Hakuna hospitali yoyote mkoa wa dodoma iliyopokea maiti ya mwanafunzi - kwahiyo hakuna mwanafunzi aliyekufa kutokana na vurugu hizo .Hata huko kudhalilishwa , wamedhalilishwaje ? kuna vyombo vya dola - kama mtu ametendwa ndivyo sivyo hiyo ndio kazi yao , ila uwe na ushahidi kama ni wewe mwenyewe kapeleke taarifa kwa wakati .2015-01-17 15:04 GMT+03:00 Demere Kitunga demeredye@gmail.com [Wanazuoni] <Wanazuoni@yahoogroups.com>:Lakini je, kuna mgomo kweli na kama kweli wanafunzi wanaodai haki yao wamedhalilishwa? itakuwa vema zaidi tukiweza tunaweza kuusuta uongo na wakati huohuo kuubainisha ukweli. kwa njia hiyo sisi tutakuwa nje ya ugonvi kati ya ukawa na ccm bali upande wa wananchi ambao idadi kubwa hawana chama.2015-01-17 10:38 GMT+03:00 'Salim Khatri' skhatri@orcis.com [Wanazuoni] <Wanazuoni@yahoogroups.com>:Yes, naunga mkono vita dhidi ya UONGO, UDANGANYIFU, na ULAGHAI popote pale.
Salim.
From: Wanazuoni@yahoogroups.com [mailto:Wanazuoni@yahoogroups.com]
Sent: Friday, January 16, 2015 9:53 PM
To: Wanazuoni
Subject: Re: [Wanazuoni] TAARIFA KUHUSU PICHA ZA VURUGU ZA UDOM TAREHE 14 - 1 - 2015
Bila kujali kilichotokea UDOM
Mie taarifa yangu ilikuwa kueleza ukweli kuhusu picha za uwongo zilizosambazwa mwanzo na watu wakisema ni za tukio la UDOM kumbe ni za ajali tena sio Tanzania .
2015-01-16 15:31 GMT+03:00 ado shaibu adoado75@hotmail.com [Wanazuoni] <Wanazuoni@yahoogroups.com>:
Mshale, nami sina taarifa ninayoweza kuiita ''sahihi''.
Nilisoma maelezo yafuatayo kutoka kwa Julius Mtatiro (kama yupo humu atakuja kufafanua)
.........................................
SERIKALI IMEWATEKELEZA VIJANA WALIOKUBALI KUSOMA DIPLOMA YA UALIMU NA KUACHA KUSOMA KIDATO CHA TANO NA SITA……
Itakumbukwa kuwa serikali ilifanya kampeni kubwa juu ya suala hili mwaka jana 2014. Na ikasema imejiandaa vya kutosha kuwaendeleza vijana hao wa masomo ya sayansi ili wamalizapo diploma ya "chap chap" warudi kwenye shule zetu kuondoa tatizo la ukosefu na upungufu wa walimu wa sayansi.
Vijana hao walidahiliwa pale Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa ajili ya programu hiyo lakini serikali haikuwa imejipanga kuwapa fedha za mahitaji muhimu kama ilivyohitajika. Taarifa kutoka UDOM zinaonesha kuwa, vijana hao wametangatanga na kuomba pesa za kula na kujikimu kutoka kwa wale "wakubwa zao" wanaosoma Digrii hadi imekuwa kero. Unakuta kisichana cha miaka 17 au 16 kinasoma programu hii na hakijapewa pesa za vitabu, chakula na malazi. Kinazunguka kuwaomba wakaka wa digrii ili kiishi, nani kakipeleka kitoto hiki Dodoma?Baada ya vijana hao wanaotokea mikoa mbalimbali ya Tanzania kutaabika bila kupata msaada huku hawana pesa kwa muda mrefu, waliamua kuongozana kwenda kwa Waziri Mkuu na ama Mawaziri na viongozi wengine wa serikali ili suala lao litatuliwe. Wamekutana na ukatili wa kutosha kutoka kwa polisi, wengine wamevunjika na kuumia vibaya.
Mimi ambaye nimepitia misukosuko zaidi ya hiyo wakati naongoza UDSM na TAHLISO, nachoweza kusema ni kuwa vijana wa sasa na wazee wetu wa sasa, hii ndiyo hali halisi ya nchi yetu. Tuna serikali isiyo na mipango na isiyo na haja ya kupanga na kutekeleza chochote "unresponsible government". Iweje tupange kusomesha vijana kwa programu za dharura huku hatuna fedha za kuendesha program hiyo na hasa kutosheleza mahitaji ya gharama za maisha ya wahusika?
Ni hivi karibuni tu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imetangaza kwamba imeshindwa kuwapa mikopo wanafunzi zaidi ya 20,000 kwa mwaka huu peke yake. Nikukumbusheni pia kwamba, bunge la bajeti lililokamilisha kazi yake mwezi Juni 2014 tulijionea ripoti za aibu zikionesha kuwa kuna wizara nyingi tu ziliishia kupata 40% - 50% ya bajeti iliyopangwa. Haya yote ni dalili tosha kuwa tunaishi kwenye "taifa linaloangamia" (a failed state). Kwamba hatuna uwezo wa kupanga na kutekeleza mipango yetu. Kwamba hatuna kipaumbele kwa yale tunayoyafanya.
Watoto wa watu tumewadanganya, wameacha kwenda kidato cha tano na sita kwa nia njema ya kulisaidia taifa lao kutokana na vipaji na elimu yao, badala ya kuwalipa neema na mipango thabiti tunawalipa ubabaishaji, ukatili, nia ovu na jeuri. Vijana hawa wanaoteseka leo kwa ajili ya haki zao wanapata mafunzo makubwa sana. Idadi ya vijana watakaoendelea kuichukia CCM inaongezeka kama mchanga wa baharini maana "Colonialism planted the seeds of its own destruction" – Hakika, hata CCM inapanda mbegu ya kujimaliza wenyewe.
Poleni sana wadogo zetu, poleni sana wana UDOM.
J. Mtatiro,
Alhamisi, 15 Januari 2015,
Dar Es Salaam......................................
AdoTo: Wanazuoni@yahoogroups.com
From: Wanazuoni@yahoogroups.com
Date: Fri, 16 Jan 2015 14:29:11 +0300
Subject: Re: [Wanazuoni] TAARIFA KUHUSU PICHA ZA VURUGU ZA UDOM TAREHE 14 - 1 - 2015
Na pengine kwa baadhi yetu tusiokuwa na taarifa ya nini kimejiri huko UDOM, ingekuwa vyema kama mngetusaidia kwanza with facts (nini kilitokea, lini, wapi, n.k) kisha tuzame kwenye uchambuzi. Nimeone Fumbuka amezungumzia UKAWA na mengineyo, aweza kuwa sahihi ama la, lakini kwanza tupashane habari, au?
2015-01-16 12:34 GMT+03:00 ado shaibu adoado75@hotmail.com [Wanazuoni] <Wanazuoni@yahoogroups.com>:
''Student loans hutumika duniani kote hatujaanza leo''. Kwani kwenye sakata la UDOM wanafunzi walikuwa wanapinga students loans au wanapinga kutopewa mkopo? Ukifuatilia trend za students activism, suala la kupinga cost sharing/student loans lilishanyauka miaka mingi. Sasa wanafunzi wakiandamana hawapingi mikopo, hupinga kucheleweshewa au kunyimwa mikopo.
AdoTo: Wanazuoni@yahoogroups.com; wanazuoni@yahoogroups.com
From: Wanazuoni@yahoogroups.com
Date: Fri, 16 Jan 2015 12:24:10 +0300
Subject: RE: [Wanazuoni] TAARIFA KUHUSU PICHA ZA VURUGU ZA UDOM TAREHE 14 - 1 - 2015
Kiini chake ni vijana wetu tu kupotoshwa na wanasiasa ili wachukie CCM. Ni hawaohawo UKAWA pia wanaenda Mtwara kuwambia wakatale mali "yao" isipelekwe Dar es Salaam na serkali "ya CCM". Wanasahau kuwa hata CUF wakitawala wanafunzi watakuwa ni hawo hawo. Other than that this is fairly straightfoward, student loans hutumika duniani kote hatujaanza leo.
Mwambalule,
Lukani Hai.
-------- Original message --------
From: "ado shaibu adoado75@hotmail.com [Wanazuoni]"
Date:16/01/2015 12:05 (GMT+03:00)
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com wanazuoni"
Subject: RE: [Wanazuoni] TAARIFA KUHUSU PICHA ZA VURUGU ZA UDOM TAREHE 14 - 1 - 2015
Upotoshaji wa picha ni mbaya, I concur.
Lakini, kama Wana-Jukwaa linaloitwa la Wanazuoni, tulipaswa kwenda mbali zaidi na kujadili MASUALA kwenye sakata la UDOM ( Kama yapo):
Nini kiini chake
Hatua za wanafunzi
Hatua za watawala wa chuo
Hatua za vyombo vya usalama
Suluhisho.
AdoTo: Wanazuoni@yahoogroups.com; wanabidii@googlegroups.com; wanazuoni@yahoogroups.com; wanataaluma@googlegroups.com
From: Wanazuoni@yahoogroups.com
Date: Fri, 16 Jan 2015 06:02:38 +0300
Subject: Re: [Wanazuoni] TAARIFA KUHUSU PICHA ZA VURUGU ZA UDOM TAREHE 14 - 1 - 2015
You are saying that someone is playing games with death of our children just so as to score some marks against the CCM government? Just like the non-existent case INCTSD-2?
-------- Original message --------
From: "Yona Maro oldmoshi@gmail.com [Wanazuoni]"
Date:15/01/2015 23:32 (GMT+03:00)
To: wanabidii ,Wanazuoni ,wanataaluma@googlegroups.com
Subject: [Wanazuoni] TAARIFA KUHUSU PICHA ZA VURUGU ZA UDOM TAREHE 14 - 1 - 2015
Nilitoa malalamiko saa 4 zilizopita kwamba Picha inayoonekana hapa chini sio ya UDOM kuliko kuwa na vurugu baada ya FFU kuzima maandamano hayo .
Picha hii ni ya ajali ya BODA BODA kwenye nchi nyingine ambayo sio Tanzania .
Tafadhali angalia Linki zifuatazo nimeweka vyanzo vya picha hii
Gonga Hap goo.gl/9h653D
Gong Hapa goo.gl/aorQGP
--
Baruani I. Mshale
PostDoctoral Research Fellow,CIFOR
Nairobi
--
Yona Fares Maro
Institut d'études de sécurité - SA
__._,_.___
Reply via web post • Reply to sender • Reply to group • Start a New Topic • Messages in this topic (12)
.![]()
__,_._,___--Yona Fares MaroInstitut d'études de sécurité - SA
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:
Post a Comment