Monday, 19 May 2014

Re: [wanabidii] KASHFA YA ESCROW ISITUVURUGE

Katabazi.

Nimekuelewa vizuri sana. Ndio maana Jakaya anasisitiza " akili za kuambiwa changanya na zako".

Tutabwatuka huku, Halafu kesho na kesho kutwa wanaelewana Halafu wanasema eti 'KWENYE SIASA HAKUNA URAFIKI WALA UADUI WA KUDUMU'..

Sent from Yahoo Mail on Android



From: 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
To: WANABIDII <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: [wanabidii] KASHFA YA ESCROW ISITUVURUGE
Sent: Mon, May 19, 2014 7:00:07 AM

KASHFA YA ESCROW ISITUVURUGE

Na Happiness Katabazi
MIONGONI wa Wimbo unaotamba hapa nchini ni Homa ya Dengue na kile kinachoitwa eti ni vigogo wa serikali  wanaotuhumiwa kuhusika Katika kashfa  ya ufisadi  wa Sh Bilioni 200  Katika Akaunti ya Baraza la Usuluhishi la Migogoro ya Kibiashara (ESCROW) ya Benki Kuu (BoT).

Makala yangu itazungumzia Wimbo huo wa pili wa kashfa ya ESCROW ambayo  Mbunge wa Kigoma Kusini(NCCR-Mageuzi), David Kafulila amedai Kuwa ndiye yeye ameiibua kashfa hiyo  ambapo  aliwataja wahusika wakuu wa kashfa hiyo Kuwa ni  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter  Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliachim Maswi, Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Jaji  Frederick Werema na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba.

Kafulila alisema  kuwa ufisadi huo ni lazima mbivu na mbichi zifahamike, na kwamba haungi mkono uamuzi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wa kuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza suala hili kwa kuwa linagusa mamlaka kubwa katika dola, badala yake iundwe Kamati Teule ya Bunge.

Muda mfupi baada ya Kafulila kutoa tuhuma hizo Bunge, hakukubaliana na ombi la Kafulila lililotaka iundwe Kamati Teule ya Bunge na badala yake akaiagiza TAKUKURU na OFISI ha CAG Ifanye uchunguzi wake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo.

Kwa jicho la Sheria tuhuma zilizotolewa na Kafulila zitabaki Kuwa tuhuma, na Kafulila atahesabika kwanza Kuwa yeye ni mtoa  taarifa za tuhuma hizo.Hivyo kitendo Cha Kafulila kunukiliwa na Gazeti hili toleo la Jumatano ya wiki hii Kuwa  uamuzi huo wa Pinda una Mashaka makubwa na kwamba tuhuma hizo zinahusu viongozi wakubwa wa dola hivyo eti ni Vyema  Kamati ya Teule ya Bunge iundwe uchunguze siyoni Kama Ina mantiki.

Kwani TAKUKURU imeanzishwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana Rushwa ya Mwaka 2007 Namba 11/2007.Na kifungu Cha 7 Cha Sheria hiyo kimeanisha Kazi za Takukuru na miongoni mwa Kazi za Takukuru ni kufanya uchunguzi makosa ya kula Njama Kutenda kosa, kuchunguza tuhuma za makosa ya rushwa yanayowahusu maofisa wa serikali.

Aidha OFISI ya CAG nayoilianzishwa na inayo majukumu yake mengi tu ikiwemo ya kukagua mahesabu Katika Fedha za serikali na imekuwa Ikitimiza majukumu yake na kutoa taarifa zake kwa umma.

Na Taasisi hizo zimeanzishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kafulila ni miongoni mwa wa Bunge wa Bunge Hilo.

Sasa Inashangaza  Kama siyo kutisha kusikilizwa  mtunga  Sheria Huyo Akisema uamuzi huo wa Pinda una Mashaka kwasababu yeye alikuwa akitaka Bunge iunde Kamati Teule.

Kama Kafulila alikuwa Hana Imani na Takukuru, CAG ni kwanini alitoa tuhuma hizo bungeni akitaka mbivu na mbichi sijulikane? Kumbe anaamini Takukuru, CAG ni wa chafu ni kwanini aliibua tuhuma hizo tena akitaka uchunguzi ufanyike? Hivi MWISHO wa siku alifikiri Takukuru, CAG hazitausishwa Katika uchunguzi huo

Tuhuma hizo zinahusu Fedha za serikali , Ofisi  ya ya CAG lazima ili usiishie mAana ipo pale kwa kutazama matumizi ya Fedha za serikali zimetumika Kama iliyokusudiwa?

Maana hata Kama Kamati Teuli ya Bunge ingeundwa Mwisho wa siku ripoti hiyo ya uchunguzi wa Kamati Teuli ya Bunge Ingepelekwa Takukuru au Polisi ili zichunguze kuona je kuna ushahidi wa kutosha wa kuweza kuwafungulia Mashitaka watuhumiwa? maana Polisi  na Takukuru Ndio wenye majukumu hayo Kimsingi.

Pia Itakumbukwwa kashfa ya wizi Katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), iliibuliwa Bungeni, Kamati ya Teule ya Bunge haikuundwa Matokeo yake Rais Jakaya Kikwete alitenda TIMU ya Uchunguzi wa tuhuma hizo ambayo ilishirikisha polisi, Wanasheria toka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tasisi nyingine za serikali ambayo ilikuwa na Ofisi zake Mikocheni ambapo ili fanyakazi yake vizuri  Mwisho wa siku Uchunguzi huo ulimfanya Mkurugenzi wa Mashitaka , Dk.Eliezer Felelshi Kufungua jumla ya Kesi 12 za EPA m Novemba 4 Mwaka 2008  ambapo hadi sasa jumla ya Kesi Nne zimetolewa hukumu na baadhi ya washitakiwa walipatikana na hatia za makosa waliyoshitakiwa na wengine waliachiwa Huru kwasababu ushahidi haukuwagusa.

Mfano mwingine ni tuhuma za mkataba wa kampuni ya Richmond Ambapo kelele zilipigwa na wabunge hadi Kamati Teuli ya Bunge ikaundwa Mwaka 2007 na Mwanzoni Mwaka 2008 Kamati Teuli ikabainika kulikuwa na ouzo Katika mkataba huo na kumtaka Aliyekuwa waziri makuu Edward Lowassa ajipime na Kamati hiyo ikaamuru Wamiliki wa kampuni hiyo Naeem Gire na Mohamed Gire na baadhi ya Maofisa wa serikali wawajibishwe  Hali iliyosababisha Lowassa kuwajibika Kuwajibika kwa kujiudhuru  wadhifa  huo ambao alidumu nao kwa Kipindi  kifupi sana.

Baada ya ripoti ya Kamati hiyo kusomwa, baadhi ya wabunge kwasababu wanazozijua wa kaanza  kuishinikiza Takukuru iwashitaki watu Hao Hali iliyosababisha Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru , Dk.Edward Hosea na baadhi ya wabunge kuingia Kwenye malumbano Kwani Hosea alikuwa akitaka Takukuru iachwe ifanyekazi yake kwa  Uhuru na siyo kuingiliwa na wanasiasa Hali iliyosababisha kila kukicha kukimbia wabunge hao wakawa wanaishambulia  Takukuru na Kumbe wabunge Hao walikuwa wa mama  zao chafu za kuaribiana kisiasa.

Wananchi ambao walikuwa hawaelewi Njama hiyo waliwaunga mkono wabunge Hao wengine ambao walipachika jina la ' wabunge wanaopambana  na  ufisadi", Leo hii wanasiasa Hao wapo  kimya utafikiri ufisadi ndani ya nchi hii umekwisha.Dhambi sana.

Mwisho wa siku Takukuru iliamua kumfungulia Kesi ya Kutoa taarifa za uongo Kwenye Kikao Cha Tenda Cha Tanesco kuhusu uwezo wa kampuni ya Richmond, mshitakiwa alikuwa ni Neem Gire Mwaka Juzi Hakimu Mkazi wa Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Waliarwande Lema alimuoa Gire Hana Kesi ya Kujibu  na Mkurugenzi wa Mashitaka DPP- Dk.Feleshi hakulidhika na uamuzi huo anakimbilia Mahakama Kuu Ambapo Jaji Lawrence Kaduri alitenga uamuzi huo na akaamuru jarada la Kesi hiyo lirudishwe Mahakama ya Kisutu na Gire aanze kujitetea na Gire naye kupitia Wakili wake Alex Mgongolwa hawakubaliani na uamuzi wa Mahakama Kuu, wamekimbilia Mahakama ya Rufaa.

Kwa  hiyo binafsi naweza Kusema Kuwa sikubali Kuwa tuhuma ni za kweli na sikatai Kuwa tuhuma hizo zilizoibuliwa na Kafulila  Kuwa ni za uongo Katika Hatua hii ya awali.

Nasubiri  vyombo vyenye mamlaka ya kufanyia uchunguzi  zitakapotoa  ripoti za uchunguzi wake.

Kwani tuna Mifano hayo ambayo inafunza kupitia wanasiasa wetu ambao Walijifanya ni mabingwa wa kuibua kile wanachokiita ufisadi  wakati Sheria zote za Tanzania ikiwemo  Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002 , haina kosa linaloitwa ufisadi. Sijui wenzetu hawa kosa la ufisadi wanaotaka watu washitakiwa nalo sijui wanakipata katika kifungu gani na cha sheria gani.

Mbunge Zitto Kabwe aliuaminisha umma Kuwa Ana ushahidi kuhusu Majina na namba za Akaunti za watu walioficha  Fedha nje ya nchi na baadhi ya watu waliomua mini, lakini siku zote njia ya muongo ni Fupi, Mwanasheria  Mkuu wa Serikali Jaji Werema aliliambia  Bunge Kuwa Zitto ni muongo aliwasilisha kumuita  Ofisini kwake na akamtaka atoe ushahidi chini ya kiapo  , Zitto akasema hana ushahidi, na hadi Leo kimya kabisa utafikiri Zitto  siyo yeye Aliyokuwa akibwatuka  majukwaa na kujinadi Kuwa anaushahidi wa Majina ya walioficha Fedha nchini Uswiss.

Pia kuna wanasiasa wengine ambao Walijitapa ndani na nje ya Bunge Kuwa wanaushahidi wa Majina ya watu walioiba fedha kwenye akaunti ya EPA kupitia kampuni ya Kagoda hadi Leo hii hawajaenda kutoa ushahidi thabiti Katika vyombo hisika, Wanaishia kubwatuka majukwaani na kuwaaminisha Ujinga huo baadhi ya  waandishi wa Habari ambao hawajui kilichopo nyuma ya tuhuma zinazoibuliwaga na baadhi ya wanasiasa.

Wiki iliyopita Spika Anna Makinda  Mara Tatu wakati akiendesha Bunge aliwataka baadhi ya wabunge waache kutumia na baadhi ya watu walionje ya Bunge Kuja bungeni  Kusemea maslahi binafsi ya watu wakiwa tuma na kuwataka wabunge Hao watumie akili zao.

Ushauri  huu ni mzito sana kutolewa na Spika kwa wabunge na Hakuna Shaka Makinda alikuwa anasababu anayoifahamu  ndiyo mAana Akaamua kutoa ushauri huo licha Spika Makinda hakutaja jina la Mbunge anayetumiwa.

Hivyo ushauri wangu kwanza kwa waandishi wa Habari wenzangu  kuhusu tuhuma hiyo iliyoibuliwa na Kafulila tuwe makini na tusimame Katika Maadili ya taaluma yetu.Kafulila tumemsikia, serikali kupitia Pinda imeishachukua Hatua  KWA kuanzia Pinda ameanza Taasisi hizo mbili zifanyie Kazi tuhuma za Kafulila.

Hivyo ni vyema sasa tuziachie Taasisi hizo zifanyi kazi yake Kwa Uhuru na Mwisho wa siku zije zitoe ripoti yake.

Tusikubali ama kutumiwa na wafanyabiashara, wanasiasa, Wanasheria kuwachafua watu wengine wanaotuhumiwa Katika tuhuma hizo na Kafulila pia isivyohalali Kwani Tayari naona kuna Dalili za wazi ambazo ni chafu za miongoni mwetu kuanzia kutumiwa na Makundi yanayoasimiana Katika kashfa hii.

Pili, Takukuru, CAG visikubali kuingiliwa kufanyakazi yake na Makundi yenye Hira Katika Sakata hili Kwani endapo watakubali kufanyakazi KWA shinikizo la wanasiasa Mwisho wa siku watajikuta wanaumbuka Mbele ya safari Kama serikali ilivyoumbuka Mara mbili Kwenye Kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Ricky Mahalu na Grace Martin Kwani Chanzo kikubwa Cha Kesi hii kilianzia na uzushi uliozushwa pale Bungeni  Mwaka 2004 ambalo  mwanasiasa mmoja alijitapa Kuwa Balozi Costa Mahalu  amekwapua fedha za ujenzi wa Jengo  la ubalozi Wa Tanzania nchini Italia kumbe ni uzushi.

Tatu , Kafulila kwa Kuwa Tayari umeishanukuliwa ukisema uamuzi wa Pinda una Mashaka nao , ni wazi hata vyombo hivyo Vya  uchunguzi vikitoa Matokeo ya uchunguzi ambao wewe hutapendezewa nao, hatakubaliana na ripoti ya uchunguzi.

Basi minakushauri Kafulila tumia    Kifungu Cha 99 Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002, uombe uruhusiwe Kuwa  Mwendesha Mashitaka Binafsi(Private Prosecutor), ili uweze kuendesha Kesi hiyo mahakamani mAana Tayari umejinasibu Kuwa una ushahidi wa kutosha kuhusu tuhuma hizo.

Ni sisi wenyewe wananchi wa Tanzania Tulitaka nchi yetu iongozwe na Utawala wa Sheria, kwahiyo Takukuru, CAG, Cheo Cha Waziri wa Mkuu na Spika vimeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Hivyo tuheshimu wanapokuwa wanatimiza majukumu Yao na anayeona Hana Imani na vyombo Vya dola, aende kuishi nchi ambazo anaamini vyombo vyao Vya dola vinaaminika.

Na wananchi huko vijiweni Tusikubali kutoa hukumu Kuwa. Fulani n fisadi , hafai kuongoza, afukuzwe Kazi eti tu mwanasiasa Fulani kajitapa kuibua tuhuma za ufisadi.

Kwani ni hawa hawa wanasiasa Ndio wamekuwa wakituingiza Kwenye ushabiki wa mambo ya kijinga Mwisho wa siku wanatoa na soremba.

Ni hawa hawa wanasiasa walijiapiza Kuwa kampuni ya Richmond ni ya Kitapeli na ni kampuni ya mfukoni .Wananchi tukaamini  Kumbe walikuwa nalo jambo.

Mwisho wa siku kampuni hiyo ikabadilishwa jina ikaitwa Dowans .Kelele  zikazidi  hadi kufikishana mahakamani na Mwisho wa siku Tanesco ikashindwa Kesi iliyoishitaki  Dowans kule katika Baraza la Usulushi wa Migogoro ya Kibiashara ya Kimataifa (ICC), Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Na Hatimaye Tayari serikali ya Tanzania imeishailipa Fedha nyingi kampuni ya Dowans ,kutokana na upuuzi huu wa wanasiasa uchwara ambao ni mabingwa wa kuzua mambo na kuchafuana.

Kampuni ya Richmond tuliyoaminishwa na wasasiasa uchwara Kuwa ni kampuni ya mfukoni ilibadilishwa toka jina la Richmond Kuja Dowans, na Mwishoe HIvi sasa inaitwa Sympion Power Na inatoa huduma zake kama kawaida hapa nchini.

Na mwaka jana  Rais wa Marekani Baraka Obama alivyokuja Tanzania  aliizindua  kampuni hiyo,na Hao wanasiasa waliotuaminisha uongo kuhusu uwezo wa kampuni hiyo Kuwa ni ya mfukoni nao walikuwepo Kwenye msafara wa ziara hiyo ya Obama kuzindua Sympion .Na leo wanasiasa hao, na wanaharakati  waliokuwa wakishabikia kuiponda kampuni hiyo leo wapo kimya utafikiri wamefariki.

Tujifunze kutokana makosa, tusiwe wepesi kuamini  kila kitu kinachoibuliwa na baadhi ya wanasiasa wetu uchwara Kwani wengine ni Mavuvuzera wa wafanyabiashara, makampuni  na wanasiasa,na makuadi wa Makundi yanayoasimiana Katika magomvi Yao ama ya Kugombea Tenda Fulani, Biashara , vyeo na magomvi mengine.

Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Mei 18 mwaka 2014
0716 774494
www.katabazihappy.blospot.com


Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment