Tuesday, 20 May 2014

Re: [wanabidii] KASHFA YA ESCROW ISITUVURUGE

Wadau nimeisoma vizuri makala ya Bi Happines Katabazi, na pia nikazisoma comments za Bw. Julius Mtatiro kisha nikapata majibu yafuatayo.
Tatizo la kifalsafa
1.      Mashaka ya Mtatiro yapo mbali kuliko hata makala yenyewe kwa maana ya kwamba ingawaje Katabazi anao uhuru wa kutoa maoni yake lakini chombo anachokitumikia kinamilikiwa na watu wa CHADEMA. Kwa mwandishi makini na mkongwe kama bibie huyo anafahamu fika "editorial policy" ya gazeti lake. kwa hiyo akiandika habari ambayo ni controversial basi ni lazima watu waweke mashaka kwamba anamtumikia nani?
2.      Inawezekana hata shaka hiyo ya Mtatiro ikaongezeka zaidi katika kipindi hiki ambacho CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi wameungana katika UKAWA umoja ambao sasa unaelekea kuunda kitu kama political alliance kitu ambacho ni habari njema kwa wanamageuzi na Watanzania wote wanaoitakia mema nchi yao.
3.      Jazba ya Katabazi ya kutukana watu na kuwaita majina ya ovyo ovyo labda ndiyo iliyomtia mashaka zaidi Mtatiro. Hapa nachota kipande chake kutoka kwenye para ya mwisho kama kilivyoandikwa na yeye mwenyewe bila kurekebisha chochote..
"tusiwe wepesi kuamini   kila kitu kinachoibuliwa na baadhi ya wanasiasa wetu uchwara Kwani wengine ni Mavuvuzera wa wafanyabiashara, makampuni  na wanasiasa,na makuadi wa Makundi yanayoasimiana Katika magomvi Yao ama ya Kugombea Tenda Fulani, Biashara , vyeo na magomvi mengine".  Kitaalamu mimi kama mwandishi naweza kuhisi kwamba katika makundi hayo yanayohasimiana yeye pia ana kundi lake sasa ni vigumu kufahamu analitumikiaje kundi hilo na hasa ukizingatia kwamba yeye ni mwandishi na mwanafunzi wa wa sheria.
 
     Tatizo la uelewa
1.      Tatizo la Bi. Katabazi katika muktadha wa makala yake na majibu aliyoyatoa baada ya kukosolewa na wasomaji wengi, ni uelewa mdogo juu ya utendaji katika mifumo yenye kuendekeza rushwa. Ili kupata picha halisi ningemshauri asome vitabu viwili muhimu:
i.                    Maurice Duverger: Politics the Master Science
ii.                  Patrick Chabal & Jean-Paschal Daloz: Africa Works: Disorder as Political Instrument
kimsingi vitabu vyote hivyo viwili vinazungumzia juu ya vitu viwili vinavyoitwa "patronage" na "coalescence". Katika patronage suala ni je nani anamteua yupi? mfumo wa uteuzi umekaaje? na hapo ndipo linakuja jambo la coalescence likimaanisha kwamba baada ya uteuzi wale walioteuliwa hutendaje kazi zao? kwa maana hiyo uteuzi ndiyo una maana kubwa kuliko hata hizo sheria anazozingumzia Bi. Katabazi au kwa lugha nyepesi mahakimu na majaji hupindisha sheria ili kukidhi matakwa ya wanasiasa waliowateua au wakati mwingine kwa kulinda maslahi na nyadhifa zao kwa hiyo hizo sheria hubakia kama maandishi yasiyokuwa na uzito wowote. Hivyo basi kwa muktadha huo, CAG, PCCB. Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa n.k. wanaweza kutumika kisiasa zaidi kulingana na nani ameteuliwa kuongoza taasisi hizo nyeti.
 
Farasi wa huruma
Farasi wa huruma ni neno ambalo nimelitafsiri japo siyo katika tafsiri rasmi likimaanisha "inept horse" hilo ni neno linalotumika katika siasa pia katika journalism kimsingi Mtatiro hakumkosoa Katabazi kwa sababu ni mwanamke bali kwa sababu aliona kasoro katika makala ile, sasa hili la kuwadharau waandishi wanawake linatoka wapi? inept horse ni farasi anayedandiwa na watu pale wanaposhindwa kujenga hoja zikakubalika na hivyo hukimbilia katika kitu ambacho kinaweza kuwapatia kuungwa mkono kwa huruma. Ndiyo maana mwanasiasa Mkristu akishindwa kuongoza nchi atasema naonewa kwa sababu mimi ni Mkristu na mwanasiasa Muislamu akishindwa atasema vivyo hivyo naonewa kwa sababu mimi ni Muislamu…hapo atakuwa anadandia farasi wa huruma ili watu wa dini au dhehebu lake wamuunge mkono. nawatakieni siku njema.
Elias Mhegera-0754-826272
Elias Mhegera
Media & Information Officer 
Tanzania Human Rights Defenders Coalition 
Tel: 255-0754-826272
        255-0715-076272
Email: mhegeraelias@yahoo.com 
             mhegera@gmail.com 
The only thing we have to fear is fear itself 
On Wednesday, May 21, 2014 2:51 AM, 'Julius Mtatiro' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Dada Happiness Katabazi,

Nilichelewa kusoma maoni yako kwa sababu ya kuwa na ratiba ngumu. Nakuandikia majibu haya nikiwa katika treni kutoka Dortmund kwenda Berlin hapa Ujerumani. Pole sana na nisamehe  kwa kukuudhi na maoni yangu. Narudia kukuomba unisamehe ikiwa chochote kimekukwaza baada ya kutoa maoni yale. Baada ya kusoma maoni yangu haya ya pili naamini kuna chochote cha msingi utakipata hata kama ni kidogo. Na hicho kiendelee kusaidia na kuboresha uandishi wako ambao nitaendelea kuuheshimu.

INFACT, niliandika mistari michache tu mara baada ya kuwa nimesoma makala yako na kwa kweli nilitarajia mjadala utakuwa wa hoja zaidi. Kama mwandishi mzoefu sana nilitarajia utakuja na hoja za msingi za kutetea msimamo wa makala yako, kwa bahati mbaya umehama kabisa huko, umetumia muda mwingi kunishambulia, kunionesha mie si lolote, ni mwanasiasa uchwara, ulinipa hisani sana wakati nimetiwa gerezani kwa masuala ya utetezi wa wanafunzi wa vyuo vikuu, ulivyoisaidia CUF n.k. 

Kwa bahati mbaya, vyote ulivyovieleza havina uhusiano wowote na makala yako na havina uhusiano wowote na maoni yangu juu ya makala yako. Kwa kifupi umejaribu kuanzisha mambo mengi na kuyakuza ukijaribu kuyaoanisha na hoja yako lakini bado hayajaunganika, na kwa wachambuzi wazuri na wasahihisha mantiki za habari na masuala kadha wa kadha wanaweza kupata mwanya mkubwa wa kuonesha mapungufu zaidi na zaidi.

Mbaya zaidi, umejaribu kujificha nyuma ya waandishi wa kike kwa kutumia dhana ya siku hizi ya "haki za wanawake" ili wenye huruma waone hivyo na kuniona mie ni mpuuzi na kiongozi nisiyejitambua na nisiyejua umuhimu wa ninachokisema. Huko ulikoenda kujificha nitakutoa dada! ntakuleta hapa sebuleni tujadiliane juu ya hoja. Na ulichosahau dada yangu ni kuwa kila neno binadamu aliandikalo huwa linajibiwa. Sasa katika kuyatafakari mashambulizi yako nitajikita katika maeneo kadhaa;

Eneo la kwanza nitakaloanzia, umeeleza kwa kirefu namna ulivyo mwandishi nguli na mwanasheria makini, nitakuonesha mapungufu yako katika jambo hilo na kukuachia ujipime mwenyewe, lakini kubwa nitataka ujifunze zaidi kuwa hizo sheria unazojua na huo uandishi ulio nao ni safari moja tu, lakini lazima utambue kuwa, wewe kama binadamu una safari ndefu mno ya kujifunza zaidi na zaidi kwa sababu hata waandishi NGULI kama Jenerali Ulimwengu hadi leo wanaendelea kujifunza na wenzio wakikosolewa wanaleta hoja, hawaji na matusi, dharau, kejeli na kujinasibu.

Pili, nitaongelea dhana ya kuandikiwa makala yako na nitakujulisha mantiki yangu huku pia nikikuongezea mbinu za kuwa mstahimilivu ili uendelee kuwa na mchango mkubwa katika jamii na kwa muda mrefu.

Tatu, nitaongelea suala la mimi kuwa mwanasiasa uchwara, Kafulila  na Zitto kwa upande mwingine, kwa sababu sote umetugusa na U-UCHWARA katika siasa, hapa nitakupa mifano michache.

Nne nitaongelea ukinda wangu katika siasa na nitakubaliana na mtizamo wako huku nikikazia dhana ya mimi kujiunga CUF pamoja na dhana ya harakati za mageuzi na uchanga wangu.

Tano, nitaongelea dhana ya kudharau waandishi wa kike huku nikiiunganisha na mantiki ya makala yako ambayo niliitolea maoni.

Sita, nitajadili dhana ya kuwa KINARA na MZUSHA VURUGU pale UDSM na namna nilivyokuwa nikimbembeleza mhariri wako ili mje kunisaidia kuripoti kesi ile pamoja na taswira ya AIBU niliyopata kwa kutupwa kizimbani kwa kutumia DEFENDER ya polisi.

Saba, nitakupa ushauri wa bure kama mwandishi ninayemheshmu sana. Masuala hayo saba yatakuwa ufafanuzi wangu wa kina katika hoja yako ya awali. Yote haya saba nitayaeleza katika barua pepe ya pili baada ya hii. Naomba uendelee kufuatilia.

-----------------------------------------------------
Julius Sunday Mtatiro,
Deputy Secretary General, 
The Civic United Front (CUF),
Tanzania Mainland, 
P.O Box 10979, 
Dar Es Salaam - Tanzania. 

Office Tel;   +255222862506,                  
Phone;       +255717536759
Email;        juliusmtatiro@yahoo.com 
Twitter;       https://twitter.com/Julius_Mtatiro 
Face book; https://www.facebook.com/julius.mtatiro 
Website;    https://www.cuf.or.tz
    
On 20 May 2014, at 23:36, "'ananilea nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Binti yangu Katabazi.
Awali nikupongeze kwa juhudi kubwa unazozifanya kulijenga taifa letu. Pili  niungane  na waliotangulia kukushauri kuwa kabla ya kupeleka gazetini makala yako ni vema ukaisoma kwa umakini kuepuka makosa ya  yasiyo ya lazima.
 
Tatu  napenda kukukumbusha kuwa  siyo kila anayeshinda kesi mahakamani ndiye aliyestahili haki katika kesi husika.  Katika  nchi zinazoendelea hasa   zile  ambazo   zimegubikwa na rushwa na ufisadi si ajabu  mwenye haki akaikosa  mahakamani. Kadhalika si ajabu wajanja, wakiwepo watawala wajanja wakasuka dili za kifisadi  kuibia umma kwa  kutumia udhaifu uliopo katika  mifumo  ya kuendesha nchi ikiwepo mifumo ya sheria . Nasi wanahabari tunapaswa kujua hili na tusimame imara kupigania mabadiliko. 

Vile vile  kwa maoni yangu naona wanasiasa nao wanapaswa kutumia majukwaa yao ikiwa ni pamoja na Bunge  kuibua na kuchunguza dili za kifisadi hata kama ufisadi huo hauwezi kutiwa hatiani kutokana na udhaifu uliopo katika sheria za nchi. Tukikaa kimya nchi itaendelea kuliwa na wajanja wachache humu umma mpana ukitaabika kwa ufukara.
 
Hivyo kwa mtazamo wangu  naona  si sahihi wewe  kutolea mfano kesi ya  DOWANS  kwamba  kampuni hiyo ilishinda kesi  ingawa awali   wanaharakati na baadhi ya wanasiasa  walikuwa wamepiga kelele kwamba kuilipa DOWANS  ni kuibia  wananchi mchana kweupe, wananchi ambao kila uchao wanaumia kwa kulipa gharama kubwa za umeme kila uchao.

On Tuesday, May 20, 2014 8:24 PM, 'mhegeraelias' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

My dear friend Happy Katabazi usipende sana malumbano na watu bali chukua mazuri dharau kejeli it is true bado inayo nafasi na safari ndefu ya kujifunza vyote sheria na uandishi ndiyo maana hata watu wenye Phd huwa wansoma post doctoral studies!

'Joseph Haule' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Unsubscrib
On Tuesday, May 20, 2014 2:56 PM, 'jbifabusha' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Ningekuwa mwandishi mzalendo ningeweka kichwa cha habari "KASHIFA YA ESCROW ISIPUUZWE"

Sent from Samsung Mobile

-------- Original message --------
From: Nzweke Mussa <tugutunm@gmail.com>
Date:
To: Mailing List <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: Re: [wanabidii] KASHFA YA ESCROW ISITUVURUGE

Duh.....!!!

Nzweke Mussa Tugutu
Area Sales Executive
Nyanza Bottling Company Ltd
Box 1242
Bukoba, Tanzania.
Mobile: +255754894535
+255784894535
Mail ID: tugutunm@yahoo.com
tugutunm@gmail.com
Instagram: nzweke
On May 20, 2014 1:30 PM, "Mgaywa GMD Magafu" <gmdmagafu@gmail.com> wrote:
Dada Happy. Utakavyo "go and make a correction", tafadhali fanya proofreading. Usifanye "proof leading". Hiyo "proof leading" nina wasiwasi inaweza tena ikaingiza human error kwenye makala yako.

2014-05-20 10:22 GMT+02:00 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Asante kwa kusoma ila namimi sikubaliani na mtazamo Wenu ila na heshima.minataka Kuonyesha nimekosea para gani.ili Niobe kweli nimekosea.mkieleza kijumlajumla siwawezi.ni kweli nimesema sikubali wala sikatai Kuwa tuhuma zilizoibuliwa na rafiki yangu Kafulila Kuwa ni za uongo au ukweli kwasababu Tayari serikali na Bunge kupitia Mh.makinda na Pinda wameishaigiza TAKUKURU na CAG wafanyeni uchunguzi, Ndio kwanza wapo Kwenye uchunguzi lakini baadhi yenu mmeishatoa hukumu.Misio wa hivyo naheshimu Sheria na vyombo husika kwasababu vimeanzishwa KWA Sheria za nchi,papara ya nini.tusubiri ripoti ya uchunguzi Ndio tutafanikiwa ni kweli au uongo.kwani ni uongo hapa nchini Hakuna wanasiasa uchwara ambao wanapenda kudandia Gari KWA Mbele?Najiamini Makala yangu ipo sahihi anayepinga aichambue nimekosea wapi.ni kweli inawezekana Ina matatizo proof leading but in law we sa that is human error ,I will go and make a correction.
Sent from my iPad

On May 20, 2014, at 9:56 AM, "'Jovi kamuntu' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Hapiness Katabazi,

Kama Happiness alikuwa ana cha kuandika ungeacha tu. Kwasababu makala yake imeenda mbele na kurudi nyuma. Hapingi wala hakubali

Mimi sikuelewa huyu Happiness ana maana gani.

Jovin Bifabusha
DIRECTOR
KWF
P. O. Box 313
Skype: jovin.bifabusha
Karagwe, Tanzania

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

No comments:

Post a Comment