Tuesday, 23 December 2014

Re: [wanabidii] WALIOMUITA PRO.MUHONGO NI MUHONGO KAMA JINA LAKE AIBU YAO

Naanza kutafakali 50% kwa 50%...na wanawake wenyewe type hii...unless....

'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

>Jaaa mmoja alikutana na rafiki yake akaanza kushangaa. Huyu akauliza 'Mbona unashangaa' Jamaa akamwambia nashangaa kukuona maana niliambiwa umekufa. Huyu akasema hapana sikufa. Huyu akasema 'Aliyeniambia namuamini kuliko wewe hawezi kunidanganya'
>
>Katabazi anasema kwa kuwa rais amesema hela zilizoko kwenye acount ya ESCROW si za umma basi sio za umma. Kwa nini? Rais kasema. Huyu mtu ana tatizo gani?
>Fedha ziko huko kwa sababu UMMA (kupitia TANESCO) unafikir kuna fedha zake kwa hiyo unasubiri usuruhishi ili (UMMA) upate haki yake. Fedha hizo zimekwapuliwa kabla ya uamuzi kutolewa. Basi kwa kuwa rais kasema wote tunakubaliana naye?
>Siku Rais akiamka na kusema moja kwongeza sita ni tisa Katabazi atawashauri wataalamu wa hesabu wabadilishe majibu. Hii kali
>--------------------------------------------
>On Tue, 12/23/14, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Subject: [wanabidii] WALIOMUITA PRO.MUHONGO NI MUHONGO KAMA JINA LAKE AIBU YAO
> To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Tuesday, December 23, 2014, 12:08 PM
>
> WALIOMUITA  PRO.MUHONGO NI
> MUHONGO  KAMA JINA LAKE AIBU YAO
>
> Na Happiness Katabazi
>
> WALE wazushi,Visarata Mtaa,Washambenga,wenye nongwa Kama
> ndugu wa mume ambao Katika zogo la Escrow,walimu hukumu
> Waziri wa Nishati na Madini, Professa Sospiter Muhongo
> Kuwa  ni Muhongo  kama jina lake na kwamba ni
> fisadi wa Escrwo  Leo hii wameziweka wapi sura zao?
>
> Licha ya Profesa Muhongo kutoa utetezi wake kupitia hotuba
> yake ndani Bunge ambapo pamoja na mambo mengine ,msomi Huyo
> alisema Fedha za Escrwo siyo za umma watu wakiwemo wanasiasa
> uchwara ambao ni wabunge walimpinga  na kumuhukumu Kuwa
> ni Muongo mkubwa Kama jina lake na kwamba Fedha za a Escrow
> ni za umma.
>
> Lakini Jana Baba mwenye nyumba nyumba, Profesa Jakaya
> Kikwete katika hotuba yake alikubaliana na Muhongo Kuwa
> Fedha zile siyo za umma ni za IPTL na hazijaibwa wala
> Kubebwa kwa Magunia Kama Zitto Kabwe wakati akisoma ripoti
> ya PAC bungeni alisema Fedha za Escrow zilibebwa kwa Magunia
> bila kufuata Taratibu ya Sheria ya Benki Kuu.
>
> Waswahili wanamsemo wao usemao ' Mnafki hafi hadi
> ameumbuka'. Hivyo wanafki,Majaji mama DDP ,DCI ,majaji
> ,Mashushushu wa 'Kichina' ,mabush Lawyer ,wazushi na
> mahakimu uchwara ambao mlijipachika majukumu yasiyo ya kwenu
> ya kuhukumu Watu na kuwaita wakina Muhongo ni wezi ,wamekula
> Rushwa ,wamechota Fedha ya umma ya Escrow  hotuba ya
> jana imewaumbua.
>
> Naendelea kusisitiza tuache tabia ya kuhukumu au kushabikia
> jambo wakati Hatuna vielelezo Vya kutosha Kwani tukae
> tukijua uzushi unaumuiza watu wasiyo na hatia Katika baadhi
> ya mambo machafu wasiyo yatenda.
>
> Leo hii kila kona watu wamepandikizwa chuki Mbaya sana
> ambapo baadhi ya wananchi ambao wao wakisikia jambo hawataki
> kilifanya utafiti wanaliamini, wanaamini Muhongo ni fisadi,
> kaiba Fedha za Escrow Kumbe ni uzushi tu unafanywa na wahuni
> wachache kwa Malengo Yao binafsi.
>
> Narudia tena Kusema naipongeza hotuba ya Jana ya Rais Jakaya
> Kikwete Kwani kwa MTu mwenye akili timamu, na aliyekuwa na
> kiu ya kutaka kufahamu ukweli kuhusu zogo la Escrow
> ametambua ukweli ni upi na Kamati ya PAC inayoongozwa na
> Zitto Kabwe kuna baadhi ya mambo iliyopo tosha.
>
> PAC ilipotosha umma Katika ripoti yake ilisema Kiwango Cha
> Fedha kilichokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni Sh.Bilioni
> 306.7. Wakati ukweli ni kwamba kiasi kilichokuwa kwenye
> Akaunti ya Escrow ni Bilioni 202.9. PAC ilisema Fedha za
> Escrow ni za umma, Rais amewaumbua amesema siyo za umma ni
> za IPTL.
>
> Hali iliyosababisha   wananchi kuwajengea
> Chuki ya wazi wakina Muhongo, Profesa Anna Tibaijuka, Katibu
> Mkuu Eliachim Maswi na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa
> serikali Jaji Fredrick Werema ,CCM na serikali kwa ujumla
> Kuwa Si wazalendo kwa taifa na hao PAC na uongo wao Katika
> baadhi ya ripoti Yao ambayo imebainika Kuwa na dosari ndiyo
> wazalendo wa kweli.
>
> Kwa hotuba ya jana naweza kusema Tibaijuka  amepata
> hati yenye Mashaka, Muhongo,Maswi wamepata hati safi. Kwa
> hiyo Hakuna Ofisa wa serikali aliyetaja hati chafu.
>
> Kamati ya PAC mlipewa Fedha za walipa kodi mkafanyekazi kazi
> ya uchunguzi Matokeo yake mmekuja na ripoti ambayo baadhi ya
> uchunguzi wake mlikusanya vielelezo Vya uongo ambavyo
> viliingiza taifa kwenye zogo. Kama ni Waungwana, Ombeni
> radhi kwa watanzania kwa Udhahifu huo ili tuendelee bila
> kuitilia Shaka Kamati yenu siku za usoni .
>
> Hakuna rufaa tena Escrow na mjadala wa Escrow hapa duniani
> uliotungwa na Rais Kikwete rasmi   jana ,
> nafasi iliyobaki ya kujadili Escrow labda  ni mbinguni
> ambako huko hatuna mamlaka nako.
>
> Atakaye pinga hotuba yake kwa sasa atakuwa anapinga na rais
> na anaweza kuhesabika ni mtu anayehatarisha usalama wa
> nchi  maana ki ukweli Rais ndiyo kiongozi juu wa
> Tanzania na ameishasema kuwa fedha za Escrow siyo za umma ni
> za IPTL.
>
> Mnaolazimisha kuwa fedha za Escrow ni za

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment