Thursday, 15 May 2014

Re: [wanabidii] UJUMBE KWA WACHUNGAJI, MAPADRI NA WAKRISTO

Ndugu Anna,ukisoma kitabu cha ufunua,Yesu anasema kwa kanisa la..
...na kanisa la.....andika. Ujumbe kusema kanisa haimaanishi Mungu anazingumzia kanisa. Binafsi nilipousoma ujumbe huu sikutaka kufikiri sana kama author ni nani,lkn je kinachoelezwa ni kweli ukilinganisha na nyakati zetu hizi?Nikajua ni ujumbe wa kweli na unaofaa kuusikia na kubadilika.Ngupula

'annesekiete sekiete' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Pole ndg.yangu MUNGU gani huyo aliye na makanisa?tunaambiwa tusome maandiko tusije angamia.MUNGU mmoja,KANISA moja,na UBATIZO mmoja.barikiwa.

Sent from Yahoo Mail on Android



From: 'frank patrick materu' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
To: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: [wanabidii] UJUMBE KWA WACHUNGAJI, MAPADRI NA WAKRISTO
Sent: Thu, May 15, 2014 6:36:57 AM



Bwana Mungu asema" Nataka toba ya kitaifa ya kanisa, maombolezo na vilio" 

Ulipokelewa na Dkt. Augostino Maquengo
 
Bwana alinitembelea asubuhi mara tu nilipofika ofisini. Niliuhisi uwepo wake kisha mkono ukanijia juu ya mabega yangu. Nami nilihisi moto juu yangu na nikaisikia sauti ya Bwana ikiniongelesha ikisema: " Yaandike haya na uwaambie." Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenyezi Mungu kwa wachungaji, wainjilisti, mapadri na watumishi wengine:  "Ghadhabu yangu itawamaliza" Nanyi hamtanyakuliwa, kwani mmeziacha njia zangu na kuwafanya kondoo wangu mali yenu binafsi na chanzo cha utajiri wenu.
 
Kwa hiyo Bwana  asema, sitawanyakua wachungaji hawa, wanjilisti na watumishi wangu waliopenda mafanikio na kunyakuliwa, badala ya ujumbe wa toba, kubadilika, na kuja kwangu ambako kuko karibu. Kanisa wanalolisema kuwa langu, limekuwa ukumbi wa starehe likiongozwa na wachungaji, mapadri na mashemasi wa kanisa. Wanakula na kunywa na kusherehekea nyumbani mwangu na mbele yangu pasipo kuogopa, kutetemeka au kuniheshimu. 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment