Thursday, 4 December 2014

Re: [wanabidii] ZITTO KABWE UNAJIANDALIA ANGUKO

kwa taarifa za karibuni Zito amesikika akisema yeye ataendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa chadema na anaomba maridhiano na viongozi yafanyike na pia uchunguzi ufanyike na endapo atagundulika alikose hatasita kuomba radhi.

Haya ndio maneno ya Muungwana hayo mambo mengine ni propaganda.

 Fanyeni kazi kwa bidii na maarifa mjenge taifa lenye hehima na ustawi na sio fedheha iliyopo na ufisadi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.


On Friday, 5 December 2014, 8:45, 'eid omari' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Yawezekana Bw; Katabazi ana interest kwenye Sakata la ESCROW au chuki binafsi na Bw; Zitto. 


Omary Iddy,DAGROFORESTRY RESEARCH TANZANIA FORESTY RESEARCH INSTITUTE(TAFORI)P.O BOX 1257,SHINYANGATANZANIA.Tel:+255 28 276 3249MOBILE:+255 713 728 672FAX:+255 28 276 2198EMAIL:eidomari@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 12/4/14, 'weston mbuba' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] ZITTO KABWE UNAJIANDALIA ANGUKO
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, December 4, 2014, 5:22 PM

Katabazi bado
unamwamini Werema?Kama utakuwa bado unamwamini utakuwa wa
ajabu kabisa.




    On Thursday,
December 4, 2014 11:58 AM, 'eid omari' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:

   

  Nildhani tunajibu hoja
fulani kwa kuhusianisha na issue iliyopo (recent news),
kumbe unaweza kujibu au kusema kitu chochote bila kujali
muda na uhusiano wa kinachosemwa.

Omary Iddy,DAGROFORESTRY RESEARCH TANZANIA
FORESTY RESEARCH INSTITUTE(TAFORI)P.O BOX
1257,SHINYANGATANZANIA.Tel:+255 28 276 3249MOBILE:+255 713
728 672FAX:+255 28 276 2198EMAIL:eidomari@yahoo.com

--------------------------------------------
On Mon, 12/1/14, 'leonard magwayega'
via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

  Subject: Re:
[wanabidii] ZITTO KABWE UNAJIANDALIA ANGUKO

To: "wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>,
"Wanazuoni" <wanazuoni@yahoogroups.com>
  Date: Monday, December 1, 2014, 10:02 AM
 
  WE KATABAZI UTAACHA LINI
  KUROPOKA? AU NA WEWE UMEPATA MGAO WA ESCROW
MAANA WAPO
  WAANDISHI KAMA WEWE WENYE TAMAA
YA PESA NAO
  WAMO.
 
      On Saturday,
  November
29, 2014 10:48 AM, Yona Maro
  <oldmoshi@gmail.com>
wrote:
    
 
  ZITTO KABWE UNAJIANDALIA

ANGUKONa Happiness KatabaziMTUME Muhammad S.A.W amewahi
  kunukuliwa akizitaja alama kuu tatu za
mnafiki. Ambazo ni ;
  "Mnafiki akisema
anasema uongo,mnafiki akiaidi hatimizi na

mnafki akiaminiwa ,haaminiki'.Nukuu hiyo ya Mtume
inapendwa mno
  kutumiwa na rafiki yangu
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Rombo

(Chadema), Joseph Selasini,katika harakati zake za
kisiasa
  tangu nimfahamu akiwa Chama Cha
NCCR-Mageuzi.Na nanukuu hiyo ndiyo imekuwa kama
  salamu yangu mimi na yeye pindi
tunapowasiliana kwa simu au
  kukutana hana
kwa ana na mwishowe tunaishia kucheka sana

kutokana na sifa hizo za Mnafiki.Alhamisi wiki hii huko
Bungeni,
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) ,
Jaji Fredrick Werema
  akiwa bungeni
alimuumbua Mbunge wa Kigoma Kaskazini ,Zitto
  Kabwe kwa vielelezo kuwa Zitto alishakiri
chini ya kiapo
  ofisini kwa Jaji Werema
kwamba hana majina wala akaunti za
  watu hao
, kinyume cha kauli yake huko nyuma alipowahi
  kusema kuwa anawajua.Jaji Werema alilazimika
kusema hayo
  muda mfupi bungeni baada ya
Zitto kusisitiza kuwa serikali
  haionyeshi
nia ya kuwachukulia hatua walioficha fedha hizo
  nje ya nchini.Jaji Werema ambaye ni
Mwanasheria
  Kitaaluma aliigeukia taaluma
yake na kuanza kutoa vielelezo
  vinavyopinga
kauli hiyo ya Zitto kwamba serikali haina nia
  ya kuwawajibisha walioficha fedha hizo, ambapo
Jaji huyo
  alisema Februali 28 mwaka 2013 ,
Kamati iliyoundwa
  kuchunguza kama fedha
hizo ni haramu , kutambua benki
  walizoficha
, kuandaa mashitaka na kisha kuishauri

