Thursday, 4 December 2014

Re: [wanabidii] ZITTO KABWE UNAJIANDALIA ANGUKO

Nildhani tunajibu hoja fulani kwa kuhusianisha na issue iliyopo (recent news), kumbe unaweza kujibu au kusema kitu chochote bila kujali muda na uhusiano wa kinachosemwa.

Omary Iddy,DAGROFORESTRY RESEARCH TANZANIA FORESTY RESEARCH INSTITUTE(TAFORI)P.O BOX 1257,SHINYANGATANZANIA.Tel:+255 28 276 3249MOBILE:+255 713 728 672FAX:+255 28 276 2198EMAIL:eidomari@yahoo.com

--------------------------------------------
On Mon, 12/1/14, 'leonard magwayega' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] ZITTO KABWE UNAJIANDALIA ANGUKO
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "Wanazuoni" <wanazuoni@yahoogroups.com>
Date: Monday, December 1, 2014, 10:02 AM

WE KATABAZI UTAACHA LINI
KUROPOKA? AU NA WEWE UMEPATA MGAO WA ESCROW MAANA WAPO
WAANDISHI KAMA WEWE WENYE TAMAA YA PESA NAO
WAMO.

On Saturday,
November 29, 2014 10:48 AM, Yona Maro
<oldmoshi@gmail.com> wrote:


ZITTO KABWE UNAJIANDALIA
ANGUKONa Happiness KatabaziMTUME Muhammad S.A.W amewahi
kunukuliwa akizitaja alama kuu tatu za mnafiki. Ambazo ni ;
"Mnafiki akisema anasema uongo,mnafiki akiaidi hatimizi na
mnafki akiaminiwa ,haaminiki'.Nukuu hiyo ya Mtume inapendwa mno
kutumiwa na rafiki yangu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Rombo
(Chadema), Joseph Selasini,katika harakati zake za kisiasa
tangu nimfahamu akiwa Chama Cha NCCR-Mageuzi.Na nanukuu hiyo ndiyo imekuwa kama
salamu yangu mimi na yeye pindi tunapowasiliana kwa simu au
kukutana hana kwa ana na mwishowe tunaishia kucheka sana
kutokana na sifa hizo za Mnafiki.Alhamisi wiki hii huko Bungeni,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) , Jaji Fredrick Werema
akiwa bungeni alimuumbua Mbunge wa Kigoma Kaskazini ,Zitto
Kabwe kwa vielelezo kuwa Zitto alishakiri chini ya kiapo
ofisini kwa Jaji Werema kwamba hana majina wala akaunti za
watu hao , kinyume cha kauli yake huko nyuma alipowahi
kusema kuwa anawajua.Jaji Werema alilazimika kusema hayo
muda mfupi bungeni baada ya Zitto kusisitiza kuwa serikali
haionyeshi nia ya kuwachukulia hatua walioficha fedha hizo
nje ya nchini.Jaji Werema ambaye ni Mwanasheria
Kitaaluma aliigeukia taaluma yake na kuanza kutoa vielelezo
vinavyopinga kauli hiyo ya Zitto kwamba serikali haina nia
ya kuwawajibisha walioficha fedha hizo, ambapo Jaji huyo
alisema Februali 28 mwaka 2013 , Kamati iliyoundwa
kuchunguza kama fedha hizo ni haramu , kutambua benki
walizoficha , kuandaa mashitaka na kisha kuishauri
serikali."Februali 28 mwaka 3013, Kama
"Februari 28, mwaka 2013, Kamati ilikutana hapa bungeni
katika ofisi yangu na ilipomuita Mheshimiwa Zitto aje atoe
ushahidi, alikuja akatwambia anazo nyaraka na taarifa ila
akaomba ahakikishiwe usalama ili pale ambapo angezileta
pasingelikuwa na mtu wa kumzonga."Pia, alitaka mimi nitoe kiapo
ambacho baada ya kutaja hayo majina halafu ikawa siyo kweli,
basi yeye awe 'free' (huru), kwa hiyo alitaka apewe
kinga ya kiapo."Machi 23 tulipomuita aje
akatukwepa, akasema anakwenda Tanga kwenye mafunzo ya
mgambo, kwa hiyo, tukaona tumsubiri hadi
atakapomaliza."Aprili 12, mwaka 2013, tukakutana
naye hapa Dodoma katika viwanja vya Bunge, akasema hawezi
kutwambia chochote kwa sababu alikuwa akijiandaa kwenda
Afrika Kusini."Mei 4 tulimuita tena kwenye
kamati hapa Dodoma na katikati ya mahojiano alidai ana jambo
muhumu lenye maslahi kwa taifa, akasema anaomba aondoke
atarudi, kamati ilimruhusu, hata hivyo hakurudi
tena."Tulipompigia simu alisema alikuwa
Dar es Salaam na alikuwa 'busy' akijiandaa kwa kongamano
la Kigoda cha Mwalimu Nyerere."Mei 24 kamati ilimfuata Dar es
Salaam, akasema hana nafasi kwa sababu wakati huo alikuwa
akijiandaa kuisaidia Timu ya Taifa," alisema Jaji Werema
na kuongeza:"Kamati iliamua sheria ichukue
mkondo wake kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya
Jinai, Kifungu cha sita ndipo tukachukua maelezo ya Zitto
Kabwe chini ya kiapo na akatwambia hakuwa na jina, wala
akaunti ya Mtanzania yeyote aliyeficha fedha nje."Lakini, leo hapa amesema serikali
haina nia ya kurudisha fedha zilizofichwa Uswisi. Kwa maana
hiyo, Mheshimiwa Naibu Spika, Zitto Kabwe ni mzito na
nakubaliana na Lema (Mbunge wa Arusha Mjini) aliyesema hapa,
kwamba Zitto alete majina hayo.Itakumbukwa kuwa kwa takribani mwaka
mmoja sasa Zitto amekuwa akilandalanda mitaani na kunukuliwa
na vyombo vya habari kuwa kuna vigogo wameficha fedha nchini
Uswis na anawajua. Kweli kwa watu wanaopenda kudakia mambo
bila kufanyia utafiti nao wakajikuta wanaiomba wimbo huo
aliokuwa akiumba Zitto.Ambapo mwisho wa siku Jaji Werema
,Alhamsi ya wiki hii bungeni alikuja kufumbua macho
watanzania kuwa huyu huyo Zitto aliyekuwa anatamba mitaani
kuwa anawajua walioficha fedha, aliitwa kwenye Kamati hiyo
maalum ili akaisaidie kutoa hayo majina ya namba za akaunti
zao lakini hakwenda na matokeo yake Zitto alikwenda ofisini
kwa Jaji Werema chini ya hati ya kiapo kuwa hayafahamu
majina wala akaunti za watu hao.Kisheria tunasema kila tuhuma
inayoibuliwa au kesi inayofunguliwa mahakamani lazima iwe na
mlalamikaji ambaye mlalamikaji huyo anapaswa kufika katika
mamlaka husika kuisaidia kutoa vielelezo anavyodai kuwa watu
fulani wamevunja sheria.Sasa kwa muktadha huu ambapo Zitto
aliaminisha umma kuwa kitendo hicho cha kufichwa fedha nje
ya nchi kimemkera na ushahidi anao, kwanini Zitto huyu kwa
zaidi ya mara nne ameitwa kwenye Kamati hiyo akashindwa
kufika kutoa vielelezo hivyo?Je alikuwa na lengo moyoni na
akilini mwake?Maana tuhuma hizo alizoziibua ni kubwa sana na
serikali yoyote makini nilazima tu ingeanza kufanyiakazi
tuhuma hizo na hivyo ndivyo ilivyofanya serikali ya
Tanzania, baada ya Zitto kuibua skendo hiyo , serikali
iliamua kuunda kamati ya kuchunguza ukweli wa tuhuma hiyo ,
lakini cha kustaajabisha muibuaji wa skendo hiyo Zitto
ambaye alikuwa akijitapa kuwa ana ushahidi, hakuweza kwenda
kwenye Kamati hiyo kutoa ushahidi.Naweza kusema pia kama yaliyosema na
Jaji Werema ni kweli, basi watanzania hatuna budi ya
kumwambia Zitto tena bila haya kuwa anaichezea serikali yetu
sambamba na kuchezea rasilimali watu na fedha za walipa
kodi.Kwani ni yeye aliyeshupalia skendo
hiyo na serikali ikajikuta inatumia fedha za kuunda kamati,
kutumia rasilimali watu na muda wa serikali muda kuja kuhoji
watu mbalimbali ambapo mwisho wa siku Zitto ndiyo alikuwa
mtu muhimu sana wa kuisaidia Kamati hiyo kupata ukweli wa
tuhuma hizo lakini cha kushangaza Zitto inaelezwa alishindwa
kutoa ushirikiano kwa Kamati hiyo.Kama kweli maelezo ya Jaji Werema ni
ya kweli,Je wananchi wamuite Zitto ni Mnafiki ,Mzandiki,
muongo, msahaulifu, au ni mtu anayekurupuka?Maana inashangaza kwa watu wenye
kumbukumbu na Zitto kipindi kile alivyokuwa amekomaa na
skendo hiyo, leo hii Jaji Werema anakuja kuliambia Bunge eti
Zitto ameeleza chini ya kiapo kuwa hana majina wala hafahamu
akaunti za vigogo na kwamba alikwepa kwenda kwenye Kamati
kuhojiwa?Hapo ndiyo ninampomheshimu Mbunge wa
Vunjo(TLP), Agustine Mrema enzi zile alipoibua kashfa wa
wizi wa Sh.milioni 900 kwa mawaziri wa serikali ya awamu ya
tatu iliyokuwa ikiongozwa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa
kuwa wametafuna fedha hizo na kweli Mrema alikubali kuhojiwa
na Kamati ya Bunge na akafunguliwa kesi hiyo katika Mahakama
ya Kisutu na alishinda kesi hiyo.Mrema aliibua kashfa hiyo
iliyomhusisha Rais Mkapa na baadhi ya mawaziri wake kwenye
mikutano yake kisiasa , na alipoitwa kuhojiwa kwenye kamati
ya bunge kipindi hicho hakukimbia, alikwenda na akahojiwa na
mwisho wa siku alifunguliwa kesi katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu kutoka na kuibuka kashfa hiyo ambayo upande wa
jamhuri ulidai kashfa hiyo ni uzushi, lakini mahakama
ilimwachiria huru Mrema.Hivyo Mrema awe ni funzo kwa
wanasiasa wengine walioibuka hivi sasa ambao wanajifanya
mahiri sana wa kudai wanaibua tuhuma za ufisadi lakini
wakiitwa katika mamlaka husika kutoa ushahidi huo
,wanakwepa.Aprili 12 mwaka 2012 gazeti hili
lilichapisha makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari
kisemacho 'Zitto Kabwe ,Mbona U msahaulifu?Maudhui ya makala hiyo nilikuwa
namuelezea Zitto kumbe na yeye ni jamiii ile ya baadhi ya
wanasiasa wale wale wenye hulka za kinyang'au ambao
wanakasumba ya kuzungumza uongo mbele ya umma, ili umma
uwapende na uamini kuwa kiongozi huyo ni mtu safi na mtetezi
wa wanyonge, kumbe siyo kweli. Ieleweke wazi hapo nyuma
Zitto alipata bahati ya kupata umaarufu ndani ya jamii kwa
kile kilichoelezwa ni mwanasiasa kijana ambaye ana misimamo
thabiti na asiyeyumba katika kile anachikiami.Sisi waumini wa sheria tunasema
tuhuma zitabaki kuwa tuhuma hadi pale zitakapothibitika na
mahakama au vikao husika vya chama chake.Lakini kwa kuwa
mungu ni mwema kadri siku zinavyozidi kwenda mbele atazidi
kutuonyesha kama kweli Zitto ni mwanasiasa msafi ,mhadilifu
kuliko wanasiasa wenzake wanaotoka katika vyama mbalimbali
vya siasa.Na kweli utabili wangu huo umetimia
kwa hivi karibuni Kamati Kuu ya Chadema, ikatangaza kumvua
nyadhifa zote ndani ya chama hicho kwa kile kilichodaiwa
kuwa wamebaini kuwa Zitto anakisaliti chama chao.Hali
iliyosababisha baadhi ya wanananchi kuanza kumtazama tofauti
Zitto.Itakumbukwa kuwa Zitto alikuwa
msatili wa mbele kushinikiza baadhi ya watumishi wa serikali
na viongozi wakiwemo mawaziri na Waziri Mkuu Mizengo Pinda
wawajibishwe kwa kile alichokuwa akikidai kuwa wameshindwa
kutekeleza majukumu yao na wengine wamekuwa wakikabiliwa na
tuhuma mbalimbali na kweli kuna mawaziri waliondolewa kwenye
baraza la mawaziri kwasababu ya tuhuma hizo zilizokuwa
zikiibuliwa na Zitto na mwisho wa siku zikaungwa mkono na
wananchi.Waswahili wanamsemo wao usemao
'linalomkuta Boko na Mamba pia litamkuta kwasababu wote
wanaishi majini'. Kwa hiyo yaliyowakuta baadhi ya mawaziri
kwa kuondolewa kwenye baraza la mawaziri kwa kigezo cha
tuhuma tu...ndicho ambacho kimemkuta Zitto leo hii kwa
Kamati Kuu ya chama chake kumvua nyadhifa zake zote kwa
tuhuma kuwa ni msaliti.Iwe Chadema walimsukia zengwe Zitto
na kuamua kumpokonya madaraka kwa kisingizio cha usaliti au
ni kweli.Minaona itakuwa ni funzo sasa kwa
Zitto kujifunza kuwa siyo jambo jema tena kwake kuendelea na
kasumba yake ya kupenda kushinikiza wanasiasa wenzake hasa
wa CCM wawajibishwe au kupokonywa madaraka kwasababu
wanakabiliwa na tuhuma za ufisadi na kuutaka urais mwaka
2015.Kwa uzoefu wangu kwa wanasiasa wengi
wa nchi hii ni mabingwa kuwatengenezea wenzao majungu, fitna
na mwisho wa siku majungu wanayapeleka kwenye vyombo vya
habari kwa kuwatumia baadhi ya waandishi wa habari
kuwachafua mahasimu wao na kweli wanafanikiwa na majungu
hayo kwa kuwachafua maasimu wao na mwisho wa siku maasimu
wao wanachafuka mbele ya jamii na kama asimu wake ni mbunge,
wananchi wake katika chaguzi zijazo wananchi wake
hawamchagui tena kwa kisingizio kuwa mbunge wao huyo
anakabiliwa na tuhuma za ufisadi kumbe wakati mwingine ni
uzushi mtupu.Ushauri wangu kwa Zitto ni kwamba
akubali kuwa ule umaarufu aliokuwa nao zamani umeporomoka
sana na hakuna ubishi kuwa itamgharimu kipindi kirefu sana
kuuurejesha ndiyo atashindwa kabisa kuurejesha.Hivyo ni vyema yeye binafsi ajipe
muda na atafakari ni wapi amekosea hadi leo hii kila kukicha
umaarufu wake unazidi kuporoka, uadilifu wake unatiliwa
shaka na chama chake na baadhi ya wananchi.Kwanini Mwanasheria Mkuu wa serikali
Jaji Werema ameamua kumtolea uvivu bungeni na kumuumbua kuwa
Zitto kuwa aliitwa kwenye Kamati hakufika kuhojiwa na
alipoitwa ofisini kwa Jaji Werema alitoa maelezo yake chini
ya kiapo kuwa hana majina ya vigogo wala majina ya akaunti
za vigogo walioficha fedha Uswiss.Naheshimu mchango wa Zitto katika
medani ya siasa nchini ila sipendezwi na tuhuma mbalimbali
zilizomzingira Zitto kwani wananchi walionekana kumuamini
Zitto kuwa ni mwanasiasa msafi kuliko wengine lakini ghafla
baadhi ya wananchi wanaripotiwa kwenye vyombo vya habari
wakisema hawana imani naye tena.Kwa nini hili Zitto
anaruhusu litokee?Pia namshauri Zitto hivi sasa ni
vyema akajiepusha kujadili hadharani masuala yanayohusu
uadilifu wa wanasiasa wenzake , kwani tayari nayeye hivi
sasa anaandamwa na tuhuma hizo za ukosefu wa
uadilifu.Pia awe makini sana na hao watu
wanaomshauri kwenda kwenye vyombo vya habari kujadili
masuala kadha wa kadhaa kwani hao hao leo hii wanaojifanya
kukushauri kujadili masuala kadha wa kadhaa mbele ya adhara
ndiyo hao hao mwisho wa siku watakucheka.Kwa wanaoifahamu jamii ya
Watanzania, tunaelewa kuwa Watanzania wengi ni kama tuna
ugonjwa wa usahalifu.Tunashikia bango jambo fulani mwisho
siku tunalisahau tunadandia hoja nyingine.Ni sisi watanzania tulishupalia wee
Dk.Steven Ulimboka , Absalom Kibanda, mauji ya Daud
Mwangosi, Idara ya Usalama wa Taifa livyotuhumiwa na Chadema
kuiba kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010,mgomo wa
madaktari ,shinikizo la kutaka aliyekuwa Waziri Mkuu Edwar
Lowassa, na aliyekuwa waziri Andrew Chenge wajiudhuru na
kwamba ni mafisadi, vurugu za kugombea ujenzi wa bomba la
gesi Mtwara na vurugu za kisiasa Arusha lakini leo hii nani
tena anazungumzia mambo hayo.Hakuna.Watoto wa mjini tunasema hivi nyimbo
zinazotamba Tanzania kwa sasa ni kifo cha Rais wa Zamani wa
Afrika Kusini, Nelson Mandela, kile kinachodaiwa ni mgogoro
ndani ya Chadema na Zitto ,Zitto kuvuliwa nyadhifa zake kwa
madai kuwa ni msaliti .Kwahiyo ni vema akatulia ,watanzania
watasahau tuhuma zake.Nimalizie kwa kumtaka Zitto Kabwe,
asikubali kuingia kwenye nukuu hiyo ya Mtume Mtume Muhamad
kuwa; ' "Mnafiki akisema anasema uongo,mnafiki akiaidi
atimizi na mnafki akiaminiwa ,aaminiki'.Mungu ibariki Tanzania0716 774494
www.katabazihappy.blogspot.com
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili,Desemba 15 Mwaka
2013







--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment