Wednesday, 2 September 2015

RE: [wanabidii] Hotuba ya Dr. Slaa kwa Watanzania toka Hoteli ya Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015

Ni kweli Mbegu.
Sasa imebaki kwa Gamanywa kujitokeza na kufanya moja kati ya haya:
1) Kukaa kimya ili watu wajue hakusingiziwa.
2) 2) Akanushe kumwambia Slaa habari hizo watu waamue nani mkweli kwa kutegemeana na wawili hawa wanavyofahamika
3) 3) akiri kumwambia Slaa maneno hayo lakini haikuwa kweli.
4) Akiri kuwa alimwambia Slaa maneno hayo na kuwa ni kweli.
Ukweli wenyewe ni upi:
Kuwa alikuwa anamshawishi Slaa akubaliane na hayo maana maaskofu 30 wamehongwa.
Kuwa ziliagizwa hela za kununua gari ndani ya dakika zilikuwa zimeletwa
Hii itawasaidia Watanzania kuona kilichokuwa hakijaonekana kwa wengi. Itasaidia kufanya maamuzi ya busara 20 October na kumwachia aliyeahidi mahakama maalum kuanzia kwa hao.
--------------------------------------------
On Wed, 9/2/15, Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com> wrote:

Subject: RE: [wanabidii] Hotuba ya Dr. Slaa kwa Watanzania toka Hoteli ya Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015
To: "Wanabidii Mawazo" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, September 2, 2015, 12:27 AM




Ni kweli Elisa, lakini context inaelekea
kuonyesha kuwa kile alichoambiwa na Gamanywa ndicho
anachokiamini na ndicho anachokiwasilisha na kutaka watu
waamini!
 
> Date: Tue, 1 Sep 2015 14:09:47 -0700
> From: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: Re: [wanabidii] Hotuba ya Dr. Slaa kwa
Watanzania toka Hoteli ya Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> Hii ndiyo hatari ya kukariri kapengele kamoja au mstari
mmoja. ukitaka kuelewa unasoma paragraph . Swala la maaskofu
alikuwa anaeleza alichoambiwa na Gwasma hivyo mashehe
hawaingii
> --------------------------------------------
> On Wed, 9/2/15, Neatness Msemo <nmuzeh@gmail.com>
wrote:
>
> Subject: Re: [wanabidii] Hotuba ya Dr. Slaa kwa
Watanzania toka Hoteli ya Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Wednesday, September 2, 2015, 12:06 AM
>
> Ameonyesha udini
> kuchochea kuwa maaskofu wamehongwa anataka waislam
wajione
> kuwa lowasa ni wakristo hii ni mbaya ametumwa
tunamsamehe
> bure yaani hasira imezidi
> On Sep 1, 2015 11:49
> PM, "Neatness Msemo"
<nmuzeh@gmail.com>
> wrote:
> Nadhani ni vema sana kuangalia kwa makini kwani
> pamoja na ukweli au uongo wa anayezungumza  je
chanzo cha
> haya yote source yake ni hasita au kukosa au nia yake
ni
> kumwaga mboga lakini watanzania wamechoka kwani
hakuna
> msafi
> On Sep 1, 2015 11:01
> PM, "'mpombe mtalika' via
Wanabidii"
> <wanabidii@googlegroups.com>
> wrote:
> Slaa:
> Watanzania wana kiu ya kujua kwanini amekuwa kimya kwa
muda
> mrefu sasa licha ya
> harakati za kisiasa kuendelea.
>
>
>
> Muda utakaotumika ni saa moja, hakuna muda mrefu
sana.
>
> Ameamua kufanya hayo kwa kuwa imefika mahali ukweli
lazima
> usemwe na
> upotoshwaji ukomeshwa. Namna pekee ya kufanya hivyo
ni
> kutoka hadharani na
> kuusema ukweli.
>
>
>
>
>
> Sote
> tunafahamu kuwa hana tabia ya kuchenga mambo, mengi
> yamesemwa na watu tofauti,
> kwenye mitandao, magazeti na viongozi wake! Hana
ugomvi na
> kiongozi yoyote, kwa
> kuwa siasa sio ugomvi. Kama binadamu wa kawaida hana
chuki
> wala hasira na
> binadamu mwingine yoyote!
>
>
>
> Iwe wazi kuwa katika Taifa kuna misingi ambayo
inaongoza
> taifa. Inapofika
> mahali taifa linaongozwa kwa msingi ya propaganda na
> upotoshwaji matokeo yake
> ni vurugu kubwa katika taifa. Yeye amekataa hayo
yote!
>
>
>
> Anasema kuwa YEYE hakuwa likizo kama inavyosemwa na
viongozi
> wake! Atafafanua
> kwa kifupi! Kilichotokea ni kuwa aliamua kuachana na
siasa,
> tarehe 28 Julai
> 2015, majira ya saa tatu usiku, baada ya kuona
yanayofanyika
> ndani ya chama
> chake hayamridhishi.
>
>
>
> Kinachosemwa ni kuwa Dr. Slaa alishiriki tangu mwanzo
kwenye
> mchakato. Anasema
> ni kweli alishirii kwenye majadiliano, akaweka msingi
na
> msimamo wako. Kuna
> wakati wengi wanashinda kutokana na wingi wao, wewe
> unayeamini katika misingi
> inabidi uachie ngazi.
>
>
>
> Baada ya Edward Lowassa kukatwa na CCM Dodoma, Mshenga
wake
> alimpigia simu na
> kuuliza nini kifuate baada ya tukio la dodoma.
Akamuambia
> wawasiliane na
> mwenyekiti Freeman Mbowe, Gwajima nae akafika kwenye
kikao
> hicho.
>
>
>
> Msimamo wa Slaa ni kuwa ni lazima kumsikiliza mtu
kabla ya
> kuamua nini cha
> kufanya. chadema ni cham cha siasa na hakiwezi
kumkataa mtu
> yeyote kujiunga na
> chama.Wakaweka vijana kuchunguza nini wanataka hao
wanaotaka
> kujiunga na chama!
>
>
>
> Slaa akataka kwanza Lowassa atangaze kutoka kwenye
chama
> chake alichopo, kisha
> atangaze anakwenda kwenye chama gani. Atumie nafasi
hiyo ya
> mkutano huo
> ajisafishe na tuhuma zote ambazo amekuwa akituhumiwa
na
> watu.
>
>
>
> Chadema ni cham ambacho kwa muda mrefu kimejijenga
kwa
> msingi, na ni lazima
> wapokee mtu ambaye hawezi kukichafua chama chao.
Lowassa
> hakutangaza kujitoa,
> wala kujisafisha hadi kwenye mkutano ambao uliandaliwa
na
> chadema. Slaa
> hakuhudhuria ule mkutano.
>
>
>
> Kwenye kila jambo kuna jambo la kuzingatia. Mtu
anayejiunga
> popote anakuja kama
> mtaji au kama mzigo? Lowassa anakuja chadema kama
asset au
> liability? Ijulikane,
> suala sio urais! Mpaka siku hiyo Slaa hakuwa amechukua
fomu
> ya Urais kwenye
> chama chake. Slaa hakuwa anamzuia Lowassa kugombea
urais
> chadema. Alitaka
> mgombea mwenye sifa na uwezo wa kukitoa Chama cha
> Mapinduzi.
>
>
>
> Hakutamka popote kuwa anataka kugombea, hata 2010
> hakugombea, aliombwa
> kugombea! Urais wake binafsi hauwezi kuikomboa nchi
bila
> mchango wa jamii
> nzima.
>
>
>
>
>
> Mwafrika,
> [01.09.15 15:45]
>
> Suala la adha Lowaasa ni msizo au mtaji halikujibiwa
hadi
> siku ya mkutano
> tajwa. Wakataka kujua anapokuja anakuja na akina nani,
ni
> wafuasi wa aina gani;
> vijana wa bodaboda, vijana wasio na ajira au watu
> waliosombwa tu, au wanakuja
> kwenye mapambano?
>
>
>
> Jibu lilikuwa ni kuwa tungepata wabunge 50 na
wenyeviti wa
> CCM mkoa wasiopungua
> 22, wenyeviti wa CCM wilaya 88. Slaa akakiri kuwa kama
ni
> hivyo kutakuwa na
> tetemeko (la kisiasa).
>
>
>
> Wakahitaji majina ya hao waliotajwa kwa kuwa walikuwa
kwenye
> mchakato wa
> kupitisha majina kwenye chama. KAtibu mkuu makini
huwezi
> kuchukuwa watu usiowajua.
> Hakuna jina nililopewa mpaka tarehe 25.
>
>
>
> Tarehe 25 wakamfata na kumuambia aitishe Kamati Kuu
ya
> chama. Akakubali lakini
> akatahadjharisha kuwa hajapata majina na hajapata jibu
kuwa
> Lowassa ni asset au
> liability. Lakini akaitisha kikao kwa kuwa ni jukumu
la
> kikatiba la katiba.
>
> Mwenyekiti akapiga simu, anasikia kuwa hajaridhika.
Tangu
> 2004 Slaa hajawahi
> kugombana na mwenyekiti wake, isingekuwa sawa kama
> wangetofautiana kwenye kikao
> rasmi.
>
>
>
> Wakakutana na Mwenyekiti, Gwajima, Lissu na
wakajadiliana
> mpaka saa 9 mchana.
> Maneno kuwa alikuwa anakubaliana na mpango huo tangu
mwanzo
> SI KWELI!
>
> Mkutano ukashindikana. Wdau wakasema waende nyumbani
kwa
> Lowassa, Slaa akakataa
> wakaenda Kamati kuu.
>
>
>
> Kikao kikafanyika hadi saa 12 jioni. Ikaundwa kamati
ndogo
> ya kumshawishi Slaa.
> Akakataa! Akaandika barua ya kujiuzulu kwa kamati,
Prof.
> Safari akaichana barua
> yake. Akaandika barua nyingine kwa Makamu-Zanzibar,
makamu
> akamuambia kuwa haya
> mambo yamepangwa, asijisumbue!
>
>
>
> Wanasema siasa ni mchezo mchafu, yeye anaaamini kuwa
siasa
> ni sayansi! Asubuhi
> ya kesho akaandika barua, wasichojua ni kuwa
kujiuzulu
> hakuhitaji barua. Maneno
> yakazuka kuwa Slaa hajaandika barua! Upotoshwaji
ukaendelea
> kuwa Slaa
> atazungumza na waandishi wa habari, wengine wakasema
> amefungiwa, amefungiwa na
> mkewe na kadhalika! Ukweli ni kuwa alikuwa na Lissu,
Gwajima
> na Mbowe tangu
> asubuhi.
>
>
>
> Maamuzi aliyoyafanya yanatokana nadhamiri yake!
Josephine
> nae ni mwanaharakati,
> ana sababu ya kuwa na uchungu. Alipigwa mwaka 2011
wakati
> wengine walijificha!
> Propaganda hizo tumeshazisoea!
>
>
>
> Kama kuna mwenye ushahidi wa propaganda hizi aje,
audited
> report zipo!
> Josephine halipwi na chama! Watu wanasema kuwa Slaa
analipwa
> mil. 7, yeye
> ameendelea kula mihogo na maharage kama walivyoahidi
mwaka
> 2010. Wana uchungu
> na harakati!
>
>
>
> Kikubwa katika harakati ni credibilty, jina la chama
> kilichojengwa kwa muda
> mrefu kisichafuliwe kwa namna yoyote! Mwanasiasa
yoyote
> hataki kuchaguliwa, na
> Slaa nae hataki kuchaguliwa! Wanasema kuna maslahi
mapana ya
> taifa, ni nani
> anayapima? Lazima kuwe na kipimo cha kuapima hayo
maslahi
> badala ya kutegemea
> mtazamo wa mtu!
>
>
>
> Anafafanua suala la liability sasa!
>
>
>
> Wamekuwa waongo kwa kuwa hakuna kipengele hata kimoja
cha
> madai ya Slaa
> kimetekelezwa. Alisema wabunge waje kabla ya kura ya
maoni
> ya CCM, kuja baada
> ya hapo ni kutafuta kichaka cha kujificha!
>
>
>
> Watanzania wameijenga Chadema kwa damu yao, rasilimali
zao!
> Watu hawawezi
> kukimbilia kirahisi wakati sio wasafi, akiwemo Sumaye
na
> wengine. Nani hajua
> kama Sumaye ni fisadi? Kwa muda mrefu Slaa haongei na
Sumaye
> kwa kuwa
> alimtuhumu kwa ufisaidi.
>
>
>
> Sumaye ni mtu ambaye wanahabari walidai kuwa Sumaye
alisema
> kuwa atahama chama
> endapo Lowassa atateuliwa, leo akageuka! 
> Leo anamsafisha Lowaasa, dhambi haisafishwa kwa
> dhambi. Anakumbusha jina
> la Mr. Zero (jina la utani la Sumaye).  Chama
> kimepokea makapi, na katibu alitahadharisha kuwa
chama
> hakipokei makapi! Hakuna
> ambaye alijitoa kwa hiari, wengi walikuja baada ya
kukatwa.
> Wenyeviti wengi ni
> mzigo, akiwemo Msindai.
>
>
>
> Anangoja ajibu amlipue hadharani kwa kuwa alikuwa
mwenyekiti
> wa kamati ya bunge
> hesabu za serikali z mitaa. Siku aliyoambiwa aitishe
kamati
> kuu aliuliza
> majina, akaambiwa anakuja chizi! Chizi ni nani, hata
nyie
> hamumjui! Anaitwa
> chizi kwa kuwa ni mwizi wa kura ndani ya CCM.
>
>
>
> Kuna haja gani ya kushindana kama tunampango wa kuiba
kura
> pia. Wakamtaja
> Guninita, nani asiyemjua udhaifu wake? Hawezi kuandika
hata
> ukurasa mmoja wa
> ripoti, amehama vyama mara kadhaa!
>
>
>
> Mwafrika, [01.09.15 15:45]
>
> Viongozi wa Chadema wamepata kigugumizi, waseme nani
> ameongeza thamani kwenye
> chama? Najua maneno ya kuwa ni lazima kuiondoa CCM
kwanza
> hata ikibidi tuweke
> mkataba na shetani, mimi ni padre wa Kanisa Katoliki!
> Kuwaondoa CCM kwa namna
> yoyote hakuleti maendeleo. CCM itaondolewa kwa
program
> siriaz, sio kutumia watu
> wale wale!
>
>
>
> Lazima tujue nini kilifanya Watanzania waamini
chadema, kwa
> kuwa waliamini wana
> misingi isiyoyumba na uadilifu. Leo tunasimamia
uadilifu?
> Wanasema mwenye
> ushahidi aende mahakamani. Kama tusingewatuhumu Mramba
na
> Yona wasingefikishwa
> kizimbani. Chadema imefungwa mdomo kwa kisingizio cha
> ushahidi!
>
>
>
> Ni bora kukaa kimya kuliko kupotosha. Anasema nukuu
ya
> biblia kuhusu
> wapotoshaji! Inapofika mahali unapoambiwa hakuna
mwenye
> dhambi ni makosa,
> dhambi haisahihishwi kwa dhambi nyingine! CCM
wamekuwa
> waoga, wamewalea watu
> hawa kwa muda mrefu!
>
>
>
> Kwa Wafrika choo ni neno baya, kwa wazungu choo ni
rest
> room! Choo cha
> Kitanzania huwezi kukihamisha ndani ya chumba cha
kulala na
> ukakiita choo,
> huwezi kulala kwa kuwa kitanuka, tena zaidi! Ufisadi
ilikuwa
> ajenda iliyowapa
> umaarufu CHADEMA, leo wamewachukua. Waanweza kuwa na
ujasiri
> wa kukemea
> ufisadi?
>
>
>
> Mwaka 2008 Slaa alikuwa bungeni wakati wa sakata la
> Richmond, anafahamu kwa
> uzuri anachokimaanisha. Bahati mbaya waandishi
hawasomi
> makaratasi, na wabunge
> wa CCM pia.
>
>
>
> Lowassa hatuhumiwi kwa habari ya Richmond pekee!
Lowassa
> aliambiwa na Slaa
> aache kulalamika, atangaze uhalali au uharamu wa
Richmond,
> anamtaka aseme hao
> 'wakubwa' ni akina nani? Ni afadhali sifa
yake
> iharibike kuliko kusema uongo.
>
>
>
> Ni aheri kupotea kwenye siasa za dunia kuliko
kusimamia
> uongo! Msingi wa kwanza
> wa Richmond: Ili uelewe ni lazima urudi kwenye taarifa
ya
> Kamati ya Mwakyembe,
> Slaa alifuatwa asubuhi ya siku ile kupewa rushwa,
anashuru
> Sitta na Mwakyembe
> wajitokeze!
>
>
>
> Akamuuliza mtoa rushwa kama anatoa m.500 kwa mbunge,
atakuwa
> nazo ngapi?
> Aliwaambia Sumaye na Lowassa kuwa rushwa ni jambo
> linaloanzia kifuani kwanza.
> Mwanzo wa jambo hili ni taarifa ya Baraza la Mawaziri
la
> 10.2.2006. Kamati ya
> mwakyembe iliangalia faili la kikao kile kisha
kuandika
> ripoti!
>
>
>
> Suala hili lilianzia wakati wa utawala wa mkapa
kutokana na
> dharura ya umeme
> nchini, wakawasiliana na kampuni moja ya Amerika
Kaskazini
> kwa suluhu ya muda
> mfupi ya umeme. Serikali ya Kikwete ikapokea lile
suala.
> Wakaruhusu mpango uendelee,
> ila kwa kufuata sheria. Hiyo ilikuwa kauli ya Baraza
la
> Mawaziri!
>
>
>
> Wakati auala lile linaamuliwa, Lowassa alikuwa Waziri
Mkuu!
> Na ndie mwenye
> mandate ya maamuzi ya Serikali, iweje leo akane
kuhusika?
> Taarifa ya Mwakyembe
> inapotoshwa! Taarifa ilitaka Waziri Mkuu ajipime, au
bunge
> limjadili na
> kumchukulia hatua. Lowassa akakimbia kwa kuwa alijua
Bunge
> lingemfukuza kazi!
>
>
>
> Waliioomba tenda walikuwa 26, waliorudisha walikuwa
8.
> Kamati ya Tathmini
> ikaona hakuna anayefaa hata mmoja! Waziri Msabaha
akaagiza
> taarifa ile ifutwe
> na tathmini ifanyike upya, mara ya kwanza, ya pili, ya
tatu
> na ya nne. Jeuri wa
> Msabaha ilitoka wapi? Baraza likaamua baadaye tenda
> iliyopewa kwa kampuni ya
> kwanza ifutwe! Lowassa alishiriki!
>
>
>
> TANESCO wakatoa ushauriwa wao, Mamlaka husika
ikatafute
> internatonal tender ya
> kununua turbine! Lowassa akaingilia mchakato dakika
za
> mwisho, akamuagiza
> katibu muhtasi wake!
>
>
>
> Kwanini Lowassa, kwa kuwa anagombea urais, rais
asiyeaminika
> hawezi
> kuchaguliwa!
>
> Lowassa alishawahi kumuita Slaa kuhusu habari ya
Meremeta,
> na kumuambia kuwa
> taarifa yake inaiaibisha Serikali! Kampuni ya jeshi
imewahi
> kutengeneza gari,
> imehujumiwa na wahuni. Akamtaka Lowassa amuambie ni
nani
> aliyehusika?
>
>
>
> Akamuita mwingine kwnye Speaker lounge. Slaa
akamuambia kuwa
> yeye ni fisadi
> kichwani, rohoni mpaka...!
>
>
>
> Tunamsifia Lowassa kuwa an=taleta maji wakti jimbo la
> Lowassa halina maji na
> ufisadi mkubwa umefanyika kwneye jimbo hilo.
Mnazungumzia
> shule za kata wakati
> wakati hamjua zimeanza wapi? Slaa anataja nafasi
alizowahi
> kushika Afrika.
> Uamuzi wa kujenga shule za kata ulifikiwa mwaka 90
huko
> Thailand, mpango huo
> ukaitwa Education for All, sio MMES kama unavyoitwa
leo!
>
>
>
> Mwafrika, [01.09.15 15:45]
>
> Anasoma barua ya Ibrahim Msabaha kwa Flugence
Kazaura,
> mkurugenzi wa bodi wa
> TANESCO!
>
>
>
> Mpango ulikuwa kuondoa suala la umeme mikononi mwa
tanesko
> kwa kuwa imeshindwa
> kutekeleza. Ugomvi wake na Masha ni kwa kuwa Lowassa
> alimlaumu Masha kuingilia
> mchakato wa serikali, akawekewa kinasa sauti
chumbani.
> Waziri Mkuu haruhusiwi
> na sheria kuingilia mchakato wowote wa tenda.
>
>
>
> Kwenye kampuni nane zilizowasilisha maombi ya zabuni,
> Richmond ni kampuni
> iliyokuwa mbovu. Ilikuwa ni kampuni ya steshenari,
sio
> umeme!Wakadai wana
> ushirikiano na kampuni nyingine ya umeme, kampuni
hiyo
> ikakataa kujihusisha na
> Richmond, wala kuzalisha na majenereta!
>
>
>
> Bill Clinton aliwai kukutwa na kashfa, walitaka
kumchukulia
> hatua si kwa sababu
> ya zinaa, bali kwa kuwa alifanya uongo! Kwa kuwa
alidanganya
> umma! Hata sheria
> za Tanzania zinakataza kuongopa, hata kesi za uchaguzi
za
> Slaa zimethibitisha
> hilo.
>
>
>
> Lowassa anadai yeye alisimamisha tenda, Slaa
anaonesha
> uthibitisho wa hilo kwa
> barua za Lowassa kwenda kwa Msabaha zinazokanusha
hilo,
> 'Anaisoma'! Waziri Mkuu
> aliharakisha mchakato wa tenda, tofauti na sheria ya
PPRA.
> Barua imeandikwa
> miezi mitatu baada ya mkataba kusainiwa, kwa maagizo
ya
> Waziri Mkuu.
>
>
>
> Tanesko ikaagizwa kusaini mkataba ambao haikuhusika
kwenye
> kuujadili! Anaona
> aishie hapo... Anaupigia chapuo mdahalo wa Sitta na
> Mwakyembe, anasema Lowaasa
> nae afike kuondoa utata na kusema ukweli!
>
>
>
> Chadema ni chama kilichotoa matumaini kwa vijana
wengi!
> Isifike mahali tukawa
> washabiki kama 2005 ambapo watu waliahidiwa maisha
bora,
> wakajikaanga kutokana
> na ushabiki! Anatoa ushahidi wa kitakwimu wa mfumuko
wa
> bei...
>
>
>
> Slaa ana uchungu kuona chama alichokijenga, kikifikia
hatua
> ya kusomba watu kwa
> mabasi na malori kisha mkasema mafuriko hayazuiliki!
Hayuko
> tayari,... Anakataa
> kuwa ZEZETA! Ajenda ya Chadema ni nini, ilikuwa ni
rushwa!
> Wananchi waliamini
> kwa kuwa msingi huo ndio unakijenga chama!
>
>
>
> Sehemu kubwa ya kilichosemwa Jangwani ni ilani ambayo
> ilishaandaliwa tayari,
> hakuna kipya kilichosemwa. Kinachomuuma ni chama
makini kuwa
> kibovu zaidi ya
> Chama cha Mapinduzi! Hatuwezi kujenga maadili tukiwa
na watu
> wachafu, anaishi
> na mwanamke bila kufunga ndoa kwa kuwa Serikali ya
CCM
> haitaki afunge ndoa.
> Kesi yake ililetwa na mawaziri, waandishi wa habari na
mtu
> kutoka IKULU. Ndoa
> inafungwa na Mungu!
>
>
>
> Scotland Yard iliamrisha Lowassa achunguzwe, inakuwaje
leo
> tunamtetea? Huu ni
> ushabiki usio na vielelezo, Slaa ana ushahidi! Hakuna
> ulazima wa kwenda
> mahakamani kwa kuwa kesi ya rushwa ni jinai, ni kesi
ya
> serikali! Slaa au
> mwingine hana locus ya kwenda mahakamani kwa kesi ya
jinai!
> Mwakyembe alisema
> kesi ya jinai haina mwisho (kama zilizyo za madai).
chadema
> iliahidi kusafisha
> nchi kwanza endapo itashika dola, huku maendeleo
> yakiendelea!
>
>
>
> Anasoma barua ya mchakato wa Richmond kuwa DOWANS.
Kampuni
> imesajiliwa Costa
> Rica, na mwenyekiti asiye na anuani, simu wala jengo!
Siku
> iliyosajiliwa,
> mmiliki alisajili makampuni mengine 99! Zaidi ya hayo
ana
> makampuni mengine
> zaidi ya 50, DOWANS ni jina tu. Kampuni haipo! Dowans
sio
> kampuni halisi huko
> Kosta Rika, nchi nzima hakuna kampuni yenye uwezo wa
> kuzalisha umeme kwa
> kiwango hicho!
>
>
>
> Leo Lowaassa anatuambia tufunge mdomo, huu ni
udikteta!
> Anakumbusha sakata lake
> na Waziri Marmo... Mabilioni ya fedha yanalipwa kwa
kampuni
> ambayo haipo!
> Tunapenda ushabiki... Acha sifa iharibike!
>
>
>
> Anasema hataki kuingia kwenye mambo ya Babu Seya! Vyuo
vikuu
> vinatumia kesi ya
> Babu Seya kama case study. Mtoto mdogo hawezi kutoa
ushahidi
> mahakamani, haki
> inapuuzwa kwa kuwa mtoto hawezi kutoa ushahidi!
>
>
>
> Kesi ya Ulawiti rais hana mamlaka nayo, anatoa wapi
kiburi
> cha kusema kuwa
> atamtoa? Aliyeagiza polisi kuingia na polisi kuingia
na mbwa
> msikiti wa
> mwembechai ni Sumaye, akiwa waziri mkubwa. Leo hii ni
mpiga
> kampeni wa Lowassa!
> Leo tunataka kura kwa namna yoyote! Ni afadhali
kutokuwa na
> rais wa aina ya mtu
> huyu! anayesaka kura kwa kusaka huruma za watu. Slaa
hayuko
> tayari kuona hilo
> linatokea... Anahitimisha kwa kusema hajagusa
chochote
> kuhusu ilani wala
> mkakati!
>
>
>
> Mwafrika, [01.09.15 15:45]
>
> Kama taifa tuna kazi kubwa ya kuchambua vitu nje ya
> shamrashamra, maneno
> matamu! Tumeshaumwa na nyoka, tusilaghaiwe na maneno
ya watu
> hawa tena! Utendaji
> uliotukuka unapimwa kwa utafiti, sio kwa ukasuku na
kunukuu
> maneno ya
> wanasiasa!
>
>
>
> Lowassa alipokuwa Waziri Mkuu, matatizo ya wakulima
na
> wafugaji yalikuwepo,
> alifanya nini? Lowassa aliwahi kubadili mpaka wa
Monduli na
> Karatu na
> kusababisha mgogoro! Mkampenia wake, Sumaye
alisababisha
> matatizo ya ardhi
> Mvomero, akipora ardhi ambayo ilitakiwa yajengwe makao
makuu
> ya Mvomero!
> Mengine ya Sumaye ameyaweka kiporo, hisa zake za
kampuni
> aziweke wazi kama
> Sekretarieti ya Maadili inavyotaka!
>
>
>
> Kutotangaza mali kunatosha kumtoa mtu ubunge! Sembuse
> Urais?
>
>
>
> ==============================
=========================
>
>
>
> Ukweli huwa una tabia ya kuegemea upande, anasemea
> speculation kuwa ameisema
> chadema peke yake. Anasema amestaafu siasa, hana
chama
> lakini bado anabaki kuwa
> mtanzania, mtetezi wa wanyonge na atabaki hivyo!
Ataendelea
> kuwatumikia
> watanzania kadiri ya Mungu alivyomjalia vipawa! Kama
> alivyoombwa kugombea urais
> 2010!
>
>
>
> Anaweza kuwatumikia Watanzania bila kuwa na chama!
>
>
>
> Anasema kuwa hajapata vitisho kama alivyopata kipindi
hiki,
> inazidi hata wakati
> alipotangaza List of Shame. Rostam ndiye anafadhili
kampeni
> za urais wa
> Lowassa! Anamnukuu vitisho vyake! anakiri kuwa
maaskofu
> wamehongwa, Rostam
> akiwa anaona, m60-m300! Anasema hatenda chama
chochote,
> anasisitiza! Amejitoa
> rasmi siasa za vyama vya siasa... Ataendelea kuwa
msimamiaji
> wa anachokiamini!
>
>
>
> Anawataka watu aliowataja watoke hadharani, anatoa
baraka za
> KIMUNGU kwa nchi
> na watu wake!
>
>
>
> MASWALI!
>
>
>
> Swali: Unawammbia nini Watanzania kuelekea uchaguzi,
ni rais
> yupi anafaa?
>
> Amesema hana chama, hampigii kampeni mtu yoyote!
Amesema
> anafanya uchambuzi wa
> madhara ambayo taifa litapata endapo watamchagua
Lowassa, na
> kwa kuwa na uzoefu
> nao kwa muda mrefu!
>
>
>
> Hataki kufanya kampeni yoyote. Anawaelimisha
Watanzania
> kuacha ushabiki
> utakaowagharimu! Ni watu wachache wanoweza kumtaja mtu
kwa
> majina, kuna tofauti
> ya wanaotaja ajenda tu na wanaotaja majina.
>
>
>
> Rostam alimuambia kuwa ana dakika 5 za kuishi, apige
magoti
> na kusali! Aliweka
> roho yake rehani kwa ustawi wa taifa
hili...Anakumbusha ya
> Mwembeyanga na namna
> Usalama wa Taifa walivyokuwa na tension. Magazeti
mengi
> yaliogopa hata kuandika
> habari, isipokuwa MWanaHalisi!
>
>
>
> Swali: Siasa ingekuwa asset kama angekuja na wabunge
kadhaa.
> Angekuja kama asset,
> mengine yangesafishika? Kulikuwa na vigezo viwili, ama
asset
> na liability,
> yaani hayo madhambi yote aliyoyasema. Baada ya hayo
> wangefanya tathmini kama
> anapokelewa au hapokelewi. Anatoa mfano wa Shirikisho
la
> Afrika Mashariki na
> nchi zinazotaka kujiunga!
>
>
>
> Swali: Waliopokelewa ni makapi. Je wewe ulikuwa kapi
95?
>
>
>
> Anauliza kama watu wanaamini yeye alikuwa kapi?
Tupime
> vigezo... Makapi ni watu
> waliokataliwa na watu wao baada ya kuwa wabunge kwa
muda
> mrefu. CCM wakasema
> kuwa hakuwa mwenzao: hakuwa anahonga, hakuwa anapokea
rushwa
> na kadhalika! Kuingia
> kwa tiketi ya Chadema ulikuwa ukombozi kwake!
>
>
>
> Swali: Umetangaza kustaafu siasa, una kadi za vyama
viwili.
> Unazirudisha au
> unakaa nazo?
>
>
>
> Watanzania tuelimika, kadi sio uanachama. Kadi ni mali
ya
> mwanachama, unaweza
> kuichoma, kuweka kumbukumbu au vyovyote, sawa na kadi
ya
> ndoa ambayo
> hairudishwi hata kama ndoa itavunjika. Tuulize maswali
ya
> kujenga.
>
>
>
> Swali: Anaoneka baada ya kukosa urais anamshambulia
> Lowassa!
>
>
>
> Wapi Slaa alichukua fomu ya Urais, hakuwa na nia na
urais
> wala hawezi
> kukasirika. Tuache ushabiki, tuwe na mtiririko na
kuzingatia
> hoja! Mwandishi
> awe msikivu sana... Ameeleza tangu mwanzo, hana chuki
wala
> ugomvi na mtu
> yoyote!
>
>
>
> Chama cha Mapinduzi kilishakuja kumpa ofa kadhaa
kuachia
> jimbo la Karatu, akaweka
> sharti la mkataba wenye sahihi za watu watatu; Rais,
Slaa na
> Yesu Kristo.
>
>
>
> Swali: Kama wewe uliweza kuhama, wengine nao
hawawezi?
>
>
>
> Dr. Slaa hakuwa na uchafu wowote, tatizo halikuwa
kuhama
> chama, tatizo ni watu
> wa aina gani wanahama chama?
>
>
>
> Swali: Unahamasisha uwazi, mbona wewe umemficha muovu
mmoja?
>
>
> Silaha haziwekwi zote mezani, amewaomba anaowatuhumu
> wajitokeze!
> CHANZO kwa hisani
> ya jf
>
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>  
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>  
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and
hence
> statements and facts must be presented responsibly.
Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed
to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
> from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>  
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email
ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>  
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and
hence
> statements and facts must be presented responsibly.
Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed
to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
> from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email
ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility for any legal consequences of his or her
postings, and hence statements and facts must be presented
responsibly. Your continued membership signifies that you
agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules
and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to
the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving
emails from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment