Tuesday, 20 May 2014

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] SABABU ZA CCM KUKATAA KATIBA MPYA

Hata hivyo ikumbukwe kuwa hili wazo la katiba mpya sio wazo lao! Ilikuwa ni shinikizo tu kutoka upinzani.

On Wednesday, 21 May 2014, 0:56, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:



Kumbuka walivyobadilisha Sheria na kuvunja tume mara baada ya (tume hiyo) kuwasilisha draft ya Katiba badala ya tume kuwemo bungeni ili kujibu hoja zote ambazo hazina majibu wakati wa Mjadala. Jiuliza walikusudia nini.
Kumbuka walivyobadili ratiba ya uwakilishaji hoja na ufunguzi wa Bunge. Eti Tume inawakilisha hoja yake kabla bunge halijazinduliwa na Rais.
Mambo haya na mengine unaogopa kusema na chama kinazeeka? Wana lengo la kulifikisha taifa katika ilipofikia Somalia? hawalioni hilo kweli.
nafika mahala nawaza kuwa mijadala hii ina maana gani kuwaambia wajumbe wa CCM busara wasiyoweza kuikubali. Nani angetarajia Kinana na mangula wangeuingia upuuzi huu? Kwa tunaowajua tangu enzi za mwalimu????
On Tuesday, May 20, 2014 10:13 PM, Tumaini Makene <makenet84@gmail.com> wrote:


Umeweka mfupa kwenye kisu au kinyume chake...pia ni sahihi zaidi!
Watu wengi hawajui kwa nini CCM walilazimisha mjadala uanze na Sura ya Kwanza na Sita!
Watu wengi pia hawajui kwa nini CCM kupitia maoni ya walio wengi walikuwa wakisema vipengele c, e na f kwenye Ibara ya 5 Sura ya Kwanza ambayo inahusu tunu za taifa (walikuwa wanatamka hetufi tu bila kusema vinahusu nini) viondolewe.
Ukiangalia vifungu hivyo ndivyo vilikuwa vinahusu uwazi, uadilifu na uwajibikaji.
On May 20, 2014 9:58 PM, "'Gikaro Ryoba' via Mabadiliko Forum" <mabadilikotanzania@googlegroups.com> wrote:

Kwa uchache, vifuatavyo ni vifungu vilivyomo katika sura mbalimbali za Rasimu ya Pili ya Katiba ambavyo ni vigumu kumeza kwa wanaCCM, hali iliyowafanya wavuruge zoezi la upatikanaji wa Katiba Mpya ili katiba ya zamani iendelee kutumika kwa manufaa yao. Kisingizio cha gharama za kuendesha Serikali 3 ni kiinimacho tu:
 
1.-(2) Jamhuri ya Muungano itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa zifuatazo:
(a)   utu;
(b)   uzalendo;
(c)    uadilifu;
(d)   umoja;
(e)    uwazi;
(f)    uwajibikaji; na
(g)   lugha ya Taifa.
 
SABABU:
Hizi tunu za Taifa ni mwiba mkali kwa CCM kwa kuwa hawana utu, uzalendo, umoja, uwazi wala uwajibikaji wowote. Hawana mpango wa kuzizingatia tunu hizi, ndio maana wanazipinga kwa nguvu zote ndani ya bunge la katiba huku watanzania wote tukiwasikiliza kwa mshangao mkubwa. Kila raia mwenye uchungu na nchi hii ameshikwa na bumbwazi kusikia kwamba CCM hawataki Tunu za Taifa. Hivi hawa CCM wanataka kutupeleka wapi jamani?
 
13.-(2) Dhamana ya uongozi na heshima kwa kiongozi wa umma itazingatia mambo yafuatayo:
(a)   uteuzi kwa misingi ya mwenendo wa mtu, uwezo, sifa, au uchaguzi uliyo huru na wa haki;
(b)   uwezo pasipo upendeleo katika kufanya uamuzi, na kuhakikisha kwamba uamuzi haufuati udugu, ukabila, udini, upendeleo, rushwa au ubaguzi wa aina yoyote.
 
SABABU:
  1. Kidonge hiki ni kichungu sana kwa CCM kumeza. Watanzania tunashuhudia jinsi serikali ya CCM inavyogawa vyeo kwa makada wake kama zawadi bila kuzingatia elimu, weledi, uwezo au sifa. Wakuu wa mikoa na wilaya huteuliwa tu kama njugu kwa makada au marafiki wa mwenye mamlaka ya uteuzi bila kuzingatia elimu au uwezo wa wahusika. Mara nyingi tumeona watu wa ajabuajabu, wasiokuwa na elimu na uzoefu wowote wakiteuliwa kushika vyeo hivi vya kifalme. Hali ni hiyo hiyo hata katika uteuzi wa watumishi wa umma kama vila makatibu wakuu, mawaziri, wakurugenzi, nk.
  2. Sote ni mashahidi jinsi serikali ya CCM ilivyojaa upendeleo, rushwa, ukabila, udini, na ubaguzi wa kila namna. Uteuzi wa viongozi wa umma katika nafasi mbalimbali za utumishi hutolewa kwa upendeleo na kwa itikadi za kidini, kikabila na hata kikanda. Kwa hiyo, CCM hawakipendi hiki kifungu kwa kuwa kinawabana wasifanye madudu katika ofisi za umma na kuteuana kishikaji katika kujaza nafasi za utumishi wa umma kama walivyozoea.
 
 
 
42.-(1) Kila mtu ana haki ya:
(a)   kupata fursa ya kupata elimu BORA bila ya vikwazo;
(b)   kupata elimu BORA ya MSINGI bila ya malipo na inayomtayarisha kikamilifu mwanafunzi ama kuendelea na elimu ya ngazi inayofuata au kuweka msingi wa kuanza kujitegemea;
(c)    kupata elimu BORA inayotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu; na
(d)   kupata fursa sawa ya kupata elimu ya juu ilimradi ana sifa stahiki za kupata elimu hiyo, bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
 
SABABU:
  1. CCM hawapendi kuona watanzania wakipata elimu BORA kwa kuwa wanafahamu fika kwamba wananchi wakielimika hawatatawalika. Kwa kuwa wanafahamu kwamba mtaji wao ni ujinga wa watanzania, hawako tayari kuwaelimisha kwani kufanya hivyo ni sawa na kunoa kisu ambacho kitawakata wao wenyewe. Badala ya kuboresha elimu, wako tayari kufungua shule za kata ambazo zinazalisha vilaza zaidi.
  2. Kwa kuwa haki hii itakuwa ni ya kikatiba itakuwa rashisi kwa wazazi ambao watoto wao hawajaelimishwa ipasavyo kufungua kesi mahakamani kuidai serikali fidia, jambo amabalo CCM hawataki hata kulisikia. Wanataka watu waendelee kueleimishwa chini ya kiwango, huku wakikwepa kuchukuliwa hatua kwa uzembe huo.
  3. CCM hawataki kuona wanafunzi wakisoma bure kwa sababu fedha ambazo zinatengwa kwa ajili ya elimu huliwa na mafisadi wa CCM bila ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Wahisani hutoa Tsh 10,000 kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi kwa mwaka lakini fedha hizo haziwafikii wanafunzi ila huishia kwenye matumbo mapana ya mafisadi wa CCM. Hili suala likiwa la kikatiba, CCM watashitakiwa kwa kushindwa kufikisha fedha hizo mashuleni, jambo ambalo wasingependa liwatokee.
 
 
101.-(2) Watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa Mawaziri au Naibu Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano:
 
(a)   Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wabunge wa Jamhuri ya Tanganyika, Wajmbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar au madiwani katika Nchi Washirika.
(b)   Mtu aliyewahi kutiwa hatiani kwa makosa ya ubadhirifu wa mali za umma, ama katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali za Nchi Washirika.
 
SABABU:
  1. Wabunge wa CCM wamezoea kuteuliwa kuwa mawaziri hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kutafuna rasilimali za taifa bila kunawa. Hawawezi kukubali waukose uwaziri kwani kwao uwaziri sio utumishi bali ni ulaji na utapanyaji wa mali za umma na rasilimali za taifa.
  2. Watu wengi wa CCM ni mafisadi. Kamwe hawakipendi kifungu hiki kwani wengi wao watakosa vyeo endapo katiba mpya itapita na karibu wote wataishia Segerea. Wangependa tuendelee na katiba iliyopo ambayo haina meno ya kuwabana mafisadi na wabadhirifu wa mali za wananchi.
 
125.-(2) Mtu hatakuwa na sifa za kugombea kuteuliwa kuwa mbunge ikiwa:
(a)   mtu huyo aliwahi kuwa Mbunge kwa vipindi vitatu vya miaka 5
 
SABABU:
  1. CCM hawapendi kuwepo na ukomo wa ubunge kwa kuwa wanadhani kwamba wao walizaliwa kwa ajili ya kutawala.
  2. Kuwa mbunge kunawawezesha CCM kuteuliwa kuwa mawaziri hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kufanya ufisadi na kutafuna mali za umma. Na kwa vile CCM ni mafisadi wa kutupwa hawataki kabisa kupoteza fursa hii adhimu ya kuendelea na ufisadi wao wa jadi.
 

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/1400612301.69236.YahooMailNeo%40web125302.mail.ne1.yahoo.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


No comments:

Post a Comment