Ndyo maana nikacheka. Nilitamani habari za kamanda aliyekuwa akiagiza askari kubrush viatu wasiwe wachafu vitani ni nani na mambo mengine. Inahitaji kuhakikisha pia kama alikuwa Mkuu wa Mkoa muda gani baada ya vita na mambo mengine ambayo yangenogesha mada.
--------------------------------------------
On Sun, 5/22/16, Hosea Ndaki <hosea.ndaki@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Jenerali Kiwelu: Nilimnyima Sokoine siri za kijeshi vit
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, May 22, 2016, 10:59 AM
alienda
mto kagera kujenga daraja, anasema amin aliondoka mwenyewe
hapa kuna mapungufu ya habari, anasema wakati majeshi
yanavuka mpaka alienda makao makuu dar kuweka mambo sawa
napo kuna taarifa hazijakaa sawa, mwandishi awahoji na
wengine kama balozi mahiga na gen gemoghe.
2016-05-20 21:55 GMT+03:00
'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
He he he
he! Aya ya ya ya
--------------------------------------------
On Fri, 5/20/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Subject: [wanabidii] Jenerali Kiwelu: Nilimnyima Sokoine
siri za kijeshi vit
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, May 20, 2016, 8:28 PM
Asema katika Vita ya Kegara udhibiti wa mawasiliano na
taarifa ulikuwa wa kiwango cha juu.
Raia
Mwema: Hali ilikuwaje kule eneo la mapambano wakati wa
vita
ya Kagera?
Jenerali
Kikwelu: Kazi ilikuwa ngumu sana. Maana vijana wangu
waliokuwa
kule mbele, wale askari wa JWTZ walikuwa katika nusu
morali, maana
ukishatoka kwenye mstari wa mbele ukarudi nyuma morali
ya
vita
inapungua. Kwa
hiyo kazi ya kwanza ilikuwa kuwajenga
kisaikolojia.
Kazi ya pili ilikuwa ni kupata reinforcement
(kuongeza
nguvu) kazi ambayo niliyomwachia Ernest Mwita Kiaro,
hata
CDF naye
alikuja akakaa mahala fulani pale Bukoba (jirani), kwa
hiyo
Dar es
Salaam tulimpa kazi Mwakalindile ndiye aliyekuwa
anakaimu
kama Chief of
Staff, halafu Kiaro, chifu wa mgambo kazi yake ilikuwa
kukusanya mgambo
wote nchini, akina Mwakalindile ni kukusanya JKT, Polisi
na
Magareza,
wote walikuja kule.
Ninaposema
kulikuwa na changamoto kubwa sana
ni kwamba hawa askari hata siku moja hawakuwahi kuwa eneo
la
vita ama
eneo la mafunzo ya kivita kwa pamoja. Kwa hiyo, ilikuwa
kazi
kubwa,
ndiyo maana ikatuchukua muda pale kabla hatujaruka
daraja,
ilikuwa ni
lazima nifanye mafunzo ya pamoja ili kuwaweka watu
(askari
kutoka
Magereza, Polisi, Mgambo na JKT) waweze kufanya kazi
pamoja.
Lengo
ilikuwa kuondoa fikra za kitabaka vitani, kuachana na
mambo
ya
huyu mgambo au JKT. Kwa hiyo nilianzisha range ya
kupiga
silaha, mtu
unampa risasi kumi anapiga zote wash out (anakosa
kulenga
shabaha),
maana sisi (jeshini) tuna kitu kinaitwa bull, inner,
outer
n.k… sasa
huyu unampa risasi zote anapiga wash out, tunampa
nyingine,
akipiga ile
target namwambia umepiga bega (target hasa ni kifuani
kwenye
moyo au
kichwani) sasa wakati mwingine ukimpa risasi tano…
mbili
anapiga ndani,
nikasema sasa wameiva.
Kwa
hiyo ilikuwa ni mafunzo ya msingi. Kwa mfano, ukiwa
porini
na ndege ya adui inakuja ufanye nini.
Unaulizwa ukiona ndege ya adui inatoka kule wewe
unakwenda
wapi? Namna
gani mnaweza kusonga mbele, mnajihami vipi na namna
gani
mnaweza
kupumzika kwa sababu askari hawezi kupumzika chini ya
kivuli
cha mti.
Sasa baada ya mafunzo hayo ya pamoja, tukaridhika
askari
wetu wameiva,
tukaanza kusonga mbele kutoka Katoro hadi tukafika karibu
na
mpakani,
tukaweka kambi ambayo mpaka leo ipo pale, nyuma ya
Mtukula.
Raia
Mwema: Labda ungeeleza kuhusu Daraja la Kagera
kushambuliwa
na adui?
Jenerali
Kiwelu: Daraja hili wakati nimefika tu, kutoka kupewa
ile
amri
(ya kwenda vitani)… nimefika Kaboya, siku hiyo hiyo
jioni
nikatoka
kwenda kutazama daraja. Nikafika darajani upande wa
kulia
kama unakwenda
Mtukula umbali wa kilomita moja, nikaliona daraja
ambalo
baada ya
dakika 15 nikiwa pale likalipuka, kwa hiyo sikuweza
kuwahi
kuweka askari
pale darajani.
Wakati nafika pale na mtu mmoja anaitwa Kanali
Kitete tunatazama…nataka sasa kufanya mbinu namna
gani
nitavuka daraja
ili majeshi yangu yakae upande mwingine.
Basi
nikarudi zangu
Kaboya kwa ajili ya kuanza kufanya mkakati mwingine
maana
pale daraja
limekwishavunjwa, nikaripoti daraja limevunjwa…hakuna
daraja kuanzia
sasa. Ndipo tukaanza mipango mingine kuhusu daraja,
tukaleta
madaraja ya
muda na mtu mmoja anaitwa Brigedia Rajabu ndiye
aliyekuja
na vifaa
hivyo kutoka kikosi chetu cha uhandishi na tukamweka
sehemu
ya umbali wa
kama kilomita tano kutoka kwenye daraja, ndipo
alipofanya
mafunzo yake
ili baadaye kufunga daraja la muda.
Raia
Mwema: Ilichukua muda gani hadi kufanikisha daraja hilo
la
muda?
Jenerali
Kiwelu: Unajua kuna wanazungumza kwa ushabiki mambo ya
vita
tu
wakati hawajui chochote kuhusu vita, watu hawa mimi
nawaita
majitu,
hawajui maana ya vita. Wapo wengine wanafikiri jeshi hii
la
Tanzania
lilikuwa tayari kwamba unakwenda tu kwenye vita, sasa
ukiwaambia kwamba
jeshi hili tulipokwenda kwenye vita tulikuwa na
mchanganiyo
wa watu wote
hawa, halafu pia kuleta vifaa vya kuvuka daraja,
kuwafundisha namna ya
kuweka daraja, kuleta vifaru, ndipo wataona ugumu wa
kazi
iliyokuwapo.
Pale
ni lazima uwe na nguvu ya kutosha kuhakikisha kwamba
mkiruka
(daraja) hakuna kurudishwa nyuma. Kama nilivyotangulia
kusema wale
askari wetu waliokuwa kule awali, walikuwa wachache na
walivurumishwa na
adui kiasi cha morali yao kuwa chini kivita, kwa hiyo
ilikuwa ni lazima
nihakikishe sasa watu wangu ni imara, vifaa viko.
Tulikuwa
tunafanya mipango na ukaguzi pamoja na makamanda wangu,
akina Jenerali
Marwa, Jenerali Luhanga, Mayunga, Walden… tunakwenda
hadi
tunafika pale
kwenye daraja kwa sababu Idi Amin alirudisha majeshi
yake
(Uganda)
akiamini kazi imekwisha. Sasa tulikuwa na makamanda
wangu
hao tunakwenda
pale kupanga mikakati, lakini, swali kwamba wapi
tupite
(kuvuka daraja)
na lini sikuwaambia.
Hakuna
mtu aliyejua hata Edward Sokoine
(aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Mwalimu
Nyerere)
alikuja
akaniuliza …. sasa General nafikiri tumechelewa sana
kuruka (daraja),
sasa unaruka lini na unapitia wapi?
Nikamwambia
hiyo ni siri ya
kijeshi… akasema hata mimi? Nikamwambia ndiyo mzee.
Kwa
hiyo mimi
nilikuwa napita kando ya ule mto kwa gari hadi Murongo,
halafu watu
wanapiga mabomu kila sehemu lakini hawajui tunaruka
wapi
kupitia wapi..
.tuliweka watu (askari) hadi eneo la Kakunyu huku
Bukoba
Vijijini, kwa
hiyo kuna ambao walijua tunaruka kupitia huko. Hatimaye
nikaona sehemu
ya kuruka ni pale pale walipovunja (daraja), lakini
sikuwaambia
wapiganaji wetu.
Sasa
imefika siku ya kuruka, ndani ya saa 24.
Nikawaita makamanda wangu nikawaambia sasa inabidi
turuke
kwenda
kumshambulia adui, vifaa na kila kitu tayari, na askari
kama
tulivyofanya mafunzo wako tayari. Makamanda wakasema
tunangoja tu amri
yako, nikasema amri itatoka, wakauliza na kutaka
niwaambie
tunaruka
kupitia eneo gapi, nikasema nitawaambia.
Ilipofika
saa tano usiku
nikawaambia makamanda… Marwa utakuwa katikati,
Mayunga
ukiruka tu
unakwenda kushoto kuelekea eneo la Mbarara, Walden
ukiruka
tu unaelekea
eneo la Minziro, Luhanga ukiruka tu unafuata njia ya
Marwa
halafu
makamanda wengine watakuwa tayari kusubiri lolote
(reserve).
Baada ya
maelekezo hayo nikawataka waende kuwaambia askari wao
kwamba
tunaruka
leo (usiku huo), nikamwita Mhandisi Mkuu Rajabu na
kumwambia
utatandaza
daraja lako (juu ya mto) saa nane usiku…akafanya kazi
hiyo.
Saa
nane usiku mpaka kufika saa tisa kuelekea saa 10
(takriban
saa mbili
hivi mfululizo) vikosi vikaanza kuruka kwa mujibu wa amri
ya
operesheni
(operation order) ilivyotamkwa. Ilikuwa bahati mbaya
nilipoteza askari
mmoja tu pale wakati wa kuvuka daraja.
Baada
ya hapo tulifanya
mashambulizi, kazi ya kwanza ilikuwa ni kukamata eneo.
Nimeeleza kazi
niliyopewa nilitakiwa kurudisha heshima ya nchi hii na
heshima ya nchi
ni kurudisha mipaka yetu pale ilipokuwa awali na hivyo
tukahakikisha
tumefika Mtukula, wengine wamefika Minziro na wengine
mpakani na Uganda
kule.
Sasa jukumu la msingi la kurejesha mipaka ya
nchi likawa
limekamilika na Rais Julius Nyerere akaja kule na
akasimama
eneo lenye
kilima pale na tukamweleza kwamba sasa mzee kazi ya
kwanza
uliyotutuma
tumeimaliza, mipaka yetu sasa iko salama, akasema
vizuri
lakini huyu
"mshenzi" huyu ametuharibia mambo mengi sana si
bado
yuko kule (nchini
mwake), basi kazi bado haijakwisha.
Ndipo tukaingia hatua ya
pili, maana sehemu ya kwanza ya ukombozi wa nchi yetu
ikawa
imekwisha
ikafuata hatua hiyo ya pili ambayo ni kumwadhibu
adui. Raia
Mwema: Je, baada ya kazi hiyo ya kwanza kukamilika
ulirejeshwa kwenye nafasi ya Mnadhimu Mkuu (Chief of
Staff)?
Jenerali
Kiwelu: Pale kilichofanyika ni kwamba baada ya kumaliza
ile
kazi ya awali, tukaingia sasa kazi ya kuandaa na
kutekeleza
operesheni
ya kuvuka mpaka ambayo ni tofauti na opereshani ya
kumwondoa
adui
nyumbani kwako.
Sasa
unakwenda nyumbani kwake lazima uwe na
mkakati, sambamba na nguvu ya kutosha kwenda kwake, kwa
hiyo
rais
ikabidi afanye utaratibu wa kumtafuta kamanda wa
kuingia
Uganda, mimi si
ndiye niliyekuwa Chief of Staff na mkuu wa majeshi
akiwa
Twalipo ambaye
naye hayuko makao makuu, kwa maana hiyo akiwa huku
mbele
(vitani) kule
makao makuu hakuna maandalizi yoyote, nani anaanda
nini…
nani anafanya
nini.
Kwa
hiyo ilibidi nirudi Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam
na pale (vitani kuelekea ndani ya Uganda) nikamkabidhi
Msuguri, mimi
nakamwambia nakwenda (makao makuu) kukufanyia kazi ya
kuandaa vifaa,
wewe kazi yako ni kwenda ndani kumwadhibu Idi Amin.
Nikarudi
makao makuu
nilikuwa na mtu mmoja alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi,
Kanali Bakari,
basi tukafanya kazi na Bakari, tunkaenda hadi nchi za
nje
kutafuta
nguvu…. zana za kivita.
Wako
marafiki walitusaidia, sina sababu ya
kuwataja sana lakini kati ya nchi rafiki tulizokwenda
ni
pamoja na
Urusi, China, Korea na Bulgaria. Ikabidi tukusanye vifaa
na
ndipo hapo
wananchi walichangia mambo mengi sana, wapo
waliojitolea
magari yao,
vyakula, mifugo kama ng'ombe ili kuwawezesha
wapiganaji
wetu kule mstari
na hatimaye Msuguri akuvuka mpaka akiwa na uhakika wa
nguvu
za kutosha
na uangalizi huku nyuma anakotoka.
Raia
Mwema: Kwa wakati huo wewe
ndiye uliyekuwa makao makuu Dar, sasa uliwezaje
kudhibiti
link
(viunganishi vya taarifa) za silaha mlizopata kutoka nje
ya
nchi?
Jenerali
Kiwelu: Kwanza wakati nikiwa pale Kagera tulikuwa
tumedhibiti
sana uvujaji wa taarifa. Unajua kuna mkutano mmoja mkubwa
wa
kimataifa
ulikuwa unaendelea pale Arusha uliokuwa umehusisha nchi
nyingi huku vita
pia ikiendelea na hao washiriki wa mkutano hawakujua
chochote
kilichokuwa kikiendelea nilidhibiti uvujaji wa taarifa,
viongozi wengine
tuliwapa amri maalumu hakuna kufika kwenye eneo la vita
na
wala kupewa
taarifa yoyote, ni kama tulivyokuwa tunapambana
kuwasaidia
kule Msumbiji
siku moja tukakuta mzee mmoja wa kizungu kule Tunduru
anayo
redio
ameijichimbia ndani, kumbe alikuwa anawasiliana kwa maana
ya
kupeleka
taarifa, tukamkamata.
Hata pale Karagwe, tulikuwa na watu fulani
pale ambao ni kanisa fulani sitaki kuwataja nao pia
walikuwa
na redio ya
mawasiliano, ukiona utafikiri mtu anapiga kinanda
kumbe
anapeleka
taarifa, kwa hiyo tukafunga njia zote za mawasiliano,
nikasema hakuna
mawasiliano ya aina yoyote na taarifa zozote kwenda
Ikulu
nitapeleka,
tulihakikisha taarifa hazivuji vinginevyo tusingeweza
kuvuka
pale.
Raia Mwema: Vipi kuhusu Yoweri Museven (Rais wa
sasa wa Uganda), alikuwa sehemu ya mapambano?
Jenerali
Kiwelu: Museven yeye alitokea huku nyuma kapitia
Karagwe
kalala kijijini pale wakati Mayunga amekwishavuka
mpaka,
akaungana na
Mayunga, ukweli ni kwamba Jeshi la Tanzania na chini ya
Luteni Jenerali
Mayunga ndiye aliyekabidhiwa kazi ya kupita Mbarara na
kutoka hapo
kuelekea Kampala, na wengine wakapita Minziro kwenda
kuungana kule.
Museven hakuwa na jukumu la kuongoza ni kama alisaidia
mambo
kadhaa
yakiwamo masuala ya taarifa.
Raia
Mwema: Vipi kuhusu uteuzi wako kuwa mkuu wa mkoa?
Jenerali Kiwelu: Baada ya vita, tukawapokea
vijana kutoka Uganda pale
Bunazi, nikafanya kazi ya kuwasambaza na kuwarudisha
kule
walikotoka,
wengine Ruvuma, Kigoma na maeneo mengine ya nchi.
Tukahakikisha wamerudi
na kupewa haki zao.
Baada ya kumaliza pale Bunazi, nikarudi Dar
es Salaam kwenye kitengo changu cha Mnadhimu Mkuu, sasa
makamanda wote
wakawa wamerejea kutoka vitani. Ikabidi sasa jeshi
lipangwe
upya….unajua
watu walikwishaonja kutoa roho za watu huwezi kucheza
nao
hivi hivi,
ikabidi sasa tupangane upya.
Namna
gani jeshi litakavyoendeshwa
na kwa hiyo, Amiri Jeshi Mkuu akapanga upya…akasema
sasa
wewe bwana
umemaliza kazi hii nakushukuru…sasa nataka kukupa
kazi
nyingine…nikamwambia sawa, nipo tayari kwa kazi
yoyote,
akaniambia
utakwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, nikamwambia
naenda
lakini hii kazi
sijawahi kufanya sasa ukiona nafanya vibaya uniite, na
mimi
nikiona
kuna tatizo nitakuja.
Kwa hiyo nikaenda zangu Tanga ndipo wakati huo
yakafanyika mabadiliko, Twalipo akatoka pale akawa Waziri
wa
Ulinzi,
Msuguri akawa Mkuu wa Majeshi halafu na Jenerali Kombe
akawa
Mnadhimu
Mkuu, tukaendelea.
Raia
Mwema: Nini hasa unachojivunia katika wadhifa wako wa
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga?
Jenerali Kiwelu: Tanga kuna mambo mengi. Lakini
moja kubwa ni kwamba
pale Tanga wale Waswahili wangu wa Tanga ni wavivu,
hawakuwa
watu wa
maendeleo. Sasa walikuwa wanakaa pale kwenye nyumba zao
za
nyasi mjini,
nikawaambia sikilizeni hatuwezi kuishi hivi…mtu
lazima
afanye kazi na
mjiwekee kipato na mtengeneze nyumba.
Wakauliza tunatengenezaje
na hatuna mashamba kwa ajili ya kutupatia kipato?
Nikafanya
uamuzi,
nikaenda barabara ya kuelekea Muheza kuna mashamba ya
mkonge
pale na
hapakuwa na mtu anayelima, nikasema nitachukua haya
mashamba
na wala
sikuuliza ni ya nani.
Nikawaambia
nyie mtakwenda kulima pale na
kutakuwa na mabasi asubuhi na jioni ya kwenda na kurudi
shambani, na
kwamba wakishavuna watapata chakula lakini nikataka
watengeneze nyumba
zao na watoto wasome kwa kipato watakachopata.
Nikamwambia ofisa
husika apime viwanja, lakini nikawaambia nyumba zao
wasizivunje
isipokuwa wajenge kuta kwa kuzizunguka na baada ya
kufika
hatua ya
kupaua, wanaweza kuvunja nyumba za ndani yake za nyasi,
ndivyo nyumba
nyingi za Tanga zilivyojengwa kwa wakati huo.
Nilikaa
pale kwa
miaka nadhani mitatu tangu mwaka 1980 kisha
nikahamishiwa
Rukwa ambako
nako pia kuna mambo mengi niliyofanya. Uzuri wa Rukwa
watu
wa kule ni
wachapa kazi lakini tatizo lao walikuwa wanachapa kazi
bila
utaratibu.
Nikawaambia msilime tu mahindi ya kutosha nyumba yako
tu
bali limeni kwa
malengo ya kupata kipato. Nikawataka walime kwa
utaratibu,
wajue
masuala ya mbegu, maandalizi ya shamba.
Lakini
haikuwa kazi
rahisi kwa sababu ilibidi tutengeneze kitu kama shule
kijijini kwa ajili
ya kumfundisha mtu kulima, kuandaa shamba, kupanda,
kupalilia hadi
kuvuna, ni miezi minne…watano amevuna ameweka kwenye
kihenge, anakuwa
amefaulu. Sasa mtu anapokuwa anajifunza kulima alikuwa
akijifunza kilimo
cha kisasa, kupanda kwa mistari, kutumia mbolea,
kutumia
dawa za
kudhibiti wadudu na baada ya kuvuna, ajue namna ya
kutunza
mazao.
Sasa
katika kuandaa mashamba wengine walikuwa wanatumia
majembe
madogo
ya kukokotwa kwa ng'ombe na wengine majembe ya mkono,
uongozi ngazi ya
mkoa ilibidi tufanye utaratibu na tulifanikwa kwenda
kununua
majembe
kutoka Zimbabwe ya kukokota kwa ng'ombe na ya
kupandia.
Niliomba fedha
nikapewa za mbegu ambazo kule hakuna, nikaagiza mbegu
kutoka
Kenya
lakini hazikuwa zinatosha, nikaenda kwenye wizara (ya
kilimo) natafuta
mbegu nako hakuna.
Lakini
nikaona sio siku zote kwenda kutafuta
mbegu, nikaanzisha shamba la mbegu eneo la Mlundikwa,
mwaka
wa pili
tukawa sasa tunaweza kupata mbegu zetu na tukajua namna
ya
kuziweka
katika madaraja ya ubora.
Sasa
baada ya kuwa na uhakika wa mbegu
tukaingia hatua ya matumizi ya majembe ya ng'ombe,
tulipomaliza mwaka wa
kwanza na wa pili, ule mwaka wa tatu tukafaulu na
kupata
mazao mengi,
maana nia yangu pale ilikuwa ni kupata mavuno mengi ili
kushindana na
wenzangu wa mikoa mingine ya kilimo, na ikibidi hata
kuwazidi lakini kwa
manufaa ya watu wangu hasa katika kuongeza kipato chao
mara
dufu au
zaidi.
Raia Mwema: Kwa hiyo kuwapo kwako Rukwa
kulisababisha mkoa
huo kuwa miongoni mwa mikoa mingine mikubwa ya kilimo
kama
Mbeya,
Ruvuma na Iringa?
Jenerali Kiwelu: Kwanza mimi nikiwa kule
nilijua Mbeya ambako nilikuwa napita pale, Iringa na
Ruvuma
ndio
iliyokuwa mikoa mitatu mikubwa na mashuhuri kwa kilimo,
ikiitwa "The Big
Three". Nikasema hawa hawawezi kuwa Big Three na
mimi
napita mikoa yao,
changamoto yangu ya kwanza nikasema lazima niingie
pale
kwenye orodha
ya Big Three ili tuwe Big Four.
Raia
Mwema: Baadaye ulipelekwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera,
hali
ilikuwaje kule?
Jenerali
Kiwelu: Unajua ule Mkoa wa Kagera unafafana hali ya hewa
na
mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro na Arusha, mimi sehemu ya
asili ni
Kilimanjaro ambako mazao ni pamoja na kahawa na migomba
kule
nako mazao
ni hayo hayo, tofauti iliyokuwapo ni kwamba kule
Kilimanjaro
tulikuwa
tunalima kahawa aina ya Arabika sasa Kagera ilikuwa
nafasi
yangu ya
kujifunza kilimo cha kahawa aina ya Robusta, ikawa
lazima
niwainue wale
wakulima tuone tunafanya vizuri zaidi. Sasa kule kwa
sababu
wengi ni
wabishi kweli kweli wanataka lazima waone vitendo kwa
mfano,
ikabidi
niwe na shamba la mfano na hata sasa baada ya kustaafu
bado
naendelea na
kilimo kwenye shamba langu.
Chanzo Raia Mwema.
Maoni Yangu
Tumeeona
jinsi Generala Kiwelu alimvyomnyima Sokoine taarifa za
vita
kwa kumwambia ni siri ya kijeshi na Sokoine pamoja na
wadhifa aliokuwa
nao aliheshimu hilo hakutaka zaidi ya jibu
alilojibiwa.
Hivyo
basi wanasiasa wetu wa kizazi hiki waige mfano wa
Sokoine
kwa kuheshimu
vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kutotaka kila
kitu
kuwa wazi
ikiwemo eti kwa kuwa wao ni wabunge au wanasiasa wapo
kwa
niaba ya
wananchi hapo watakuwa hawavitendei haki vyombo vyetu
hivyo
kwani
vinafanya kazi kubwa ya kuhakikisha tuna kuwa na amani
pamoja na
uturuvu.
Hata huko Marekani na ulaya huwezi kukuta
wanasiasa
wanataka mambo ya jeshi na vyombo vingine vya ulinzi na
usalama kuwekwa
hadharani kama wa hapa kwetu wanavyotaka ili wapate
umaarufu
wa kisiasa.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly.
Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment