Friday, 6 November 2015

Re: [wanabidii] URAIS WA DR. MAGUFULI, NI FUNZO TOSHA KWA WENGINE

Ndaki
Hata kama mwanasiasa atakueleza jinsi ya kuondoka hapa tulipo katika umasikini na mikakati ikiwepo-jee wewe mwenyewe unajiondoaje katika umasikini huo? Mipango yako inayochukua fursa zilizopo au utaitekelezaje?

Wanahamia wakimbizi vijijini unakuta wanalima kama kichaa. Huko asubuhi utaona wanavijiji jirani watanzania wanakimbilia kununua mazao kutoka kwao. Ardhi ni yao wapo wapo tu. Ukifika baadhi ya maeneo walikohamia wasukuma na mifugo yao ukiwauliza kuhusu vuakula upatikanaji wake watakueleza-siku hizi chakula si tabu kuna 'Wasukuma" wanalima hao! Vianzi, mihogo si tabu tena. Vijiji vya Songea wakiwaita wakinga-matreka!! yaani labour migrants wanakwenda kule vijiji jirani na Seleous na maeneo mengine wanalima hao kama vibarua! Msimu ukipita wanaondoka kurudi kwao. Unakuta mabonde mazuri, kuna kila kitu ila watu wanakunywa pombe kuanzia asubuhi hadi jioni daily. Vijijini ukipita biashara kuu ni vilabu vya pombe, mitumba. Vicoba vikianzishwa kwa wajasiriamali havidumu; SACCOS wanakopa kisha wanatoroka hela hawatumii ipasa-wanaua ushirika. Unakuta youth groups na wazee wao washauri wanakopa katika account iliyoanzishwa kufunguliwa SACCOS halafu kurudisha hiyo
laki moja, 2 au tatu baada ya miezi iliyokubaliwa pamoja na faida ya 10% hakuna. Inapita miaka 3 halipi na kisha anaanza mizengwe inabidi muende kwenye sheria.

Kwa nini akili zetu hazifanyi kazi sawasawa? Kuna kila kitu kijijini, mfumo wa mipango miradi, mafunzo ya upangaji hutolewa. Hata palipo na miradi ya wahisani, NGOs local and foreign uendelevu wa miradi baada ya kukabidhiwa pamoja na mafunzo kutolewa unakuwa mdogo? Re-inventing the wheel daima!
Tujiulize-unafika kijijini unakuta kuna nyumba ya zamani toka ujio wa wajerumani iliyojengwa kwa matofari ya tope bila cement nje ikapakwa chokaa iliyotokana na mawe ya chokaa. Au ilijengwa kwa tope ikapakwa chokaa na sakafu ya kokoto na rojo ya gypsum ambayo inatokana na mawe yaliyo katika mazingira yetu. Zipo hizo nyumba katika mijengo ya sisal estates, magodown na nyumba za railway, vituo vya police, shule za msingi au mijengo ya estate farms ambayo sasa ni baadhi ya majengo ya shule zetu na zile primary and secondary school za zamani na majengo ya staff. Utayaona majengo haya DSM pia keko, mgulani, kurasini, magomeni na mikoa mingine-Morogoro, Kilosa, Mikumi kituo cha police na railway station; kwenye makanisa etc. Inakuwaje leo mwanakijiji anachoma tofari anamaliza misitu lakini nyumba anayokaa anavujiwa, nyasi zipo za bure na tope lakini unamchungulia ndani unamuona. Makuti na nyasi ni za bure tope na mvua inanyesha maji ya bure. Haoni tofauti
ajitume atumie resources hizo aboreshe nyumba yake?...Mabadilikooo! Rais ajae atuletee maendeleo!! Unauza kariakoo unapata millioni 300-800 kwa nyumba nzee ya plot ya high density ambayo uliipata kwa shs 60,000/= mwaka 1974. Ukizipata pesa unazimaliza unahamia bondeni Jangwani, Mchikichini kwenye Kinyesi-Mabadilikooo! Ukawa ndio Jibu. Huna senti, umezimaliza na hata ulipopewa plot uhame na mabati na simenti juu ukauza ukarudi kinyesini. Bado unaelewa uchafu ni mbaya-upo kwenye bwawa la kinyesi unaishi, aunakunywa pombe kucha.

Una mifugo mingi elfu 5-10+ lakini huwezi kutoa mbuzi mmoja au 5 uchangie borehole ya kupata maji safi ya kunywa wewe na mifugo yako mkasimamia mradi wa kijiji chenu. Na ikijengwa kwa hela za GVT au donors-unatoboa mabomba, unaiba na kuuza chuma chakavu. sasa ufwanywe nini? Unaona kila kitu serikali ifanye wewe utumie tu huwajibiki! Kwa nini kijana uuze ardhi ya wazazi wako na nymba, ulewee kisha unaona mama-kibibi kinatolewa vyombo nje hakijui pakwenda? Kwa nini mtu upange foleni kutwa zahanati mhudumi mara katoka, mara karudi anaongea na simu tu na kiongozi hachukui hatua? Hatuoni yanayoonekana? Umepewa chandarua lakini unazolea takataka. Adhibu hata wale ambao hawana nyumba na choo bora watesao familia. Mbona miradi ya nyumba bora za soil cement, interlocking blocks za burnt bricks, kujenga kwa kutumia chokaa, mawe na gypsum yaliyojaa semi arid areas kama Monduli, Babati, Grumeti etc; ujenzi wa kutumia mbao za mnazi imefanyika. Tupewe nini sisi
tuelekee?

Sera na mikakati mizuri ipo lakini utekelezaji ni tatizo. Usimamizi mbovu sekta zote kutokana na ubinafsi, udugu, rushwa, chupi street ndio zinatuponza katika usimamizi wa ufanisi wa utendaji na utekelezaji Sera na Mikakati na sheria. Kama Sheria ya Mazingira na Majengo ipo-inakuwaje mtu ajenge hoteli, kiwanda ndani ya eneo la ulinzi la Bahari? Nani aliruhusu kiwanda kwa mfano kijenge na kiwe hatarishi. Nani alikagua mchoro wa kiwanda na eneo kitakapojengwa akaona panafaa na aina hiyo ya kiwanda inaweza kujengwa hapo. Kuwa Mchoro na emission zitakazotolewa umezingatia National na International Standard? Kwamba kuna ktk mchoro waste processing na stabilization pond kabla liquid waste haijaindia katika bwawa la serikali au underground liquid waste disposal sysyem (Pipes) yaende bwawani au baharini? Kama mfumo wa sera na sheria upo haukuzingatiwa kiasi kwamba kiwanda kipo pasipo takiwa na kinamwaga uchafu ktk mtaro wazi na kutesa watu-Kamata Officers wote
waliokagua mchoro na site na kuidhinisha ambao wamedanganya upper levelswakaweka sahihi kumbe hapastaili. Fukuza kazi na mafao yao yagharimie cost zote za kazi, ubomoaji kiwanda hicho. Watakoma na kuogopa ufisadi, uroho na ujinga.

Unategemea wanasiasa wakueleze ni kwa mna gani tutatoka hapa tulipo na kufikia uchumi wa kati ambao tumebakiza per capital chache au kubwa-Nani anakueleza ukipiga debe na kupata 30 elfu per day au kuuza eneo lako milioni kadhaa au kufanya kibarua cha degradation ya ardhi kujaza lori mchanga kutwa lori 6 watu 3 mnaondoka na 190,000 au elfu 60+ kila mmoja lakini kesho huna umezinywa zote? Nani anakutuma uzimalize badala ya kufanya masuala ya maendeleo? Kama hatubadiliki kifikra na kiutendaji-hata aje jembe wa namna gani-hatutafika pa kuridhisha kamwe!!

Yuleyule


--------------------------------------------
On Fri, 6/11/15, Hosea Ndaki <hosea.ndaki@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] URAIS WA DR. MAGUFULI, NI FUNZO TOSHA KWA WENGINE
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, 6 November, 2015, 19:14

Katika chaguzi hizi za
vyama vingi tuna mambo mengi ya kujifunza kutokana na
chaguzi hizi, wapo viongozi wanaopatikana kwa kuwekwa na
magenge ya watu wenye maslahi binafsi na wapo viongozi
wanaopambwa na porojo za majukwaani, tumeona matumizi ya
picha za uongo, matangazo mfululizo kama tunauza vocha za
tigo na mihemuko ya kutengeneza.

Lakini tatizo kubwa ninaloliona sijui kama na wengine
wanaliona ni ukosefu wa mtizamo mpana wa kisera. Ukitizama
uchaguzi wa 1995 2005 na 2015 chama kile kile kina maono
tofauti kabisa si chama tawala wala chama pinzani.

Ipo haja ya kutizama upya namna tunavyoendesha siasa
zetu, tunaendesha siasa kana kwamba tunagombania utajiri.
jana nilikuwa naangalia documentary ya fisi na simba
yanagombania mzoga wa nyati. Fisi anautaka na simba anautaka
ni makelele vitisho na majigambo kwa kwenda mbele.

Kusema utaondoa umasikini wa watanzania kwa miaka
mitano ni uongo wa mchana kweupe hata kumi nako
nikuwadanganya watu, mwaka 2010 chadema wajigamba kufuta
ufisadi na nyumba za tembe na kuuza mfuko wa saruji elfu
tano leo hawazungumzi hilo tena wamekuja na mambo mengine
kabisa ya elimu bure na kufuta ufukara.

mwaka 2010 ccm walikuja na sera ya kufuta umasikini,
leo hawazungumzi tena habari ya kufuta umasikini wanakuja na
sera ya kufunga mafisadi kuna jamaa aliniambia ile kofia ya
caw boy nje imeandikwa "hapa ni kazi tu" ndani
imeandikwa "jitegemee" sasa tufuate maandishi ya
ndani au nje? je nimafisadi yaleyale ya slaa 2010 au
nimengine tena yameibuka?

Ipo haja ya kukaa chini na kuweka sera za nchi za
muda mfupi na muda mrefu ili tujue vipa umbele vyetu hasa ni
nini, ili wakati wa kampeni tuwashindanishe wagombea kwa
namna gani tutafikia malengo tuliyojiwekea na sio ukiwakuta
mama lishe unawambia utawapa steel wire za kusugulia
masufuria, ukiwakuta machinga unawambia siwafukuzi
barabarani, ukiwakuta bodaboda unawambia hakuna kuvaa helmet
bora wakushangilie tu. hapana hatuwezi kujenga nchi kwa
mtindo huo.

Katika uchaguzi uliopita nilitegemea wanasiasa
watueleze ni kwa mna gani tutatoka hapa tulipo na kufikia
uchumi wa kati ambao tumebakiza per capital ya us$ 15 tu.
Magufuli alisema masikini nchi hii ni 28% ya watanzania
lakini je nani aliyesema kuwa kufikia 2020 watakuwa wamebaki
12% angalau

2015-11-06 16:27
GMT+03:00 fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>:
Urais wa Dr Magufuli, ni funzo tosha kwa watu
wengine
Miezi kama minne iliyopita ni watu wachache sana waliokuwa
wakiamini
kwamba Dr Magufuli atakuja kuwa Rais wa nchi yetu, Hii
ilitokana na
mfumo uliokuwepo huko nyuma wa kuchagua mgombea ku-base
zaidi kwenye
makundi ndani ya Chama na umaarufu wa mgombea.
Kilichomwibua
Dr Magufuli ni record yake ya uchapakazi, uadilifu,
kutoyumbishwa hovyo
hovyo kwa sababu ya kusimamia kile anachokiamini kwa manufaa
ya wananchi
na taifa kwa ujumla, Hiyo
imejidhihirisha zaidi katika wizara zote alizowahi
kuziongoza mfano
Ujenzi na Miundombinu pamoja na Kilimo na
ufugaji.
Fundisho tunalopata hapa ni kwamba usingoje mpaka upewe
nafasi
kubwa ya utumishi ndio uanze kuonyesha namna ya kuwatumikia
wananchi.
Piga kazi tu hata kama huna cheo chochote, usingoje mpaka
uwe Waziri,
Mbunge, M /"kiti serikali ya mtaa, nk*
WASIPOKUONA BINADAMU MUNGU ATAKUONA NA KUKUINUA
TU



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment