Sunday, 22 May 2016

Re: [wanabidii] Jenerali Kiwelu: Nilimnyima Sokoine siri za kijeshi vit

alienda mto kagera kujenga daraja, anasema amin aliondoka mwenyewe hapa kuna mapungufu ya habari, anasema wakati majeshi yanavuka mpaka alienda makao makuu dar kuweka mambo sawa napo kuna taarifa hazijakaa sawa, mwandishi awahoji na wengine kama balozi mahiga na gen gemoghe.

2016-05-20 21:55 GMT+03:00 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
He he he he! Aya ya ya ya
--------------------------------------------
On Fri, 5/20/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

 Subject: [wanabidii] Jenerali Kiwelu: Nilimnyima Sokoine siri za kijeshi vit
 To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: Friday, May 20, 2016, 8:28 PM


 Asema katika Vita ya Kegara udhibiti wa mawasiliano na
 taarifa ulikuwa wa kiwango cha juu.
  Raia
 Mwema: Hali ilikuwaje kule eneo la mapambano wakati wa vita
 ya Kagera?


 Jenerali
 Kikwelu: Kazi ilikuwa ngumu sana. Maana vijana wangu
 waliokuwa
  kule mbele, wale askari wa JWTZ walikuwa katika nusu
 morali, maana
 ukishatoka kwenye mstari wa mbele ukarudi nyuma morali ya
 vita
 inapungua. Kwa
 hiyo kazi ya kwanza ilikuwa kuwajenga
 kisaikolojia.
  Kazi ya pili ilikuwa ni kupata reinforcement
 (kuongeza
 nguvu) kazi ambayo niliyomwachia Ernest Mwita Kiaro, hata
 CDF naye
 alikuja akakaa mahala fulani pale Bukoba (jirani), kwa hiyo
 Dar es
 Salaam tulimpa kazi Mwakalindile ndiye aliyekuwa anakaimu
 kama Chief of
 Staff, halafu Kiaro, chifu wa mgambo kazi yake ilikuwa
 kukusanya mgambo
 wote nchini, akina Mwakalindile ni kukusanya JKT, Polisi na
 Magareza,
 wote walikuja kule.
  Ninaposema
 kulikuwa na changamoto kubwa sana
 ni kwamba hawa askari hata siku moja hawakuwahi kuwa eneo la
 vita ama
 eneo la mafunzo ya kivita kwa pamoja. Kwa hiyo, ilikuwa kazi
 kubwa,
 ndiyo maana ikatuchukua muda pale kabla hatujaruka daraja,
 ilikuwa ni
 lazima nifanye mafunzo ya pamoja ili kuwaweka watu (askari
 kutoka
 Magereza, Polisi, Mgambo na JKT) waweze kufanya kazi
 pamoja.

 Lengo
 ilikuwa kuondoa fikra za kitabaka vitani, kuachana na mambo
 ya
 huyu mgambo au JKT. Kwa hiyo nilianzisha range ya kupiga
 silaha, mtu
 unampa risasi kumi anapiga zote wash out (anakosa kulenga
 shabaha),
 maana sisi (jeshini) tuna kitu kinaitwa bull, inner, outer
 n.k… sasa
 huyu unampa risasi zote anapiga wash out, tunampa nyingine,
 akipiga ile
 target namwambia umepiga bega (target hasa ni kifuani kwenye
 moyo au
 kichwani) sasa wakati mwingine ukimpa risasi tano… mbili
 anapiga ndani,
 nikasema sasa wameiva.
  Kwa
 hiyo ilikuwa ni mafunzo ya msingi. Kwa mfano, ukiwa porini
 na ndege ya adui inakuja ufanye nini.
  Unaulizwa ukiona ndege ya adui inatoka kule wewe unakwenda
 wapi? Namna
 gani mnaweza kusonga mbele, mnajihami vipi na namna gani
 mnaweza
 kupumzika kwa sababu askari hawezi kupumzika chini ya kivuli
 cha mti.
 Sasa baada ya mafunzo hayo ya pamoja, tukaridhika askari
 wetu wameiva,
 tukaanza kusonga mbele kutoka Katoro hadi tukafika karibu na
 mpakani,
 tukaweka kambi ambayo mpaka leo ipo pale, nyuma ya
 Mtukula.
  Raia
 Mwema: Labda ungeeleza kuhusu Daraja la Kagera kushambuliwa
 na adui?

  Jenerali
 Kiwelu: Daraja hili wakati nimefika tu, kutoka kupewa ile
 amri
  (ya kwenda vitani)… nimefika Kaboya, siku hiyo hiyo jioni
 nikatoka
 kwenda kutazama daraja. Nikafika darajani upande wa kulia
 kama unakwenda
  Mtukula umbali wa kilomita moja, nikaliona daraja ambalo
 baada ya
 dakika 15 nikiwa pale likalipuka, kwa hiyo sikuweza kuwahi
 kuweka askari
  pale darajani.

 Wakati nafika pale na mtu mmoja anaitwa Kanali
 Kitete tunatazama…nataka sasa kufanya mbinu namna gani
 nitavuka daraja
 ili majeshi yangu yakae upande mwingine.
  Basi
 nikarudi zangu
 Kaboya kwa ajili ya kuanza kufanya mkakati mwingine maana
 pale daraja
 limekwishavunjwa, nikaripoti daraja limevunjwa…hakuna
 daraja kuanzia
 sasa. Ndipo tukaanza mipango mingine kuhusu daraja, tukaleta
 madaraja ya
  muda na mtu mmoja anaitwa Brigedia Rajabu ndiye aliyekuja
 na vifaa
 hivyo kutoka kikosi chetu cha uhandishi na tukamweka sehemu
 ya umbali wa
  kama kilomita tano kutoka kwenye daraja, ndipo alipofanya
 mafunzo yake
 ili baadaye kufunga daraja la muda.
  Raia
 Mwema: Ilichukua muda gani hadi kufanikisha daraja hilo la
 muda?

  Jenerali
 Kiwelu: Unajua kuna wanazungumza kwa ushabiki mambo ya vita
 tu
  wakati hawajui chochote kuhusu vita, watu hawa mimi nawaita
 majitu,
 hawajui maana ya vita. Wapo wengine wanafikiri jeshi hii la
 Tanzania
 lilikuwa tayari kwamba unakwenda tu kwenye vita, sasa
 ukiwaambia kwamba
 jeshi hili tulipokwenda kwenye vita tulikuwa na mchanganiyo
 wa watu wote
  hawa, halafu pia kuleta vifaa vya kuvuka daraja,
 kuwafundisha namna ya
 kuweka daraja, kuleta vifaru, ndipo wataona ugumu wa kazi
 iliyokuwapo.

  Pale
 ni lazima uwe na nguvu ya kutosha kuhakikisha kwamba mkiruka

 (daraja) hakuna kurudishwa nyuma. Kama nilivyotangulia
 kusema wale
 askari wetu waliokuwa kule awali, walikuwa wachache na
 walivurumishwa na
  adui kiasi cha morali yao kuwa chini kivita, kwa hiyo
 ilikuwa ni lazima
  nihakikishe sasa watu wangu ni imara, vifaa viko.
  Tulikuwa

 tunafanya mipango na ukaguzi pamoja na makamanda wangu,
 akina Jenerali
 Marwa, Jenerali Luhanga, Mayunga, Walden… tunakwenda hadi
 tunafika pale
 kwenye daraja kwa sababu Idi Amin alirudisha majeshi yake
 (Uganda)
 akiamini kazi imekwisha. Sasa tulikuwa na makamanda wangu
 hao tunakwenda
  pale kupanga mikakati, lakini, swali kwamba wapi tupite
 (kuvuka daraja)
  na lini sikuwaambia.
  Hakuna
 mtu aliyejua hata Edward Sokoine
 (aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Mwalimu Nyerere)
 alikuja
 akaniuliza …. sasa General nafikiri tumechelewa sana
 kuruka (daraja),
 sasa unaruka lini na unapitia wapi?
  Nikamwambia
 hiyo ni siri ya
 kijeshi… akasema hata mimi? Nikamwambia ndiyo mzee. Kwa
 hiyo mimi
 nilikuwa napita kando ya ule mto kwa gari hadi Murongo,
 halafu watu
 wanapiga mabomu kila sehemu lakini hawajui tunaruka wapi
 kupitia wapi..
 .tuliweka watu (askari) hadi eneo la Kakunyu huku Bukoba
 Vijijini, kwa
 hiyo kuna ambao walijua tunaruka kupitia huko. Hatimaye
 nikaona sehemu
 ya kuruka ni pale pale walipovunja (daraja), lakini
 sikuwaambia
 wapiganaji wetu.

 Sasa
 imefika siku ya kuruka, ndani ya saa 24.
 Nikawaita makamanda wangu nikawaambia sasa inabidi turuke
 kwenda
 kumshambulia adui, vifaa na kila kitu tayari, na askari kama

 tulivyofanya mafunzo wako tayari. Makamanda wakasema
 tunangoja tu amri
 yako, nikasema amri itatoka, wakauliza na kutaka niwaambie
 tunaruka
 kupitia eneo gapi, nikasema nitawaambia.
  Ilipofika
 saa tano usiku
  nikawaambia makamanda… Marwa utakuwa katikati, Mayunga
 ukiruka tu
 unakwenda kushoto kuelekea eneo la Mbarara, Walden ukiruka
 tu unaelekea
 eneo la Minziro, Luhanga ukiruka tu unafuata njia ya Marwa
 halafu
 makamanda wengine watakuwa tayari kusubiri lolote (reserve).
 Baada ya
 maelekezo hayo nikawataka waende kuwaambia askari wao kwamba
 tunaruka
 leo (usiku huo), nikamwita Mhandisi Mkuu Rajabu na kumwambia
 utatandaza
 daraja lako (juu ya mto) saa nane usiku…akafanya kazi
 hiyo.
  Saa
 nane usiku mpaka kufika saa tisa kuelekea saa 10 (takriban
 saa mbili
 hivi mfululizo) vikosi vikaanza kuruka kwa mujibu wa amri ya
 operesheni
 (operation order) ilivyotamkwa. Ilikuwa bahati mbaya
 nilipoteza askari
 mmoja tu pale wakati wa kuvuka daraja.
  Baada
 ya hapo tulifanya
 mashambulizi, kazi ya kwanza ilikuwa ni kukamata eneo.
 Nimeeleza kazi
 niliyopewa nilitakiwa kurudisha heshima ya nchi hii na
 heshima ya nchi
 ni kurudisha mipaka yetu pale ilipokuwa awali na hivyo
 tukahakikisha
 tumefika Mtukula, wengine wamefika Minziro na wengine
 mpakani na Uganda
 kule.
  Sasa jukumu la msingi la kurejesha mipaka ya
 nchi likawa
 limekamilika na Rais Julius Nyerere akaja kule na akasimama
 eneo lenye
 kilima pale na tukamweleza kwamba sasa mzee kazi ya kwanza
 uliyotutuma
 tumeimaliza, mipaka yetu sasa iko salama, akasema vizuri
 lakini huyu
 "mshenzi" huyu ametuharibia mambo mengi sana si bado
 yuko kule (nchini
 mwake), basi kazi bado haijakwisha.
  Ndipo tukaingia hatua ya
 pili, maana sehemu ya kwanza ya ukombozi wa nchi yetu ikawa
 imekwisha
 ikafuata hatua hiyo ya pili ambayo ni kumwadhibu
 adui. Raia
 Mwema: Je, baada ya kazi hiyo ya kwanza kukamilika
 ulirejeshwa kwenye nafasi ya Mnadhimu Mkuu (Chief of
 Staff)?

  Jenerali
 Kiwelu: Pale kilichofanyika ni kwamba baada ya kumaliza ile
 kazi ya awali, tukaingia sasa kazi ya kuandaa na kutekeleza
 operesheni
 ya kuvuka mpaka ambayo ni tofauti na opereshani ya kumwondoa
 adui
 nyumbani kwako.
  Sasa
 unakwenda nyumbani kwake lazima uwe na
 mkakati, sambamba na nguvu ya kutosha kwenda kwake, kwa hiyo
 rais
 ikabidi afanye utaratibu wa kumtafuta kamanda wa kuingia
 Uganda, mimi si
  ndiye niliyekuwa Chief of Staff na mkuu wa majeshi akiwa
 Twalipo ambaye
  naye hayuko makao makuu, kwa maana hiyo akiwa huku mbele
 (vitani) kule
 makao makuu hakuna maandalizi yoyote, nani anaanda nini…
 nani anafanya
 nini.
  Kwa
 hiyo ilibidi nirudi Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam
 na pale (vitani kuelekea ndani ya Uganda) nikamkabidhi
 Msuguri, mimi
 nakamwambia nakwenda (makao makuu) kukufanyia kazi ya
 kuandaa vifaa,
 wewe kazi yako ni kwenda ndani kumwadhibu Idi Amin. Nikarudi
 makao makuu
  nilikuwa na mtu mmoja alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi,
 Kanali Bakari,
 basi tukafanya kazi na Bakari, tunkaenda hadi nchi za nje
 kutafuta
 nguvu…. zana za kivita.


 Wako
 marafiki walitusaidia, sina sababu ya
 kuwataja sana lakini kati ya nchi rafiki tulizokwenda ni
 pamoja na
 Urusi, China, Korea na Bulgaria. Ikabidi tukusanye vifaa na
 ndipo hapo
 wananchi walichangia mambo mengi sana, wapo waliojitolea
 magari yao,
 vyakula, mifugo kama ng'ombe ili kuwawezesha wapiganaji
 wetu kule mstari
  na hatimaye Msuguri akuvuka mpaka akiwa na uhakika wa nguvu
 za kutosha
 na uangalizi huku nyuma anakotoka.


 Raia
 Mwema: Kwa wakati huo wewe
 ndiye uliyekuwa makao makuu Dar, sasa uliwezaje kudhibiti
 link
 (viunganishi vya taarifa) za silaha mlizopata kutoka nje ya
 nchi?


 Jenerali
 Kiwelu: Kwanza wakati nikiwa pale Kagera tulikuwa
 tumedhibiti
 sana uvujaji wa taarifa. Unajua kuna mkutano mmoja mkubwa wa
 kimataifa
 ulikuwa unaendelea pale Arusha uliokuwa umehusisha nchi
 nyingi huku vita
  pia ikiendelea na hao washiriki wa mkutano hawakujua
 chochote
 kilichokuwa kikiendelea nilidhibiti uvujaji wa taarifa,
 viongozi wengine
  tuliwapa amri maalumu hakuna kufika kwenye eneo la vita na
 wala kupewa
 taarifa yoyote, ni kama tulivyokuwa tunapambana kuwasaidia
 kule Msumbiji
  siku moja tukakuta mzee mmoja wa kizungu kule Tunduru anayo
 redio
 ameijichimbia ndani, kumbe alikuwa anawasiliana kwa maana ya
 kupeleka
 taarifa, tukamkamata.
  Hata pale Karagwe, tulikuwa na watu fulani
 pale ambao ni kanisa fulani sitaki kuwataja nao pia walikuwa
 na redio ya
  mawasiliano, ukiona utafikiri mtu anapiga kinanda kumbe
 anapeleka
 taarifa, kwa hiyo tukafunga njia zote za mawasiliano,
 nikasema hakuna
 mawasiliano ya aina yoyote na taarifa zozote kwenda Ikulu
 nitapeleka,
 tulihakikisha taarifa hazivuji vinginevyo tusingeweza kuvuka
 pale.
  Raia Mwema: Vipi kuhusu Yoweri Museven (Rais wa
 sasa wa Uganda), alikuwa sehemu ya mapambano?

  Jenerali
 Kiwelu: Museven yeye alitokea huku nyuma kapitia Karagwe
 kalala kijijini pale wakati Mayunga amekwishavuka mpaka,
 akaungana na
 Mayunga, ukweli ni kwamba Jeshi la Tanzania na chini ya
 Luteni Jenerali
 Mayunga ndiye aliyekabidhiwa kazi ya kupita Mbarara na
 kutoka hapo
 kuelekea Kampala, na wengine wakapita Minziro kwenda
 kuungana kule.
 Museven hakuwa na jukumu la kuongoza ni kama alisaidia mambo
 kadhaa
 yakiwamo masuala ya taarifa.
  Raia
 Mwema: Vipi kuhusu uteuzi wako kuwa mkuu wa mkoa?

  Jenerali Kiwelu: Baada ya vita, tukawapokea
 vijana kutoka Uganda pale
 Bunazi, nikafanya kazi ya kuwasambaza na kuwarudisha kule
 walikotoka,
 wengine Ruvuma, Kigoma na maeneo mengine ya nchi.
 Tukahakikisha wamerudi
  na kupewa haki zao.
 Baada ya kumaliza pale Bunazi, nikarudi Dar
 es Salaam kwenye kitengo changu cha Mnadhimu Mkuu, sasa
 makamanda wote
 wakawa wamerejea kutoka vitani. Ikabidi sasa jeshi lipangwe
 upya….unajua
  watu walikwishaonja kutoa roho za watu huwezi kucheza nao
 hivi hivi,
 ikabidi sasa tupangane upya.
  Namna
 gani jeshi litakavyoendeshwa
 na kwa hiyo, Amiri Jeshi Mkuu akapanga upya…akasema sasa
 wewe bwana
 umemaliza kazi hii nakushukuru…sasa nataka kukupa kazi
 nyingine…nikamwambia sawa, nipo tayari kwa kazi yoyote,
 akaniambia
 utakwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, nikamwambia naenda
 lakini hii kazi
  sijawahi kufanya sasa ukiona nafanya vibaya uniite, na mimi
 nikiona
 kuna tatizo nitakuja.
  Kwa hiyo nikaenda zangu Tanga ndipo wakati huo
 yakafanyika mabadiliko, Twalipo akatoka pale akawa Waziri wa
 Ulinzi,
 Msuguri akawa Mkuu wa Majeshi halafu na Jenerali Kombe akawa
 Mnadhimu
 Mkuu, tukaendelea.

 Raia
 Mwema: Nini hasa unachojivunia katika wadhifa wako wa Mkuu
 wa Mkoa wa Tanga?

  Jenerali Kiwelu: Tanga kuna mambo mengi. Lakini
 moja kubwa ni kwamba
 pale Tanga wale Waswahili wangu wa Tanga ni wavivu, hawakuwa
 watu wa
 maendeleo. Sasa walikuwa wanakaa pale kwenye nyumba zao za
 nyasi mjini,
 nikawaambia sikilizeni hatuwezi kuishi hivi…mtu lazima
 afanye kazi na
 mjiwekee kipato na mtengeneze nyumba.
  Wakauliza tunatengenezaje
 na hatuna mashamba kwa ajili ya kutupatia kipato? Nikafanya
 uamuzi,
 nikaenda barabara ya kuelekea Muheza kuna mashamba ya mkonge
 pale na
 hapakuwa na mtu anayelima, nikasema nitachukua haya mashamba
 na wala
 sikuuliza ni ya nani.
  Nikawaambia
 nyie mtakwenda kulima pale na
 kutakuwa na mabasi asubuhi na jioni ya kwenda na kurudi
 shambani, na
 kwamba wakishavuna watapata chakula lakini nikataka
 watengeneze nyumba
 zao na watoto wasome kwa kipato watakachopata.
 Nikamwambia ofisa
 husika apime viwanja, lakini nikawaambia nyumba zao
 wasizivunje
 isipokuwa wajenge kuta kwa kuzizunguka na baada ya kufika
 hatua ya
 kupaua, wanaweza kuvunja nyumba za ndani yake za nyasi,
 ndivyo nyumba
 nyingi za Tanga zilivyojengwa kwa wakati huo.
  Nilikaa
 pale kwa
 miaka nadhani mitatu tangu mwaka 1980 kisha nikahamishiwa
 Rukwa ambako
 nako pia kuna mambo mengi niliyofanya. Uzuri wa Rukwa watu
 wa kule ni
 wachapa kazi lakini tatizo lao walikuwa wanachapa kazi bila
 utaratibu.
 Nikawaambia msilime tu mahindi ya kutosha nyumba yako tu
 bali limeni kwa
  malengo ya kupata kipato. Nikawataka walime kwa utaratibu,
 wajue
 masuala ya mbegu, maandalizi ya shamba.
  Lakini
 haikuwa kazi
 rahisi kwa sababu ilibidi tutengeneze kitu kama shule
 kijijini kwa ajili
  ya kumfundisha mtu kulima, kuandaa shamba, kupanda,
 kupalilia hadi
 kuvuna, ni miezi minne…watano amevuna ameweka kwenye
 kihenge, anakuwa
 amefaulu. Sasa mtu anapokuwa anajifunza kulima alikuwa
 akijifunza kilimo
  cha kisasa, kupanda kwa mistari, kutumia mbolea, kutumia
 dawa za
 kudhibiti wadudu na baada ya kuvuna, ajue namna ya kutunza
 mazao.

  Sasa
 katika kuandaa mashamba wengine walikuwa wanatumia majembe
 madogo
 ya kukokotwa kwa ng'ombe na wengine majembe ya mkono,
 uongozi ngazi ya
 mkoa ilibidi tufanye utaratibu na tulifanikwa kwenda kununua
 majembe
 kutoka Zimbabwe ya kukokota kwa ng'ombe na ya kupandia.
 Niliomba fedha
 nikapewa za mbegu ambazo kule hakuna, nikaagiza mbegu kutoka
 Kenya
 lakini hazikuwa zinatosha, nikaenda kwenye wizara (ya
 kilimo) natafuta
 mbegu nako hakuna.
  Lakini
 nikaona sio siku zote kwenda kutafuta
 mbegu, nikaanzisha shamba la mbegu eneo la Mlundikwa, mwaka
 wa pili
 tukawa sasa tunaweza kupata mbegu zetu na tukajua namna ya
 kuziweka
 katika madaraja ya ubora.
  Sasa
 baada ya kuwa na uhakika wa mbegu
 tukaingia hatua ya matumizi ya majembe ya ng'ombe,
 tulipomaliza mwaka wa
  kwanza na wa pili, ule mwaka wa tatu tukafaulu na kupata
 mazao mengi,
 maana nia yangu pale ilikuwa ni kupata mavuno mengi ili
 kushindana na
 wenzangu wa mikoa mingine ya kilimo, na ikibidi hata
 kuwazidi lakini kwa
  manufaa ya watu wangu hasa katika kuongeza kipato chao mara
 dufu au
 zaidi.
  Raia Mwema: Kwa hiyo kuwapo kwako Rukwa
 kulisababisha mkoa
  huo kuwa miongoni mwa mikoa mingine mikubwa ya kilimo kama
 Mbeya,
 Ruvuma na Iringa?
 Jenerali Kiwelu: Kwanza mimi nikiwa kule
 nilijua Mbeya ambako nilikuwa napita pale, Iringa na Ruvuma
 ndio
 iliyokuwa mikoa mitatu mikubwa na mashuhuri kwa kilimo,
 ikiitwa "The Big
  Three". Nikasema hawa hawawezi kuwa Big Three na mimi
 napita mikoa yao,
  changamoto yangu ya kwanza nikasema lazima niingie pale
 kwenye orodha
 ya Big Three ili tuwe Big Four.
  Raia
 Mwema: Baadaye ulipelekwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera, hali
 ilikuwaje kule?

  Jenerali
 Kiwelu: Unajua ule Mkoa wa Kagera unafafana hali ya hewa na
 mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro na Arusha, mimi sehemu ya
 asili ni
 Kilimanjaro ambako mazao ni pamoja na kahawa na migomba kule
 nako mazao
 ni hayo hayo, tofauti iliyokuwapo ni kwamba kule Kilimanjaro
 tulikuwa
 tunalima kahawa aina ya Arabika sasa Kagera ilikuwa nafasi
 yangu ya
 kujifunza kilimo cha kahawa aina ya Robusta, ikawa lazima
 niwainue wale
 wakulima tuone tunafanya vizuri zaidi. Sasa kule kwa sababu
 wengi ni
 wabishi kweli kweli wanataka lazima waone vitendo kwa mfano,
 ikabidi
 niwe na shamba la mfano na hata sasa baada ya kustaafu bado
 naendelea na
  kilimo kwenye shamba langu.
  Chanzo Raia Mwema.
  Maoni Yangu

  Tumeeona
 jinsi Generala Kiwelu alimvyomnyima Sokoine taarifa za vita
 kwa kumwambia ni siri ya kijeshi na Sokoine pamoja na
 wadhifa aliokuwa
 nao aliheshimu hilo hakutaka zaidi ya jibu
 alilojibiwa.
  Hivyo

 basi wanasiasa wetu wa kizazi hiki waige mfano wa Sokoine
 kwa kuheshimu
 vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kutotaka kila kitu
 kuwa wazi
 ikiwemo eti kwa kuwa wao ni wabunge au wanasiasa wapo kwa
 niaba ya
 wananchi hapo watakuwa hawavitendei haki vyombo vyetu hivyo
 kwani
 vinafanya kazi kubwa ya kuhakikisha tuna kuwa na amani
 pamoja na
 uturuvu.
  Hata huko Marekani na ulaya huwezi kukuta
 wanasiasa
 wanataka mambo ya jeshi na vyombo vingine vya ulinzi na
 usalama kuwekwa
 hadharani kama wa hapa kwetu wanavyotaka ili wapate umaarufu
 wa kisiasa.





 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment