Monday, 4 August 2014

Re: [wanabidii] VIONGOZI WA UKAWA WANAZIDI KUKATISHA TAMAA

Ndugu Kipamila unatania au ndo umetoa hoja hizo toka moyoni?
Kutokuwepo kwa Ukawa bungeni ni tatizo kubwa sana kwa mtu anayejaribu kuangalia ustawi wa nchi yetu kwa leo na siku zijazo. Katiba ya nchi si katiba ya Vikoba. Umeanza kwa kuuliza swali zuri sana kwamba kama hakuna litakaloharibika basi tuachane na UKAWA wabunge waliopo wa CCM watengeneze katiba.

Nakukumbusha kitu kimoja kwamba aliyedai katiba mpya si CCM ni upinzani na hapo mwanzo CCM kama CCM walikataa wazo hilo ila cha kushangaza ghafla bi vuu rais akakubali mchakato wa kutengeneza katiba uanze. Mimi na wewe hakuna ajuaye ni kwa nini alibadilisha mawazo na kukubaliana na wapinzani. Yawezekana ni shinikizo la wafadhili au janja fulani ili kuwaridhisha wapinzani kwamba kuna mabadiliko kumbe ndo katiba iendelee kujichanganya zaidi.
Umenichekesha sana ulipoandika maneno "Naungana kwa asilimia 100 na wabunge waliobaki bungeni kutengeneza katiba itakayo mpa heshima rais na itakayobariki wabunge kuwa mawaziri, Mungu libariki bunge la katiba liendelee kwa amani bila matusi.

Hapa ndo swali lako linajibiwa kwamba kwa wabunge waliobaki kutengeneza katiba itakayompa heshima rais haiwezekani hata kidogo uelewe kwamba tayari wabunge hao wa CCM tayari wamekwishapioshana na maoni ya wananchi kwa kug'ang'niza kuingiza muundo wa serikali 2. Ndugu yangu Kipamila unataka wanasiasa wafie kwenye ofisi za serikali kwa kutokuwa na ukomo wa kugombea? Nchi yetu ina wasomi wengi sana hivyo hatuitaji mbunge mwenye hati miliki ya jimbo. Mbona urais una kikomo? Kwa nini udiwani na ubunge visiwe na ukomo wa muda?  Kwa wajumbe waliobaki kwenye BMK kutengeneza katiba hatuitakii mema nchi yetu na wala haitampa heshima rais wetu


2014-08-04 11:53 GMT+03:00 'Fred Hans Kipamila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Kwanini tunawataka ukawa walejee bungeni, wasipoingia wao bunge haliwezi kuendelea? Na kama hivyo ndivyo mbona halikusimama pale tu walipoondoka bungeni? Ikiwa hakuna kitachoharibika kwanini tusiachane nao tukaendelea na mambo yetu bila wao kuwapo na katiba mpya kwa ajili ya watu wetu ikapatikana. Hivi katiba hii tunawatengenezea ukawa au watu wetu walitupa ridhaa ya kuliongoza taifa hili kwa kishindo kama siyo kimbunga. Hakuna sababu ya kuhangaika na ukawa mbona kwenye bunge la bajeti walitoka na bajeti ikapitishwa kinashindikana nini hapa kwenye bunge la kaitba hadi tunawabembeleza hivi, hawa ni akina nani hasas? Tunababaishwaje na Lipumba ambaye amegombea urais mara zote tangu kuanza kwa vyama vingi bila mafaniko, ananini jipya kwenye bunge la katiba hadi tumuogope, je anatubabaisha Mbatia ambaye hata ubunge amepewa kwa huruma ya JK tu, anan nini jipya? Je, tunahahgaishwa na Mbowe ambaye hata alipogombea urais kwa kuruka na helikopta hakuambulia
 chochote cha maana, ana kipya gani safari hii?
Tieni jamani kwa moyo mmoja tukatengenze katiba kwa ajili ya watu wetu tuachane na ukawa, hawana jipya hawa wanataka kupitisha rasmu isiyo na mashiko hata kidogo, katiba gani inayopunguza idadi ya mawaziri kutoka 60 hadi 15? wanataka sisi tukale wapi wamejaa wivu hawa, katiba gani inayohuburi mbunge asiwe waziri, heshima ya ubunge itakuwa nini si tutabakia kuwa sawa tu na madiwani? katiba gani inayotaka tutumikie majimbo kwa mihula mitatu tu, tuachane nao hawa wana wivu wa kike.
Katiba gani gani hii inayopunguza madaraka ya rais kiasi cha kumtaka akiteua wapendwa wake wakathibitishwe bungeni, hii si katiba hata kidogo.
Naungana kwa asilimia 100 na wabunge waliobaki bungeni kutengeneza katiba itakayo mpa heshima rais na itakayobariki wabunge kuwa mawaziri, Mungu libariki bunge la katiba liendelee kwa amani bila matusi
--------------------------------------------
On Mon, 8/4/14, 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

 Subject: Re: [wanabidii] VIONGOZI WA UKAWA WANAZIDI KUKATISHA TAMAA
 To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: Monday, August 4, 2014, 4:08 AM

 Kinachotakiwa ni kila
 mmoja wa pande yoyote ile kuona na kukubali kosa lake na
 kukubali uamuzi wa pamoja sio kila mmoja kutaka lake ndio
 liwe jibu bila kusikiliza wenzake. Pili, kama kila
 lililosemwa na Tume ya Katiba ndio jibu-kusingekuwa na haja
 ya bunge la katiba kwani si tume imeshaandika? Kuwepo na
 bunge la katiba ina maana kunatakiwa kusanifu na kuweka sawa
 baadhi ya mambo yaliyoandikwa na tume ili katiba ikamilike.
 Ubinafsi, ufahari, kutaka kuonekana, ubishi, uroho wa
 madaraka ndio unaotuletea vita Afrika siku hadi
 siku.Hata pale penye kila kitu mfano raslimali,
 asasi zenye madaraka na wataalamu bado kuna uzembe ktk
 utendaji na mambo yaliyowazi kabisa kukemewa. Haya na
 tumalize hayo mabilioni kwa posho na tuishie malumbano
 yasiyotija. Vikao vya usuluhishi vya kupoteza mihela, kuita
 washauri kwa
  mabilioni wakati kila kitu kipo wazi mikononi mwetu-kuacha
 ukawa, ukiwa, wehu wa madaraka na ubinafsi pande zote ili
 kufikia maridhiano.



     On Friday, 1 August
 2014, 21:18, 'Ngupula GW' via Wanabidii
 <wanabidii@googlegroups.com> wrote:



   Tatizo watu mnasahau,taifa lisilotenda
 haki,halisimama kamwe..haki huliinua taifa...na ndio maana
 kwangu mimi mtu asiyemjua Mungu hawez kuwa na hekima kwani
 hakuna hekima isiyotokana na Mungu..ngupula

  misangocharles via Wanabidii
 <wanabidii@googlegroups.com>
  wrote:

 Kinachokera
 katika mjadala huu ni watu kujifanya vipofu kutoangalia
 upande wa pili badala yake kuonesha ubaya wa ukawa tu. Nani
 alifurahishwa na mwenendo ule wa bunge maalum la katiba?
 Upendeleo wa waziwazi wa kiti, dharau, kejeli na matusi
 mazito! Haya hayasemwi! Mkoje ninyi watu? Sent from my
 BlackBerry® smartphone from Vodacom
 TanzaniaFrom:  "'Hildegarda
 Kiwasila' via Wanabidii"
 <wanabidii@googlegroups.com>
 Sender:  wanabidii@googlegroups.com
 Date: Fri, 1 Aug 2014 17:07:19
 +0100To:
 wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>ReplyTo:
  wanabidii@googlegroups.com
 Subject: Re: [wanabidii] VIONGOZI WA UKAWA
 WANAZIDI KUKATISHA TAMAA
 Hapa inaonekana nia ya
 masuala yao si katiba. wana lingine ndani ya kificho cha
 UKAWA na katiba. Waafrika sisi Mungu atupe nini? Kil;a mara
 nchi zetu ni ubinafsi, malumbano mpaka kufikia vita vya
 kuharibu nchi, kuua na kuharibu uchumi. hao wa Libya, Misri
 wamepata nini. Congo nako, Nigeria na nchi nyingine Africa
 utata mtupu.Mzuingu anafurahi kuona monkeys tunaendelea
 kuota na kukuza mikia yetu badala ya kushirikiana, kuelewana
 na kuleta maendeleo. Mmakonde kasema-Yonda ni Yonda tu
 mtupie tu ndizi!! Mungu tusaidie tufunuke tuache misifa na
 ubinafsi.



      On Friday, 1 August
 2014, 18:16, Leila Abdul <hifadhi@gmail.com> wrote:


  VIONGOZI wa vyama vya
 siasa vinavyounda Umoja wa Kataba ya Wananchi (Ukawa),
 wanadaiwa kumkatisha tamaa na kumvunja moyo Msajili wa Vyama
 vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, katika kufikia
 maridhiano ya pande mbili zinazotishia kukwamisha mchakato
 wa upatikanaji wa Katiba mpya.
 Habari za uhakika kutoka ndani ya
 kikao cha maridhiano kati ya wajumbe wa Ukawa na wajumbe wa
 Chama cha Mapinduzi (CCM), kilichokutana kutwa nzima ya jana
 katika hoteli ya Sea Cliff, Dar es Salaam, na baadaye
 kuthibitishwa na baadhi ya maofisa wa Ofisa ya Msajili
  waliokuwa eneo hilo la hoteli, zinasema wajumbe wa Ukawa
 wamekuwa ni watu wasioeleweka kutokana na tabia yao kuibua
 mambo
  mapya kila kinapoitishwa kikao baina ya pande mbili
 hizo.
 Kikao hicho cha
 jana kilichofanyika chini ya upatanishi wa Msajili
 waVyama, Jaji Mutungi, kinaelezwa kuwa cha nne
 tangu Msajili huyo aanzejuhudi za kuwaweka pamoja
 wajumbe wa pande mbili hizo za Ukawa na CCM, ili pamoja na
 mambo mengine, vikao vya Bunge Maalum la Katiba kwa ajili ya
 kutafuta Katiba mpya viweze kuendelea kama kawaida mjini
 Dodoma.
 Kwa mujibu wa
 habari hizo, kikao hicho cha jana kilitarajiwa kuwa kikao
 cha mwisho cha maridhiano katika juhudi hizo za kukwamua
 mchakato huo ili kuwapa wajumbe wa Ukawa, ambao pia ni
 wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, nafasi ya kujiandaa na
 safari ya kuelekea Dodoma kwenye vikao vya Bunge hilo
 vinavyotarajiwa kuanza rasmi Jumanne ijayo, Agosti 5, mwaka
 huu.
 Hata hivyo, hadi
 tunakwenda mitamboni jana, kulikuwa na taarifa za ndani ya
 kikao hicho zinazoeleza
  wazi kwamba hakukuwa na uwezekano wowote wa pande mbili
 hizo kufikia maridhiano baada ya Ukawa kuwasilisha hoja zao
 tisa mpya, badala ya hoja mbili ambazo ziliridhiwa na pande
 mbili hizo katika kikao kilichopita ambacho kilikuwa ni cha
 tatu, kwamba zingejadiliwa katika kikao jana na kufikia
 hitimisho la majadiliano hayo.
 Kwa mujibu wa habari hizo, hoja tisa
 hizo zilizowasilishwa na Ukawa katika kikao hicho cha jana,
 zilishajadiliwa na kufikiwa muafaka na pande mbili hizo
 katika kikao kilichopita, zikawekwa kiporo hoja mbili ambazo
 ndizo zilipaswa kujadiliwa jana kabla ya kufikia
 hitimisho.
 "Hawa
 Ukawa wanamvuruga tu Msajili kwa sababu hawaeleweki ni kitu
 gani hasa wanachokitaka…kwa kweli wamem-put off (kuvunja
 moyo, kuvunja nguvu) Msajili wa vyama vya siasa, uwezekano
 wa kufikia maafikiano na maridhiano ili tuweze kurejea
 bungeni kuendelea na mchakato wa kutafuta Katiba mpya ni
 mdogo sana,"
  kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya kikao kwa sharti la
 kutotajwa.
 Nje ya
 kikao hicho, baadhi ya maofisa wa Ofisi ya Msajili
 walionyeshakushangazwa na hali hiyo ya kutofikia
 muafaka,



 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment