Haule-kutumia sheria ni muhimu katika kujenga nidhamu. Hapa kwetu sheria imetawaliwa na rushwa kuanzia nyumbani (mkosaji kuhonga familia isitokee mahakamani), police hadi mahakamani. Utashangaa kezi za ubakaji mtu kakamatwa mubashara lakini ktk kesi 150 za namna hiyokiwilaya ni 4 tu zilizokamilika. Utafika kijijini utaonyeshwa karatasi za watu kukatwa mapanga kutokana na magomvi yaardhi au wakulima na wafugaji na ukakuta mtuhumiwa katorokea polisi alikowekwa ndani.
Kama upo maeneo ya wafugaji tuseme Naberera-Manyara au Kijiji cha Kwaba-Moro Rural na wote mnalima, wewe mluguru au Mha-watalishia shamba lako wewe si mfugaji wa Kimasai au Kimang'ati. Wanaoishi Engerosambu Loliondo ambao ni non-Maa wanakwenda mbali kulima kwa Wasonjo ili kukwepa adhabu hii nao ni walimu wa shule ya Msingi.
Nimeshuhudia mauaji kati ya Waikoma na wamasai wa kutoka Serengeti ambao walikuwa wanaingia Ikoma Robanda kuiba mifugo. Mnakuta mholore tu asubuhi fisi amekwisha kula mfugaji wa kutoka NCAA na maeneo ya vijiji vingine vya serengeti kuja kuiba mifugo Ikoma Robanda. Wananchi kwa wananchi wakiuana kwa mishale ya sumu na Mikuki ktk kupambana na wizi wa mifugo. Hapo hakuwa askari polisi hata na waikoma wakiuawa walipokuwa wakifuatilia mifugo yao kuikamata kuirudisha nyumbani. Sio tu serikali kuonea-Sisi wenyewe tunabaguana na kuoneana kichizi. Ila kamakila mtu atazingatia sheria, maadili na kukaa kwake afanye ya maendeleo yake bila bugdha kwawengine-hakutokuwa na haja ya kutumiapilisi kupiga watu. Huyo panya road wako anza kuwajibika nawe mwenyewe badala ya kumfuga na kutaka serikali imshughulikie. Akipigwa na watu wenye hasira auawe-muuaji afungwe wakati yeye naye ameuliwa mtu, ameporwa mali na mke na watoto kubakwa mbele ya macho yake na iliyowatokea hivyo kesi inachukua karne! Unaua!! Mama yangu anapigwa bakora nimuache aliyemchapa bakora shambani kwake-ninaweka mazao yangu shambani sumu ya panya mifugo ikijakula mazao inapukutika! nikienda police na mahakamani-kesi kaiendi wamepewa pesa-hawazingatii haki na sheria!! Tunajimaliza wenyewe. Kwa jinsi hiyo basi-Rais wa Ufilipino ameamua kuua wauza madawa ya kulevya ili kukomesha ujinga huo. Sisi hapa tunawaweka jela, kuwapa dawa ya kutuliza athari na kuwalisha bure! Na bado daily tunakamata wengine na toni za unga huo. wanajua hatari yake, inakatazwa na sheria kali lakini-Bado wanaendelea!
Wakati wa kampeni za ubunge jimbo la Mikumi-usiku baadhi ya wagombea wakifanya vikao vya siri na wafugaji kuwaahidi kuwapa wayatakayo wakipewa kura. Utakuta viongozi wanapewa mifugo halafu wafugaji wanaichunga na kuingia mahala pasiporuhusiwa. Wakiulizwa wanasema-hii ni ya kiongozi fulani. Ndio maana unakuta-hawachukui hatua na wanaokiuka sheria kwani vitambi vyao baadhi yao vinatokana na rushwa in cash and inkind ndio maanakutoamatamko hawataki. Baadhi ya vituo askari wa chini hawaridhishwi na kiongozi wa juu kwa kuwa ni mla rushwa hivyo wao hujiamulia wenyewe wanapoona utata bosi wao hataki kuutatua.
Tabia ya bongoland ya Kauli mbiu ndio utendaji uwepo kama vile suala hilo ni geni! Nchi ya Viwanda ina ugeni gani, au kujiajiri ufanye kazi ni geni? Kufanya mazoezi mpaka uambiwe pia usafi uondoe taka zinazoziba mifereji ya maji pamoja na maji kufurika mpaka kitandani kwako ;lakini bado uambiwe kwa kauli ya Rais. kampeni za mtu ni afya, kazi ni uhai, kial mtu afanye kazi, ulinzi mazingira panda mti ndio ukate mti na mambo mengi sana nchi hii-Sera, Mikakati yake hakuna mfano-utekelezaji tu ndio tata na Unduma kuwili kibao!
Watoto wa shule kuna elimu rika, wanaelimishwa mpaka vipindi vya TV kuhusu ubaya wa mimba za utotoni na vipeperushi, mabango yanagawiwa na gender NGOs. mnatoka semina za stadi za maisha barabarani music unalia-wanacheza matusi ya nguoni barabarani! Katika siku ya Wanawake Duniani-kituko mbele ya mkutano wa hadhara mshehereshaji kupiga nyimbo kukaribisha watu kucheza-wanawake watu wazima hawakuinuka kucheza bali wanafunzi wa sekondari ba chuo cha ufundi-aibu watoto wakike walivyokuwa wakicheza mbele wa wageni waheshimiwa, wazazi wao na watu wengine-viuno mpaka kukaa chini. Fedhehakubwa. Simu walizokuwa nazo wakitumia kupiga picha ni zile za bei kali sana! hawajui nini na wanaona athari kwa wenzao waliofikuzwa shule. wanapata mafunzo shuleni kuliko wazee wa zamani wao wliyapata jandoni wao kona zote wanasoma ubaya na uzuri wa hili na lile. Ni sawa na wale wa Jangwani-maji mpaka juu ya paa kila mwaka anapata athari mbaya eti bado anataka aelimishwe ubaya wa kuishi bondeni. Lakinipia-kazoea kuishi hali ya namna hiyo!
Hebu angalia zonal livestock units, vyuo vya kilimo na vijiji ambako wana mashamba ya mfano. angalia juhudi za miradi ya extension kuanzia Training and Visit System kama approach ya ukulima bora unamuelimisha darasani kisha kumuoonyesha shambani mashamba ya mfano na zawadi kwa wakulima bora, mpaka bustani za kata na mashamba ya ujamaa ya vijiji; mpaka ikaja Shamba Darasa la vikundi wanalima bustani za mfano mpaka kuvuna halafu kila mmoja anatakiwa kufanya hivyo shambani kwake, vijitabu, picha na kwengine video zinaonyeshwa. Wakitoka hapo wanaiga-imeishia hapo hapo na akilima mwaka huu kama alivyofundishwa-haendelei tena mwaka kesho eti inachukua muda sana unapotea. Lakini mavuno anapata haba na anataka msaadawa chakula! Ndio maana wengine tunaona -badala ya mapigano na wananchi-sheriakali itekelezwe kilimo na ufugaji na uvuvi endelevu iwe sheria badala ya mapambano. Hakuna vibali vya mbao, mkaa kama mtu hana shamba lake la miti. No kibali cha nyama ya punda kama mwekezaji wa nyama hiyo hana ranch ya mifugo hiyo-punda. Ukiwawekea namba za nyumba, huduma na kukufanya kodi kutoka kwa hao walihamia mabondeni-unarasimisha uwepo wao. Usiweke huduma ya aina yoyote au kukusanya kodi bali BOMOA makazi yao!! Pale mtu alipo rasmi au kisheria-achangie huduma husika-miongozo ipo mizuri ay kila sekta kama ni Maji, Mifugo, Kilimo etc. TASAF ipo mnachangia Bwawa au mradi wa Maji na Jumuiya yenu ya Watumia maji inasimamia mradi wenu; wahudumu au volunteers wa mifugo, wakilimo, Village Health Workers, mafundi maji wa vijiji (village water technicians) wanafundishwa. Hakuna lisilokuwepo bongoland! Utekelezaji umefanyika wa mambo mengi lakini uendelevu ndio NIL kutokana na tamaa binafsi, undumakuwili ktk tabia zetu na miono ya umimi na tumboni street kwa raia wa kawaida, wasomi wanasiasa na wamaofisini! Tupo nyumba kutokana na hulka zetu. Ndio unaona eti-Rais kasema, tunatekelewa wito wa Rais na kulaumu uongozi wote uliopita.
Ameanza baba wa Taifa hakuna alilobakiza kuongoza na la kusema-Tupo pale pale. Mpaka liberalization of the Economy wakati wa Mh Mkapa tumepewa ardhi na hati kujenga viwanda na mikopo juu-Tumefanya maeneo yard za magari, karakana, kujenga nyumba za sherehe na shule international. Tanganyika packers ipo wapi? Canvas Industry ya morogoro ipo wapi? Majengo ya viwanda tumeweka frame za biashara tumepangisha! kisha tunakimbilia kuleta vipodozi haram na tunajua vinakatazwa na tunaleta kuharibu taifa! Biashara za mitumba tunajaza hapo kiwandani magunia kibao na used cars ndio yard yake. Ukifirisiwa mali ulipe deni-unajipiga risasi!
Huyo mtu mzima ndio anachukua mahari mtoto wa miaka 12 aolewe asiende shule, ana nyumba anapangisha mashoga, anaficha wahamiaji haram. Mama mtu mzima ndio anacheza ngomamatusi yanguoni anaitwa "Chura" eti mpaka serikali ikataze Chura! Mume, baba, ndugu wa damu, mama, majirani-wanashangiliaChura na kumtunza. watoto wapo wanamwangalia mama anacheza chura hadharani! halafu wanawake-Tunadai haki sawa ila jukwaani tupo na vichupi wanaume wamevaa kamilifu. Tunagojea tusombwe na serikali kama hao wabwia unga halafu-Siasa itaingia-Tundu Lissu kuja kuwa wakili kuikomoa CCM kwani mtu ana haki ya kuvaa na kucheza atakavyo. Chura si kosa-Siasa ndani against maadili ya kiafrika!
Sisi tu watu wa ajabu, hata ajapo huyo Mnyarwanda, Burundi, Mkenya-tunamuabudu-tunamwoza na kumpa ardhi, tunamchagua kuwa kiongozi wa kijiji, tunamtafutia makaratasi ya uraia daily tupo kwake kujipendekeza na kuombaomba-wanatucheka!
--------------------------------------------
On Fri, 10/3/17, 'lucas haule' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] MWIGULU: MWENDENDO HUU WA POLISI, UNAKUHITAJI KUFANYA ZAIDI.
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, 10 March, 2017, 8:09
Hakuna nchi iliyofanikiwa
kwa ulinzi ulinzi wake wa ndani kwa kutumia mitutu ya
bunduki au ukali na ukatili wa askari wake.Ulinzi
ni mfumo na siyo mabunduki na maderaya, mfumo huu hujengwa
kupitia mila na desturi zetu, pale tunapo jenga stadi za
maisha taratibu hupenyesheshwa mambo haya.Yale
yote tunayoyaona sasa, ni zao la kizazi fulani katika jamii
yetu.Tumeibuka
na katabia ka hajabu sana sasa hivi, tunakwepa kujadili kitu
husika na kukimbilia kutaja tuliyokuwa tumeyahifadhi
moyoni.Jamii
inajengewa ubaguzi ( kiafya, kielimu, kiuchumi, kitabaka,
kikabila, kikanda,kicheo, kivyama, kirika
n.k.)Watoto wetu hawajui mipaka yao( wanasubiriwa
wakosee ndiyo wakanywe na mambo kama hayo)Mtindo
wetu wa kurekebisha/ kukosoana umekosa upendo ( imekuwa ni
uadui, kutiana aibu-- yaani hatuja acha kuimbiana kikojozi
kakojoa na ngua kaitia moto)Hatuna
sera ya kitaifa tunayoweza kusema wote tunaelekea huko( tuna
sera za vyama au za watawala kwa vipindi vyao, hata
ukiwauliza mbona unau au kukandamiza wananchi, watakwambia
sisi tuna nafuu sana, angalia rwanda, uganda? Sasa sisi
tunaishi kusudi tuwafikie hao kwa ukatili na kuhadhri UTU?
)Matatizo
madogo madogo ya wafanya kazi, wakulima, wafugaji, wafanya
biashara hayashughulikiwa kwa ufasaha na kwa wakati. (
yanakuja kushughulikiwa kidharula)Wanasiasa
wenye upeo mdogo au hawajui siasa( wapo tayari wakati wa
kampeni kuunga mkono makundi haramu)Sisi
siyo watanzania kamili na wala siyo wa hayo mataifa mengine(
tunaigaiga tu, mara china, mara India na singapol, mara
umarekani- Uchumi wa kibepari, siasa ya ujamaa, elimu ya
kijima)Watu
wazima/wazee, viongozi wa dini, viongozi wa nchi, viongozi
wa michezo na wengine. Hawana aibu ( Viongozi wa dini wapo
kwa ajili ya kuendesha ibada za mazishi tu, viongozi wa
kiserikali wanajitahidi kufuta historia za watangulizi wao,
bila kujali uzuri au ubaya wa hizo historia, wa vyama vyote
na michezo, hawajiamini, wanajilinda na kilekisichokuwepo,
wanabadili sheria zao kila kukicha, walafi, hawafii itikadi
zao)
From: 'Hildegarda
Kiwasila' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
To:
wanabidii@googlegroups.com
Cc:
Wanazuoni@yahoogroups.com
Sent: Friday, March 10,
2017 7:25 AM
Subject: Re:
[wanabidii] MWIGULU: MWENDENDO HUU WA POLISI, UNAKUHITAJI
KUFANYA ZAIDI.
USA
kwenyewe pamoja na demokrasia tunaona katika TV-CNN
wanabondana na police. Wanaandamana kumpinga Trump lakini
kama inavyotokea bongoland-wanavunja maduka na kuiba (watu
weusikibao ktk kuvunja maduka hayokama tulivyo hapa bongo!).
Nani haoni hii ktk TV? Wanapigana na police na police kuua
au kuuawa. Police amevaa vivalo utadhania ni jeshi la
taifa kama JWTZ kwetu, wana mbwa waliofundishwa jinsi ya
kumkamata mtu wanamkamata, wana magari mazito ajabu kama ya
kivita ila ya maji ya washawasha wanawamwagia wanaoandamana
wasiotii sheria. Tunaiona hii pia ktk mitandao ya magazeti.
Iiatoke si USA pekee na nchi za Europe lakini USA ndio
kiboko. Na wapo police wanaoua kiuonevu mfano mauaji ya
black people. Kesi hizo zinaonekana kwetu pia.
Inashangaza TZ-wananchi
wanapovamia na wanapochoma kituo cha polisi kumtoa
mtuhumiwa, kuua polisi- wananchi sisi hatuandamani. Wakulima
Kilosa na Moro Rural wanavyopigwa mapanga na kuuawa ila
wakimuua mfugaji ni issue mpaka magazeti ya ulaya. Ila
wakilosa-wafe tu! Bibi kalima mashama yake miaka 70 leo hii
anakuja kuchapwa bakora asifukuze mifugo isile na kesi zipo
kibao haziendi wala fidia ya kuchapwa na gharama zao za
matibabu hawalipwi!
Mume kafa Mikumi (babu mtu mzima) kwa shock ya
mkewe (bibi mtu mzima) kubakwa shambani akifukuza mifugo
isile mpunga wake. Morani katorokea police station (rushwa)
bibi kilema hadi leo mume alipoambia kuhusu bibi kulazwa St
Kizito kwa kubakwa akifukuza mifugo-kapata shock akaanguka
na akafa. Fidia ipo wapi. Hakieleweki hadi leo!
Waliotoa taarifa za
ujambazi wanapofuatwa na majambazi husika au ndugu zao,
washirika wao hukatwa mapanga na kuchomwa moto kuuawa au
kuumizwa-Mbona hatuandamani kamwe kama ile ya Ulimboka
kuweka semina, makongamano kujadili haya kama inavyokuwa hao
ambayo hufanywa kisiasa?
Game scout
ndani ya wildlife protected area wanapolinda na kufukuza
wavamizi humo hukuta wahusika hao wana mishale ya sumu,
mikuki na silaha kali za kivita kuliko walizo nao askari hao
wa wanyama pori au wa protected forests. Wao wana SR au G3
wenzao wana LMG na mkanda mrefu wa risasi silaha walizonunua
toka wakimbizi na ujambazi mwingine. Akijihami game scout
aue raia hao-maandamano, media lawama juu kwa serikali,
makongamano donor funded hapo ndio NGO hupata ulaji!
Wakikamata wanaolima
bhangi humo, kulima mazao na kujaza mifugo na kuipeleka
mifugo vituo husika na wakifuatiliwa na husika askari hao
kupigwa vibaya-hakuna lawama ila lawama askari hao
wanapopiga raia kujitetea au kuua kutokana na hayo. Lazima
tuheshimu sheria pia sio kutetea upande mmoja tu.
Kama nchi hii inataka iwe
salama-ni kwa serikali sasa kuacha SIASA kutumia sheria.
Mwana SIASA anayetetea ujinga-atumbuliwe. Pamoja na kuweka
hela za mabasi na dreni sa mwendokasi, ndege za bombadier na
barabara za fast train etc-kipaumbele pia kiwe
katika-Participatory Land Use Planning Vijijini na
kukamilisha upimaji mijini na ramani zake. Pia, kuhakikisha
kulikopimwa zamani ramani inakaa sawa kwa KUBOMOA bila ya
FIDIA wale waliobadili mchoro kwa maeneo yao kwa kufunga
barabara, kuvamia public open land na ROW ya barabara, Reli.
Sheria kali iwekwe na kulazimisha sustainable fishing,
farming, livestock keeping iwe SHERIA. Na upande wa
uchimbaji madini yaaina yoyote mpaka mawe na kokoto, mchanga
Mining Act izingatiwe na Land Recovery ifanyike kwa lazima
na mchimbaji aliyepewa leseni. Hii itaepusha kuwepo na
mashimo ambayo watu huvamia, kujenga nyumba na mvua ikija
wanatesa watoto kwani mashimo yanajaa maji. Wengine
huyatumia kuyafanya sewage dumping site bila ya kuzingatia
viwango vya liquid waste stabilization pond.
Wizara ya Mambo ya Ndani
na ya Ardhi, Mali Asili na Mazingira wahakikishe kuwa vita
haitotokea kati ya Raia na Askari wa aina yoyote ile kwa
kuhakikisha Land Use Planning na kuwapa hati miliki wahusika
iliyopigwa chapa-Haihamishiki inakamilika na kupiga marufuku
migratory farming and livestock keeping. Kaa kwako utumie
ardhi yako kiendelevu. Hii itapunguza hayo ya kupigana na
wafukaji na kutumia muda mwingi wa kazi ktk kukata mazao
yaluyolimwa ndani ya misitu ya hifadhi pamoja na bhangi.
Kila mmoja TZ akae pale alipopewa ardhi na serikali au
aliporithi kutoka ukoo/wazazi wake au aliponunua na kupata
hati miliki. Mbona Ulaya wameweza sisi tuna ardhi kubwa sana
na matumizi hayajafika hata 50% ya arable land tuliyonayo?
Kulazimisha ufugaji endelevu ni mpaka kuwafanya wafugaji
wapande mahindi na majani ya lishe ya mifugo ambayo
huyafuata maeneo mbali mbali. Kama mahindi, kunde ni chakula
cha mifugo akila anatoamaziwa mengi-ktk ekari kumi za boma
laki panga ekari5 mahindi na majani ya mifugo badala ya
kuweka mifugo elfu 2 katika ekari 5 weka sustainable level
na walishe chakula na pumba za mazao uliyopanda na mabua,
vigunzi vyake watoe maziwa sana! Sio uhamehame-Kilosa,
Lindi, ndani ya vituo vya serikali vya kilimo na mifugo
upeleke vurugu kisha mkipambana na askari wa serikali iwe
sababu. Ulifikaje hapo? Serikali nayo isitake kufumbia macho
mambo yanayoonekana kwa kuitetea jamii yenye makosa. Mwisho
askari wetu watakaa tu kuangalia wakulima na wafugaji
wakiharibu protected areas, wakiuana kwa kuogopa
kuwa-akienda akitupiwa mkuki, akirusha risasi itaua mtu na
yeye kufungwa maisha! Hivyo-wakiona wataangalia tu,
wakipigiwa simu-watasema tunakuja-hawatotokea. Kama vile
inavyotokea barabarani na wafanya biashara ndogo ndogo.
Wanajua hawatakiwi wawe hapo, askari wakienda kuwaondoa
wanawarushia mawe kugoma kuondoka nao askari/mgambo hutumia
virugu. Kisha tunalalama-lack of democracy! Ndio wanawaacha
wanaanika na kutandika nguo, chupi an sidiria ning'inia
mpaka nje ya majengo ya serikali na porivate sector, viatu
vimetandazwa njia za waenda kwa miguu Independence Avenue
yote na mapishi marabarani mpaka kando ya barabara za kwenda
Ikulu! Waache usiwaonee wanaganga njaa!
Huu ndio wakati wa kujenga
nidhamu kila kona. wakati wa kulinda mazingiza ili tupunguze
athari za climate change; kuweza kuzalisha mazao ya
mashambani, mifugo na samaki ili kulisha viwanda. Utalii
ukue na sio kuachia mifugo na kilimo kinakua ndani ya
wildlife protected areas. Wanalima kiwango kikubwa sana
ndani ya NCAA na Loliondo. Wageni wafugaji na mifugo kutoka
Kenya wamejaa. IRA-UDSM wakurugenzi wake ndio waliokuwa
Chairperson wa Board ya NCAA wanalijua hili; Socio-economic
studies za NCAA za Planning for Conservation with
Development wamezifanya na hayo yamedhirika na pichaza
mashamba makubwa sio siri. Thesisza wanafunzi wa kwa mfano
UDSM Geography, IRA za conservation areas zipo na statistics
za wingi wa mifugo na ukubwa wa mashamba ndani ya NCAA;
evaluation ya benefits za kutoka NCAA, hoteli za ndani ya
Serengeti na awwekezaji zinaonyesha mafao zipo na
kinachoendelea na hao wafaidika ni kinyume na kinachotakiwa
katika ulinzi wa mazingira. Pamoja na miradi mingi ya
mazingira kila kona iliyohusisha wananchi kuanzia Pwani yote
hadi bara kwa misaada ya donors-bado uharibifu ni mkubwa
kwani sisi ni SIKIO la KUFA na kulalamika ndio TIJA, ukweli
kwetu ni Kivuri cha Giza ila uongo ndio Sifa. Kwa sasa tuna
Waziri ambae Culture ya Kabila lake ni Kiboko katika Ulinzi
wa Mazingira-ardhi, misitu, wanyamapori, maji! Na mifugo
kwao na kilimo vina sheria kali!! Sasa imebaki kula Dawa
tu akili zikae sawa-hatokubali uzushi na ujinga atazingatia
sheria za nchi. Mh Mwigulu ana akili timamu na anatoka jamii
ya wafugaji pia naye alifuga kuanzia utoto kachunga
ng'ombe! Sasa hapa Kazi tu. Kuwafunga hao askari walioua
si Kibali kuwa uovu na ujinga uendelee wa kuvamia usiko
ruhusiwa (mwananchi).
Wengine
hujifanya mchana wapo kijijini kwao wametulia. Lakini usiku
huvamia misitu kukata miti, kujaza malori na kusafirisha
magogo. Pengine hao askari waliovamia kijiji cha wafugaji
walilifuata hili. tatizo hawakutoa taarifa na kupata kibali
cha uvamizi. Viongozi wengine wa juu hupewa rushwa mpaka ya
mifugo wakamezea na kunyamazia mengi-atoe kibali cha kuvamia
eneo! Tuna kesi Mikumi Police Station ya Wakala wa TIGO
kufanya wizi wa Mtandaoni kuhamisha hela kutoka TigoPesa
ssimu ya muhusika kupeleka Airtel money na kufuta maelezo au
message zote ktk simu ya jamaa muhusika alipompa amsaidie
kutoa hizo hela. Vidhibiti vya Tigo, M-Pesa ilikotoka hela
vimepelekwa na zina mihuri ya ofisi husika kuonyeshahela
zilipotoka, kuingia na kuhamishwa na muda pia. Lakini Wakala
anapeta-anatoa taarifa zake za mkono ndio zinaaminiwa.
Ameshaibia hivyo wengi wasio naufahamu wa wapi pa kwenda
kuanziakuiba laki 3 mpaka milioni na bado anapeta
(Rushwa!).
Hivyo basi-wafugaji
wengine hutulia na mifugo mchana usiku huhana aukuisafirisha
kulishia mashamba ya wenzao kucha asubuhi wanarudi kijijini
kwao tuli wametumia. Iangaliwe-hata kama askari waliingia
kijiji cha wafugaji-kuna sababu tu lazima ambapo
haijagunduliwa! Maeneo ay Kilosa, Morogoro rural hukuta
wamelishia mashamba usiku na kuwafanya wenye mashamba kulala
porini/mashambani juu ya miti kulinda mashamba yao. Fikiria
vijana wa kiume, baba mwenye mke alale shambani mbali mpaka
mavuno (angalia picha ya wanavyokaa mitini usiku, nimeipiga
mwenyewe). Familia inaathirika kiasi gani kwa baba
kutokuwepo nao kwa usalama wao home?
Askari mwonevu kuchukuliwa
hatua ni safi kabisa. Mwingine atatakakulipiza kisasi
(askari) mahala pasipohusu kabisa kuonea pia ili apate
vijisenti toka mtu huyo ili amwachie. Mwingine anatafuta
sifa tu aonyeshe ubabe kwa kumbonda mtu kupita kiasi hata
kama amegoma kuondoka alipoambiwa afanye hivyo. Lakini
unapofika Mahakamani ukaanza maandamano hapo, kukosha magari
na kupiga deki mshitakiwa apite ulipodeki-ni nidhamu
potofu-Upigwe tu na utumbuliwe kama ni mtumishi wa Umma!!
ila tufahamu, tunapokuwa na maelewano madogo na walinzi kama
police, FFU kupigana nao, majambazi watatumianafasi hiyo
kuja kuwavamia kwani wanajua askari hao wakiitwa hawatakuja.
Halafu ni kulalamika eti simu zilipigwa hawakuja au
zilizimwa hawapatikani. Unapochoma kituo cha polisi-unachoma
mpaka faili za kesi za nduguzo na jirani zako! halafu
ukiporwa njia jina panya Road unakwenda wapi na kituo cha
polisi umekichoma na kupiga askari? Kuna haja ya kujenga
upya nidhamu binafsi ya Raia wa Bongoland au sisi wa TZ.
Mapigano na askari na
mauaji yaja-serikali itakapoanza kuvunja majengo
yaliyojengwa mabondeni na katika right of way ya barabara,
nguzo za umeme, open space zake mijini na vijijini. Iandae
JWTZ kusaidia police. waandae maeneo ya magereza ya
kuwapeleka raia haokulala na kuamka kufanyakazi za kuzalisha
mali huko badala ya kuwaacha wajenge vibanda mabondeni
kachumba kamoja familia yote kulala humo kuongeza jamii
yenye utovu wa maadili!! Jenga nyumbaza manamba kwa kutumia
NHC bosi Mchechu anayaweza ajenge ktk mashamba ya mamlaka za
serikali (minazi, sisal, cotton farms) ili watakaovunjiwa
wasio na ajira mjini wakalime kuzalisha mazao ya kulisha
viwanda tufikie uchumi wa viwanda!!
Kama Kawa
--------------------------------------------
On Thu, 9/3/17, 'ELISA
MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Subject: Re: [wanabidii]
MWIGULU: MWENDENDO HUU WA POLISI, UNAKUHITAJI KUFANYA
ZAIDI.
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, 9 March,
2017, 12:25
Koku. Angalia hoja ya
msingi kwenye
original
article. Hii ninamjibu Emanuel na ukweli amehoji
pembeni mwa hoja ya
msingi inayojadili technical na
discipline aspects of the police when handling
the two
issues in
question. Ukiijadili kama Emma anavyoileta
utaingiza watu wengi wa
kujibu na kujitetea badala ya
waziri, RC, RPC, DC OCD.
--------------------------------------------
On Thu, 3/9/17,
'Lutgard Kokulinda Kagaruki' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Subject: Re:
[wanabidii] MWIGULU: MWENDENDO HUU WA POLISI,
UNAKUHITAJI KUFANYA
ZAIDI.
To: "wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, March
9, 2017, 9:09 AM
Elisa
we vipi?
Tunaongelea
watoto/wajukuu zetu;
hata kama hawakuwa na kibali, ndo
wapigwe kama majambazi?
LKK
On Wednesday,
March
8, 2017 11:42
PM, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Unatwambia habari za
marekani nchi tajii ina
polisi wenye vyombo vya akiba nakadhalika. Wewe
uko
marekani
itafute historia ya
nchi hiyo. Katiba yao iliandikwa na
majenerali saba na
wakasema jimbo litakalopinga vita. Sisi
hatujafika hapo.
Unafanya lkosa kufikiri (acha kuandika)
kuwa demokrasia yetu
iwe kama ilivyo ya marekani.
Tungetaka
kuanzia walipoanzia je?
--------------------------------------------
On Wed, 3/8/17,
Emmanuel
Muganda
<emuganda@gmail.com>
wrote:
Subject: Re:
[wanabidii]
MWIGULU:
MWENDENDO HUU WA POLISI, UNAKUHITAJI KUFANYA
ZAIDI.
To: "wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, March
8,
2017, 11:34 PM
Polisi
hawana haki ya
kuzuia
maandamano in
a true democratic
country. Kuna maandamano yanaweza kufanyika
spontaneously,
hiyo ni
haki ya raia.Baadfa ya
ushindi wa Trump
Wamarekani katika sehemu
mbalimbali za nchi walimiminika
mitaani kuandamana.
Hawakuhitaji kibali cha
polisi.Simba
walipowafunga Yanga juzi mashabiki
wa Simba
wangeandamana
isingekuwa nongwa. Polisi
hawakuhitaji kuombwa ruhusa.em
2017-03-08 15:13
GMT-05:00
'ELISA
MUHINGO' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Walikuwa
na haki ya kuyazuia
kwa
sababu kabla
hawajaandamana
walihiyaji kutoa taarifa ya kuandamana ili
walindwe. Kama
mazingira hayaruhuzu
basi hawapati kibali na hivyo
hawaandamani. Sasa hawa
hawakupitia utaratibu
huo.
------------------------------ --------------
On Wed, 3/8/17,
Emmanuel
Muganda
<emuganda@gmail.com>
wrote:
Subject: Re:
[wanabidii] MWIGULU:
MWENDENDO HUU WA POLISI,
UNAKUHITAJI KUFANYA
ZAIDI.
To: "wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday,
March
8, 2017, 10:56
PM
Elisa,Hapo ndipo
tunapopishana. Polisi hana
mamlaka
yoyote ya kuzuia
maandamano ya raia,
hata wanafunzi.
Walichofanya
wanafunzi
wa Simiyu
ni haki yao kabisa
polisi
hawakuwa na mamlaka
ya
kuingilia
katina
kuwazuia.
Kazi yao ilikuwa
ni
kuhakikisha
kwamba
maandamano
yanafanyika kwa
amani
si
kuyasimamisha na kuyazuia. Ni
uvunjaji
wa haki
za
binadamu/raia.em
2017-03-08
14:27
GMT-05:00
'ELISA
MUHINGO'
via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Wakati
rais akiwaapisha
watendaji wake siku
moja hivi
karibuni,
aligusia mwenendo
wa raia kutoheshimu
vyombo vya dola.
Mifano aliyotoa
ni watu
kuitwa
Polisi wakaongozana na
kwaya
na wengine kuosha
magari. Nakubaliana na
rais wetu kuwa
vyombo hivi
vinahitaji
kuheshimiwa. Ukaribu wa watu
Fulani
na viongozi
wetu wa juu
kwa
sababu mbalimbali
ulitufikisha
hapo. Mtu mwenye
hela
alijua hata
akivunja sheria
hawezi
kukamatwa. Sasa
Tanzania hakuna mwenye
uhakika huo tena.
Ni
vibaya sana kwa
raia
mmoja
kujihakikishia hilo kwamba
hata
akimuonea raia
mwenzake
hakuna
taasisi ya
kumshughulikia.
Hii ndiyo huleta
watu
kuchukua sheria
mkononi mwao.
Njia nyingine na
muhimu
ya lazima kwa
vyombo hivi
kuheshimiwa, ni
vyombo vyenyewe kujiheshimu na
kuheshimu
nafasi zao.
Matukio mawili
hivi
karibuni
yaliyotendwa na askari
polisi
wetu ni mfano
mmojawapo
wa jeshi
hili kutojiheshimu na
kwa
kweli lisitegemee
kuheshimiwa hata rais
angeagiza.
Mkoani Pwani
Polisi
wamevamia
kijiji cha wafugaji na
kuanza
kuswaga ng'ombe
na
kuwapeleka
Polisi. Wafugaji bila
kubisha
wakakubali ng'ombe
wapelekwe. Lakini wakataka
ng'ombe hao
wahesabiwe ili ijulikane ni ng'ombe
wangapi
wanachukuliwa.
Polisi
hawataki.
Wanaamua kurusha risasi
na
kuua. Anakuja
Mkuu wa
Wilaya na
kukana kuwa askari hao
walikuwa
hawakutumwa katika eneo
husika maana sio eneo
lenye
mgogoro. Ni eneo
la
wafugaji.
Wananchi wanadai hatua
zichukuliwe kwa
askari hao. Hakuna hatua
zinazochukuliwa
Mkoa mzima, mpaka
waziri wa mambo ya ndani alipofika
ndipo
akaagiza askari
hao
wakamatwe.
Hebu tuone
viashiria
hivi; na
kama ndio mfumo tuone
kama
raia wa Tanzania
wako
salama
kweli:
1. Askari
anakwenda eneo lisilo
na mgogoro na
bila
kuagizwa na
wakubwa
wake wa
kazi, anakamata mali za
raia.
2. Raia
wanakubali lakini
wanataka kuhakiki
mali
inayokamatwa.
Askari
wanakataa.
Wanaamua kuua raia hao.
3. Mkuu
wa
Wilaya
anadhibitisha Polisi hao
wamefanya
kitendo cha
kihalifu; (kwa sababu
hawakutumwa huko
kukamata
mali za raia
hao).
4. Mkoa
mzima
ambao una Mkuu
wa wilaya, OCD, RPC
na
Mkuu wa Mkoa
hakuna
anayeona na
kutumia madaraka yake
kuwakamata askari
hao. Maana yake wako huru na wanaweza
kufanya hivyo
hata
kijiji
kingine.
5. Amri
ya
kuwakamata Polisi
hao inakuja kutolewa
na
waziri.
Hivi katika
mazingira
haya raia
wajione wako salama???
Tanzania
ina mokoa karibu 30.
Mikoa kumi ikipata tatizo
linalohitaji askari
akamatwe mpaka waziri aisungukie
yote?
Nataka Mwigulu
ajijibu
(asitangaze
jibu). Sisi tunataka
kupata
jibu kwa jambo
atakalolitenda.
Mwigulu kuagiza
askari
walioua
wakamatwe,
amemdhalilisha
RPC. Kumsheshimu
RPC
wake alipashwa
kumtimua kazi.
Nitatoa
mfano. Kuna
tajiri
mmoja
alijenga kituo cha mafuta
barabarani Mwanza.
Waziri Magufuli (alikuwa hajawa
rais),
akamwagiza
Mkuu wa mkoa
kukibomoa kituo hicho. Mkuu wa
mkoa
akakataa.
Magufuli
(Inasemekana) alimpigia simu na
kumwambia
Mkuu wa Mkoa
asikilize taarifa ya
habari ya saa kumi
atatajwa mkuu wa
Mkoa
mpya
atakayefanya kazi hiyo. Simu
ilipokatwa Mkuu wa
Mkoa (inasemekana) alikwenda
kusimamia
kituo kuvunjwa na kwa
masaa kilikuwa hakipo tena.
Tunataka
tuone
kinachotokea
ambacho
inasemekana Mwigulu alifanya
(kwa
RPC) wake;
kama
Magufuli
alivyofanya kwa mkuu wa Mkoa
wa
Mwanza wakati
huo.
Kituko cha pili ni
cha
wanafunzi wa
Simiyu. Wanafunzi
wanasema
shule yao ilikuwa
inashindwa. Ameletwa mwalimu
kwa
juhudi zake
sasa
matokeo ya
mitihani yanaonyesha
mabadiliko.
Mwalimu huyo
anahamishwa. Wanafunzi
wakaamua
kuandamana.
Wamebeba
makaratasi. Polisi
wakaja kuwazuia wasiandamane.
Ni
haki kabisa
kuwazuia.
Ilitarajiwa Polisi waweke ukanda
na
kuwatangazia
wasimame
hapohapo na
kuwahoji wanataka
nini.
Sasa wanakuja na
zana
kana kwamba
watu wanauana na namna
ya
kuwatawanya ni
kuwavurunda.
Zimetoka picha
mtandaoni zikionyesha
Polisi
"wanamdhibiti"
mwanafunzi. Huyu anavuta huku, huyu
anavuta huko,
huyu
anapiga ngwara.
Mtu unajiuliza
Polisi
walikuwa wanafanya
nini
hasa? Nani
alikuwa anawaongoza
wenzake
kufanya hivyo? Huyu
mwanafunzi angeambiwa
"panda
gari hilo"
angepanda.
Angebisha
Polisi wawili
walitosha
kumshika na
kumlaza
chini na
kumuweka Pingu.
Ukiiangalia
picha hiyo hukosi
kujiuliza kiwango cha
elimu
kinachotolewa
kwa
Polisi wetu huko
chuoni! Kuna mtu aliwahi kusema
huwa
wanafundishwa
ukakamavu
na gwaride
tu. Ukilinganisha
picha
hizo na usemi huo
huwezi kumkatalia
aliyesema
wanajifunza
gwaride na
ukakamavu tu. Hakuna
busara ya
kuwashugulikia
wahalifu
inatolewa. Hakuna aina
ya maandamano na namna
ya
kuyadhibiti.
Hakuna
elimu ya
mahusiano na raia wema ili
kazi
yao iwe nyepesi.
Kuna
mtu anauza
viroba jirani yangu.
Mpaka
sasa najiuliza
nimwambie nani? Vituko
hivi ndani ya
makala
yangu sithubutu
kumwambia Polisi.
Nakubaliana na
mengine
yanayosemwa juu
yao.
Mambo haya
hayawezi kuacha
kutonesha
vidonda myoyoni
mwetu juu ya matendo ya
Polisi. Mauaji
ya
Mwangosi;
Kuburuzwa
ndani
Lipumba wakati amewambia
Polisi
kuwa
anakwenda
kuwatawanya watu waliokuwa hawajui kuwa
mkutano umekataliwa;
na
mengine mengi
tu.
Ninakumbuka
kusikia
radio
ujerumani wakielezea elimu ya
Polisi wao. Wanasema
Polisi akikutana na mtu amelala
barabarani cha kwanza
wanadhani ana kisukari, au kifafa
au
magonjwa
mengine, kabla
ya
kufikiri ni mlevi. Polisi
wana
vifaa vya
kupima
kuhakikisha
ana shida gani. Wa kwetu
watapiga mateke na
kusema ni mlevi. Mwigulu. Kati ya
mambo
ya kutopuuza ni
elimu
inayotolewa
kwa asiakri wetu.
Madaraka
na wajibu wa
Polisi
wetu. Lakini
niseme; Nitashangaa
kama
RPC wa Pwani
ataendelea
na
kazi.
Elisa Muhingo
0767 187 507
elisamuhingo@yahoo.com
--
Send
Emails to wana...@googlegroups.com
Kujiondoa
Tuma Email
kwenda
wanabidii+...@
googlegroups.com
Utapata
Email ya
kudhibitisha
ukishatuma
Disclaimer:
Everyone
posting
to
this Forum
bears
the
sole
responsibility
for
any legal
consequences
of his
or
her
postings,
and
hence
statements and facts
must be
presented
responsibly.
Your
continued membership
signifies that
you
agree
to
this
disclaimer and pledge
to abide by
our
Rules
and
Guidelines.
---
You
received this
message
because you
are
subscribed
to
the
Google
Groups
"Wanabidii"
group.
To
unsubscribe from this
group and
stop
receiving
emails
from
it, send
an
email to
wanabidii+...@
googlegroups.com.
For
more
options,
visit
https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send
Emails
to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa
Tuma Email
kwenda
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com
Utapata
Email ya
kudhibitisha
ukishatuma
Disclaimer:
Everyone
posting
to
this Forum bears
the sole
responsibility
for
any
legal
consequences
of his or
her
postings, and
hence
statements
and facts
must be presented
responsibly.
Your
continued
membership
signifies
that
you agree to
this
disclaimer
and
pledge to abide
by our Rules
and
Guidelines.
---
You
received
this
message because you are
subscribed
to
the
Google
Groups
"Wanabidii"
group.
To
unsubscribe from this
group and stop
receiving
emails
from
it,
send an email
to
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.
For
more
options,
visit
https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to
wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa
Tuma
Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com
Utapata Email
ya
kudhibitisha
ukishatuma
Disclaimer:
Everyone
posting
to this
Forum bears the sole
responsibility
for any
legal
consequences
of his or her
postings,
and
hence
statements
and
facts must be
presented
responsibly.
Your
continued
membership signifies
that you agree to
this
disclaimer
and
pledge to abide
by our Rules and
Guidelines.
---
You received
this
message because
you are
subscribed
to
the
Google
Groups
"Wanabidii" group.
To
unsubscribe
from
this group and stop receiving
emails
from it, send
an
email to
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.
For more
options,
visit
https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma
Email
kwenda
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha
ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting
to
this Forum bears
the sole
responsibility
for any
legal consequences of
his or her postings, and
hence
statements and
facts
must be
presented responsibly.
Your
continued
membership
signifies
that you agree to this
disclaimer and pledge
to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this
message because you are
subscribed to
the
Google Groups
"Wanabidii"
group.
To unsubscribe
from
this group and
stop receiving
emails
from it, send an
email
to
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.
For more options,
visit
https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma
Email
kwenda
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha
ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting
to
this Forum bears
the sole
responsibility
for any
legal consequences of
his or her postings, and
hence
statements and
facts
must be
presented responsibly.
Your
continued
membership
signifies
that you agree to this
disclaimer and pledge
to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this
message because you are
subscribed to
the
Google Groups
"Wanabidii"
group.
To unsubscribe
from
this group and
stop receiving
emails
from it, send an
email
to
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.
For more options,
visit
https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma
Email
kwenda
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this
Forum bears the
sole responsibility
for any legal
consequences of his or her postings, and hence
statements and facts
must
be presented
responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to
this
disclaimer and
pledge to abide by our
Rules and
Guidelines.
---
You received this
message
because you
are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from
this
group and stop
receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.
For more options,
visit
https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma
Email
kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha
ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this
Forum bears the
sole responsibility
for any legal
consequences of his or her postings, and hence
statements and facts
must
be presented
responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to
this
disclaimer and
pledge to abide by our
Rules and
Guidelines.
---
You received this
message
because you
are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from
this
group and stop
receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options,
visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email
kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone
posting to this
Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or
her postings, and hence statements
and facts must be
presented responsibly. Your continued
membership signifies
that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our
Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google
Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop
receiving
emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options,
visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email
kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha
ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her
postings, and
hence
statements and facts
must be presented responsibly. Your
continued membership
signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules
and
Guidelines.
---
You received this
message because you are subscribed to
the
Google Groups
"Wanabidii" group.
To
unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email
to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options,
visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email
kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone
posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal
consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must
be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to
this
disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this
group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options,
visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email
kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this
Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving
emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:
Post a Comment