Thursday, 22 January 2015

Re: [wanabidii] UVCCM Arusha waunga mkono Kinana kumsimamisha Mwigulu

Bwana Molel, let us leave the nature to take its place.Mkinzano wa watu na fikra ndio chachu ya maendeleo. Sipendi tuwaite wana uchu wa madaraka...coz the reverse may be true. Tuwaache watoe changamoto kama ambavyo katiba inaruhusu...watu wakiwaamini wakawapa...that will be good na wasipowapa na wakampa mwingne is not too late for them. Lkn, changamoto na fikra mbadala should always be there. Ngupula.

'lesian mollel' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Huyu Mwigulu nae anajiamini nini sijui ameshaona nchi ndo yeye anamtumia vibaya Sokoinei....huyu mkuu na januari kwann wana uchu hivi washauiwe watulie tu mika ijayo watatufaaa hawafahamiki na hakuna kitu ambacho tuwakumbuka nacho jamanii.......Lowasa ndio nafasi yake jamani, sawa ni haki yao lakini upepo wao bado haujavuma pande yao
Kwa nchi ilipofikia tunamhitaji Lowasa tu nilishasema utafiti wa kawaida nilioufanya lowasa ndie anakubalika kw awatanzania kwa sasa
Alichofanya kinana ni sawa maana alishaanza kampeni lakini angefanya EDO ingekua shida....kumbukeni mbio za urais 2005  kilichoshinikiza NEC kumpitisha mgombea ni upepo tuu wa wananchi hakuna tofauti na leo

From: Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, January 22, 2015 2:48 AM
Subject: [wanabidii] UVCCM Arusha waunga mkono Kinana kumsimamisha Mwigulu

UVCCM Arusha waunga mkono Kinana kumsimamisha Mwigulu
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UVCCM MKOA WA ARUSHA. 
Tarehe 22/01/2015
Ndugu wanahabari, leo tumeona vyema tutumie fursa hii ili tuweze kuzungumza machache na pongezi zetu kuhusiana na mustakabali wa chama chetu cha Mapinduzi kwa maamuzi stahiki na kuelekea uchaguzi wa 2015
Tutazungumzia mambo mawili makuu:
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha tunaunga mkono hatua iliyochukuliwa na Katibu mkuu wa CCM Taifa Mh A. Kinana kwa kuona umuhimu wa kulinda na kuhifadhi katiba, miongozo na miiko ya chama kwa kusitisha ziara za Mh Mwigulu Nchemba ambazo kimsingi zilikuwa zinakwenda kinyume na miiko na miongozo ya chama.
Hatua hii ni muhimu katika kipindi hiki kwani umoja wetu ndio nguzo ya ushindi wetu hapo Oktoba 2015. Tunampongeza komredi Abdulrahman Kinana kwa hatua hii madhubuti, ni lazima tuzuie aina yoyote ya mgawanyiko unaoletwa na watia nia hawa wasiofuata miiko ya chama kwa kutumia taaluma,nafasi zao ndani ya chama, serikalini na kete ya ujana katika kuwania madaraka huku wakitaka kuwaonea wengine.UVCCM Arusha tulijiuliza,angefanya haya Lowassa angeeleweka?
Pia tunaipongeza kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi kwa kumaliza kikao chake kule Kisiwandui Zanzibar kwakuja na maazimio makini yenye kujenga Chama na kurejesha imani kwa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu, Tarehe 13/01/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake wa Taifa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ilifanya kikao chake cha kawaida cha siku moja Kisiwandui Mjini Zanzibar. Pamoja na mambo mengine baadhi

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment