Tuwe na mapenzi mema na Tanzania yetu na tuache unafiki kama anavyosema Rais Mteule Dr. Magufuli. Tuwe wakweli na tuachane na ushabiki wa kichama. Unataka uchaguzi urudiwe kwa sababu zipi? Sababu zote ziwekwe mezani kama zipo zichambuliwe tuangalie zile zinazoweza kushughulikiwa kwenye vituo husika na kushughulikiwa kutokana na sheria zilizopo na kama ambazo zitahitaji zishughulikiwe kwa kuitisha uchaguzi zieleweke. Hii itasaidia kwa kila mpiga kura ajue kwa nini anatakiwa kupiga kura mara ya pili na kupiga kura huko ni kwa maslahi ya Taifa la Tanzania na si vinginevyo.
Tufahamu kwa sote sisi ni binadamu tunahitaji haki sawa na hapa duniani tunapita tuu. Ni wajibu wetu kufanya kila liwezekanavyo kuhakikisha kuwa tunaacha dunia na Tanzania yetu ikiwa na neema zaidi kuliko tulizozikuta ili ziwafaidishe wajukuuu, vitukuu na vilembwe wetu waseme kweli waliotanguliwa hawakutuangusha.
Ni vyema tukatafakari sana sana ni kipi cha kufanyia kwa nchi yetu kwa manufaa ya nchi yetu na sio kwa manufaa ya kikundi kichache au kwa ajili ya nafsi zetu.
Tuendelee kuomba Mungu atuonyeshe njia
Herment A. Mrema
Date: Tue, 3 Nov 2015 12:02:23 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Zanzibar; Kinachopaswa Kutafutwa Ni Maridhiano..
From: kitigwa@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com
Kudos Maggid for well done analysis of this impasse in Zanzibar. I concur with you.
On Nov 2, 2015 11:22 PM, "Maggid Mjengwa" <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
Ndugu zangu,
Nafuatilia kinachoendelea Zanzibar. Siioni namna nyingine ya kumaliza kadhia iliyotokea bali kwa pande mbili zinazokinzana kukubaliana kurudia uchaguzi. Walokosea wawajibishwe, lakini, hakuna namna nyingine yeyote ya kuhalalisha matokeo yatakayotangazwa baada ya uwepo wa kadhia, isipokuwa, kwa zoezi zima kurudiwa upya ikiwezekana chini ya uangalizi pia wa watu wa kutoka nje. Hivyo, kazi kubwa sasa na iwe kuyatafuta mariadhiano ili Zanzibar isonge mbele kutoka kwenye hali ya 'political impasse' iliyopo sasa.
Na ni heri kuyatafuta maridhiano kwanza kabla ya kuingia kwenye majadiliano, kuliko kuyatafuta maridhiano baada ya kuingia kwenye kugombana. Na MARIDHIANO ndio msingi wa UHALALI wa SULUHU itakayopatikana baina ya CUF na CCM.
Maana, tusipotanguliza busara, hekima na maslahi ya taifa, yumkini yaweza ikawa kama yale aliyopata kuyasema miaka 60 iliyopita, mwandishi yule mahiri, Mtanzania mwenzetu Shaaban Robert, aliandika; " Wasadikika wana desturi ya kutafuta fimbo baada ya kuumwa na nyoka. Tumekwisha umwa na nyoka wa matendo yetu mabaya ya zamani.
Nyoka mwenyewe amekwishakimbia. Hapatikani kwa kujilipiza kisasi, lakini, sumu yake imebakia katika jeraha tulilolipata. Sasa, shauri lililo jema ni kuzuia sumu hii isienee miilini mwetu ikaleta kifo.
Maovu yana hatari kubwa kukaa kati yetu. Tumedumu nayo kwa muda mrefu. Hayakutuletea faida ila hasara, huzuni na kilio siku zote."- Shaaban Bin Robert.
Na Mwanafalsafa Aristotle alipata kuandika, kuwa sifa kuu ya Ufalme ni Mamlaka, maana, Ufalme huwa ni sawa na Umungu Mtu. Ufalme huzaa despotism. Na HEKIMA ni sifa kuu ya Aristocracy, kwa maana ya tabaka la Uongozi . Naam, kiongozi sharti awe ni mtu mwenye hekima.
Na viongozi wanapokosa hekima wanaingia kwenye hali ya kuwa Ma-Oligarchy. Hiki ni kikundi kidogo cha wateule lakini waliojaa ubinafsi na choyo kubwa. Ni watu wasiojali maslahi ya umma bali ya kwao binafsi na kikundi chao.
Na sifa kuu ya Demokrasia ni ridhaa ya jamii. Naam, Demokrasia hujengwa katika msingi wa mariadhiano. Ikikosekana hali hiyo, ndipo makundi ya kuhasimiana huzaliwa, na hupelekea kuzaliwa kwa kinachoitwa ' mob tyranny', yaweza kusemwa uharamia au uongozi wa kimabavu wa kikundi fulani katika jamii.
Hivyo basi, Mwanafalsafa Aristotle anapendelea zaidi uwepo wa kinachoitwa ' Polity' aina ya utawala wa mchanganyiko. Utawala wenye kuhakikisha makundi yenye kuhasimiana yanapata fursa ya kugawana madaraka ili kuwepo na ' checks and balances'- kwamba kuwepo na hali ya kudhibitiana. Ndio msingi pia wa mgawanyo wa madaraka. Nchi lazima isonge mbele.
Maggid,
Dar es Salaam.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:
Post a Comment