Friday, 23 January 2015

[wanabidii] Re: UVCCM MKOA WA GEITA wapinga Mwigulu kustopishwa ziara

TAMKO KWA WANAHABARI UVCCM MKOA WA GEITA.

23/01/2015


Ndugu wanahabari, kwa masikitiko makubwa tumetoa taarifa hii kutokana na hali ya mambo ndani ya chama chetu, Tunatumia fursa hii ili tuweze kuzungumzia mustakabali wa chama chetu cha Mapinduzi.


Taarifa yetu ni fupi kabisa.


Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Geita tumesikitishwa na hatua iliyochukuliwa na Katibu mkuu wa CCM Taifa ndugu Kinana kwa kuzuia ziara za ujenzi wa chama zilizokuwa zikifanywa na Naibu Katibu mkuu Bara ambae pia ni Naibu Waziri wa Fedha ndugu Mwigulu Nchemba ambazo tunaamini kwa mujibu wa katiba ya Chama Cha Mapinduzi zilikuwa zinakwenda vyema kwa kufuata miiko na miongozo ya chama chetu.


Hatua hii inadhoofisha ukuaji wa demokrasia katika kipindi hiki kigumu kwani umoja wetu hauwezi kuwa ndio nguzo ya ushindi wetu hapo Oktoba 2015 bila demokrasia ya kweli ndani ya chama chetu. Tunaungana na vijana waumini wa ukweli katika misimamo ya utaifa ya kijana mwenzetu ndugu Mwigulu kwa hatua yake ya utulivu kwa siku hizi mbili tangu kupewa karipio lile ambalo tunaamini sio la kitaasisi.


Tunasikitika zaidi jana asubuhi 22/01/2015 kwa Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Arusha kuunga mkono karipio hili ambalo kimsingi halina taswira ya lugha ya kitaasisi zaidi ya chembe za udikteta,na uonevu. Tunaamini wenzetu hawa wamekurupuka bila kutafsiri vema aina ya barua na mstakabali wa chama chetu. Sisi vijana tunaamini tunayo dhamana chanya ya kukisemea chama chetu hata kama usemi wetu utawakwaza viongozi wetu wa juu. Vijana wenzetu waache kutumika kwa ujira wa fedha chafu za kifisadi. Rais wa Nchi hii atachaguliwa kwa nguvu ya uzalendo wake,uadilifu na Uchapa kazi unaoendana na uadilifu na sio uchapakazi bila uadilifu kwa kuwa hata vibaka ni wachapakazi katika kazi yao lakini wana nakisi ya uadilifu na Uzalendo


Tunaamini hakuna aina yoyote ya mgawanyiko unaoletwa na watia nia wanaodaiwa hawafuati miiko ya chama kwa kutumia taaluma, nafasi zao ndani ya chama, serikalini na kete ya utajiri katika kuwania madaraka, Tunaamini hivyo kwakuwa tayari watu wote wapo katika adhabu na wanatumikia kwa haki na taratibu za chama.


Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Geita tunaipongeza kamati kuu ya CCM kwa kikao chake cha Kisiwandui Zanzibar na kwa maazimio yote mazuri, tunasisitiza serikali izingatie maazimio hayo na kufanyia kazi mapendekezo kama kamati kuu ilivyoridhia.


Tunamshauri Katibu Mkuu wetu Komredi Kinana atumie fursa hii ndogo ya miezi kumi iliyopo kurejesha umoja na mshikamano ndani ya Chama bila kuegemea upande wowote, Kwakufanya hivyo tunaamini tutashinda kwa kishindo Uchaguzi mkuu hapo Oktoba 2015.


Jonathan Mabihya.
Katibu UVCCM Mkoa wa Geita

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment