchi.
Swali la Pili: Watanzania
tufanye nini kuzuia CCM kuiba kura uchaguzi wa
mwaka
huu 2015? Mimi napendekeza
yafuatayo:
Kwanza: Kila
mwananchi mwanamke mwanaume
wakiwepo wana
CCM mnaouchukia kuona watu wengi
wanateseka kwa umaskini na watawala wachache wana utajiri
wa
kupindukia, kinachotakiwa kama
mnanataka uchaguzi wa
mwaka huu uwe ni
mwamzo wa kubadilisha maisha ya kimaskini
wanayoishi mamilioni ya Watanzania, ni kutunza
kitambulisho chako (kichinjio) na siku ya
kupiga kura
tarehe 25 Oktoba mwaka huu
2015 kwenda kupiga kura kuchagua
UKAWA.
Ninaipigia debe UKAWA—umoja unaojumuisha vyama vya
CUF, NLD, NCCR Mageuzi na CHADEMA kwa
sababu wana agenda
ya ukombozi wa
wananchi.
UKAWA wana
ajenda ya kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya
wananchi. Katiba Mpya itaweka misingi mipya ya
kuongoza nchi
kuleta mabadiliko-kuondoa
umaskinini unaotengenezwa kwa
serikali ya
CCM kukwapua fedha za wananchi na jeuri ya
kupora madaraka ya wananchi—yaani CCM
kujifanya chama
dola.
Hata kama itakulazimu kusubiri
siku mbili
au hata wiki nzima hata mwezi mmoja kuweza kupiga
kura fanya hivyo usikate tamaa. Kakikisha
hukosi kupiga
kura maana hakuna
ukombozi wenye kuleta mabadiliko
katika
maisha ya wananchi wengi ambao hupatikana katika
demokrasia ya vyama vingi vya siasa bila
wananchi wenyewe
kushiriki kuleta
mabadiliko hayo kupitia sanduku huru la
kura.
Umaskini wa
wananchi ninaouzungumza ni pamoja na ukosefu
wa ajira ya
kuwapatia walio wengi wasio
watumishi wa umma fedha za
kujikimu.
Watumishi wengi wa umma mfano walimu,
madaktari, wauguzi, askari, wahudumu wa maofisa na
kulipwa
mshahara isiyokidhi mahitaji ya
msingi kama vile chakula,
mavazi na
malazi.
Kadhalika
kulima kukopwa mazao yao na kutolipwa
kwa
muda mrefu. Ukosefu wa barabara vijijini, ukosefu wa
maji, watu kufa kwa kukosa dawa ili hali
watawala wachache
wakiugua wao wana
haki ya kutumia fedha za umma kwenda
kutibiwa nchi za nje.
Elimu
duni inayosababishwa na shule ambazo
si bora hazina
chakula kwa wananfunzi,
usafiri, vitabu, maabara na miundo
mbinu
mingine muhimu. Shule hazina hazina walimu wenye
ubora na wanaofurahia kufanya kazi zao kwa
vile
wanaheshimiwa, kuthaminiwa na
kulipwa vizuri.
Vilevile umaskini na kuporw
amadaraka
wananchi kunakojidhihirisha kwa vyombo vya
dola hasa polisi kutumika kibabe
kunyanyasa wananchi
kama vile nchi yetu
bado iko kwenye ukoloni.
Pili: Kila kila Mtanzania
aliyejiandikisha kupiga kura anayeumwa na hali ya
umaskini
wa wananchi wengi anapaswa
kutunza kitambulisho chake cha
kupiga kura
(kichinjio) na asikubali kumuonyesha au kumpa
mtu yeyote hata awe mwenyekiti nyumba kumi,
mwenyekiti wa
kitongoji, kijiji, mtaa ,
polisi , mgambo au mtu yeyote
yule.
Hii ni muhimu maana wapo watu hivi
sasa wanapita nyumba kwa nyumba wakijidai
wanafanya
kampeni za nyumba kwa nyumba
kumbe ni mbinu za kuwanunua au
kuwadanganya
na kuwaogopesha wananchi wanaotaka mabadiliko
ambao Rais Mstaafu Benjami Mkapa amewaita
''MALOFA
NA WAPUMBAVU''.
Lengo la kuwadanyanga au
kuwatia woga wananchi
ni ili wasipige
kura ya kuwaletea mabadiliko kwa
kuikataa CCMambayo utawala wake umewafanya wananchi
wengi
kuwa malofa na wapumbavu huku
watawala wa serikali ya CCM
wakijilipa
fdha za wananchi na kupata utajiri wa
kukufuru.
Nawashauri
wapiga kura kama ni fedha, nguo,
chakula watakuwa
wanaletewa na CCM wakati
wanapita kwenye kampeni walizosema
watafanya nyumba kwa nyumba zipokeeni maana pengine
hizo
ni zile fedha za wananchi zilizoibiwa
mwaka jana 2014 kwenye
akaunti ya Tegeta
escrow Benki kuu ambazo nyingine
zilibebwa kwa tandarusi. Ni fedha za wananchi kuleni na
kama ni nguo vaeni ni mali yenu lakini
usimpe tena kura
yako maana atarudi tena
kwenda kukwapua nyingine na hakuna
kazi
yoyote kuwaondolea wananchi umaskini wataifanya
miaka 5 ijayo.
Aidha kila
anayepiga kampeni
UKAWA awaeleze wananchi ukweli huu.
Wananchi wakiujua ukweli kuhusu chimbuko la matatizo
yanayowakabili kuwa ni serikali ya CCM
kama taasisi
kujihusisha na ufisadi na
kuwapora wananchi madaraka,
wananchi
wataelewa na watapiga kura kikamilifu kuleta
mabadiliko—kuchagua UKAWA kuendesha
serikali tuone
miaka mitano nao watafanya
nini kuwaondolea wananchi
umaskini.
Wasipotimiza ahadi zao hasa —elimu bure hadi
chuo kikuu na Katiba Mpya uchaguzi wa 2020
watapigwa chini
kupitia sanduku huru la
kura . Bila kubadilishana vyama
kwa
kuzingatia sera za maendeleo umaskini unaowasumbua
Watanzania wengi hautaondoka nchini.
Tatu: UKAWA viweke mawakala
wenye uchungu na
maisha ya mamilioni ya
Watanzania. Mawakala ambao
hawahongeki,
hawadanganyiki. Mawakala wa UKAWA wanatakiwa
wawe ni watu wanaoweza kuvumilia njaa na
wanaoweza kukesha
hadi kazi ya kupiga,
kuhesabu kura na kutangaza mshindi
ikamilike. Maana kwenye uchaguzi wakala ukipepesa
ukipepesa macho kidogo tu wajanja
wanachakachua.
Nne:
UKAWA kuweka mawakala
makini ambao siyo
mamluki wa CCM-- watu jasiri (siyo
watu
waoga) na wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu na
wenye moyo wa kujitolea kwa faida ya walio
wengi
wanaoteseka na maisha duni. Kura
ni hesabu kwa mtu
asiyejua kusoma,
kuandika na kuhesabu ni rahisi sana
KUDANGANYIKA maana hataweza kusoma na kuelewa
kilichoandikwa.
Tano:
UKAWA kuweka mawakala
wenye uvumilivu—mtu ambaye anaweza
kuvumilia njaa ikibidi kukaa bila kula na kunywa
kwa
zaidi ya saa 24. Wako mawakala
chaguzi zilizopita kwa
kuendekeza ulaji na
unywaji wakiwa kazini kwenye vituo vya
kupiga kura, waliagiza vinywaji na vyakula na vinywaji.
Lakini wajanja waliweka kwenye vyakula na
vinywaji hivyo
dawa za usingizi. Baada ya
kula walijikula na walikuja
kuamka
uchaguzi ulikuwa umewisha na kura za mgombea
wao ambaye alikuwa anapendwa na watu
amekwishaibiwa kura
zake wakiwa usingizini.
Ninachosema hapa ni
kwamba uchaguzi ni wa
mwaka huu ni
mapambano ya mamilioni ya wananchi masikini
(wakiwepo wanaCCM wengi tu) na kikundi cha watawala wa
CCM
wanaoendelea kujitajirisha kwa kuwa
madarakani.
Hivyo
mamilioni ya wananchi
wanaoteseka na
umaskini wakiamua kuvishinda vishawishi na
ulaghai unaofanywa na watawala wa CCM uchaguzi wa mwaka
huu utaleta mabadiliko kwa mara ya kwanza
kuwezesha mfumo wa
vyama vingi kufanya kazi
Tanzania. Zaidi fursa ya mamilioni
ya
wananchi wanaoishi maisha ya kimaskini kushinda
uchaguzi wa mwaka huu 2015 ni kubwa kuliko
wakati
mwingine wowote katika historia ya
vyama vingi nchini
kwetu.
Sita: UKAWA
wahakikishe inawaelekeza mawakala wake mambo muhimu ya
kufanya wakiwa kwenye vituo vya kupiga kura.
Mambo hayo ni
pamoja na kuhakikisha
wanachukua kwa usahihi matokeo
kwenye vituo
na kisha wafuatilie kwenye halmashauri
kuhakikisha anayeshinda ndiye anatangazwa mshindi.
Umuhimu wa kufuatilia
hadi
matokeo yatangazwe ni kuhakikisha
waliopewa mamlaka
kutangaza matokeo ya
diwani, mbunge na Rais hawachakachui
matokeo. Umma ukiwa unafuatilia matokeo-wenye kutaka
kufanya mchezo mchafu watauogopa umma. Hakuna
kinachoshinda
nguvu ya umma. MUNGU IBARIKI
TANZANIA.
Ninaruhusu
Makala hii
ichapishwe na yeyote anayetaka.
Lengo ni kuelimishana ili
kuleta
mabadiliko . Ukiwa na swali: niandikie: ananilea_nkya@yahoo.com
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Sat, 8/22/15, 'raymond mauki'
via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Subject:
[wanabidii] Re: [Wanazuoni]
LOWASSA KAFARA CCM KUJARIBU
KUZUIA
MABADILIKO [1 Attachment]
To:
"Wanazuoni@yahoogroups.com"
<Wanazuoni@yahoogroups.com>,
"mabadilikotanzania@googlegroups.com"
<mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>,
"Paschally Mayega" <ngowe2006@yahoo.com>
Date: Saturday, August 22, 2015, 5:11 AM
Mama
Nkya
nimekuelewa sana
sana na sana, siku zote
nimekuwa
nikifuatilia harakati zako
ila
sikujua msimamo wako uko wapi. Nashukuru kwa
kuwaambia
watanzania kuwa kila mtu ana
uhuru wa kutoa
maoni yake
haijalishi yupo wapi, ana nafasi
gani kwa jamii au yupo
upande gani kisiasa.
Ulichokiandika ni very
simple and very
true
hata mtoto wa darasa la nne ataelewa ila cha ajabu kuna
wasomi watakuja kupinga na wanaendeta
kupinga
ulichokiandika
tena wakitumia data za uongo
kabisa. Ni
ukweli uliowazi kuwa
watanzania
wa leo sio wa mwaka 1995 wa Mrema na
nashukuru
yeye mwenyewe amekiri hilo juzi
kupitia kituo
kimoja cha
redio(clouds fm), watanzania wa
leo
wanahitaji mabadiliko
chanya na
wasipoyapata kwa amani basi watatumia njia
nyingine yoyote japo
hatupendi ifike huko.Mama
Nkya, naomba
ukipata muda unijibu haya
mawili,
Je, tufanye nini watanzania lei
hii ili kuzuia kabisa
mchezo wa ccm
kutuibia kura zetu kwenye
uchaguzi mkuu?
Ukizingatia wameshakiri kabisa watatumia njia yoyote
kushinda ikiwemo goli la mkono.Pili,
nini mchango wa wanawake kwenye harakati
hizi
za
leo,unadhani
wameamka kiasi cha
kutosha?
Asante
na
ubarikiwe sana,
RAYMOND
MAUKIKIGAMBONI,
DAR ES SALAAM.
From:"ananilea
nkya
ananilea_nkya@yahoo.com
[Wanazuoni]"
<Wanazuoni@yahoogroups.com>
Date:Fri, Aug 21, 2015 at 23:42
Subject:[Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM
KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]
[Attachment(s) from ananilea nkya
included below]
LOWASSA
KAFARA CCM KUJARIBU KUZUIA
MABADILIKO
Na
Ananilea Nkya
Nimeandika hoja hii
baada
ya kusoma na kusikia hoja
zinazotolewa
na baadhi ya
Watanzania kwamba eti CHADEMA ,
CUF,
NCCR-Mageuzi na NLD -vyama
vinavyounda
UKAWA kwa
kumsimamisha
Edward Lowassa kugombea Urais vimepoteza
usafi wa kuongoza
mapambano dhidi ya ufisadi.
Ukweli ni kwamba viongozi wa CHADEMA na UKAWA
kumsimamisha
Lowassa kuwa
mgombea urais
wamecheza kama Pele. Tena
wanastahili
pongeze kubwa
maana walitumia akili kali na
saikolojia ya hali ya juu kubaini kuwa CCM
ilikuwa
ilicheza
mchezo
mchafu kisiasa kuwatumia
wapinzania
kumpakazia
Lowassa ufisadi na
hatimaye CCM kupata nguvu ya kumtoa
Lowassa
kafara ili eti CCM
ionekane inajisafisha ufisadi.
Wanaodhani CHADEMA na UKAWA
wamekosea pengine hawajaelewa
kuwa
tangu
upepo wa mabadiliko wa kukataliwa
mfumo chama
kimoja kuwa madarakani kwa
muda mrefu
ulipoanza kuvuma
duniani kote mwishoni mwa
miaka ya 1980, baadhi ya wanaCCM
hawajakubali kwa dhati kabisa ukweli huo na
kuamini kwamba
CCM
inaweza kupunzishwa kuongoza nchi
angalao
kwa miaka
mitano.
Hasa
baada ya Mwalimu
Nyerere CCM kuondoka duniani, CCM
imebaki
na viongozi ambao hawako tayari
kutumia
ujasiri
kuongoza mabadiliko kwa
amani. Baadhi ya vongozi wanaojali
zaidi
maslahi ya wana CCM
wachache wanaotumia kauli kama
hirizi
kauli aliyowahi kuitoa Mwalimu Nyerere
kuwa
bila CCM
imara—Tanzania itayumba
kujidanganya wenyewe na kudanganya
wananchi.
Wanasahau kwamba Mwalimu
Nyerere kama
mwanafalsafa na
mwanasiasa
makini alikuwa anatoa maamuzi ya kijasiri
kwa
faida ya taifa na wananchi kulingana
na hali
halisi ya
wakati
husika kwa kusoma upepo wa
wananchi. Kwa
mfano
Nyerere aliwahi kusema
CCM si mama yake akimaanisha Tanzania
na
Watanzania ni muhimu
zaidi kuliko umuhimu wa CCM kuwa
madarakani.
Mfano
Mwalimu Nyerere
mwaka 1992 alionyesha mfano
kwamba
maslahi
ya nchi
na wananchi ndiyo muhimu kuliko maslahi ya
CCM alipokubali kwenda kinyume na uamuzi
wa
wanaCCM wengi
waliokuwa
wamekataaa—mabadiliko—kuanzishwa vyama vingi
nchini ili vyama vibadilishane uongozi wa
nchi
--kuharakisha
maendeleo ya wananchi.
Lakini baada ya Mwalimu kuondoka dunaini kila
mwanaCCM
anayechaguliwa
kuwa Rais, kwa
kuogopa kulaumiwa kwamba
eti
kama CCM
haitachaguliwa kupitia sanduku huru la kura atabeba
lawama za kufanya CCM iondoke madarakani,
serikali zote za
CCM baada
ya Mwalimu
Nyerere kuondoka duaniani
zimekuwa
zinajihusisha na
ufisadi.
Serikali ya CCM imekuwa
ikikwapua kwa wizi
wa wazi mabilioni
ya
fedha za umma na kufanya maovu mengine mengi kuhakikisha
CCM haiondoki madarakani. Hivyo chaguzi
zinafanyika kama
geresha
tu—kudanganya
wafadhili na mataifa kuwa
Tanzania
ni nchi
ya
demokrasia ya vyama vingi.
Mfano
uchaguzi wa mwaka 2005 serikali ya
CCM chini ya Rais
Mkapa ilikwapua fedha
za wananchi kutoka Benki
Kuu Akaunti
ya EPA shilling bilioni 133
ambazo ziliiwezesha CCM kumweka
madarakani
Rais Kikwete.
Mwaka jana 2014 serikali ya
CCM chini ya
Kikwete ilikwapua
shilingi
bilioni 306 kutoka akaunti ya Tegeta escrow
Benki
Kuu kwa ajili ya kuiwezesha CCM
kushinda
uchaguzi wa
serikali za mitaa na uchaguzi
mkuu
unaofanyika tarehe 25
Oktoba mwaka huu
2015.
CCM
wakishaingia madarakani jambo muhimu
kuliko
yote Rais na
serikali yake
analolifanyia ni kubuni ufisadi wa kuipatia
CCM fedha na mbinu nyingine
za kuiwezesha CCM ibaki
madarakani
uchaguzi unaofuta. Hakuna kazi
muhimu ya
kuwaondolea wananchi umaskini
inayofanyika kwa kiwango na
juhudi
kubwa.
Kwa sababu hiyo, kikundi kidogo cha
watawala, wengi wakiwa
ni
kutoka CCM na
familia zao wamejikuta
wakinufaika kwa kuwa
matajiri kufuru kwa
muda mfupi ili hali
wananchi wengi
wakibaki maskini na mafukara
wa kutupa.
Mfano wabunge (kikundi cha
watu wasiozidi
400) wengi wakiwa
ni
wanachama wa CCM kila mmoja analipwa si chini ya
milioni 10 kila mwezi kama mishahara,
wacha
marupurupu na
posho za vikao vya kamati,
posho za safari
na mamilioni
mafao kila
baada ya miaka mitano. Lengo wawe na
fedha
nyingi za kununua kura za wapiga
kura maskini
uchaguzi
unaofuata CCM ibaki madarakani.
Ndiyo sababu kila mwananchi wakiwepo watu
muhimu kama walimu
wa vyuo
vikukuu na
madaktari hivi sasa nao
wameamua kuwa
wanasiasa.
Zaidi baadhi ya
wanaotafuta
madaraka ya kisiasa
wanatumia
mbinu chafu
sana ikiwa ni pamoja na ushirikina wa kuuwa
watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism)
waweze
kupata nafasi
ya
kuingia katika kundi la
watawala—kupata
utajiri wa
kutisha katika
kipindi cha miaka mitano.
Mfamo Wabunge
waliomaliza
muda wao mwaka huu 2015 kila
mmoja
ameondoka na kiinua mgongo zaidi ya
shilingi milioni
200. Hii ni kufuru
katika nchi inayojinasibu kuwa ni
maskini
na inapita huko na
huko duniani kuomba misaada!
Hata
hivyo kwa kadri ufukara unavyoendelea
kuwatafuna
wananchi wengi, na kwa
kadri
uelewa wa wananchi
wanaoteseka kwa
umaskini unavyoongezeka kwamba CCM na
utawala wa serikali yake ndicho chanzo cha
umaskini wao,
CCM
imebaini kuwa haiwezi tena
kushinda
uchaguzi kupitia
sanduku huru la
kura kwa kutegemea kete moja tu—kununua
wananchi mafukara peke
yake.
Hivyo
katika miaka ya hivi karibuni CCM imeanza kuendesha
siasa za maji taka—kuchafuana wao kwa wao
na
hatimaye
wameamua
kutoana kafara-lengo kuu
likiwa ni kuzuia
wananchi
wasitumie
sandundu la kura kufanya mabadiliko—kuchagua
vyama vingine kuongoza nchi.
Hivyo Rais Kikwete, hata kama ndani ya
umungu
wa moyo wake
hakubaliani na CCM inavyotumia
ubabe
kukataa mabadiliko
kinyume na asili
ya binadamu, amekuwa akifanya mambo
kutimiza matakwa ya baadhi
ya wanaCCM —kujaribu kuzuia
mabadiliko—ili tu kuepuka lawama- amalize
muda wake bila
kuonekana ndiye
kasababisha
wananchi kuipunzisha CCM
uongozi
kwa
kipindi cha
miaka mitano.
Kwa
kufanya hivyo Rais Kikwete amejikuta akiporwa ujasiri
wake aliokuwa nao kama mwanasiasa
ambaye
Mwalimu Nyerere
alimuamini.
Kumbuka Mwalimu Nyerere
alinukuliwa na gazeti
la Nipashe na
Majira 26/5/95 akisema
baada ya Rais Mwinyi baadhi ya
vijana
ambao alikuwa anaona wana nia ya
dhati kabisa na
uwezo mkubwa wa
kuongoza Tanzania ni
Benjamin Mkapa,
Jakaya
Kikwete na Edward
Lowassa.
Lakini
kwa
Kikwete kukubali kuyumbishwa na wana
CCM wachache
wasiokubali mabadiliko
anaonekana kufumbia
macho utekelezaji
wa kile mwanafalsafa
Mwalimu nyerere alichokisema---kwamba
Watanzania wanataka mabadiliko.
Mfano Rais
Kikwete alipata
fursa ya kusimamia mabadiliko kwa
kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya
wananchi.
Lakini kikundi
kidogo cha
wahafidhina ndani ya CCM
kilimtisha
akajikuta
anaweka pembeni ujasiri wake aliokuwa
nao
wa kusimamia mabadiliko hayo muhimu kwa
maendeleo ya
taifa hili.
Kama
uamini jiulize ni
kwa nini Kikwete aliachia Bunge la
Katiba lililojaa asilimia 80 ya wanachama
likazika Rasimu
ya Katiba ya wananchi
pale
Dodoma mwaka jana 2014 -- Rasimu
ambayo
ingeleta Katiba
yakuweka misingi ya kuleta
madadiliko
Tanzania—mabadiliko ya
kuhakikisha
kikundi
kidogo cha watawala
hakijitajirishi kwa ufisadi na kujigawia
mali za umma huku
mamilioni ya wananchi wakibaki maskini
na
mafukara wa kutupa?
Baada ya
Kikwete kupoteza fursa ya kuleta
mabadiliko kwa
kuandika Katiba Mpya,
umma uliofukarishwa
umeendelea
kupata uelewa kuwa CCM na
serikali yake ndicho chanzo cha
umaskini
wao.
Hivyo ili kuendelea kubaki madarakani
serikali ya CCM
imekuwa
ikijihusisha na
ufisadi ili ipate fedha
za
kuwarubuni
walala hoi
wakati wa kampeni za uchaguzi.
Mfano
mwaka 1995 Rais
Benjamini Mkapa alijikuta serikali
yake
ikifanya ufisadi katika akaunti EPA
(bilioni 122)
zilizotumiwa na CCM
kumuweka Kikwete madarakani.
Ukitafakari utaona kwamba
katika ufisadi Tegeta escow,
serikali ya
CCM imekapua billion 306 mara tatu
ya
ufisadi wa
EPA mwaka 1995 ilipokwapua
bilioni 122 ili kipate fedha
nyingi zaidi
la kuwalaghai
wapiga kura mafukara ambao
wameendelea kupata uelewa kuwa CCM inaiba
fedha za umma
kununua wapiga kura wakati
wa kampeni za
uchaguzi.
Hivyo serikali ya CCM
inayoongozwa na
Kikwete ambayo
imeshuhudia
nguvu ya wananchi kudai mabadiliko ikiwa
kubwa
kuliko wakati mwingine wowote,
inajaribu kila
mbinu chafu na
safi ili CCM ibaki
madarakani baada ya uchaguzi mwaka
huu.
Ndiyo sababu serikali
ya CCM kupitia
msemaji wa chama
hicho Nape Nnauye imeanza
kuwaambia Watanzania kuwa CCM
lazima
ishinde uchaguzi wa mwaka huu hata kama ni
kwa
kutumia goli la mkono (wizi au lolote
lile
chafu).
Zaidi Rais Kikwete amefikishwa
mahali pabaya
kulazimika kubuni
mchezo mchafu
kujaribu kuwadanganya
Watanzania kuwa eti CCM na serikali yake ni safi,
haijihusishi na ufisadi unaofukarisha
wananchi
isipokuwa
wanachama wachache wa CCM ndio
mafisadi.
Ili kujaribu kutafuta
kujenga uhalali wa CCM kubaki
madarakani
baada ya uchaguzi wa mwaka huu
2015, Kikwete
amejikuta akilazimika
kumtoa kafara
Lowassa kwa
kumpakazia ufisadi wa
Richmond.
Wananchi wanauliza
kama
Lowassa alikuwa ndiye mhusika wa
Richmond ni kwa nini
Spika wa Bunge Anna Makinda
(mmoja
wa watawala wa CCM), hakuagiza
tume ya Bunge iliyoongozwa
na Mbunge wa CCM
Harrison Mwakyembe kumhoji
Waziri Mkuu
Edward
Lowassa?
Pili wananchi wanahoji
kama
CCM haijamtoa Lowassa kafara
kwa
kumbebesha ufisadi wa
chama hicho ili kupumbaza hasira
ya
wananchi dhidi ya ufisadi wa CCM kwenye
uchaguzi wa
Oktoba mwaka huu 2015 ni
kwa
nini Rais Kikwete alikubali
Waziri wake
Mkuu Edward
Lowassa ajiuzulu kwa ufisadi wa
Richmond 2008 wakati ufisadi wa kutisha
ulifanywa na
serikali ya CCM kwenye
akaunti
ya Tegeta escrow 2014
Kikwete aliwatetea
mawaziri waliogawiwa fedha hizo na Ikulu
ilikuwa ndiyo mtuhumiwa namba moja?
Mimi si
mwanasiasa wa chama
chochote cha siasa hapa nchini
ninachoangalia ni chanzo cha umaskini wa
wananchi wengi
Tanzania.
Ndiyo
sababu Watanzania wengi nikiwepo mimi mwenyewe kwa
sababu tulipewa habari nusu nusu
zilizotolewa kimkakati na
serikali ya CCM
kuhusu kashfa ya Richmond
kumpakazia
Lowassa
ufisadi, tulipubwazwa tukaisaidia CCM kumchafua
Lowassa kuwa ni fisadi wa Richmond.
Lakini baadhi ya wananchi walianza
kujua
kuna ukweli
uliofishwa kuhusu Richmond pale
TV moja
ilipokuwa imemwalika
Lowassa aotoe
yake ya moyoni live siku chache baada ya
kujiuzulu, lakini kipindi
hicho cha TV kikafutwa ghafla.
Hata hivyo ukweli huo umekuja kujulikana mwezi
Julai mwaka
huu Lowassa
alipotoa hadharani
baada ya kuachana na CCM
na
kujiunga na
CHADEMA.
Sasa wananchi
wamefahamu kuwa CCM chini ya serikali
ya
Rais Kikwete iliamua kumtoa Lowassa
kafara kwa
kumpakazia
ufisadi wa Richmond ili
kuiokoa CCM
isiadhibiwe vikali
na wananchi
kwenye sanduku huru la kura –kwa
ufisadi
alinawasababishia umaskini na
ufukara.
Ndiyo sababu hivi
sasa CCM na baadhi ya
wanahabar
wanapakazia CHADEMA na
UKAWA kuwa eti ni mafisadi
baada ya
kumpokea Lowassa
(kafara wa CCM) na kumpitisha
kuwa
mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Isitosha
hivi sasa kikundi cha watawala
wachache wa
serikali ya CCM wanahaha na
wanamzonga Kikwete
azuie
mabadiliko kwa mkono kwa kufanya
kila
uchafu kupumbaza
Watanzania kwa
kutumia kete ya eti Lowassa ni fisadi wa
Richmond hivyo hana sifa ya kugombea
Urais
wa Tanzania,
bali
Magufuli ndiye mtu
safi.
Wananchi wenye akili zao wanajiuliza hivi
mwenye kashfa za
kifisadi
kati ya Lowassa
na Magufuli ni nani? Ni
Lowassa
aliyepakaziwa
Richmond au ni Magufuli aliyeongoza
watawala
kujiuzia kwa bei chee nyuma
za
umma zilizogarimu wanannchi
mabilioni ya
fedha?
Wananchi pia wanajiuliza
kama Lowassa ni
fisadi wa Richmond
ni kwa nini serikali ya
CCM
haijamshitaki mahakamani miaka
minane
tangu ufisadi huo ulipotokea?
Hivyo
pengine baada ya
Lowassa kutafakari nafsi yake na
kuona
kuwa CCM imemtoa kafara asigombee
Urais
ili kuzuia
mabadiliko, ameamua
kufanya maamuzi magumu ya kuhama CCM
--kushiriki kuongoza
masikini na mafukara wanaotafuta
mabadiliko.
Lowassa ameamua
kutekeleza alichokitabiri
Mwalimu Nyerere
kwamba
CCM isipokubali kuongoza wananchi wapate
mabadiliko
wanayoyataka—wananchi
watayatafuta mabadiliko hayo nje
ya
CCM.
Ni dhahiri CCM ilipoteza fursa adimu ya
kuongoza wananchi
kwenye
kuleta mabadiliko
kwa kuandika Katiba
Mpya-- kuweka
misingi ya
kukomesha mfumo wa utawala unaowezesha
watawala
kuwa matajiri wa kupindukia
huku
mamilioni ya wananchi
wakiwa mafukara na
nchi
ikinuka aibu ya umaskini wa
kijitakia ikiwa rasilimali nyingi za
asili.
Wanaomchochea Rais
Kikwete asikubali
mabadiliko yachukue
mkondo wake, wameunda
timu
ya kampeni yanye wajumbe wengi
waliohusika kumpakazia Lowassa ufisadi wa
Richmond ili
eti
kwenye
kampeni waendelee kumpaka
ufisadi
Lowassa, CHADEMA
na UKAWA
wakidhani Watanzania hawana akili ya
kutafakari.
Lengo lao ni moja.
Wanajua kabisa kuwa kwa
kutumia sanduku
huru la CCM haiwezi
kuchaguliwa. Wanataka kutumia
kisingizio
kuwa CHADEMA na UKAWA
imechafuka eti kwa
kumsimamisha Lowassa
Urais ambaye CCM
imemtoa karafa –
kwa kumpakazia ufisadi
wa
Richmond.
Lakini
baada ya kupata salamu za wananchi kupitia
mafuriko
yao kwenye kumtambulisha Lowassa
kwamba wao
wanaelewa fisadi
kamili ni CCM, sasa CCM
imeshtuka imeanza kutumia polisi
kuwaadhibu
wananchi. Pengine baadaye
itatumia jeshi
kabisa.
Zaidi imeamua kujaribu
kampeni za
ardhini -nyumba kwa
nyumba, bila shaka
kutumia
mabilioni ya fedha serikali ya
CCM
ilizokwapua Tegeta escrow kununua shahada na
kura za
mafukara.
Kwenye
kampeni za nyumba kwa nyumba mtu
kwa mtu ndiko
ufisadi mbaya wa kisiasa
unakofanyika—kununua, kutisha na
kuumiza wananchi
mafukara.
Swali ni
je Watanzania wangapi wapiga kura
watakubali CCM
inapopita majumbani
mwao
kuuza shahada zao kwa sukari,
kanga au
fedha hata kama
CCM itaamua kumpa kila mpiga kura
shilingi milioni moja?
Ni
mpiga kura gani atakayekubali KUDANGANYIKA
kwa
kununuliwa na CCM kwa vijizawadi
vya fedha
nguo KUSALITI
mamilioni ya watanzania
wanaoendelea kuteseka kwa ufukara
kila
baada ya uchaguzi kwisha na CCM kubaki
madarakani?
Wananchi pia wanauliza
je mabilioni ya
escrow yatawanunua
wajumbe wa NEC ili
wavuruge daftari la wapiga kura, au
wachakachue kama uchaguzi wa 2010 au
wataharibu daftari
la
wapiga kura, mashine na vifaa vya
kupigia kura, au
kuchelewesha kwa
makusudi
kufungua vituo vya wapiga kura
ili
kuvuruga uchaguzi
CCM ishinde kwa goli la mkono?
Kadhalika wananchi wanauliza wanaomshinikiza
Kikwete
asikubali
mabadiliko wakiona hilo
haliwezekani je
watamuua
Lowassa waliomtoa
kafara au viongozi wa CHADEMA na UKAWA
waliompokea Lowassa na
kumwezesha kufikia azma yake ya
kujitolea
kuwatumikia watanzania ili
kuvuruga
uchaguziwa
mwaka huu?
Wananchi wanauliza maswali hayo baada ya
kubaini kwamba
huenda wasiomtakia
mema
Kikwete astaafu kwa amani
wamejaribu
kuwalaghai
baadhi ya viongozi wakuu wa UKAWA ili
kujaribu kuvuruga UKAWA – lakini UKAWA kwa
vile ni sauti
ya
mafukara-sauti ya umma
imeendelea kuwa
moto mkali wa
nyika dhidi
ya CCM.
Hivyo binafsi
namshauri Rais
Kikwete akubali kuwa baba
wa
pili wa Taifa
hili
baada ya Nyerere kuondoka. Akubali
kusimamia wananchi watumie sanduku huru la
kura kwenye
uchaguzi wa mwaka huu 2015
kupata mabadiliko
ya uongozi
wanayoyataka.
Wananchi wana imani na
UKAWA kwamba wakiingia
madarakani
Katiba mpya inayotokana na maoni
ya wananchi itaandikwa.
Huo utakuwa ni mwanzo wa
mabadiliko wanayoyataka
wananchi—kuhakikisha watawala hawajitajirishi
kupindukia
kufisadi fedha
za wananchi huku
wananchi wengi wakibaki
mafukara.
CHADEMA na
UKAWA wasipotimiza hili na kuonyesha
kwa vitendo maendeleo watakayokuwa
wameyaleta kwa miaka
mitano, ni lazima
wananchi watatumia sanduku la kura
kuwapunzisha.
Ninaamini ni wenye kutetea
maslahi binafsi tu ndiye
atakayemlaumu
Rais
Kikwete kwamba eti CCM
isipochaguliwa
Oktoba 25,
Kikwete atakuwa ni chanzo cha wananchi
kuamua
kuipunzisha CCM kwa miaka
mitano.
Nitakuwa wa kwanza kuwapinga watu hao na
kumtetea Kikwete
hata kama ni kwa
kuamua
kuingia kwenye siasa kwa
kujiunga
na CCM
.
Hakika Rais Kikwete
ukisimamia
wananchi wazungumze
kuhusu
hatma ya
uongozi
wan chi yao kwa kutumia sanduku huru la
kura bila CCM kuingiza mkono mchafu, wewe
mwenyewe
ukistaafu utaishi
kwa amani na
furaha huku baadhi yetu
tukikuona kama baba
wa Pili
Taifa taifa hili, baada ya
Mwalimu
Nyerere.
Mwisho ninaruhusu
yeyote
anayetaka kuchapisha au kutangaza
redioni
natelevisheni
niyoyoyaandika hapa TV au kuchapisha
na
kuwasambazia Watanzania wote popote walipo
ujumbe huu
afanye hivyo. Wanawaza
kuwasambazia watu mitaani,
kwenyemikutano
ya kampeni, mashuleni vyuoni
popote
pale—lengo
likiwa moja—sote Watanzania tuujue ukweli
kuhusu ufisadi na mchango wake katika
kuwafanya Watanzania
waishi
katika
umaskini. Lakini muhimu kila
Mtanzania ajue
hakuna mshindi wa
kujisifu—mshindi ni nchi
yetu
Tanzania
na Watanzania wote.
MUNGU IBARIKI YANZANIA.
Ananilea
Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
__._,_.___
Attachment(s)
from ananilea nkya
| View
attachments on the
web
1 of 1 File(s)
LOWASSA KAFARA WA
CCM.docx
Posted by: ananilea
nkya
<ananilea_nkya@yahoo.com>
Reply
via web post
•
Reply to
sender
•
Reply to group
•
Start a
New
Topic
•
Messages in
this
topic
(1)
Visit Your Group
New
Members
2
• Privacy • Unsubscribe • Terms of
Use
.
__,_._,___
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the
sole
responsibility
for
any legal consequences
of his or her
postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you
agree
to this
disclaimer
and pledge to abide by
our Rules and
Guidelines.
---
You received this
message because you are subscribed to
the
Google Groups
"Wanabidii"
group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email
kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the
sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your
continued
membership signifies that you
agree to this disclaimer and
pledge to
abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop
receiving emails from it, send an
email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree
to this
disclaimer and pledge to abide by
our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii"
group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Unapokea Email hizi kwa
sababu umejiunga na Jukwaa la
'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii:
mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more
options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are
subscribed to the
Google Groups
"Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop
receiving emails
from it, send an email to
mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send
email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on
the web visit
https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAN5khk7sowgC0R%2Bmyb8awOO85DX3-Bnp66JJ6CP6zLGnLnhXTg%40mail.gmail.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment