Tuesday, 1 September 2015

Re: [Mabadiliko] Re: [wanabidii] WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2O15

Mama Anilea;
Time will tell and it is also a good don for almost all the time.
Tusubiri tu,kwani kesi ya jinai haifi, hukaa hata miaka sitini (kwa mujibu wa Mwakyembe) alipokuwa akiongea na wananchi wa Kyela hapo majuzi.
Mwisho wao tutaujua tu,Magufuli katoa ahadi ya kuanzisha mahakama ya mafisadi kama akiwa Presdo.
 
Reuben



On Tuesday, September 1, 2015 7:25 PM, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Ndugu  Mokili  Juma, Reuben Mwandumbya,  Omukunirwa Ireneus,  na Wa Sembeye

Nanawashukuruniu sana kwa kusoma  hadi mwisho makala yangu niliyoposti jioni ya leo.
Ndugu Mokili Juma,  nakushukuru zaidi kwa  kunishauri kwamba nipitie makala zangu  kwa makini  kabla ya kuposti ili kuondoa makosa madogo madogo. Lakini hilo la kumpa mtu mwingine anisomee  bahati mbaya sina mtu wa kumpa asome maana niko nje ya nchi—niko mwenyewe. Kadhalika ninaamini kwamba kama ni makosa madogo madogo yasiyo ya kimaudhui msomaji anaweza kusahihisha na kama ni mtu anataka kuitumia kuchapisha gazetini au blog  ni vema  kuyaondoa makosa  hayo madogo madogo.

Nisema kuwa ninapoandika humu hoja zangu  ninachojaribu kufanya  ni kutoa mchango wangu wa mawazo  ili sote tujadili hatma ya nchi yetu kwa kuzingatia ukweli hata kama ukweli huo unaumiza.
Mokili kama umesoma andiko langu vema  nimeeleza sababu ya wananchi  kupiga kura ya hapana CCM. Kama huafikiani na sababu nilizotoa nawe andika  hoja  yako tuzijadili hapa maana tunachoshindanisha hapa ni hoja---hoja zilizojikita kwenye ukweli  bila woga.

Ndugu Reuben Mwandumbya , Wa Sembeye na Omukunirwa Ireneus.
Kama mnakumbuka Profesa Lipumba  awali alisema amemkubali Lowassa  baada ya kubaini ufisadi  nchini chanzo chake ni  serikali CCM na kwamba  hata baada ya Lowassa kuachia Uwaziri Mkuu kumekuwa na ufisadi kibao na alitolea mfano ufisadi wa Tegeta escrow.  Lipumba alipoachia uenyekiti wa CUF alisema tatizo lake  nafsi inamsuta kwa  kumpa mtu aliyetoka CCM kugombea Urais  kupitia vyama vya upinzani.  Lakini kumbuka hata Mwalimu Nyerere alisema upinzani wa kweli utakaowaondolea  wananchi umaskini utapatikana pale CCM itakapopasuka. Je kuna ubaya gani mtu aliyetoka CCM kugombea Urais  vyama vya upinzani?
 
Lakini  mimi wacha ya Lipumba au  Dr Slaa  kujiweka pembeni  maana hawa wawili nao  walikuwa  wanataka kugombea Urais kupitia UKAWA.

Swali langu siku zote limekuwa hili: Kama Edward  Lowassa ndiye fisadi wa Richmond  na mtu hatari Tanzania kwa ufisadi na  serikali  ya CCM  haikuhusika na ufisadi huo wa Richmond  wala wa Tegeta escrow ni kwa nini serikali ya CCM haikumpeleka mahakamani Lowassa  kwa ufisadi wa Richmond miaka minane imepita sasa? 

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Tue, 9/1/15, Ireneus Kakuru Mushongi <ireneuskakurumushongi@gmail.com> wrote:

Subject: [Mabadiliko] Re: [wanabidii] WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2O15
To: "wanabidii@googlegroups com" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>, "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "Paschally Mayega" <ngowe2006@yahoo.com>
Date: Tuesday, September 1, 2015, 4:21 PM

Mama
Nkya
Hebu weka vizuri hicho
kichwa hapo juu. Kwa kuwa una mahaba na UKAWA sema ama
andika hivi WANAUKAWA TUFANYE NINI ILI TUSHINDE
UCHAGUZI..Sio wananchi hapa kila mtu ni mwananchi bila
kujali itikadi ya chama chake. Unawaambia wananchi wote ama
wana UKAWA tu? Sijaelewa hapa nani mwananchi na na nani sio
mwananchi and are the wananchi against each other..are all
wananchi fighting the common enemy? Wagombea pia bila kujali
vyama vyao na itikadi zao ni wananchi tu! 
Sema nani (Mwananchi fulani)
kumshinda mwananchi wa chama fulani... Usifumbe macho au
kufunika uso huku ukidhani huonekani.
Kuwa wazi kama ambavyo umekuwa wazi
baada ya mapinduzi (ya wanaCCM) ndani ya CHADEMA... na
kubadilisha kabisa dhana ya mabadiliko ambayo ndiyo kimsingi
iliijenga CDM na hatimaye kuendelea kuiua dhana hii kadiri
muda unavyokwenda. Watu wanaoijua spidi ya JPM hawatokaa
ndani ya CCM sababu they will be next in a new reformed CCM
hasa baada ya shedding inayoendelea. So lazima wacheze na
opportunities (Diversification). UKAWA ikiwini then they
will safeguard their interests sababu sasa dhana ya ufisadi
sio issue tena huko CDM, the moment ukitumbukia, you are
automatically clean. Hata hawa champions wa Radar, Escrow,
Kagoda, kesho wakifanya Shedding wakahamia UKAWA, they are
auto-cleaned kadiri tunavyoona maana mnajitahidi kuja na
kiLa aina ya strategy za kuwanawisha.
.......na
lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa
limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani,
litakuwa limefunguliwa
mbinguni...... (Mt.16:19) 
Kuwa
specific..



Omukunirwa
Ireneus 



 

2015-09-01 17:51 GMT+03:00
'mokili juma' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Sawa dadangu Nkya.
Nimeisoma makala yako ndefu kuhusu "Wananchi wafanye
nini washinde Uchaguzi 2015". Lakini ajabu ukiingia
ndani unaongelea haja ya Wananchi kuiondoa CCM kwa Kupiga
Kura mwaka 2025!!!!!Nakushauri tena,
Tulia dadangu......... Acha jazba!!!  Unapoandika makala
jaribu kumpa mtu mwingine mmoja ama hata ikiwezekana, wawili
ili waisome na kufanya masahihisho kabla ya
"kuipost" kwa wasomaji. Badilika
Anna! 


      On Tuesday,
September 1, 2015 5:26 PM, 'ananilea nkya' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
   

  WANANCHI WAFANYE NINI  WASHINDE UCHAGUZI
2015?
Na Ananilea  Nkya

Mmoja wa  watu waliosoma 
makala yangu Raymond Mauki, makala  niliyoandika  kwamba
CCM ilimtoa  Edward Lowassa kafara  kwa kumpakazia
ufisadi  wa Richmond  ili chama hicho  kidanganye
wananchi kwamba fisadi ni Lowassa  na CCM ni chama safi,
amenishukuru kwa mchango wangu kwa taifa  kupitia ile
makala. Baada ya kuisoma ameniomba nijubu  maswali mawili.


Kwenye malaka hiyo
iiliandika  kwa serikali ya CCM ndiyo fisadi wa  fedha za
umma na hivyo chanzo cha wananchi wengi hapa nchini kuwa
maskini.  Nilitoa mfano wa serikali ya CCM kuwa fisadi 
kusimamia  wizi wa fedha za umma kwenye  akaunti ya Tegeta
Escrow shilingi bilioni 306 mwaka jana 2014. Nilitoa pia
mfano wa ufisadi wa Richmond kwamba ni serikali ya CCM
yenyewe  ilihusika lakini walidanganya umma kwamba muhusika
ni Edward Lowassa.
 
Uthibitisho ni kwamba kama Lowassa ndiye
alikuwa  fisadi wa Richmond leo hii angekuwa yuko jela kama
Mramba na Yona.  Nilisema pia kwamba hivi sasa   nchi
imejaa ufisadi unaofanywa na  watawala wa serikali ya CCM
kwa hiyo hata mgombea wa CCM wa sasa John Pombe Magufuli 
wanayejidai  ni mtu msafi akichaguliwa  yerikali yake
italazimika kufanya ufisadi penda asipende.   Na yeye
mwenyewe  Magufuli amekaririwa akisema  kwamba ataika
mfano marais waliomtangulia.
 
Kwa hiyo nikawashauri wananchi wapiga kura
wakiwepo wanaCCM  kwamba kama wanataka nchi yetu iondokane
na ufisadi wa fedha za umma na jeuri ya watawala wa CCM
kujitajirisha huku wananchi wengi wakiwa ni maskini wa
kutupa, na tena  watawala hadi kufikia kuwatukana wananchi
masikini kwamba ni  malofa na wapumbavu ni lazima 
wananchi wafanye mabadiliko—waiondoe CCM madarakani mwaka
huu 2025  kwa kutumia sanduku huru la kura  hapo tarehe 25
Oktoba .

Maswali mawili
ambayo msomaji wangu alitaka niyajibu   ni haya 
ifuatavyo:
Swali la kwanza: Nini mchango wa
wanawake kwenye harakati hizi za  leo,unadhani wameamka
kiasi cha kutosha?

Mchango
wa wanawake katika kuleta mabadiliko katika maisha yao
kupitia   uchaguzi wa mwaka huu 2015  ni mkubwa na muhimu
sana. Wanawake kwa wingi wao  wakijitokeza kusikiliza
kampeni za uchaguzi kisha wakijitokeza kupiga  kura na
wakaipigia kura UKAWA  wataleta mabadiliko.  Hivyo kila
mwanamke aliyejiandikisha kupiga kura, namshauri atunze
kitambulisho chake   cha kupiga kura(kichinjio). 

  Afanye hivyo kwa 
kutokukubali kumuonyesha mtu yeyote kitambulisho chake.
Kitambulisho chako ni siri yako  (ni silaha yako) ya itunze
kama mboni ya jicho hakuna mtu mwingine yeyote hata kama ni
kiongozi, hata kama ni polisi au mgambo  hapaswi kukiona
kitambulisho (kichinjio)n chako.  Zaidi hata kama huyo mtu
atakuwa amekuletea zawadi ya kanga, kitende, fulana, sukari,
fedha au chochote kile mwanamke USIDANGANYIKE.

Mimi sina chama chochote cha
siasa nimefungamana nacho lakini nasisitiza wanawake
waipigie kura  UKAWA  kwa  sababu  ilani ya UKAWA ina
agenda kuu mbili muhimu zinazogusa maisha ya wanawake moja
kwa moja.

Kwanza UKAWA
wana  agenda ya kutoa elimu bure hadi Chuo Kikuu. Hili ni
muhimu kwa  sababu elimu ndiyo msingi wa maendeleo yote kwa
mtu binafsi wakiwopo watoto wa kike, familia na taifa
zima. 

Pili  UKAWA wana
agenda ya  kuandika Katiba  Mpya inayotokana na  maoni ya
wananchi.  Moja ya jambo muhimu katika Katiba  ya wananchi
ni  kuweka uhusiano mpya kati ya viongozi na wananchi.
Katiba Mpya itazuia viongozi kujitajirisha  kwa mali za
umma huku mamilioni ya wananchi wakiwepo wanawake
wakitaabika kwa umaskini.
 
Fedha za  nchi  zinazotafunwa na watawala
wachache zitatumika  kwa mfano  kuboresha  elimu, huduma
za afya,maji, umeme,  kujenga viwanda kuwapatia maelefu ya
watu  ajira.   Pili Katiba mpya itaweka misingi imara ya
kuhakikisha  uwakilishi wa wanawake  kwenye vyombo vya
maamuzi unafikiwa asilimia 50/50.

  Kashalika Katiba  Mpya italeta usawa wa kweli
wa kijinsia nchini na usawa huo utaanza kuonekana dhahiri 
uchaguzi wa 2020  kwa kutoa   idadi sawa  wanawake na
wanaume  madiwani kwenye kata  na  idadi sawa ya wabunge
wanawake na wanaume majimboni. Kadhalika kwenye vijiji na
mitaa mwanamke akiwa mwenyekiti mwanaume atakuwa Makamu
mwenyekiti.
 
Utaratibu
wa viti maaluma utatumika  kwa watu   wenye ulemavu peke
yake. Kila aina ya ulemavu itakuwa  mbunge mwanamke na
mwanaume.  Hayo ndiyo mabadiliko kamili nay a kweli kuhusu
usawa wa kijinsia  unaotakiwa Tanania ili nchi yetu na watu
wake waondokane na umaskini.
 
Katika uchaguzi wa mwaka huu kuna vyama 
vinajinasibu eti  vimezingatia usawa wa jinsia kwa kuweka
mwanamke mgombea mwenza au mgombea wa Urais.  Ni sawa
lakini hiyo ni geresha ya danganya toto  kwa sababu kwa
mfumo wa sasa ambapo  usawa  wa 50 kwa 50 haujawekewa
misingi kwenye Katiba  wanawake  wanatumika tu  kama
wanaume  kupitisha sheria na sera za maendeleo za
kunufaisha kikundi kidogo cha watawala wananchi wanaume na
wanawake wakibaki mafukara wa kuputa.

Usawa wa jinsia  wa  kweli na wa kudumu 
hauwezi kufikiwa hapa nchini  bila Katiba Mpya ya wananchi
kuandikwa  na kuweka misingi ya kutekeleza  usawa wa
jinsia kwa vitendo—misingi inayowaondolea wanawake vikwazo
vya kugombea na  kushinda sawa na wanaume majimboni na
kwenye kata na siyo viti maalum vya upendeleo—miaka 50
baada ya nchi kupa uhuru. 
Kwa hiyo ushuri
wangu kwa wanawake  na wale wote wanaofanya kampeni  UKAWA
ni kuwaeleza wanawake na wananchi ukweli kwamba  wakitaka
mabadiliko ya kweli katika maisha yao wachague UKAWA  ndio
waliobeba ajenga ya ukombozi—agenda ya kuwaletea
Watanzania mabadiliko ya kweli yatakayojengwa kwenye misingi
imara –Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi. 


Swali la Pili: Watanzania
tufanye nini  kuzuia CCM  kuiba kura  uchaguzi wa  mwaka
huu 2015?  Mimi napendekeza yafuatayo:

Kwanza: Kila mwananchi mwanamke mwanaume
wakiwepo wana CCM mnaouchukia   kuona watu wengi 
wanateseka kwa umaskini na watawala wachache wana utajiri wa
kupindukia,  kinachotakiwa  kama mnanataka uchaguzi wa
mwaka huu uwe ni mwamzo wa kubadilisha maisha  ya kimaskini
wanayoishi mamilioni ya Watanzania, ni kutunza
kitambulisho  chako (kichinjio)  na siku ya kupiga kura 
tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015 kwenda kupiga kura kuchagua
UKAWA. Ninaipigia debe UKAWA—umoja unaojumuisha vyama vya
CUF, NLD, NCCR Mageuzi na CHADEMA  kwa sababu  wana agenda
ya ukombozi wa wananchi.
UKAWA   wana
ajenda ya kuandika  Katiba Mpya inayotokana na maoni ya
wananchi. Katiba Mpya itaweka misingi mipya ya kuongoza nchi
kuleta mabadiliko-kuondoa umaskinini unaotengenezwa kwa 
serikali ya CCM kukwapua fedha za wananchi  na jeuri ya
kupora madaraka ya wananchi—yaani CCM kujifanya chama
dola.  
Hata kama itakulazimu kusubiri
siku mbili au hata wiki nzima hata mwezi mmoja kuweza kupiga
kura fanya hivyo usikate tamaa. Kakikisha hukosi kupiga
kura  maana hakuna ukombozi  wenye kuleta mabadiliko 
katika maisha ya wananchi wengi ambao hupatikana  katika
demokrasia ya vyama vingi vya siasa bila wananchi wenyewe 
kushiriki  kuleta mabadiliko hayo kupitia sanduku huru la
kura.

Umaskini  wa
wananchi ninaouzungumza ni pamoja na ukosefu wa ajira ya
kuwapatia walio wengi  wasio watumishi wa umma fedha za
kujikimu.   Watumishi wengi wa umma  mfano  walimu,
madaktari, wauguzi, askari, wahudumu wa maofisa na kulipwa 
mshahara isiyokidhi mahitaji  ya msingi kama vile chakula,
mavazi na malazi.
 
Kadhalika kulima kukopwa mazao yao na kutolipwa
kwa muda mrefu.  Ukosefu wa barabara vijijini, ukosefu wa
maji, watu kufa kwa kukosa dawa ili hali watawala wachache 
wakiugua  wao wana haki ya kutumia fedha za umma kwenda
kutibiwa nchi za nje.

Elimu
duni inayosababishwa na shule ambazo si bora hazina 
chakula kwa wananfunzi, usafiri, vitabu, maabara na miundo
mbinu  mingine muhimu. Shule hazina hazina walimu  wenye
ubora na  wanaofurahia kufanya kazi zao kwa vile
wanaheshimiwa, kuthaminiwa  na kulipwa vizuri.
 
Vilevile umaskini na kuporw
amadaraka wananchi kunakojidhihirisha kwa vyombo vya 
dola  hasa polisi  kutumika  kibabe kunyanyasa wananchi
kama vile nchi yetu bado iko kwenye ukoloni.

Pili: Kila  kila Mtanzania
aliyejiandikisha kupiga kura anayeumwa na hali ya umaskini
wa wananchi wengi   anapaswa kutunza kitambulisho chake cha
kupiga kura (kichinjio) na asikubali kumuonyesha au kumpa
mtu yeyote hata awe mwenyekiti nyumba kumi, mwenyekiti wa
kitongoji, kijiji, mtaa , polisi  , mgambo au  mtu yeyote
yule.
Hii ni muhimu maana wapo watu hivi
sasa  wanapita nyumba kwa nyumba wakijidai wanafanya
kampeni za nyumba kwa nyumba kumbe ni mbinu za kuwanunua au
kuwadanganya na kuwaogopesha wananchi wanaotaka mabadiliko 
ambao Rais Mstaafu Benjami Mkapa amewaita ''MALOFA
NA WAPUMBAVU''.
 
Lengo la kuwadanyanga au kuwatia woga wananchi
ni ili  wasipige  kura  ya kuwaletea mabadiliko  kwa
kuikataa CCMambayo utawala wake  umewafanya wananchi wengi
kuwa malofa na wapumbavu huku watawala wa serikali  ya CCM
wakijilipa fdha za wananchi  na kupata utajiri  wa
kukufuru.
 
Nawashauri
wapiga kura kama ni fedha, nguo, chakula  watakuwa
wanaletewa na CCM wakati wanapita kwenye kampeni walizosema
watafanya nyumba kwa nyumba zipokeeni  maana pengine  hizo
ni zile fedha za wananchi zilizoibiwa mwaka jana 2014 kwenye
akaunti ya Tegeta escrow  Benki kuu ambazo nyingine
zilibebwa kwa  tandarusi. Ni fedha za wananchi kuleni na
kama ni nguo vaeni  ni mali yenu lakini usimpe tena kura
yako maana atarudi tena kwenda kukwapua nyingine na hakuna
kazi yoyote kuwaondolea wananchi umaskini   wataifanya
miaka 5 ijayo.

Aidha kila
anayepiga kampeni UKAWA  awaeleze wananchi ukweli huu.
Wananchi wakiujua ukweli  kuhusu chimbuko la matatizo
yanayowakabili  kuwa ni  serikali ya CCM kama taasisi
kujihusisha na ufisadi na kuwapora wananchi madaraka, 
wananchi wataelewa na watapiga kura  kikamilifu kuleta
mabadiliko—kuchagua  UKAWA  kuendesha serikali tuone
miaka mitano nao watafanya nini kuwaondolea wananchi
umaskini. Wasipotimiza ahadi zao hasa —elimu bure hadi
chuo kikuu na Katiba Mpya  uchaguzi wa 2020 watapigwa chini
kupitia sanduku huru la kura . Bila kubadilishana vyama 
kwa kuzingatia sera za maendeleo  umaskini unaowasumbua
Watanzania wengi hautaondoka nchini.

Tatu: UKAWA viweke mawakala wenye uchungu na 
maisha  ya mamilioni ya Watanzania. Mawakala ambao
hawahongeki, hawadanganyiki. Mawakala wa UKAWA wanatakiwa
wawe ni watu  wanaoweza kuvumilia njaa na wanaoweza kukesha
hadi kazi ya kupiga, kuhesabu kura na kutangaza mshindi 
ikamilike. Maana kwenye uchaguzi  wakala  ukipepesa
ukipepesa macho kidogo tu wajanja wanachakachua.

Nne:  UKAWA kuweka mawakala
makini  ambao siyo mamluki wa CCM-- watu  jasiri (siyo
watu waoga) na wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu na
wenye moyo wa kujitolea kwa faida ya walio wengi
wanaoteseka  na maisha duni.  Kura ni hesabu kwa mtu
asiyejua kusoma,  kuandika  na kuhesabu ni rahisi sana
KUDANGANYIKA  maana hataweza kusoma na kuelewa
kilichoandikwa.

Tano:
UKAWA kuweka mawakala wenye uvumilivu—mtu ambaye anaweza
kuvumilia njaa ikibidi  kukaa  bila kula  na kunywa  kwa
zaidi ya  saa 24. Wako mawakala chaguzi zilizopita kwa
kuendekeza ulaji na unywaji  wakiwa kazini kwenye vituo vya
kupiga kura, waliagiza vinywaji na  vyakula na vinywaji.
Lakini wajanja  waliweka kwenye vyakula na vinywaji hivyo 
dawa za usingizi. Baada ya kula walijikula na  walikuja
kuamka  uchaguzi  ulikuwa umewisha  na  kura za mgombea
wao ambaye alikuwa anapendwa  na watu amekwishaibiwa kura
zake wakiwa usingizini.

Ninachosema hapa ni kwamba  uchaguzi ni wa
mwaka huu ni mapambano ya mamilioni ya wananchi masikini
(wakiwepo wanaCCM wengi tu)  na kikundi cha watawala wa CCM
wanaoendelea kujitajirisha kwa kuwa madarakani.

Hivyo mamilioni ya wananchi
wanaoteseka na umaskini wakiamua kuvishinda vishawishi na
ulaghai unaofanywa na watawala wa CCM  uchaguzi wa mwaka
huu utaleta mabadiliko kwa mara ya kwanza kuwezesha mfumo wa
vyama vingi kufanya kazi Tanzania. Zaidi fursa ya mamilioni
ya wananchi  wanaoishi maisha ya kimaskini kushinda
uchaguzi wa mwaka huu 2015  ni kubwa  kuliko wakati
mwingine wowote katika historia ya vyama vingi nchini
kwetu.

Sita:  UKAWA 
wahakikishe inawaelekeza  mawakala wake mambo muhimu ya
kufanya wakiwa kwenye vituo vya kupiga kura.  Mambo hayo ni
pamoja na   kuhakikisha wanachukua kwa usahihi matokeo
kwenye vituo na kisha wafuatilie kwenye halmashauri
kuhakikisha anayeshinda ndiye anatangazwa mshindi.
 
Umuhimu wa kufuatilia hadi
matokeo yatangazwe ni kuhakikisha waliopewa mamlaka
kutangaza matokeo ya diwani, mbunge na Rais hawachakachui
matokeo. Umma  ukiwa unafuatilia matokeo-wenye kutaka
kufanya mchezo mchafu watauogopa umma. Hakuna kinachoshinda
nguvu ya umma. MUNGU IBARIKI TANZANIA. 

Ninaruhusu Makala hii
ichapishwe na yeyote anayetaka. Lengo ni kuelimishana  ili
kuleta mabadiliko . Ukiwa na swali: niandikie:  ananilea_nkya@yahoo.com


 
Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Sat, 8/22/15, 'raymond mauki' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

  Subject:
[wanabidii] Re: [Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM KUJARIBU
KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]
  To:
"Wanazuoni@yahoogroups.com"
<Wanazuoni@yahoogroups.com>,
"mabadilikotanzania@googlegroups.com"
<mabadilikotanzania@googlegroups.com>
  Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>,
"Paschally Mayega" <ngowe2006@yahoo.com>
  Date: Saturday, August 22, 2015, 5:11 AM
 
 
  Mama Nkya
nimekuelewa sana
  sana na sana, siku zote
nimekuwa nikifuatilia harakati zako
  ila
sikujua msimamo wako uko wapi. Nashukuru kwa kuwaambia
  watanzania kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa
maoni yake
  haijalishi yupo wapi, ana nafasi
gani kwa jamii au yupo
  upande gani kisiasa.
Ulichokiandika ni very simple and very
  true
hata mtoto wa darasa la nne ataelewa ila cha ajabu kuna
  wasomi watakuja kupinga na wanaendeta kupinga
ulichokiandika
  tena wakitumia data za uongo
kabisa. Ni ukweli uliowazi kuwa
  watanzania
wa leo sio wa mwaka 1995 wa Mrema na nashukuru
  yeye mwenyewe amekiri hilo juzi kupitia kituo
kimoja cha
  redio(clouds fm), watanzania wa
leo wanahitaji mabadiliko
  chanya na
wasipoyapata kwa amani basi watatumia njia

nyingine yoyote japo hatupendi ifike huko.Mama
  Nkya, naomba ukipata muda unijibu haya
mawili, 
   Je, tufanye nini watanzania lei
hii ili kuzuia kabisa
  mchezo wa ccm
kutuibia kura zetu kwenye uchaguzi mkuu?

Ukizingatia wameshakiri kabisa watatumia njia yoyote
  kushinda ikiwemo goli la mkono.Pili,
  nini mchango wa wanawake kwenye harakati hizi
za
  leo,unadhani wameamka kiasi cha
kutosha? 
  Asante
  na
ubarikiwe sana,
  RAYMOND

MAUKIKIGAMBONI,
  DAR ES SALAAM.
 
  From:"ananilea
nkya
  ananilea_nkya@yahoo.com
[Wanazuoni]"
  <Wanazuoni@yahoogroups.com>
  Date:Fri, Aug 21, 2015 at 23:42
  Subject:[Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM
  KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]
 
 
   
 
 
 
  
 
 
    
      
              
     
   [Attachment(s) from ananilea nkya

included below]
        
      
       LOWASSA
KAFARA CCM KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO
 
  
 
  Na
Ananilea Nkya
 
 
 
  Nimeandika  hoja hii baada
ya kusoma na kusikia  hoja
  zinazotolewa
na  baadhi ya Watanzania kwamba  eti CHADEMA ,
  CUF, NCCR-Mageuzi  na NLD  -vyama
vinavyounda UKAWA kwa
  kumsimamisha 
Edward Lowassa kugombea Urais  vimepoteza

usafi  wa kuongoza  mapambano dhidi ya ufisadi.
 
 
 
  Ukweli ni kwamba viongozi wa CHADEMA na UKAWA
kumsimamisha
  Lowassa kuwa mgombea urais
wamecheza kama Pele. Tena
  wanastahili
pongeze kubwa maana walitumia akili kali na

saikolojia ya hali ya juu kubaini kuwa CCM ilikuwa
ilicheza
  mchezo mchafu kisiasa kuwatumia
wapinzania kumpakazia
  Lowassa ufisadi na
hatimaye CCM kupata nguvu ya kumtoa
  Lowassa
kafara ili eti CCM ionekane inajisafisha ufisadi.
 
 
 
 
  Wanaodhani CHADEMA na UKAWA
wamekosea pengine hawajaelewa
  kuwa   tangu
upepo wa mabadiliko  wa kukataliwa mfumo chama
  kimoja kuwa madarakani kwa muda mrefu
ulipoanza kuvuma
  duniani kote mwishoni mwa
miaka ya 1980,  baadhi ya wanaCCM

hawajakubali kwa dhati kabisa  ukweli huo na kuamini kwamba

  CCM inaweza  kupunzishwa kuongoza nchi
angalao kwa miaka
  mitano.


 
 
  Hasa
baada ya Mwalimu Nyerere CCM kuondoka duniani, CCM
  imebaki na viongozi ambao hawako tayari
kutumia ujasiri
  kuongoza mabadiliko kwa
amani.  Baadhi ya vongozi wanaojali
  zaidi
maslahi ya wana CCM wachache wanaotumia kauli kama
  hirizi kauli aliyowahi kuitoa Mwalimu Nyerere
kuwa bila CCM
  imara—Tanzania itayumba
kujidanganya wenyewe na kudanganya

wananchi.
 
 
 
  Wanasahau kwamba Mwalimu
Nyerere kama mwanafalsafa na
  mwanasiasa
makini alikuwa anatoa maamuzi ya kijasiri kwa
  faida ya taifa na wananchi kulingana na hali
halisi ya
  wakati husika kwa kusoma upepo wa
wananchi. Kwa mfano
  Nyerere aliwahi kusema
CCM si mama yake akimaanisha Tanzania
  na
Watanzania ni muhimu zaidi kuliko umuhimu wa CCM kuwa
  madarakani.
 


 
  Mfano Mwalimu Nyerere
mwaka 1992 alionyesha mfano kwamba
  maslahi
ya nchi na wananchi ndiyo muhimu kuliko maslahi ya
  CCM alipokubali kwenda kinyume na uamuzi wa
wanaCCM wengi
  waliokuwa
wamekataaa—mabadiliko—kuanzishwa vyama vingi
  nchini ili vyama vibadilishane uongozi wa nchi
--kuharakisha
  maendeleo ya wananchi.
 
 
 
  Lakini baada ya Mwalimu kuondoka dunaini kila
mwanaCCM
  anayechaguliwa kuwa Rais, kwa
kuogopa kulaumiwa kwamba eti
  kama CCM
haitachaguliwa kupitia sanduku huru la kura atabeba
  lawama za kufanya CCM iondoke madarakani,
serikali zote za
  CCM baada ya Mwalimu
Nyerere kuondoka duaniani zimekuwa

zinajihusisha na ufisadi.
 


 
  Serikali ya CCM imekuwa
ikikwapua kwa wizi wa wazi mabilioni
  ya
fedha za umma na kufanya maovu mengine mengi kuhakikisha
  CCM haiondoki madarakani. Hivyo chaguzi
zinafanyika kama
  geresha tu—kudanganya
wafadhili na mataifa kuwa Tanzania
  ni nchi
ya demokrasia ya vyama vingi.
 
 
 
  Mfano
uchaguzi wa mwaka 2005 serikali ya CCM chini ya Rais
  Mkapa ilikwapua fedha za wananchi kutoka Benki
Kuu Akaunti
  ya EPA shilling bilioni 133
ambazo ziliiwezesha CCM kumweka
  madarakani
Rais Kikwete.
 
 
 
  Mwaka jana 2014 serikali ya
CCM chini ya Kikwete ilikwapua
  shilingi
bilioni 306 kutoka akaunti ya Tegeta escrow Benki
  Kuu kwa ajili ya kuiwezesha CCM kushinda
uchaguzi wa
  serikali za mitaa na uchaguzi
mkuu unaofanyika tarehe 25
  Oktoba mwaka huu
2015.
 
 


  CCM wakishaingia madarakani jambo muhimu
kuliko yote Rais na
  serikali yake
analolifanyia ni kubuni ufisadi wa kuipatia

CCM fedha na mbinu nyingine za kuiwezesha CCM ibaki
  madarakani uchaguzi unaofuta. Hakuna kazi
muhimu ya
  kuwaondolea wananchi umaskini
inayofanyika kwa kiwango na
  juhudi
kubwa.
 
 


  Kwa sababu hiyo,   kikundi kidogo cha
watawala, wengi wakiwa
  ni kutoka CCM na
familia zao wamejikuta wakinufaika kwa kuwa
  matajiri kufuru kwa muda mfupi ili hali 
wananchi wengi
  wakibaki maskini na mafukara
wa kutupa.
 
 
 
  Mfano  wabunge (kikundi cha
watu wasiozidi 400) wengi wakiwa
  ni
wanachama wa CCM  kila mmoja analipwa si chini ya
  milioni  10 kila mwezi kama mishahara, wacha
marupurupu  na
  posho za vikao vya kamati,
posho za safari na  mamilioni
  mafao kila
baada ya miaka mitano.  Lengo wawe na fedha
  nyingi za kununua kura za wapiga kura maskini
uchaguzi
  unaofuata CCM ibaki madarakani.

 
 
 
  Ndiyo sababu kila mwananchi wakiwepo watu
muhimu kama walimu
  wa vyuo vikukuu na
madaktari hivi sasa nao  wameamua kuwa

wanasiasa.
 
 
 
  Zaidi baadhi ya wanaotafuta
madaraka ya kisiasa wanatumia
  mbinu chafu
sana  ikiwa ni pamoja na ushirikina wa kuuwa
  watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) waweze
kupata nafasi
  ya kuingia katika kundi la 
watawala—kupata utajiri wa
  kutisha katika
kipindi cha miaka mitano.
 


 
  Mfamo Wabunge
waliomaliza muda wao mwaka huu 2015    kila
  mmoja ameondoka na kiinua mgongo zaidi ya
shilingi milioni
  200.  Hii ni kufuru
katika nchi inayojinasibu kuwa ni
  maskini
na inapita huko na huko duniani kuomba misaada!
 
 
 
  Hata hivyo kwa kadri ufukara unavyoendelea
kuwatafuna
  wananchi wengi, na kwa kadri
uelewa wa  wananchi
  wanaoteseka kwa 
umaskini  unavyoongezeka kwamba CCM na

utawala wa  serikali yake ndicho chanzo cha umaskini wao,

  CCM  imebaini kuwa haiwezi tena 
kushinda uchaguzi kupitia
  sanduku huru la
kura kwa kutegemea kete moja tu—kununua

wananchi mafukara  peke yake.
 
 
 
  Hivyo
katika miaka ya hivi karibuni CCM imeanza kuendesha
  siasa za maji taka—kuchafuana wao kwa wao na
hatimaye
  wameamua kutoana kafara-lengo kuu
likiwa ni kuzuia wananchi
  wasitumie
sandundu la kura kufanya mabadiliko—kuchagua
  vyama vingine kuongoza nchi. 
 
 
 
  Hivyo Rais Kikwete, hata kama ndani ya umungu
wa moyo wake
  hakubaliani na CCM inavyotumia
ubabe kukataa mabadiliko
  kinyume na asili
ya binadamu, amekuwa akifanya mambo

kutimiza matakwa ya baadhi ya wanaCCM —kujaribu kuzuia
  mabadiliko—ili tu kuepuka lawama- amalize
muda wake bila
  kuonekana ndiye kasababisha
wananchi kuipunzisha CCM uongozi
  kwa
kipindi cha miaka mitano.
 
  
 
  Kwa
kufanya hivyo Rais Kikwete amejikuta akiporwa ujasiri
  wake aliokuwa nao kama mwanasiasa   ambaye
Mwalimu Nyerere
  alimuamini.
 
 
 
  Kumbuka Mwalimu Nyerere alinukuliwa na gazeti
la  Nipashe na
  Majira 26/5/95 akisema 
baada ya Rais Mwinyi  baadhi ya
  vijana
ambao alikuwa anaona wana nia ya dhati kabisa  na
  uwezo mkubwa wa kuongoza Tanzania  ni
Benjamin Mkapa, Jakaya
  Kikwete na Edward
Lowassa.
 
  Lakini kwa
Kikwete kukubali kuyumbishwa na wana CCM wachache
  wasiokubali mabadiliko anaonekana kufumbia
macho utekelezaji
  wa kile mwanafalsafa
Mwalimu nyerere alichokisema---kwamba

Watanzania wanataka mabadiliko.
 
 
 
  Mfano Rais
Kikwete alipata fursa ya kusimamia mabadiliko kwa
  kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya
wananchi.
  Lakini kikundi kidogo cha
wahafidhina ndani ya CCM
  kilimtisha
akajikuta anaweka pembeni ujasiri wake aliokuwa
  nao wa kusimamia mabadiliko hayo muhimu kwa
maendeleo ya
  taifa hili.


 
 
  Kama
uamini jiulize ni kwa   nini  Kikwete aliachia Bunge la
  Katiba lililojaa asilimia 80  ya wanachama
likazika Rasimu
  ya Katiba ya wananchi pale
Dodoma mwaka jana 2014  -- Rasimu
  ambayo
ingeleta Katiba yakuweka  misingi ya kuleta
  madadiliko Tanzania—mabadiliko ya
kuhakikisha kikundi
  kidogo cha watawala
hakijitajirishi kwa ufisadi na kujigawia

mali  za umma huku mamilioni ya wananchi wakibaki maskini
na
  mafukara wa kutupa?
 
 
 
  Baada ya
Kikwete kupoteza fursa  ya kuleta mabadiliko  kwa
  kuandika Katiba Mpya,  umma uliofukarishwa 
umeendelea
  kupata uelewa kuwa CCM na
serikali  yake ndicho chanzo cha
  umaskini
wao. 
 
 


  Hivyo ili kuendelea  kubaki madarakani 
serikali ya CCM
  imekuwa  ikijihusisha na
ufisadi ili ipate fedha za
  kuwarubuni
walala hoi wakati wa kampeni za uchaguzi.


 
 
  Mfano
mwaka 1995 Rais Benjamini Mkapa alijikuta serikali
  yake ikifanya ufisadi  katika  akaunti EPA
(bilioni 122)
  zilizotumiwa na CCM
kumuweka  Kikwete madarakani.
 
 
 

Ukitafakari utaona kwamba katika ufisadi Tegeta escow,
  serikali ya CCM imekapua billion 306 mara tatu
ya ufisadi wa
  EPA mwaka 1995 ilipokwapua
bilioni 122 ili kipate fedha
  nyingi zaidi
la kuwalaghai wapiga kura mafukara ambao

wameendelea kupata uelewa kuwa CCM inaiba fedha za umma
  kununua wapiga kura wakati wa kampeni za
uchaguzi.
 
 
 
  Hivyo serikali ya CCM
inayoongozwa na Kikwete ambayo
  imeshuhudia
nguvu ya wananchi kudai mabadiliko ikiwa kubwa
  kuliko wakati mwingine wowote, inajaribu kila
mbinu chafu na
  safi ili CCM ibaki
madarakani baada ya uchaguzi mwaka
  huu.
 
 
 
  Ndiyo sababu  serikali ya CCM  kupitia
msemaji wa chama
  hicho Nape Nnauye imeanza
kuwaambia Watanzania kuwa  CCM
  lazima
ishinde uchaguzi wa mwaka huu hata kama ni kwa
  kutumia goli la mkono (wizi au lolote lile
chafu).
 
 


  Zaidi  Rais   Kikwete  amefikishwa
mahali  pabaya
  kulazimika  kubuni 
mchezo  mchafu kujaribu kuwadanganya

Watanzania  kuwa eti  CCM na serikali yake ni safi,
  haijihusishi na ufisadi unaofukarisha wananchi
isipokuwa
  wanachama wachache wa CCM ndio
mafisadi.
 
 
 
  Ili  kujaribu kutafuta
kujenga  uhalali wa CCM kubaki
  madarakani
baada ya uchaguzi wa  mwaka huu 2015, Kikwete
  amejikuta akilazimika  kumtoa  kafara
Lowassa  kwa
  kumpakazia  ufisadi wa 
Richmond.
 
 
 
  Wananchi wanauliza kama
Lowassa alikuwa ndiye mhusika  wa

Richmond  ni kwa nini   Spika wa Bunge  Anna Makinda
(mmoja
  wa watawala  wa CCM),  hakuagiza 
tume ya Bunge iliyoongozwa
  na Mbunge wa CCM
Harrison Mwakyembe kumhoji Waziri Mkuu

Edward Lowassa?
 
 
 
  Pili wananchi wanahoji kama
CCM haijamtoa Lowassa kafara
  kwa
kumbebesha ufisadi wa chama hicho  ili kupumbaza hasira
  ya  wananchi dhidi ya ufisadi wa CCM kwenye
uchaguzi wa
  Oktoba mwaka huu 2015  ni kwa
nini  Rais Kikwete alikubali
  Waziri wake
Mkuu  Edward Lowassa  ajiuzulu kwa ufisadi wa
  Richmond 2008 wakati ufisadi wa kutisha 
ulifanywa na
  serikali ya CCM kwenye akaunti
ya Tegeta escrow 2014
  Kikwete aliwatetea
mawaziri  waliogawiwa fedha hizo na Ikulu

ilikuwa ndiyo mtuhumiwa namba moja?
 
 
 
  Mimi si
mwanasiasa wa chama chochote cha siasa hapa nchini
  ninachoangalia ni chanzo cha umaskini wa
wananchi wengi
  Tanzania.


 
 

Ndiyo sababu Watanzania wengi nikiwepo mimi mwenyewe kwa
  sababu  tulipewa habari nusu nusu
zilizotolewa kimkakati na
  serikali ya CCM
kuhusu kashfa ya Richmond  kumpakazia

Lowassa ufisadi, tulipubwazwa tukaisaidia CCM  kumchafua
  Lowassa kuwa ni fisadi wa Richmond.  
 
 
 
  Lakini baadhi ya wananchi walianza  kujua
kuna ukweli
  uliofishwa kuhusu Richmond pale
TV moja ilipokuwa imemwalika
  Lowassa aotoe
yake ya moyoni live siku chache baada ya

kujiuzulu, lakini kipindi hicho cha TV kikafutwa ghafla.
 
 
 
  Hata hivyo ukweli huo umekuja kujulikana mwezi
Julai mwaka
  huu Lowassa alipotoa hadharani
baada ya kuachana na CCM na
  kujiunga na
CHADEMA.
 
 
 
  Sasa wananchi   
wamefahamu kuwa  CCM  chini ya serikali ya
  Rais Kikwete iliamua kumtoa Lowassa kafara kwa
kumpakazia
  ufisadi wa   Richmond  ili 
kuiokoa CCM isiadhibiwe vikali
  na wananchi
kwenye sanduku huru la kura  –kwa ufisadi
  alinawasababishia umaskini na ufukara.
 
 
 
  Ndiyo sababu  hivi sasa  CCM na baadhi ya
wanahabar
  wanapakazia  CHADEMA  na 
UKAWA  kuwa  eti ni mafisadi 
  baada ya
kumpokea Lowassa (kafara wa CCM)  na  kumpitisha
  kuwa mgombea wa  Urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
 
 
 
 
  Isitosha
hivi sasa kikundi  cha watawala wachache wa
  serikali ya CCM wanahaha na wanamzonga Kikwete
azuie
  mabadiliko kwa mkono kwa  kufanya
kila uchafu  kupumbaza
  Watanzania kwa
kutumia kete ya eti   Lowassa ni  fisadi wa
  Richmond  hivyo hana sifa ya kugombea Urais
wa Tanzania,
  bali Magufuli ndiye mtu
safi.
 
 


  Wananchi wenye akili zao wanajiuliza hivi
mwenye kashfa za
  kifisadi kati ya Lowassa
na Magufuli ni nani?  Ni Lowassa

aliyepakaziwa Richmond au ni Magufuli aliyeongoza
watawala
  kujiuzia kwa bei chee nyuma za
umma zilizogarimu wanannchi
  mabilioni ya
fedha?
 
 


  Wananchi pia wanajiuliza kama Lowassa ni
fisadi wa Richmond
  ni kwa nini serikali ya
CCM haijamshitaki mahakamani miaka
  minane
tangu ufisadi huo ulipotokea?
 
 
 
  Hivyo 
pengine  baada ya Lowassa kutafakari nafsi yake na
  kuona kuwa CCM imemtoa kafara asigombee
Urais  ili kuzuia
  mabadiliko, ameamua
kufanya  maamuzi magumu  ya kuhama CCM

--kushiriki kuongoza masikini  na mafukara  wanaotafuta
  mabadiliko.
 


 
  Lowassa ameamua
kutekeleza alichokitabiri Mwalimu Nyerere

kwamba CCM isipokubali kuongoza wananchi wapate
mabadiliko
  wanayoyataka—wananchi
watayatafuta mabadiliko hayo  nje
  ya
CCM.
 
 


  Ni dhahiri CCM ilipoteza fursa adimu ya
kuongoza wananchi
  kwenye kuleta mabadiliko
kwa kuandika Katiba  Mpya-- kuweka

misingi ya kukomesha mfumo wa utawala  unaowezesha
watawala
  kuwa matajiri wa kupindukia  huku
mamilioni ya wananchi
  wakiwa mafukara na
nchi ikinuka aibu ya umaskini  wa

kijitakia  ikiwa rasilimali nyingi za asili.
 
 
 
  Wanaomchochea Rais Kikwete asikubali
mabadiliko yachukue
  mkondo wake, wameunda
timu ya kampeni yanye wajumbe wengi

waliohusika kumpakazia Lowassa ufisadi wa Richmond ili
eti
  kwenye kampeni waendelee kumpaka
ufisadi  Lowassa, CHADEMA
  na UKAWA
wakidhani Watanzania hawana akili ya kutafakari.
 
 
 
  Lengo lao ni moja. Wanajua kabisa kuwa kwa
kutumia sanduku
  huru la CCM  haiwezi
kuchaguliwa. Wanataka kutumia
  kisingizio 
kuwa  CHADEMA  na UKAWA imechafuka eti kwa
  kumsimamisha Lowassa Urais  ambaye CCM
imemtoa karafa –
  kwa kumpakazia ufisadi
wa Richmond.
 
  Lakini
baada ya kupata salamu za wananchi kupitia mafuriko
  yao kwenye kumtambulisha Lowassa kwamba wao
wanaelewa fisadi
  kamili ni CCM, sasa CCM
imeshtuka imeanza kutumia polisi
  kuwaadhibu
wananchi. Pengine baadaye itatumia jeshi

kabisa.
 
 


  Zaidi imeamua kujaribu kampeni za 
ardhini -nyumba kwa
  nyumba, bila shaka
kutumia mabilioni ya fedha serikali ya
  CCM
ilizokwapua Tegeta escrow kununua shahada na kura za
  mafukara.
 
 
 
  Kwenye
kampeni za   nyumba kwa nyumba mtu kwa mtu ndiko
  ufisadi mbaya wa kisiasa
unakofanyika—kununua, kutisha na

kuumiza    wananchi mafukara.
 
  Swali ni je Watanzania wangapi wapiga kura
watakubali CCM
  inapopita majumbani mwao
kuuza shahada zao  kwa sukari,
  kanga au
fedha hata kama CCM itaamua kumpa kila mpiga kura
  shilingi milioni moja?
 
 
 
  Ni
mpiga kura gani atakayekubali KUDANGANYIKA  kwa
  kununuliwa na  CCM  kwa vijizawadi vya fedha
nguo KUSALITI 
  mamilioni ya watanzania 
wanaoendelea kuteseka  kwa ufukara
  kila
baada ya uchaguzi kwisha na CCM kubaki madarakani?
 
 
 
  Wananchi  pia wanauliza je mabilioni ya
escrow yatawanunua
  wajumbe wa NEC ili 
wavuruge daftari la wapiga kura, au

wachakachue kama uchaguzi wa 2010  au wataharibu daftari
la
  wapiga kura, mashine   na vifaa vya
kupigia kura, au
  kuchelewesha kwa makusudi
kufungua vituo vya wapiga kura
  ili 
kuvuruga uchaguzi CCM  ishinde kwa goli la mkono?
 
 
 
  Kadhalika wananchi wanauliza wanaomshinikiza
Kikwete
  asikubali mabadiliko wakiona hilo
haliwezekani je watamuua
  Lowassa waliomtoa
kafara au  viongozi wa CHADEMA na UKAWA

waliompokea Lowassa na kumwezesha kufikia azma yake ya
  kujitolea kuwatumikia watanzania  ili
kuvuruga uchaguziwa
  mwaka huu?
 
 
 
  Wananchi wanauliza maswali hayo  baada ya
kubaini kwamba
  huenda  wasiomtakia mema
Kikwete astaafu kwa amani
  wamejaribu
kuwalaghai baadhi ya viongozi wakuu wa UKAWA ili
  kujaribu kuvuruga UKAWA – lakini UKAWA kwa
vile ni sauti
  ya mafukara-sauti ya umma 
imeendelea kuwa moto mkali wa
  nyika  dhidi
ya CCM.
 
 
 
  Hivyo binafsi namshauri Rais
Kikwete akubali kuwa baba wa
  pili wa Taifa
hili baada ya Nyerere kuondoka. Akubali

kusimamia wananchi watumie sanduku huru la kura kwenye
  uchaguzi wa mwaka huu 2015 kupata mabadiliko
ya uongozi
  wanayoyataka.


 
 

Wananchi wana imani na UKAWA   kwamba wakiingia
madarakani
  Katiba mpya inayotokana na maoni
ya wananchi itaandikwa.
 


 
  Huo utakuwa ni mwanzo wa
mabadiliko wanayoyataka

wananchi—kuhakikisha watawala hawajitajirishi
kupindukia
  kufisadi fedha za wananchi huku
wananchi wengi wakibaki
  mafukara. 
CHADEMA  na UKAWA  wasipotimiza hili na kuonyesha
  kwa vitendo maendeleo watakayokuwa
wameyaleta kwa miaka
  mitano, ni lazima
wananchi watatumia sanduku la kura

kuwapunzisha.
 
 
 
  Ninaamini ni wenye kutetea
maslahi binafsi tu ndiye
  atakayemlaumu Rais
Kikwete kwamba eti CCM isipochaguliwa

Oktoba 25, Kikwete atakuwa ni chanzo  cha wananchi
kuamua
  kuipunzisha CCM  kwa miaka mitano.

 
 
 
  Nitakuwa wa kwanza kuwapinga watu hao na
kumtetea Kikwete
  hata kama ni kwa kuamua 
kuingia kwenye siasa  kwa kujiunga
  na CCM
.
 
  


  Hakika Rais Kikwete  ukisimamia 
wananchi  wazungumze kuhusu
  hatma ya
uongozi wan chi yao kwa kutumia sanduku huru la
  kura  bila CCM kuingiza  mkono mchafu, wewe
mwenyewe
  ukistaafu utaishi kwa amani na
furaha huku baadhi yetu
  tukikuona kama baba
wa Pili Taifa taifa hili, baada ya
  Mwalimu
Nyerere.
 
 
 
  Mwisho ninaruhusu yeyote
anayetaka kuchapisha au kutangaza
  redioni
natelevisheni niyoyoyaandika hapa TV au kuchapisha
  na kuwasambazia Watanzania wote popote walipo
ujumbe huu
  afanye hivyo. Wanawaza
kuwasambazia watu mitaani,
  kwenyemikutano
ya kampeni, mashuleni vyuoni popote

pale—lengo likiwa moja—sote Watanzania tuujue ukweli
  kuhusu ufisadi na mchango wake katika
kuwafanya Watanzania
  waishi katika
umaskini.   Lakini muhimu kila Mtanzania ajue
  hakuna mshindi wa kujisifu—mshindi ni  nchi
yetu Tanzania
  na  Watanzania  wote.
 
 
 
  MUNGU IBARIKI YANZANIA.
 
 
 
  Ananilea
Nkya
 
   E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
 
    
   
 
 
    
     __._,_.___
 
             Attachment(s)
  from ananilea nkya | View

attachments on the web
    
  
 
 
          1 of 1 File(s)


          
     
  
                
       LOWASSA  KAFARA WA

CCM.docx
  
         
 
    
     
 
    
   
    
         Posted by: ananilea
nkya
  <ananilea_nkya@yahoo.com
     
     
     

 
    
                         
Reply
  via web post
     
                 •
         
  
                Reply to
sender           
         

            
 
             Reply to group           
           •
       
     Start a New
  Topic
 
         •
                 
           Messages in this
  topic
                 (1)
 
                    
 
        
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
     Visit Your Group
 
     
       New
Members
       2
   

  
 
 
 
  
   
• Privacy • Unsubscribe • Terms of Use
 
 
 
 
 
 
   
 
 
  
  
 

 
 
 
     
 


 
 
   
 
 
   .


 
   


 
 
 
  __,_._,___
 


 
 
 
 
  --
 
  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
   
 
  Kujiondoa Tuma Email kwenda


  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
  kudhibitisha ukishatuma
 
   
 
  Disclaimer:
 

Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
  for any legal consequences
of his or her postings, and hence

statements and facts must be presented responsibly. Your
  continued membership signifies that you agree
to this
  disclaimer and pledge to abide by
our Rules and
  Guidelines.


  ---
 

You received this message because you are subscribed to
the
  Google Groups "Wanabidii"
group.
 
  To unsubscribe
from this group and stop receiving emails

from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
 
  For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

   




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






--

Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la
'Mabadiliko'.

Kuchangia mada tuma kwenye Email hii:
mabadilikotanzania@googlegroups.com

 

 

For more options, visit this group at:

http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Mabadiliko Forum" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.

To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.

Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.

To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAN5khk7sowgC0R%2Bmyb8awOO85DX3-Bnp66JJ6CP6zLGnLnhXTg%40mail.gmail.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment