Umesahau mengine machache Fadhili-wajitahidi majimbo yao yawe ya MFANO kulinganisha yale wa wapinzani wao CCM. yaani waonyeshe utendaji mzuri katika matumizi ya mfuko wa jimbo, kutafuta hela za wahisani-marafiki zao na kufinance miradi ya wananchi inayotokana na mipango ya bottom-up ya priority za watu wao. Badala ya kutumia hela kuhonga watu wahame watumie katika miradi ya maendeleo inayoonekana sio katika malumbano bungeni, kulele, kutoka nje kisha wao kuota vitambi wakati uzembe wa CCM na wakwao ktk maendeleo jimboni unakuwa hauna tofauti ni sawa na nyani kucheka kundule. Hao UKAWA wasaidie NGO zao hizo za kisiasa zijihusishe na community-mobilization, education, organization for implementation of sustainable projects and programs for solving own problems. Wasitegemee vitashuka kama mvua na vitaletwa na fulani tu. Hapa Kazi tu!! Wote tubadilike kifikra tusiwe tegemezi kusubiri vituke tu! Kimatendo-kwa kufanyakazi kiufanisi, kuwa na mipango kibinafsi,
kifamilia, kiukoo, kijamii ya kujitegemea tukijitambua na kujithamini ili kujiletea maendeleo.
Wabongoland, hata kukimbia kimataifa kuanzia EA na kidunia tunashindwa. Wakenya wanaogopwa dunia nzima kwa mbio. Nasi tuna makabila ambayo ni wakimbiaj. Lakini, lakini kufanya mazoezi-mpaka uwekwe hotelini upewe posho ndio ule zoezi na bado unakula na kulewa badala ya zoezi la nguvu. Umoja sio katika maneno, mabango, mapikipiki kupita mbio kugawa vipeperushi na kuichama CCM. Ni wapanzi wa UKAWA vyama vya siasa, NGO zao na jamii wanachama wao kuonyesha kiutendaji katima himaya zao practical examples za utendaji badala ya kukaa vijiweni. Tunangojea vishuke kama mvua! Mabadilikooooo! Lakini sisi wenyewe hatubadiliki kiakili na kiutendaji. Tunabwata ili tuonekane kuwa tunaipinga CCM na serikali yake ili donors wetu watupe funding zaidi. Ikija Evaluation ya utendaji wetyu kikazi katika majimbo yetu kuona hela za majimbo na za misaada zilivyotumika--hakuna tofauti na yule tunayempigia kelele na kumlaumu. Yonda ni Yonda tu kajisemea mmakonde!!
--------------------------------------------
On Fri, 6/11/15, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] HONGERA UKAWA MPEIPA NCHI SOMO
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, 6 November, 2015, 18:11
Mama Nkya umesahau
kuwaambia ukawa ili wajijenge zaidi waachane na kufanyia
hujuma ukiambiwa majimbo yako ni 10 usichukue majimbo ya
wenzako na huko ni kuzigawa kura na kumsababishia mwenzako
kushindwa kama walivyofanyiwa kina matatiro.
Wakumbushe ili ukawa wafanikiwe waache kuchukua makapi
kutoka ccm kama kina sumaye na kingunge wakisema cvm
haijafanya jambo wakati wao walokuwa watendaji wakuu.
Pia umesahau kuwahusia kuws ili umoja huo uendelee
chadema wasitafune ruzuku peke yao wawagawie na wenzao ambao
waliwaunga mkono katika urais.
Vile vile ungeeausia waende bungeni kupambana kwa hoja
wtz hatutaki kuona migomo bungeni wakafanye kazi wakiyotumwa
katika majimbo yao. Bado hujachewa wausie na hayo mama
On Nov 6, 2015 5:16 PM,
"'Mashaka Makana' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Mama Nkya
unanichanganya! Wewe ni mwanaharakati au mwanasiasa?
Sent
from Yahoo Mail on Android From:"'ananilea
nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date:Fri, Nov 6, 2015 at 17:00
Subject:[wanabidii] HONGERA UKAWA MPEIPA
NCHI SOMO
HONGERA UKAWA MPEIPA NCHI
SOMO
Na Ananilea Nkya
Baada ya uchaguzi mkuu
kukamilika, Watanzania wote wanaopigania mabadiliko
ili kila baada ya uchaguzi nchi yetu ipate uongozi
uongozi
utakaowezesha mamilioni ya Watanzania wanaoteseka kwa
umaskini kuondokana na umaskini wao, bila shaka
watavipongeza vyama vinanyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi UKAWA.
UKAWA
wametoa somo kubwa kwa nchi yetu kuhusu changamoto kuu
zinazokabili nchi yetu kufikia uchaguzi huru na wa haki kama
nitakavyoeleza katika makala hii.
Aidha wanachama na viongozi wa CCM ambao
waliamua kuchukua maamuzi magumu kuondoka katika chama
hicho na kuungana na UKAWA katika kupigania mabadiliko nao
wanastahili pongezi kubwa.
Miongoni viongozi hao ni Edward Lowassa
aliyekuwa mgombea Urais CHADEMA –UKAWA ---ambaye
ushawishi wake wa kisiasa umeacha historia ya aina yake
katika uchaguzi wa vyama vingi Tanzania.
Wengine Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Waziri
Mkuu mstaafu Mheshimiwa Fredrick Sumaye na Waziri wa Mambo
ya Ndani mstaafu Lawrence Macha.
Viongozi
hawa wamejitoa mhanga kukubali kujishusha na kuwa sehemu
ya harakati za wananchi kutafuta mabadiliko ya
kunufaisha walio wengi.
Tena wamejitoa bila kujali kudhalilishwa
kwa matusi na kunyanyaswa na vyombo vya dola kama
wanavyonyanyaswa wananchi wa kawaida.
Ninaamini ni watu wasioitakia mema Tanzania
na wasiojali maslahi ya Watanzania wengi ndio pekee
watawabeza viongozi hawa kutokana na uamuzi wao wa
kuungana na wana mabadiliko.
Lakini Watanzania wanaoelewa vema mchango
wa uongozi katika harakati za ukombozi watawapongeza na
kuwatia moyo viongozi hawa waliojitoa mhanga na kuthamini
mchango wao katika kupigania maslahi ya Watanzania walio
wengi maana bila viongozi kujitolea ili kuleta
mabadiliko, mabadiliko hayawezi kupatikana.
Zaidi ya yote vyama
vinavyounda UKAWA ambavyo ni
NLD, NCCR-Mageuzi, CHADEMA Nna CUF vinastahili pongezi
kubwa kwa sababu umoja wao katika uchaguzi wa mwaka huu
umetoa somo jipya katika siasa za vyama vingi Tanzania.
Jambo moja kubwa ambalo
UKAWA wamewathibitishia Watanzania ni kwamba vyama vya
upinzani vikishirikiana kwa dhati na kujiandaa vema
kupata viongozi makini na wenye dhamira ya kweli ya
kuleta mabadiliko kweli ya kunufaisha mamilioni ya
Watanzania maskini, wanashinda uchaguzi kwa kura
nyingi.
Jambo muhimu zaidi
sana ambalo UKAWA wametoa somo kwa Watanzania katika
uchaguzi huu ni kwamba nchi yetu bado ina safari ndefu
kufikia uchaguzi HURU NA WA HAKI unaowesha mshindi
kutangazwa mshindi na si vinginevyo. Je amani inaweza
kutamalaki kwenye jamii yetu kama uhuru na haki kwenye
uchaguzi vitaendelea kuchezewa kwenye uchaguzi?
Swali
hili msingi wake ni mgogoro ulipo sasa kuhusu
kutotangazwa kwa matokeo ya mshindi katika uchaguzi wa
Urais Zanzibar na UKAWA kutokukubali matokeo ya
Urais.
UKAWA katika
uchaguzi huu wametoa somo kwamba kuna matatizo makubwa
matatu yanayokwamisha uchaguzi huru na wa haki
Tanzania. Mambo hayo ni haya:
1)
Walioko madarakani kutokuwa na dhamira ya dhati (political
willingness) kuona mfumo wa siasa za vyama vingi
ukistawi na kuleta manufaa kwa mamilioni ya Watanzania
wanaoteseka kwa umaskini nchini. Dhamira inakosekana
kutokana walioko madarakani kunufaika na kuwepo kwao
madarakani.
2) Mifumo ya kisheria
na kitaasisi iliyokuwa inatumika kutawala wakati wa mfumo wa
chama kimoja cha siasa kuendelea kutumika katika mfumo wa
vyama vingi hivyo kunufaisha chama kilikuwa madarakani.
3)
Vyombo vya dola kutumika kisiasa kunyanyasa wananchi
wanapodai haki ya uchaguzi huru na wa haki.
Hivyo matatizo haya
yasipotafutiwa ufumbuzi wa kikatiba kabla ya uchaguzi
mwingine 2020 tbila shaka idadi ya wapiga kura
ikapungua sana uchaguzi ujao kutokana na wanachi kukata
tamaa kwamba uchaguzi hauna manufaa yoyote kw amaisha
yao.
Lakini kibaya zaidi
tusishangae umaskini ukiongezeka mara dufu
miongoni mwa mamilioni ya Watanzania tuendako maana
hata kama serikali ya Rais John Magufuli itafanya kazi
kubwa na kuweza kukuza uchumi kutoka asilimia saba (7%)
ilivyo sasa na kufikia asilimia kumi na tatu (13%) huenda
uchumi huo usiwanufaishe Watanzania wengi wanaoteseka kwa
umaskini.
Hii ni kutokana
Katiba na mifumo ya kiutawala iliyopo nchini hivi sasa
kutoa mwanya kwa watawala
kujitajirisha zaidi wao wenyewe kwa fedha na mali za
za nchi huku mamilioni ya Watanzania wakibaki maskini
wa kutupa.
Kwa hiyo kazi
kubwa aliyonayo Rais Dr John Magufuli, UKAWA, vyama
vingine vyote vya siasa na Watanzania wote ni kutafakari
hatma ya mamilioni ya Watanzania wanaoteseka kwa umaskini
kwa kuzingatia hayo matatizo matatu niliyoyaainisha hapo
juu. Mungu Ibariki Tanzania.
Note: Ninaridhia anayetaka kuchapisha andiko
hili afanya hivyo lengo likiwa ni kujifunza tuijenge nchi
yetu nzuri Tanzania.
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata
Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
No comments:
Post a Comment