Friday, 2 October 2015

Re: [wanabidii] Bomu la Magufuli

Siku zile watu walijitahidi kumchafua Mrema. Wengine wakasem ni mla rushwa. Wenye kuona mbali wakawaonya wanaomchafua kuwa mkitaka kumchafua Mrema msimuunganishe na rushwa kwa sababu hakuna atakayewaamini. Nimelikumbuka sasa watu wanapotaka kumchafulia Magufuli.
--------------------------------------------
On Fri, 10/2/15, fatma_elia via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Bomu la Magufuli
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, October 2, 2015, 10:37 AM

Sent
from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel
Tanzania.From: Emmanuel Muganda
<emuganda@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 1 Oct 2015 14:48:22
-0400To: TANZANET Mailing
List<list@tanzanet.org>;
Wanazuoni@yahoogroups.com<Wanazuoni@yahoogroups.com>;
wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>ReplyTo:
wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Bomu la
Magufuli
Habari
hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache
iliyopita ikisomeka...
Huyu Ndiye
Pombe Magufuli:

-
Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi
na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli,
katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa
mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi
sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa
Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii
kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti
katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi
lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa
vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya
'fujo' katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati
mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA
ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi
wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri
kinyume na matakwa.

Ni
chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli,
aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli
ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi
mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa
yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba
awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala
la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu.
Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku
akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari
mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu,
baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi
miwili akaacha kazi.

"Kwa
upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa
moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala
hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la
Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake
Sundi," vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo
vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba
hizo.

Habari hizo
zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia
shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba
hiyo.

"Ndipo Magufuli
aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi
wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote,
mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,"
chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30
ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za
Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja
na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa
Serikali.

Sheria hiyo
inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila
kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua
wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa
Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe
hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha,
Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A.
Bukuku.

Hata hivyo, sheria
haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za
uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi
Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi
wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha
asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri
kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza
akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini
kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi
wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti
kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni
kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri
Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James
Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea
ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa
jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo,
namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu
mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo
mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina
lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe
nyumba.

Alipoulizwa kwa
njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe
waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza
Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na
miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala
wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya
kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean
Road.

Hata hivyo, habari
hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi
na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi
mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na
analipwa kwa dola za kimarekani.

"Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli
katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu
tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi
miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi,
wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja
aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa
Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo
zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali
ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata
hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi
22,684,108,115.08.

Kwa
sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na
TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa
Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111
zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40
zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama
ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAIEmail This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook 
0
Comments :Post a
CommentNewsreelPopularArchiveRecentRSS
Feed WidgetSince February 1st,
20149960220 



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment