Saturday, 17 May 2014

Re: [wanabidii] UJUMBE WA VIJANA KULAANI VITENDO VIOVU VYA KUMVUNJIA HESHIMA BABA WA TAIFA

Muhingo.Umeandika ukweli umenigusa.  Vijana hawa wanasoma hizii!!!!
Ernest





Sent from Samsung mobile

'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Nawaonya watanzania.
Kumvunjia baba wa taifa heshima hakukuanza jana. Kumeanza zamani hata kabla hajafa.
Wote tunakumbuka akilalamika kuhusu kuanzishwa kwa azimio la Zanzibar. Kwa maneno yake alisema 'Walikwenda zanzibar wakakaa huko waliporudi wala hawakutuambia walichoazimia. Ila tuliona mienendo yao wenye akili tukajua azimio la Arusha ndiyo basi'
Baadaye ikaimarika sera ya ubinafsishaji. Inasema mashirika ya umma yasiyojiendesha kwa faida yatauzwa. Mwalimu aliilalamikia sana. Namkumbuka akilalamika kuwa mnauza CRDB kwa nini? Mnauza TCC kwa nini. maana mashirika hayo yanajiendesha.

Sasa baada ya kufa Mwalimu ndio wamezidi kumvunjia heshima. Aliacha kuchimba madini ili watanmzania wasome kwanza. Watanzania wamesoma sasa lakini migodi inamilikiwa na wageni na watanzania ni vibarua.

Ardhi iliwekwa kwa ajili ya watanzania. baba yetu wa Taifa amekufa wamekaribisha wawekezaji wanalima maekari makubwa. Mtanzania hawezi kuipata na kuilima. Atailimaje bila kuwekewa mazingira bora ya kukopa? mabenki yetu ukikopa asubuhi unatakiwa kurudisha JIONI. mWANANCHI AMBAYE NCHI YAKE INAMJALI ANADHAMINIWA NA BENKI ZA NCHI YAKE ANAKUJA NA KUPEWA HELA HAPA NA KUANZA KULIMA. HAYO MWALIMU AKIYAJUA ATAVUNJA KABURI ALIMOWEKWA KUJA KUSHANGAA.

Mwisho kwa sasa Aliacha nchi moja na serikali mbili. Aliacha nchi ina rais mmoja anayepigiwa mizinga ishirini na mmoja. sasa nchi ina katiba mbili zinazopingana. nchi ina marais wawili wenye hadhi sawa. Ukisema rais wa Muungano una maana asiye na mamlaka upande wa pili wa Muungano.

Kama vijana hawa si wahuni wa mitaani na kama kweli wanapigania heshima ya baba wa Taifa letu nitawasikia wakiyasemea na hayo. la sivyo wataeleweka kuwa wametumwa.
On Saturday, May 17, 2014 1:07 PM, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:


UJUMBE WA VIJANA KULAANI VITENDO VIOVU VYA KUMVUNJIA HESHIMA BABA WA TAIFA.

Kumekuwepo na kampeni yenye nia ovu iliyoasisiwa hivi karibuni ya kuharibu taswira na heshima ya Baba wa Taifa Mwalimu Kambarage Nyerere katika jamii ya kitanzania na kimataifa. Kampeni hiyo inayoendeshwa na vibaraka wa nchi za magharibi na Ulaya, wazandiki na maadui wa
amani Tanzania imeendelea kusambazwa kwa kasi na kwa gharama kubwa.

Kutokana na kuwepo kwa Kampeni hiyo, jumuiko la Vijana Wazalendo na wapenda Amani tumeamua kutoa tamko hili la kulaani na kupinga vitendo viovu vya baadhi ya watu kumtuhumu, kumkebehi na kumtukana Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwa kutambua Mchango wa Baba wa Taifa kama muasisi wa Taifa hili, mpigania Uhuru shupavu, Shujaa aliyekuwa na mapenzi ya dhati kwa watu wake na kwa kutambua umahiri na jitihada za kujenga Taifa lenye Muungano, Umoja, Amani na Utulivu, jumuiko la Vijana wazalendo limeamua kuukumbusha Umma wa watanzania juu ya mchango wa utumishi uliotukuka wa Mwalimu Nyerere katika ustawi wa Taifa letu, lakini pia kuhamasisha watanzania hasa Vijana kuenzi kwa Vitendo moyo wa kujituma,weledi na busara za kiuongozi, pamoja na ushujaa na ushupavu wa Mwalimu Nyerere.

Sisi Jumuiko la Vijana wazalendo, tumeona ni vyema kuja kumfariji Mama yetu, Mama Maria Nyerere pamoja na familia nzima ya Mwalimu Nyerere na Kwamba sisi kama wananchi na Vijana makini tutaendelea kuwa pamoja na familia katika kupinga na kulaani vitendo hivyo viovu vya kejeli, matusi, tuhuma na kebehi zinazoelekezwa kwa Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwa masikitiko makubwa, tumeshitushwa na kufadhaika kuona chombo kikubwa na taasisi muhimu ambayo ni muhimili mkubwa wa Serikali kama Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania linakuwa ndio uwanja wa matusi ya kumtukana muasisi wa Taifa hili, imetusikitisha na kutufedhehesha. Imefika wakati sasa, kwa Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kudhibiti na kuondoa kinga yake kwa wale wote ambao kwa ujinga na kutumika wameamua kuanzisha na kuendesha kampeni kabambe ya kutia doa taswira na heshima ya Baba wa Taifa.

Imetolewa na:

Mohamedi Nyundo.

Kiongozi wa Jumuiko la Vijana Wazalendo na Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Pwani.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment