Saturday, 26 March 2016

Re: [wanabidii] MAREKANI INA SHIDA GANI NA UCHAGUZI WA TANZANIA?

Akili zetu hazipo sawa Kim ndio maana tunashindwa kujisimamia mpaka shuruti ije au kutumika kisha tunalaumu serikali kutumia nguvu nyingi. Na shuruti ikija mfano Mkakati wa Mtu ni Kazi, Mtu ni Afya na Hapa Kazi tu. Tunafanya vitu in a temporary manner. Ile Motto ikiisha nguvu tunarudia kama kwanza. Kila siku TZ ni kuanza tena lile lile lililopita kama sera au mkakati.

Hakuna kisichofanyika kuanzia Uhuru hadi leo hii bali vyote vya sasa ni marudio tu ya tulikotoka. Tatizo hata uwekaji wa documents ni utata.

Kama tuna akili kweli huwezi ukafika kwenye vyuo vya elimu ya juu ukakuta watu wametia makopo ya maji ya plastiki ktk WC vyoo vinafurika vikiziburiwa-makopo, milembe, plastiki!, Dust bins zipo lakini chupa na box za chips walizokula zimezagaa. Ukifika campus unachosikia cha kwanza ni harufu ya kinyesi dunia yote. Hapo ni pa wasomi wa kila aina. Hatubadiliki. Maghorofa vyoo vimefura maji yanamwagika kutoka maghorofani kwenda chini nje. Kila wakati ni kuzibua uchafu huo tu. Sewerage system mifuniko tunaiba kuuza chuma chakavu lakini pamoja cha kuona hili-kiwanda cha chuma chakavu hakifungwi. Kisha pale tulipoiba mfuniko wa chuma-tunajaza takataka, zinaziba, kinyesi kinafurika kila kona-SERIKALI ndio tatizo kuu sio Sisi ambao kinyesi kinajaa ndani ya majumba yetu na chuma chakavu tuuzao ni sisi au watoto wetu. Mtaro nje ya nyumba yako umejaa takataka na malundo yapo kiwambazani kwako-upo upo unagojea serikali ije!

Kuna wasomi wa majengo lakini majengo sio friendly kwa vilema-anasota apande ngazi, anasota aende chooni. Hakuna vyoo vya vilema wanaosota kuepusha na kutambaa katika maji ya kichesi lakini wasanifu majengo kibao wana madigrii na vyoo hivyo hapo wasomapo-Havipo. Huwezi ukawa na chuo cha mifitu na mifugo na kilimo lakini vijiji na milima inayozunguka chuo inalimwa unsustainably na mifugo kwa maelfu ipo katika misitu hifadhi jirani ya chuo au wilayani chuo kilipo. Pilot areas zao za field practice or practical training zipo wapo-Lab? Hata Lab ya construction engineers unaweza kuikuta imeporomoka.

Mkosa si kiongozi tu na wewe raia au sisi raia tubadilike. Unakuta magari ya mamilioni yamepark njia za wapita kwa miguu, hapo pia pana mtaro wa maji ya kinyesi mtaroni-wanakesha wanakubywa na uchafu upo jirani na vyakula mchana havifunikwi vimejaa mainzi. kabati la wavu au la kioo lipo wazi na wasomi hao wanakula hapo. Hakuna tofauti kiakili ya msomi, tajiri na masikini asiye msomi anayeuza chips hizo. Nje ya bonge la jumba la kifahari maji ya kinyesi yamejaa ameunganisha bomba linamwaga kinyesi mfereji wazi-akili za kuazima.

Unafika ofisi ya Kata, Kiji, Mtaa-hakiingiliki na extension staff wapo hapo. Suala la kusomesha environmentalists, land officers, health officers na wengine hawana ajira. Lakini Wetlands zinapimwa viwanja vya nyumba inanikera sana sana. Haya Jumba la Yanga limejengwa bondeni mvua ikinyesha budi kuingia kwa boat ktk ghorofa hilo.

Kweli tunashindwa kujisimamia. Hata serikali ikitaka tuzingatie sheria-SIASA inaingilia-usiwaondoe wapiga KURA wangu; Mifugo maelfu ikiondolewa ktk protected forest inayotegemewa kwa maji ya mito kunywesha viwanda, kaya na taasisi zote mijini na vijijini-WANAWAONEA kukamata mifugo yao wakafuge wapi? Sio kuona umuhimu wa wafugaji kuwa na mifugo inayoweza kubebwa na uwezo wa ardhi yao, kufuga kisasa sio kulimbikiza na ardhi haikui awnavyoijaza haitatosha, hata wakiachiwa mbuga zote hazitotosha kwani watu na mifugo huongezeka. Mwisho tutakuwa jangwa kama Somali na Ethiopia-UONEVU. Wanajaza mercury mitoni na lake victoria na kuvamia misitu. Lakini madhara ni kwetu wote. Wakiunganishwa ktk NGO na mikopo kupewa ya vifaa vya kisasa-wanaona kuchelewa kutumia hivyo vifaa bora mkono pamja na madhara wanayofundishwa. Wakiondolewa na kushauriwa wapate mafao kila mwezi wampishe mwekezaji wa zana za kisasa wao hela wafanye shughuli nyingine na huzipata kila mwezi-wanapokea hela na kuvamia misitu mingine kuchimba dhahabu. Kama kawa-kurudi kulekule. Uharibifu mazingira, pombe, ulevi, umalaya. Na huko misituni wanaumwa na inzi wa Usubi. Kula dawa za usubi na mabango kibao ya kuelimisha-No way. Obama anataka kuua nonino tusizae. Kutumia condom-No way-Obama ameweka viluilui vya kuua nonino na vina ukimwi pia. Wanakuonyesha ute wa condon ulioganda ndio vimo vidudu humo. Akipata gonjwa-kalogwa. Hela anazopata kaangalie nyumba yake-nyasi na udongo ulioporomoka! Serikali ya CCM haitujali masikini! Wewe unayelewa kutwa kucha? Kuna kila kitu kijijini mharibifu na mzembe mwenyewe. Kisha unatembea kilometa 5 kutafuta maji. Ukiwekewa handpump well na World Vision-unabomoa kuuza chuma cha bomba au kukichukua kufungia mkokoteni wa punda, ng'ombe wa kubeba viroba vya mawe ya kusaga kutafuta dhahabu. Mke na watoto watembee kilometa 5 kutafuta au kuchota maji-akili za kuazima!

Lazima tubadilike. Iwe kampeni turudi makwetu tukasaidie kuelimisha jamii zetu kubadilika. Rais na mawaziri pekee hawatoweza bila ya sisi sote kukubali kubadilika na kubadili uelewa na utendaji wa jamii na makabila yetu. Kweli tunashindwa kujisimamia tunataka tena bakora za mjerumani. Kichefuchefu. Tuache pia kutetea uhalifu na uharibifu!! Ujinga, Upumbavu (Baba wa Taifa JK Nyerere alisema haya-Ujinga!!)

Kama Kawa

--------------------------------------------
On Sat, 26/3/16, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] MAREKANI INA SHIDA GANI NA UCHAGUZI WA TANZANIA?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, 26 March, 2016, 8:45

Atu,

Ni kweli tunashindwa kujisimamia, ila haimaanishi hatuwezi.
Kupewa ufadhili ni sababu ya ujinga wetu tu na makosa flani
ya uongozi uliopita.
Lazima ifike mahali TANZANIA iwe taifa
linalojitegemea kwa kila kitu. Hii ni lazima.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment