Subiri waone China, Korea, Russia inasaidia TZ kama vile ilivyokuwa zamani. Watu wanajifunza Kichina na wanajeshi kama kawa kwenda Mafunzo huko na India. Mikataba ya ujenzi kila kona wachina. Japan nayo ipo juu kimisaada na ujenzi. Hakuna nchi ya Ulaya ya mataifa makubwa inayoweza kukubali kuikosa TZ East Africa na Africa kwa ujumla. Wanatingisha tu kiberiti. Kazi yao UK, USA na Nchi za Scandinavian ni kupenda kusaidia opposition parties chini ya umbrella ya demokrasia kumbe wana yao. Pia kusaidia NGO au civil societies kihivyo. Matokeo yake CSO zipo kisiasa zaidi kuliko kuweka macho na juhudi zao katika communty-participatory development. Wapo na ofisi zao katika eneo wilayani, mkoani lakini vijijini hali ya wananchi ambao wapo kwenye resources za aina yote mbaya na CSOs zipo eneo hilo lakini kisiasa zaidi.
Hao hao ndio wahisani toka UK, USA utakuta wanashabikia vitu visivyo endelevu na msingi. Mfano kesi ya Mkomazi Game Resrrve enzi zile DIFD ilitoa mihela lakini walisahau ni early explorers toka UK walkiochora ramani za himaya za chiefs hata wa south Pare, kuandika vitabu vya kihistoria hata ta migration ya watu kutoka nchi mbali mbali kuingia Tanganyika na wakoloni kuweka reserves mbalimbali mpaka za watu. Hao hao walioanzisha National Park (wakoloni) na protected forests kwa madhumuni mazuri halafu hao hao wakaja kutaka usimamizi wa parks eti uachiwe wananchi-zikaanza vurugu Loliondo na NCAA NGO za wazungu kutaka de-gazettement ya maeneo. Walifurushwa kichizi na serikali ya TZ!
Hao wakoloni kama wa UK walichukua ardhi ya wananchi kuanzisha estate farms za pareto, mahindi, chai, ngano, miwa, kahawa. Mashamba yale kwa sasa yanapogawiwa wawekezaji wanapiga kelele wakati nasi tunataka uchumi uwe mkubwa tulishe viwanda tusitegemee unga na misaada ya vyakula kutoka World Food Program. Ningewaona wa maana kama wangetumia NGO funded by them kusaidia kwa mfano wafugaji kuanzisha livestock ranches za watu binafsi na za makundi ya umoja wa wafugaji. Lakini wao wapo kulaumu uonevu kwa wafugaji ambao hupata hela kutoka shughuli mbali mbali na kulimbikiza ktk mifugo ambayo huwa mingi na kuongeza uharibifu wa mazingira. Wakati huo huo, kuna visima vya toka ukoloni (boreholes) wafugaji hawawezi kuchanga hela (Mifugo) wakafufua na kupoata maji jirani badala ya kuvamia mashamba na mabwawa kwa wawekezaji. Mifugo kutoka Kenya imejaa Loliondo na NCAA na Monduli. Bado tunayolimbikiza kutoka utajiri wa madini Mererani, tourist activities, lodges na biashara nyingine. Ardhi ina mwisho wa kubeba mzigo. Tunavyoifanya kipara haina mimea tusitegemee kuvamia wawekezaji, au kupunguza ardhi ya wawekezaji wa ndani na nje ndio solution. Hata!! Solution ni Kilimo na Ufugaji endelevu na Sio Kilimo bila ya ulinzi wa ardhi na udongo na ufugaji wa kuwa na malimbikizo na maelfu ya mifugo. Wape ardhi, waongezee-magomvi na uvamiaji ya wengine hautoisha. Strict laws za kila sekta na kusimamia wananchi na wawekezaji kuona wanazingatia katika sekta hivyo ndio muhimu. Tuache SIASA ya kuogopa KUKOSA KURA-tusingatie Sectoral Policies, Principles za utendaji kazi efficiently, effectively with sustainable positive outputs.
Kama tutakaa na kukubali Obama, Malkia wa UK, Wajerumani, Dutch na Scandinavians watuamulie hata jinsi ya kupiga kura na masuala yote ya uchaguzi-tutakuwa wasomi wapumbavu. Wao kwao wanashindana, wanatukanana, wanapigana ngumi ktk mikutano ya kampeni sisi tunaangalia tu. Polisi wanapopiga waannchi kwao-okey. Lakini polisi wanapopambana na kupigana na wananchi kwetu-hatuna demokrasia. Mbona tunaona mapambano kwao daima na polisi wanauawa au wanabondwa nao wanabonda wananchi? Tukiendelea kujipendekeza kwao-watatuona MAFARA. Tukaze uzi, tufanyekazi sasa tuache malumbano. Anayejiona mzungu au mwarabu ahamie huko waliko wampokee Ukibaki hapa uwe wa rangi yoyote wewe ni Mtanzania na NIDA imekupa kitambulisho. tazama TV na magazeti uone wenzetu wanavyokufa njaa vitani, kubakana, kuuana kwa nyundo na mapanga, kukatana vichwa na kuzama baharini wanapokimbilia nchi za ulaya na USA. Huko sasa hawataki wakimbizi na Trump asiyetaka wakimbizi atashinda tu!! Hama huku ukakae kwao ktk makontena uache kulima na kuvua samaki na resources tele huku kasoro vichwa vyetu tu ni tata. Utegemezi na malumbano, kubweteka ndio tija kwetu kutaka vishuke kama mvua. Kukomoa na ndio tija. Leo hii mifugo imejaa ktk kilimo cha umwagiliaji cha RUVU-Bagamoyo-Japanese financed improved tradtional irrigation system. Mpunga mkubwa-wanaingiza mifugo na serikali inaangalia. Imejaa Kisanga-Malolo ktk mifereji ya Maji-tunaangalia. Inahamia kwa maelfu maeneo ambayo sasa mahinda na mpunga vimekua karibu kuchanua na wanamaliza maekari na kupiga wenye mashamba-tunaangalia!! wetlands za Kilimo zinapimwa viwanja vya majumba na viwanda. Bibi aliyeluwa analima na ni customary land yake hapati fidia ya ardhi na hana pa kwenda kulima-tunaangalia! Mjapan aliyesaidia kilimo hiki anatuonaje? Akituacha itakuwaje?
Haya ya kilimo na ufugaji na uvuvi endelevu, utunzaji misitu isivamiwe ndio majipu ya kutumbua. Wetlands zote za kusaidia food security wananchi tena walimaji wazee ndio kujae mifugo na kujengwe majumba? Wanaopewa ardhi wanakata Mikorosho, miembe, minazi na miti ya miaka 100+ inayolinda ardhi. Wazee wanategemea kuuza matunda hayo na kupanda mananasi leo hawana pa kupata kipato. Mpimie mtu ardhi yake na eneo la nyumba na shamba lake sio kupima ardhi watu wajenge tu hata vijijini hata kama miji inakuwa na kupanuka-wapimie na mashamba hawana ajira wala social security salary per month. Sio kujali issues na kumjali Obama! Tuna mengi ya kujali yetu wenyewe nchini!!
Kama Kawa
--------------------------------------------
On Thu, 24/3/16, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] MAREKANI INA SHIDA GANI NA UCHAGUZI WA TANZANIA?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, 24 March, 2016, 23:05
Mara baada ya uchaguzi mkuu October
2015 na yaliyotokea Marekani ilisita kuruhusu msaada kwa
serikali ya Tanzania. Sababu mbili ilizozitaja ni 1) Kufutwa
kwa Uchaguzi wa Zanzibar na 2) Kutaka kujua kama kweli
sheria ya mtandao ina haki ya kutumika kuwadhibiti waliokuwa
wanatumia mtandao kuvuruga uchaguzi ambao baadhi walikuwa
mikononi mwa dola.
Majuzi baada ya uchaguzi Zanzibar Marekani ililalamika kwa
uchaguzi kufanyika bila waliogoma kushirikishwa.
Marekani inajiona inakosa nini Tanzania kuwa salama na chini
ya viongozi waliodhibitishwa na tume za uchaguzi kuwa ndio
waliochaguliwa?
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment