Tuesday, 28 July 2015

Re: [wanabidii] Lowassa apigwa shinikizo kali

najaribu kuchangia hoja ya comments za Muhingo na Mollel, kwa mtazamo wangu hili halina shida kwenye siasa. lazima tukubali kwenda na mabadiliko. upepo wa siasa ndiko huko unakoelekea, lakini pia tujifunze na siasa za nchi nyingine. wakati Kibaki alipohama KANU Alisingiziwa ni fisadi lakini akashinda uraisi, na tunaona siasa za kenya zilivyobadilika baada ya changamoto za upinzani. maendeleo pia yamepatikana. Ugomvi wa ufisadi nchini sio wa mtu, ni tatizo la kimfumo. watu wengi hamtaki kelewa hili. Kwa hiyo tatizo sio Lowasa tatizo ni mfumo wa chama alichokuwapo kabla ya kuingia UKAWA. kama alikua ni fisadi kwa nini hadi leo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yake? sasa basi kama lowasa anahamia UKAWA ataendana na mfumo na sera za UKAWA ambazo zinagiga vita ufisadi wa kimfumo sio wa mtu mojamoja ili kuleta ustawi kwa watanzania. lengo ni kuleta mabadiliko ya siasa nchini kwa hiyo kama lengo la UKAWA ni kushika dola njia iliyotumika ni sahihi. The ends justify the means. Ndugu Muhingo inabidi upanue fikra kuendena na hali halisi ya siasa na kuelewa hasa maana ya mageuzi.
wasalaam
John





On Tuesday, July 28, 2015 9:55 AM, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:


Muhingo nakubaliana na wewe hata siku moja haki haichanganyani batili ukawa tuliipenda lakini mafisadi wameipenda zaidi
On Jul 28, 2015 10:00 AM, "'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
anzania ina mascientist wa ajabu. aweza kujaribu kumhamisha Sangara kutoka ziwa kubwa kama Victoria na kumuweka katika bwawa la kuchimbwa na kutarajia humo aishi na kuzaa sana. Kuna wanaojua kuwa Sangara akishaona jua basi. haishi zaidi ya masaa. Sasa tusubiri tuone wanasayansi hawa. Waliambiwa Lowasa hawezi kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera yake kuwania urais. Wakabisha mpaka wengine kuapa kuwa asipoteuliwa wafe. Wengine wakasema wanaoona kichefuchefu wale limau. Ikatokea. Sasa wanadhani CCM iliyomkataa itamruhusu auchukue urahisi kupitia mabwawa ya kuchimbwa. Nani kasema. Toka lini moja kwon geza moja ikazaa sita? Hesabu nyingine mbona rahisi. Jamani Watanzania wamechoka kubahatisha. Wamebahatisha ndani ya CCM wakafika mahala wakaamua hawatabahatisha tena. Tumaini lilikuwa UKAWA. CCM ikaona hilo. Najua kuwa kama watanazania wakitaka kubahatisha tena watabahatisha ndani ya CCM inayoonekanas kujua watanzania wamechoka nini. Watanzania hawajaichoka
 CCM. Wamezichoka sera zao za kuwavumilia mafisadi. Haiwezekani mafisadi wakakaribishwa UKAWA ikatarajia kuwa watanzania watasema sisi na ukawa. hapana. Wakati CCM inajipinda kuwatimua mafisadi UKAWA inadhani itaendelea kuwa UKAWA na mafisadi hao. Kifo cha UKAWA hakiwezi kuleta kishindo kama cha CCM. Hapana. Madereva tunajua. Ukikanyaga kuku wala gari haliyumbi. UKAWA inakufa
--------------------------------------------
On Sun, 7/26/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

 Subject: [wanabidii] Lowassa apigwa shinikizo kali
 To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: Sunday, July 26, 2015, 7:11 AM



 Kwa
 ufupi

 Washirika wake wataka
 maamuzi sasa, Mkewe, Rostam Aziz wadaiwa
 kumzuia.



 Shinikizo
  dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, la kumtaka
 akihame
 Chama Cha Mapinduzi (CCM) linazidi kuongezeka na katika timu
 yake ya
 ndani ni watu wawili tu wanaonekana kumtaka abakie ndani ya
 chama hicho.



 Habari
  za ndani ya vikao vya kujadili hatua za kuchukuliwa na
 Lowassa baada ya
  jina lake kukatwa kwenye mchakato wa kugombea urais kupitia
 CCM,
 zinasema kuwa wandani wake wanaamini kuwa hana atakachopata
 kama
 ataendelea kubaki kwenye chama hicho
 tawala.



 "Kaka
  sikiliza, inavyoelekea shinikizo dhidi ya Lowassa ni kubwa
 sana. Watu
 wake wa ndani wanataka aondoke CCM. Wanaona kama
 amedhalilishwa mno,"
 kilisema chanzo chetu ndani ya vikao
 hivyo.



 Chanzo
  hicho kilichoomba kutokutajwa jina kwa sasa, kilisema kuwa
 watu wake wa
  ndani wanaamini Lowassa akiendelea kubaki CCM atakuwa
 amewavunja moyo
 wale wote waliompigania, hasa vijana waliojaa matumaini ya
 kumuona
 akiongoza taifa hili.



 Wandani
  wa Lowassa wanaamini kuwa kama akiamua kujiunga na chama
 chenye nguvu
 cha upinzani anaweza kutimiza ndoto yake ya kuwatumikia
 Watanzania kama
 rais wa awamu ya tano.



 Chanzo
  chetu kinasema kuwa Lowassa mwenyewe amekwisha kuamua
 kufanya uamuzi
 mgumu, ila kuna msuguano juu ya namna ya kuondoka
 CCM.



 Taarifa
  zaidi zinasema kuwa watu wawili katika timu ya ndani ya
 Lowassa ndio
 wanaelekea kuwa na mawazo tofauti. Hawa ni Rostam Aziz,
 mwanasiasa na
 mfanyabiashara mashuhuri nchini na mtu mwingine
 anayetofautiana na
 mkakati huu mpya wa kung'oka CCM ni mkewe, Mama Regina
 Lowassa.



 Chanzo
  chetu kinasema kuwa wawili hao wanaamini mapigo ambayo
 Lowassa
 amekumbana nayo ni mengi na yanatosha, kwa maana hiyo
 ingefaa tu
 apumzike.



 "Sijui
  ni kwa nini RA (Rostam Aziz) anakuwa skeptical (shaka). Si
 unakumbuka
 ndiye aliyesema amechoshwa na siasa uchwara... sasa sijui
 kwa nini
 anapunguza makali," chanzo
 kilisema.



 Hata
  hivyo, vyanzo vyetu vinaongeza kuwa pamoja na upinzani huo
 Lowassa
 anadaiwa kuwa amekwisha kuamua na kinachosubiriwa sasa ni
 muda tu wa
 kutamka anakokwenda.



 Wakati
  hali ikiwa hivyo ndani ya kambi ya Lowassa, kuna taarifa za
 kuaminika
 kuwa kumekuwa na mashauriano baina ya watu wake na viongozi
 waandamizi
 wa kambi ya upinzani juu ya mwelekeo wake wa
 kisiasa.



 Mwandani
  mwingine katika kambi ya Lowassa alisema kimsingi yeye
 (Lowassa)
 amekwisha kuamua, anachofanya ni kuona kwamba watu wake wa
 karibu
 hawadhuriki na uamuzi wake huo.



 Chanzo
  hicho kiliiambia NIPASHE kuwa wenye msimamo mkali katika
 kambi ya
 Lowassa wanaamini utabiri wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
 kuwa upinzani
  utatoka ndani ya CCM utatimia mwaka
 huu.



 "Mnakumbuka ya Mrema
 (Augustino) alipoondoka CCM siasa za Tanzania zilibadilika
 mpaka leo? Sasa safari hii ni zaidi,"
 alisema.



 Takriban wiki mbili sasa,
 Lowassa amekuwa na jambo kubwa moyoni analitaka kuwaambia
 Watanzania.



 Mara
  ya kwanza alikuwa afanye mkutano na waandishi wa habari
 Julai 13 mwaka
 huu mjini Dodoma majira ya asubuhi, lakini mkutano huo
 ukahamishiwa Dar
 es Salaam ambako pia ukaahirishwa kwa muda
 usiojulikana.

 Tangu wakati huo kumekuwa
 na tetesi kuwa alikuwa atangaze kujiondoa
 CCM.



 Lowassa
  ni miongoni mwa makada 38 waliojitosa kuwania kuteuliwa
 kuwa wagombea
 wa nafasi ya urais wa CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika
 Oktoba 25,
 mwaka huu. Hata hivyo, jina lake halikuwamo katika orodha ya
 makada
 watano waliopitishwa kwenye vikao vya juu vya chama hicho
 ambavyo
 mwishowe vilimteua John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais
 atakayekabiliana na wagombea wa upinzani katika uchaguzi
 mkuu huo.



 CHANZO:
 NIPASHE



 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


No comments:

Post a Comment