serikali."Februali 28 mwaka 3013, Kama

"Februari 28, mwaka 2013, Kamati ilikutana hapa bungeni
  katika ofisi yangu na ilipomuita Mheshimiwa
Zitto aje atoe
  ushahidi, alikuja akatwambia
anazo nyaraka na taarifa ila
  akaomba
ahakikishiwe usalama ili pale ambapo angezileta
  pasingelikuwa na mtu wa kumzonga."Pia,
alitaka mimi nitoe kiapo
  ambacho baada ya
kutaja hayo majina halafu ikawa siyo kweli,

basi yeye awe 'free' (huru), kwa hiyo alitaka apewe
  kinga ya kiapo."Machi 23 tulipomuita aje
  akatukwepa, akasema anakwenda Tanga kwenye
mafunzo ya
  mgambo, kwa hiyo, tukaona
tumsubiri hadi
  atakapomaliza."Aprili 12,
mwaka 2013, tukakutana
  naye hapa Dodoma
katika viwanja vya Bunge, akasema hawezi

kutwambia chochote kwa sababu alikuwa akijiandaa kwenda
  Afrika Kusini."Mei 4 tulimuita tena
kwenye
  kamati hapa Dodoma na katikati ya
mahojiano alidai ana jambo
  muhumu lenye
maslahi kwa taifa, akasema anaomba aondoke

atarudi, kamati ilimruhusu, hata hivyo hakurudi
  tena."Tulipompigia simu alisema alikuwa
  Dar es Salaam na alikuwa 'busy' akijiandaa
kwa kongamano
  la Kigoda cha Mwalimu
Nyerere."Mei 24 kamati ilimfuata Dar es

Salaam, akasema hana nafasi kwa sababu wakati huo alikuwa
  akijiandaa kuisaidia Timu ya Taifa," alisema
Jaji Werema
  na kuongeza:"Kamati iliamua
sheria ichukue
  mkondo wake kwa mujibu wa
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya
  Jinai,
Kifungu cha sita ndipo tukachukua maelezo ya Zitto
  Kabwe chini ya kiapo na akatwambia hakuwa na
jina, wala
  akaunti ya Mtanzania yeyote
aliyeficha fedha nje."Lakini, leo hapa amesema serikali
  haina nia ya kurudisha fedha zilizofichwa
Uswisi. Kwa maana
  hiyo, Mheshimiwa Naibu
Spika, Zitto Kabwe ni mzito na
  nakubaliana
na Lema (Mbunge wa Arusha Mjini) aliyesema hapa,
  kwamba Zitto alete majina hayo.Itakumbukwa
kuwa kwa takribani mwaka
  mmoja sasa Zitto
amekuwa akilandalanda mitaani na kunukuliwa

na vyombo vya habari kuwa kuna vigogo wameficha fedha
nchini
  Uswis na anawajua. Kweli kwa watu
wanaopenda kudakia mambo
  bila kufanyia
utafiti nao wakajikuta wanaiomba wimbo huo

aliokuwa akiumba Zitto.Ambapo mwisho wa siku Jaji Werema
  ,Alhamsi ya wiki hii bungeni alikuja kufumbua
macho
  watanzania kuwa huyu huyo Zitto
aliyekuwa anatamba mitaani
  kuwa anawajua
walioficha fedha, aliitwa kwenye Kamati hiyo
  maalum ili akaisaidie kutoa hayo majina ya
namba za akaunti
  zao lakini hakwenda na
matokeo yake Zitto alikwenda ofisini
  kwa
Jaji Werema chini ya hati ya kiapo kuwa hayafahamu
  majina wala akaunti za watu hao.Kisheria
tunasema kila tuhuma
  inayoibuliwa au kesi
inayofunguliwa mahakamani lazima iwe na

mlalamikaji ambaye mlalamikaji huyo anapaswa kufika
katika
  mamlaka husika kuisaidia kutoa
vielelezo anavyodai kuwa watu
  fulani
wamevunja sheria.Sasa kwa muktadha huu ambapo Zitto
  aliaminisha umma kuwa kitendo hicho cha
kufichwa fedha nje
  ya nchi kimemkera na
ushahidi anao, kwanini Zitto huyu kwa
  zaidi
ya mara nne ameitwa kwenye Kamati hiyo akashindwa
  kufika kutoa vielelezo hivyo?Je alikuwa na
lengo moyoni na
  akilini mwake?Maana tuhuma
hizo alizoziibua ni kubwa sana na
  serikali
yoyote makini nilazima tu ingeanza kufanyiakazi
  tuhuma hizo na hivyo ndivyo ilivyofanya
serikali ya
  Tanzania, baada ya Zitto kuibua
skendo hiyo , serikali
  iliamua kuunda
kamati ya kuchunguza ukweli wa tuhuma hiyo ,
  lakini cha kustaajabisha muibuaji wa skendo
hiyo Zitto
  ambaye alikuwa akijitapa kuwa
ana ushahidi, hakuweza kwenda
  kwenye Kamati
hiyo kutoa ushahidi.Naweza kusema pia kama yaliyosema na
  Jaji Werema ni kweli, basi watanzania hatuna
budi ya
  kumwambia Zitto tena bila haya kuwa
anaichezea serikali yetu
  sambamba na
kuchezea rasilimali watu na fedha za walipa

kodi.Kwani ni yeye aliyeshupalia skendo

hiyo na serikali ikajikuta inatumia fedha za kuunda
kamati,
  kutumia rasilimali watu na muda wa
serikali muda kuja kuhoji
  watu mbalimbali
ambapo mwisho wa siku Zitto ndiyo alikuwa

mtu muhimu sana wa kuisaidia Kamati hiyo kupata ukweli wa
  tuhuma hizo lakini cha kushangaza Zitto
inaelezwa alishindwa
  kutoa ushirikiano kwa
Kamati hiyo.Kama kweli maelezo ya Jaji Werema ni
  ya kweli,Je wananchi wamuite Zitto ni Mnafiki
,Mzandiki,
  muongo, msahaulifu, au ni mtu
anayekurupuka?Maana inashangaza kwa watu wenye
  kumbukumbu na Zitto kipindi kile alivyokuwa
amekomaa na
  skendo hiyo, leo hii Jaji
Werema anakuja kuliambia Bunge eti
  Zitto
ameeleza chini ya kiapo kuwa hana majina wala hafahamu
  akaunti za vigogo na kwamba alikwepa kwenda
kwenye Kamati
  kuhojiwa?Hapo ndiyo
ninampomheshimu Mbunge wa
  Vunjo(TLP),
Agustine Mrema enzi zile alipoibua kashfa wa
  wizi wa Sh.milioni 900 kwa mawaziri wa
serikali ya awamu ya
  tatu iliyokuwa
ikiongozwa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

kuwa wametafuna fedha hizo na kweli Mrema alikubali
kuhojiwa
  na Kamati ya Bunge na akafunguliwa
kesi hiyo katika Mahakama
  ya Kisutu na
alishinda kesi hiyo.Mrema aliibua kashfa hiyo
  iliyomhusisha Rais Mkapa na baadhi ya mawaziri
wake kwenye
  mikutano yake kisiasa , na
alipoitwa kuhojiwa kwenye kamati
  ya bunge
kipindi hicho hakukimbia, alikwenda na akahojiwa na
  mwisho wa siku alifunguliwa kesi katika
Mahakama ya Hakimu
  Mkazi Kisutu kutoka na
kuibuka kashfa hiyo ambayo upande wa

jamhuri ulidai kashfa hiyo ni uzushi, lakini mahakama
  ilimwachiria huru Mrema.Hivyo Mrema awe ni
funzo kwa
  wanasiasa wengine walioibuka hivi
sasa ambao wanajifanya
  mahiri sana wa kudai
wanaibua tuhuma za ufisadi lakini
  wakiitwa
katika mamlaka husika kutoa ushahidi huo

,wanakwepa.Aprili 12 mwaka 2012 gazeti hili

lilichapisha makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari
  kisemacho 'Zitto Kabwe ,Mbona U
msahaulifu?Maudhui ya makala hiyo nilikuwa

namuelezea Zitto kumbe na yeye ni jamiii ile ya baadhi ya
  wanasiasa wale wale wenye hulka za
kinyang'au ambao
  wanakasumba ya
kuzungumza uongo mbele ya umma, ili umma

uwapende na uamini kuwa kiongozi huyo ni mtu safi na
mtetezi
  wa wanyonge, kumbe siyo kweli.
Ieleweke wazi hapo nyuma
  Zitto alipata
bahati ya kupata umaarufu ndani ya jamii kwa
  kile kilichoelezwa ni mwanasiasa kijana ambaye
ana misimamo
  thabiti na asiyeyumba katika
kile anachikiami.Sisi waumini wa sheria tunasema
  tuhuma zitabaki kuwa tuhuma hadi pale
zitakapothibitika na
  mahakama au vikao
husika vya chama chake.Lakini kwa kuwa

mungu ni mwema kadri siku zinavyozidi kwenda mbele
atazidi
  kutuonyesha kama kweli Zitto ni
mwanasiasa msafi ,mhadilifu
  kuliko
wanasiasa wenzake wanaotoka katika vyama mbalimbali
  vya siasa.Na kweli utabili wangu huo
umetimia
  kwa hivi karibuni Kamati Kuu ya
Chadema, ikatangaza kumvua
  nyadhifa zote
ndani ya chama hicho kwa kile kilichodaiwa

kuwa wamebaini kuwa Zitto anakisaliti chama chao.Hali
  iliyosababisha baadhi ya wanananchi kuanza
kumtazama tofauti
  Zitto.Itakumbukwa kuwa
Zitto alikuwa
  msatili wa mbele kushinikiza
baadhi ya watumishi wa serikali
  na viongozi
wakiwemo mawaziri na Waziri Mkuu Mizengo Pinda
  wawajibishwe kwa kile alichokuwa akikidai kuwa
wameshindwa
  kutekeleza majukumu yao na
wengine wamekuwa wakikabiliwa na
  tuhuma
mbalimbali na kweli kuna mawaziri waliondolewa kwenye
  baraza la mawaziri kwasababu ya tuhuma hizo
zilizokuwa
  zikiibuliwa na Zitto na mwisho
wa siku zikaungwa mkono na

wananchi.Waswahili wanamsemo wao usemao

'linalomkuta Boko na Mamba pia litamkuta kwasababu wote
  wanaishi majini'. Kwa hiyo yaliyowakuta
baadhi ya mawaziri
  kwa kuondolewa kwenye
baraza la mawaziri kwa kigezo cha
  tuhuma
tu...ndicho ambacho kimemkuta Zitto leo hii kwa
  Kamati Kuu ya chama chake kumvua nyadhifa zake
zote kwa
  tuhuma kuwa ni msaliti.Iwe Chadema
walimsukia zengwe Zitto
  na kuamua
kumpokonya madaraka kwa kisingizio cha usaliti au
  ni kweli.Minaona itakuwa ni funzo sasa kwa
  Zitto kujifunza kuwa siyo jambo jema tena
kwake kuendelea na
  kasumba yake ya kupenda
kushinikiza wanasiasa wenzake hasa
  wa CCM
wawajibishwe au kupokonywa madaraka kwasababu
  wanakabiliwa na tuhuma za ufisadi na kuutaka
urais mwaka
  2015.Kwa uzoefu wangu kwa
wanasiasa wengi
  wa nchi hii ni mabingwa
kuwatengenezea wenzao majungu, fitna
  na
mwisho wa siku majungu wanayapeleka kwenye vyombo vya
  habari kwa kuwatumia baadhi ya waandishi wa
habari
  kuwachafua mahasimu wao na kweli
wanafanikiwa na majungu
  hayo kwa kuwachafua
maasimu wao na mwisho wa siku maasimu
  wao
wanachafuka mbele ya jamii na kama asimu wake ni mbunge,
  wananchi wake katika chaguzi zijazo wananchi
wake
  hawamchagui tena kwa kisingizio kuwa
mbunge wao huyo
  anakabiliwa na tuhuma za
ufisadi kumbe wakati mwingine ni
  uzushi
mtupu.Ushauri wangu kwa Zitto ni kwamba

akubali kuwa ule umaarufu aliokuwa nao zamani umeporomoka
  sana na hakuna ubishi kuwa itamgharimu kipindi
kirefu sana
  kuuurejesha ndiyo atashindwa
kabisa kuurejesha.Hivyo ni vyema yeye binafsi ajipe
  muda na atafakari ni wapi amekosea hadi leo
hii kila kukicha
  umaarufu wake unazidi
kuporoka, uadilifu wake unatiliwa
  shaka na
chama chake na baadhi ya wananchi.Kwanini Mwanasheria Mkuu
wa serikali
  Jaji Werema ameamua kumtolea
uvivu bungeni na kumuumbua kuwa
  Zitto kuwa
aliitwa kwenye Kamati hakufika kuhojiwa na

alipoitwa ofisini kwa Jaji Werema alitoa maelezo yake
chini
  ya kiapo kuwa hana majina ya vigogo
wala majina ya akaunti
  za vigogo walioficha
fedha Uswiss.Naheshimu mchango wa Zitto katika
  medani ya siasa nchini ila sipendezwi na
tuhuma mbalimbali
  zilizomzingira Zitto
kwani wananchi walionekana kumuamini
  Zitto
kuwa ni mwanasiasa msafi kuliko wengine lakini ghafla
  baadhi ya wananchi wanaripotiwa kwenye vyombo
vya habari
  wakisema hawana imani naye
tena.Kwa nini hili Zitto
  anaruhusu
litokee?Pia namshauri Zitto hivi sasa ni

vyema akajiepusha kujadili hadharani masuala yanayohusu
  uadilifu wa wanasiasa wenzake , kwani tayari
nayeye hivi
  sasa anaandamwa na tuhuma hizo
za ukosefu wa
  uadilifu.Pia awe makini sana
na hao watu
  wanaomshauri kwenda kwenye
vyombo vya habari kujadili
  masuala kadha wa
kadhaa kwani hao hao leo hii wanaojifanya

kukushauri kujadili masuala kadha wa kadhaa mbele ya
adhara
  ndiyo hao hao mwisho wa siku
watakucheka.Kwa wanaoifahamu jamii ya

Watanzania, tunaelewa kuwa Watanzania wengi ni kama tuna
  ugonjwa wa usahalifu.Tunashikia bango jambo
fulani mwisho
  siku tunalisahau tunadandia
hoja nyingine.Ni sisi watanzania tulishupalia wee
  Dk.Steven Ulimboka , Absalom Kibanda, mauji ya
Daud
  Mwangosi, Idara ya Usalama wa Taifa
livyotuhumiwa na Chadema
  kuiba kura katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2010,mgomo wa

madaktari ,shinikizo la kutaka aliyekuwa Waziri Mkuu
Edwar
  Lowassa, na aliyekuwa waziri Andrew
Chenge wajiudhuru na
  kwamba ni mafisadi,
vurugu za kugombea ujenzi wa bomba la
  gesi
Mtwara na vurugu za kisiasa Arusha lakini leo hii nani
  tena anazungumzia mambo hayo.Hakuna.Watoto wa
mjini tunasema hivi nyimbo
  zinazotamba
Tanzania kwa sasa ni kifo cha Rais wa Zamani wa
  Afrika Kusini, Nelson Mandela, kile
kinachodaiwa ni mgogoro
  ndani ya Chadema na
Zitto ,Zitto kuvuliwa nyadhifa zake kwa

madai kuwa ni msaliti .Kwahiyo ni vema akatulia
,watanzania
  watasahau tuhuma zake.Nimalizie
kwa kumtaka Zitto Kabwe,
  asikubali kuingia
kwenye nukuu hiyo ya Mtume Mtume Muhamad

kuwa; ' "Mnafiki akisema anasema uongo,mnafiki
akiaidi
  atimizi na mnafki akiaminiwa
,aaminiki'.Mungu ibariki Tanzania0716 774494
  www.katabazihappy.blogspot.com
  Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la
Jumapili,Desemba 15 Mwaka
  2013
 
 
 
 
 
 
 
  --
 
  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
   
 
  Kujiondoa Tuma Email kwenda


  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
  kudhibitisha ukishatuma
 
   
 
  Disclaimer:
 

Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
  for any legal consequences
of his or her postings, and hence

statements and facts must be presented responsibly. Your
  continued membership signifies that you agree
to this
  disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.
 

---
 
  You received this
message because you are subscribed to the

Google Groups "Wanabidii" group.


  To unsubscribe from this group and stop
receiving emails
  from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
 
  For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
 
 
      


 
 
  --
 
  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
   
 
  Kujiondoa Tuma Email kwenda


  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
  kudhibitisha ukishatuma
 
   
 
  Disclaimer:
 

Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
  for any legal consequences
of his or her postings, and hence

statements and facts must be presented responsibly. Your
  continued membership signifies that you agree
to this
  disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.
 

---
 
  You received this
message because you are subscribed to the

Google Groups "Wanabidii" group.


  To unsubscribe from this group and stop
receiving emails
  from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
 
  For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
 

--
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

     


--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment