Wednesday, 21 January 2015

Re: [wanabidii] KANISA KATOLIKI TUAMBIENI KILICHOMUONDOLEA WITO WILBROAD SLAA

Nimesoma maandishi haya sikuona sababu ya kuliuliza Kanisa kutwambia kwa nini Dr Slaa aliacha upadri.
Ni kwa sababu atagombea urais au
Ni kutaka kulisaidia Kanisa liondokane na mitafaruku inalokumbana nalo?
Sioni kujitoa kwa Slaa kwenye ukasisi kunavyoweza kuhusiana na uwezo wake wa kugombea urais na kuliongoza Taifa kama Rais?
Na 'kitendawili' hiki cha muda mrefu sijajua ni cha akina nani wanaotaka kuteguliwa. najua tu kuwa hakimo kwenye sababu za kugombea urais.
Nahitaji kuelimishwa sabau hasa za kutaka kujisumbua kuishughulikia mitafaruku ya kanisa katoliki na uhusiano wetu na uchaguzi ujao. Semi nyingine zinaweza kuchochea hisia za kanisa hili na siasa za nchi hii tukajikuta tunaenda tusikolenga
--------------------------------------------
On Wed, 1/21/15, Oksana Spice <worldngojobs@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] KANISA KATOLIKI TUAMBIENI KILICHOMUONDOLEA WITO WILBROAD SLAA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, January 21, 2015, 7:30 PM

KANISA
KATOLIKI TUAMBIENI KILICHOMUONDOLEA WITO WILBROAD SLAANdugu
wapendwa nawasalimu kwa jina la yeye aliyejuu.Wakati
tukielekea kuwapata viongozi wa kitaifa hapo mwezi Oktoba
mwaka huu wa 2015, nimeona leo niliombe Kanisa Katoliki
lituaidie kutegua hiki kitendawili hiki cha muda mrefu cha
mmoja wa watajwa wenye nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu
ujao alikuwa akilitumikia katika nafasi za juu kabisa za
uongozi.Naamini
Kanisa linajua vema sababu za WILBROD SLAA kuacha kuitumikia
Kanisa kama Padre. JE alifukuzwa au aliacha mwenyewe na kwa
sababu gani? Tupate kujua ili kipindi hiki ambacho
tunaelekea kuwa naye kwenye harakati za kuusaka urais tupate
kujua tuna mgombea wa aina gani.Mimi
ni mzaliwa wa Mkoa wa Arusha na mwenyeji wa mji mdogo wa
Manyara, njiani kuelekea nyumbani kwa Wilbroad Slaa yaani
KARATU.Nimeishi
kwenye mkoa wangu tangu nimezaliwa, nikasomea elimu yangu ya
msingi hadi sekondari kabla ya kuendelea na masomo ya elimu
ya juu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kwa sasa naishi
Dar kutokana na mihangaiko ya hapa na pale ili mkono upate
kwenda kinywaniKanisa
Katoliki mara kadhaa limekuwa likikumbwa na kashafa za aina
mbili na hasa mkoa wa Manyara na Arusha hususan majimbo ya
Mbulu na Karatu, Kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za
Kanisa na ile ya Mapadre kujihusisha na Mapenzi kinyume na
Sheria za Kanisa, nitatoa mfano.PADRE
mmoja wa jimbo la Mbulu(jina nalihifadhi ila kama kuna
mwingine anaifahamu hii scandal anaweza kumtaja ili
kudhihirisha ukweli wa mfano huu) aliwahi kuchukua fedha za
kanisa mil.300 akazipeleka kwa mganga wa kienyeji ili
zifanyiwe madawa kwa kuamini kuwa zitaongezeka, kilichotokea
ni mganga yule kutokomea na zile pesa bila Padre kujua .
Sakata hili liliwagharimu sana waumini kwani walilazimika
kutoa sadaka 3 badala ya 2 kama ilivyo kawaida ili kufidia
pesa zilizopotea. Nakumbuka Sakata hilo lilimhusisha pia
Makamu wa Askofu jimbo la Mbulu wakati huo akiwa father John
Nada ambapo Askofu wa jimbo hilo akiwa Yuda Thadei Rwaichi
ambaye hivi sasa ni askofu wa jimbo la Mwanza.Kuhusu
kashfa ya Mapenzi, namfahamu PADRE mmoja (jina nalihifadhi)
ambaye hivi sasa kituo chake cha kazi kipo KARATU, huyu
ameoa na ana watoto, Mke wake alikuwa mwalimu wa shule moja
ya sekondari ya kata pale Mbulu mjini ambaye kwa sasa yuko
ofisi ya utamaduni katika halmashauri ya Wilaya Mbulu.Nirudi
sasa kwenye hoja msingi, pamoja na mifano hiyo miwili bado
Kanisa limeendelea kuwavumilia watu hao na mpaka leo ni
watumishi wazuri tu wa Mungu, Swali langu ni kosa gani kubwa
ambalo SLAA alifanya ndani ya kanisa? NI muhimu sana
tukaambiwaZIPO
TETESI kuwa mambo yaliomuondoa SLAA kama mtumishi wa Mungu
aidha kwa kufukuzwa ama yeye mwenyewe kuona aibu kuwa ni
pamoja na:Kuhujumu
mradi wa ujenzi wa Nyumba za Masista kule Kurasini jijini
Dar es Salaam wakati akiwa Katibu wa Maaskofu.Kuweka
kibindoni pesa nyingi zilizopatikana kutokana na maandalizi
ya ujio nchini wa papa John Paul wa pili wakati yeye SLAA
akiwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania.Kanisa
tuambieni SLAA alifanya nini huko?Mbali
na hayo ambayo Kanisa lingetusaidia kumhusu Wilbroad Slaa,
lakini pia ingependeza kama SLAA yeye kama yeye pamoja na
kuyajibu hayo ambayo tunawasumbua viongozi wake wa kiroho
pia atujibu haya yanayoongelewa mtaani kuwa:Kupitia
Hospitali ya CCBRT alitengeneza mradi hewa wa kujenga
hospitali ya kisasa kabisa eneo la mlalakua jijini Dar es
Salaam ili apate msaada kutoka kwa wafadhili. Zipo taarifa
kuwa kutokana na mpango huo wafadhili pamoja na kukubali
kufadhili ujenzi wa hospitali hiyo lakini pia walishampa
kiasi fulani cha Magari ambayo yaliingizwa nchini pasi
kulipa kodi na hayajulikani yalipo.Nawasilisha.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment