Tuesday, 20 January 2015

Re: [wanabidii] ULIJIANDAA KIHISIA KABLA YA KUFUMANIA?

Kwanza kuandaa kumfumania mpenzi wako ujue bado hujakua, hujakomaa.
Pili huwezi kutumia neno mwizi wako kwasababu mwili ni wa yule mwenye mwili ila mlikubaliana kuwa, hisia zake za mapenzi uzitatue kwa kushirikiana na wewe.
Mimi ni mmoja wa watu ambao tuliamia sehemu fulani hapa jijini, kufika kule nikakuta kuna watu wanapenda kunyemelea wake za watu nyendo zao kisha kuwafuata wenzi wao na kuaambia mwenzi wako yuko hivi au hivi.
Mimi niliwaambia akiwatuma kuhusu mimi fanyeni lakini mimi hata mkimuona anaingia na mtu chumbani msiniambie kwa sababu bado sijaamua kuachana naye.
--------------------------------------------
On Tue, 1/20/15, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] ULIJIANDAA KIHISIA KABLA YA KUFUMANIA?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, January 20, 2015, 4:49 PM

NA
SAMWEL SASALIKwa
mfano umenasa meseji kwenye simu ya mumeo akiwekeana ahadi
na mwizi wako kwamba wakutane gesti fulani wakaibanjue amri
ya sita. Bila mumeo kujua wewe ukaandaa majeshi yako na siku
ya tukio, mumeo akiwa na mwizi wako gesti, wakiwa hawajui
hili wala lile, mnawafumania, picha za ushahidi zinapigwa,
mashahidi wanaona na mtaa mzima unajua.Au
umegundua kuwa mkeo anatoka na jamaa wa mtaa wa pili wewe
ukiwa umesafiri. Unaamua kumdanganya mwenzi wako kwamba unasafiri na
kuacha wapelelezi wa siri wafuatilie nyendo za
mkeo.Unapoondoka tu, anawasiliana na
mchepuko wake, wanapanga kukutana na kwa kuwa kuna
wapelelezi umewaacha, wanakutonya kila kitu na hatimaye
mnafanikiwa kuwanasa wakiwa eneo la tukio.ULIJIANDAA KIHISIA
KABLA YA KUFUMANIA?
Bila shaka umeanza kupata picha ninachotaka kukizungumzia
hapa. Je, katika mifano ya hapo juu ya mafumanizi ya
kupangwa, wakati unaandaa mipango ya kumfumania mwenzi wako,
kichwani mwako ulikuwa unawaza nini? Ulikuwa umeshajiandaa
kihisia?Ulikuwa unataka
ukimfumania umpe au udai talaka na huo ndiyo mwisho wa
uhusiano wenu au ulikuwa unataka kuhakikisha kama ni kweli?
Ulikuwa unataka kumkomoa mwenzi wako au mwizi wako kisha
maisha yaendelee kama kawaida?Ni ukweli ulio
wazi kwamba hakuna kitu kinachoumiza moyo kama pale
unapogundua kuwa mwenzi wako ana uhusiano na mtu mwingine.
Hata kama unahisi tu, moyo huwa unaumia sana.Yote tisa, kumi
hakuna kitendo kinachoumiza au kinachoweza kukufanya
ukaathirika mno kisaikolojia maisha yako yote kama kumfuma
laivu mwenzi wako akiwa kitandani na mtu mwingine. Awe na
nguo au asiwe na nguo, kitendo cha kuwafuma wakiwa wawili tu
chumbani, kinaweza kukufanya ukatamani ardhi ipasuke na
kukumeza.Hakuna lugha
nyepesi inayoweza kutosha kuelezea maumivu yake, wale
waliowahi kuwafumania wenzi wao watakuwa wananielewa vizuri
zaidi. Ninachotaka tujadiliane na wewe msomaji wangu ni
hiki:Je,
kuna umuhimu wa kumuandalia fumanizi mwenzi wako wakati bado
unampenda na unataka muendelee kuishi pamoja, kulea watoto
na kutimiza ndoto zenu? Naomba uwe huru kutoa mawazo yako
kwa namba za hapo juu halafu wiki ijayo tutaendelea
kuangalia mawazo ya kila mmoja na mwisho kufikia
hitimisho.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment