Friday, 6 November 2015

Re: [wanabidii] HONGERA UKAWA MPEIPA NCHI SOMO

Mama Nkya umesahau kuwaambia ukawa ili wajijenge zaidi waachane na kufanyia hujuma ukiambiwa majimbo yako ni 10 usichukue majimbo ya wenzako na huko ni kuzigawa kura na kumsababishia mwenzako kushindwa kama walivyofanyiwa kina matatiro.

Wakumbushe ili ukawa wafanikiwe waache kuchukua makapi kutoka ccm kama kina sumaye na kingunge wakisema cvm haijafanya jambo wakati  wao walokuwa watendaji wakuu.

Pia umesahau kuwahusia kuws ili umoja huo uendelee chadema wasitafune ruzuku peke yao wawagawie na wenzao ambao waliwaunga mkono katika urais.

Vile vile ungeeausia waende bungeni kupambana kwa hoja wtz hatutaki kuona migomo bungeni wakafanye kazi wakiyotumwa katika majimbo yao. Bado hujachewa wausie na hayo mama

On Nov 6, 2015 5:16 PM, "'Mashaka Makana' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Mama Nkya unanichanganya! Wewe ni mwanaharakati au mwanasiasa? 

Sent from Yahoo Mail on Android

From:"'ananilea nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date:Fri, Nov 6, 2015 at 17:00
Subject:[wanabidii] HONGERA UKAWA MPEIPA NCHI SOMO

HONGERA UKAWA MPEIPA NCHI SOMO

Na Ananilea Nkya

Baada ya uchaguzi mkuu kukamilika,  Watanzania  wote  wanaopigania mabadiliko  ili  kila baada ya uchaguzi nchi  yetu ipate uongozi  uongozi utakaowezesha  mamilioni ya Watanzania wanaoteseka kwa umaskini kuondokana na umaskini  wao,  bila shaka watavipongeza  vyama  vinanyounda  Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.

UKAWA wametoa somo kubwa kwa nchi yetu kuhusu changamoto kuu zinazokabili nchi yetu kufikia uchaguzi huru na wa haki kama nitakavyoeleza katika  makala hii.

Aidha wanachama na viongozi wa CCM ambao waliamua kuchukua maamuzi magumu  kuondoka katika chama hicho  na kuungana na UKAWA katika kupigania mabadiliko nao wanastahili pongezi kubwa.

Miongoni  viongozi hao ni  Edward Lowassa aliyekuwa mgombea Urais  CHADEMA –UKAWA ---ambaye ushawishi wake wa kisiasa umeacha historia  ya aina yake katika uchaguzi wa vyama vingi Tanzania.

Wengine Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Waziri Mkuu mstaafu Mheshimiwa  Fredrick Sumaye na Waziri wa Mambo ya Ndani mstaafu Lawrence Macha.

Viongozi hawa  wamejitoa mhanga kukubali kujishusha na kuwa sehemu ya harakati za  wananchi  kutafuta mabadiliko ya kunufaisha walio wengi.

Tena  wamejitoa  bila kujali  kudhalilishwa kwa matusi  na kunyanyaswa na vyombo vya dola kama wanavyonyanyaswa wananchi  wa kawaida.

Ninaamini  ni watu wasioitakia mema Tanzania na wasiojali maslahi ya Watanzania wengi ndio pekee watawabeza viongozi  hawa kutokana na uamuzi wao wa kuungana na wana mabadiliko.

Lakini  Watanzania  wanaoelewa vema  mchango wa  uongozi  katika harakati za ukombozi watawapongeza na kuwatia  moyo viongozi hawa waliojitoa mhanga na kuthamini mchango wao katika kupigania  maslahi ya Watanzania  walio wengi  maana bila  viongozi  kujitolea ili kuleta  mabadiliko, mabadiliko hayawezi kupatikana.

Zaidi ya yote  vyama vinavyounda UKAWA ambavyo ni  NLD,  NCCR-Mageuzi, CHADEMA Nna CUF  vinastahili pongezi kubwa kwa sababu  umoja wao katika uchaguzi wa mwaka huu umetoa somo jipya katika siasa za  vyama vingi Tanzania.

Jambo moja kubwa  ambalo UKAWA wamewathibitishia Watanzania  ni kwamba vyama vya  upinzani vikishirikiana kwa dhati  na kujiandaa vema  kupata viongozi makini  na wenye dhamira ya kweli  ya kuleta  mabadiliko kweli  ya kunufaisha mamilioni ya Watanzania maskini,  wanashinda  uchaguzi kwa kura nyingi.

Jambo muhimu zaidi sana  ambalo UKAWA  wametoa  somo kwa Watanzania katika uchaguzi huu  ni kwamba  nchi yetu bado ina safari ndefu  kufikia uchaguzi HURU NA WA HAKI unaowesha mshindi kutangazwa mshindi na si vinginevyo.  Je amani inaweza kutamalaki kwenye jamii yetu  kama uhuru na haki kwenye uchaguzi vitaendelea kuchezewa kwenye uchaguzi?

Swali hili  msingi wake  ni mgogoro ulipo sasa  kuhusu kutotangazwa kwa  matokeo ya  mshindi katika uchaguzi  wa Urais Zanzibar  na  UKAWA kutokukubali matokeo  ya Urais.

UKAWA  katika uchaguzi huu wametoa somo kwamba kuna matatizo makubwa matatu  yanayokwamisha uchaguzi huru na wa haki  Tanzania. Mambo hayo ni haya:
1)    Walioko madarakani  kutokuwa na dhamira ya dhati (political willingness)  kuona mfumo wa siasa za vyama vingi ukistawi  na kuleta manufaa kwa  mamilioni ya Watanzania wanaoteseka kwa umaskini nchini. Dhamira inakosekana kutokana walioko madarakani kunufaika na  kuwepo kwao madarakani.
2)    Mifumo ya  kisheria na kitaasisi iliyokuwa inatumika kutawala wakati wa mfumo wa chama kimoja cha siasa kuendelea kutumika katika mfumo wa vyama vingi hivyo kunufaisha chama kilikuwa madarakani.
3)    Vyombo vya dola kutumika kisiasa kunyanyasa  wananchi  wanapodai haki  ya uchaguzi huru na wa haki.

Hivyo  matatizo haya  yasipotafutiwa ufumbuzi wa  kikatiba  kabla ya uchaguzi mwingine 2020 tbila shaka  idadi ya wapiga kura  ikapungua  sana  uchaguzi ujao kutokana na wanachi kukata tamaa kwamba uchaguzi hauna manufaa yoyote kw amaisha yao.

Lakini kibaya zaidi tusishangae  umaskini  ukiongezeka  mara dufu  miongoni  mwa  mamilioni ya Watanzania tuendako  maana  hata kama  serikali  ya Rais John Magufuli itafanya kazi kubwa na kuweza kukuza uchumi  kutoka asilimia saba (7%) ilivyo sasa na kufikia asilimia  kumi na tatu (13%) huenda uchumi huo usiwanufaishe Watanzania wengi wanaoteseka kwa  umaskini.

Hii ni kutokana  Katiba na mifumo ya kiutawala iliyopo nchini hivi sasa  kutoa mwanya kwa watawala kujitajirisha  zaidi wao wenyewe kwa fedha  na mali za  za nchi  huku  mamilioni ya Watanzania  wakibaki maskini wa kutupa.

Kwa hiyo  kazi kubwa aliyonayo Rais Dr John Magufuli, UKAWA,  vyama vingine vyote vya siasa  na Watanzania wote  ni kutafakari hatma ya mamilioni ya Watanzania wanaoteseka kwa umaskini  kwa kuzingatia  hayo matatizo  matatu niliyoyaainisha hapo juu.  Mungu Ibariki Tanzania.
 
Note: Ninaridhia anayetaka kuchapisha andiko hili afanya hivyo lengo likiwa ni kujifunza tuijenge nchi yetu nzuri Tanzania.

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment