Kwanza haya makampuni ya simu kama Voda ni wezi. wanatuibia wateja ni bora waongeze kodi kwao. Ninasema hivi ni wezi kwa sababu unatozwa hela kama umeweka wimbo fulani utapata message 26/6/2013 kwa mfano kuwa Ndugu Mteja mlio wako fulani umewekwa upya kwa siku 16 zijazo kwa shs 210. Ahsante kwa kutumia huduma hii. Unapata ujumbe kama huu 5/7/2013 suku 9 baadae wanakwambia umewekwa tena kwa siku 30 na umekatwa shs 400. Unapata tena tar 6/7 umekatwa tena shs 400 kwa siku 30. Fikiria kama watu 10,000 wamekatwa 400 kila baada ya siku 5 to 10 ni shs ngapi? Ni hivyo ukienda mfano shoprite. Change ikibaki pamoja na senti 20, 35 au 40 etc hii haipo huipati. Hawana hii hela lakini hawakaribishi vipimo vyao na gharama zao visiwe na visenti ambavyo hawawezi kutoa. Hivyo zidisha kwa mfano visentti hivyo kwa mwezi kwa wateja milioni 5 x sent 40 ni shs ngapi wapatazo. Serikali iwatoze wao wafanyabiashara sio sisi makabwela.
Ukienda sehemu nyingi za biashara hawama mashine za kodi wanaandika ktk kidaftari akikuuzia kitu maana kama ne cafeteria wamebeba maandazi, chapati kutoka watu tofauti. hata taasisi za umma, zina viduka, tea rooms ambazo zinauza kwa faida havina mashine za kodi. Wao wanatafuta rahisi kuwakata wateja na wafanyakazi kodi za kupatikana kiurahisi badala ya kuweka mfumo kuwa kila mfanyabiashara alipe kodi. Mbona ulaya imewezekana? Mbona wanakwenda kusoma huko wanaona mifano. Na mpaka tutakapoweza kudhibiti biashara barabarani, saluni, viduka kila mtaa, kila nyumba havijaandikishwa; kila uwanja kuna garage ambazo hutumia umeme, maji na mzigo wa takataka na hawalipii. Saluni ndio zinamwaga maji ya kemikali uwanjani-barabarani watu na hasa watoto watembeao bila viatu hukanyanga na maji kuingia pia kwenye bomba za maji ya kunywa ambayo daima yamepasuka na kuvaa mipira. Wanatia watu maradhi lakini hawatoa kodi kulingana na idadi ya wateja na hela alizolipwa. Bado hao wapishi wa masherehe wanaolipwa mamilioni lakini hawatozwi kodi. Kodi anakatwa kubwa sana mfanyakazi tu.
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, 7 July 2013, 11:40
Subject: Re: [wanabidii] Tanzania imposes TZS 1,000 monthly charge on Sim cards
Sent: Sunday, 7 July 2013, 11:40
Subject: Re: [wanabidii] Tanzania imposes TZS 1,000 monthly charge on Sim cards
| Yona Unaunga mkono mtu kufuata maji kwenye dimbwi badala ya Mto? Serikali ikubali kuwa Mwadui wanapata hasara na makampuni ya madini hawalipi kodi ianze kutoza kwenye simcard? --- On Sat, 7/6/13, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment