Sunday, 27 September 2015

Re: [wanabidii] WATU WASIOJUA TULIKOTOKA WANAJUA WANAKOTUPELEKA?

Na ni Tanzania (labda na kenya) ambako watu waliostahili kuwa mahakamani wako wanatafuta kutafuta uongozi wa nchi. Mabadiliko ni muhimu na hayo ni sehemu ya mabadiliko
--------------------------------------------
On Sat, 9/26/15, barakathomson@rocketmail.com <barakathomson@rocketmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] WATU WASIOJUA TULIKOTOKA WANAJUA WANAKOTUPELEKA?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, September 26, 2015, 11:15 AM

Serikali haijafanya kitu ni
kibwagizo tu. UKWELI NI KWAMBA KAMA SIYO CCM KUKUMBATIA
WEZI, WALA RUSHWA, MAFISADI, MAJANGILI NA WANALOLIINGIZA
TAIFA KWENYE MIKATABA MIBOVU MRADI WAPATE 10% TUSINGEKUWA NA
HALI HII. TUMEPITWA NA KENYA, RWANDA NK. Kwa uzembe wa
watawala

Ulisikia wapi Raisi wa nchi anasamehe wezi wa mabilioni(EPA)
kama si Tanzania tu.

Sent from my HTC

----- Reply message -----
From: "'ELISA MUHINGO' via Wanabidii"
<wanabidii@googlegroups.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] WATU WASIOJUA TULIKOTOKA WANAJUA
WANAKOTUPELEKA?
Date: Sat, Sep 26, 2015 10:37



Kuna watu wanagombea uongozi wa Taifa hili katika uchaguzi
mkuu. Wanasema katika miaka 54 ya uhuru wetu hakuna
kilichofanyika. Kwa hiyo wanataka kulikomboa taifa hili.
Katika ufunguzi wa kampeni za CCM rais mstaafu aliwaita watu
hao WAPUMBAVU. Ameshambuliwa kwa neno hilo kana kwamba sio
kweli. Nami sitaki kutoa msimamo wangu katika hilo lakini
ukweli mtu kutojua kuwa Tanzania haiku kama ilivyokuwa 1961
ni tatizo kubwa sana. Kama siasa ni kutaka kutumikia watu
lazima mtu uwe unajua mazingira uliyomo ili uweze kuwaongoza
wenzako kutoka point 'C' kwenda 'G'. Sasa kama
kiongozi hajui mko wapi anawezaje kuwapeleka 'G'? Siku
ya siku akiwarudisha point 'B' mtakataaje wakati
mlimkubalia kuwa hakuna chochote? Kama technicall speaking
Mkapa hakukosea katika tamshi lake basi kukubaliana na
wanaosema miaka Hamsini hakuna kilichofanyika ni kujiunga na
wenye kipaji alichokitaja Mkapa.
Tanzania imeendelea. Kuna mambo mengi yamefanyika. Kuna
mambo mengi hayajafanyika. Ambayo yamefanyika ni msingi wa
kufanya ambayo hayajafanyika. Kwa yale ambayo hayajafanyika
kuna sababu mbili 1) Hayajafanyika kwa sababu ya yale
yaliyofanyika. Mfano tusingeweza kuanza kuchimba gesi kabla
ya kuigundua. 2) kwa sababu ya uharibifu, uzembe
nakadhalika. Ndiyo maana kuna uchaguzi. Uchaguzi ambamo
tunaweza kubadilisha viongozi au hata chama. Kabla ya
kufanya uchaguzi tunavichunguza vyama, hasa ilani zake na
baada ya hapo tunawachunguza wagombea ambao ni watekelezaji
wa ilani hizo. Hapo tutaweza kutoka tulipo kwenda mbele,
kama hatukukosea hapo.
Maisha ya watanzania yamebadilika katika mambo mengi. Mengi
sana. Tanzania yenyewe imebadilika. Imebadilika sana. Taja
jambo lolote. Ukilipima jinsi lilivyokuwa 1961/4 na
kulilinganisha na sasa, utaona mabadiliko makubwa. Nitataja
machache:
1) Tumetengeneza Tanzania. Zamani tulikuwa makabira.
Watawala wetu wakatuunga katika mataifa ambayo tuliyakomboa
kwa kuwaondoa watawala. Baadaye Tukaunganisha Tanganyika na
Zanzibar na kupata Tanzania. Kuna watu wanahoji uhalali wa
Tanzania lakini hawahoji uhalali wa Tanganyika. Tofauti ni
kuwa Tanganyika iliundwa na wakoloni lakini Tanzania
tumeiunda sisi watanzania.
=Tanganyika ilipatia uhuru wake mwaka 1961 Na kuungana na
Zanzibar 1964 na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
2) Nakumbuka mwaka 1962 alikuja Chifu wa eneo letu (Omukama
Lutinwa) shuleni Katarabuga Wilayani Missenyi. Wanafunzi
tulijikusanya na kupiga magoti katika uwanja na walimu
wakajipanga kumsalimia wakiwa wameinama. Salamu yenyewe
inasema Uinulimwe muweza-Habuka Lugaba. Inadhalilisha.
Ukilinganisha na sasa ona kwenye mitandao hii
tunavyomchambua Kikwete. Hata kuandika neon Kikwete bila
kuweka neno Mheshimiwa, au Mtukufu, enzi hizo ningekamatwa.
3) Myaka hiyo ya mwanzo wa uhuru Kupiga mswaki asubuhi
lilikuwa somo darasani. Kuvaa nguo ya ndani kabla ya kaptura
ilikuwa hadithi au watoto wa matajiri na tulikuwa
tunaonyeshana –fulani anavaa chupi. Mwalimu Nyerere
aliwahi kusema alivaa nguo akiwa na myaka 12 wakati akienda
shule. Tulitembea kilomita 10 kuifuata shule ya dhehebu letu
na kuipita shule isiyo ya dhehebu letu. Ni tofauti na sasa.
Mswaki ni wazazi wanamfundisha mtoto nyumbani, nk nk nk.
Tukiziangalia idadi ya shule karibu kila kijiji kina shule
ya msingi, kila kata ina shule ya sekondari kila wilaya ina
chuo cha aina Fulani.
4) Mpaka 1980 nadhani; magazeti yalikuwa ni UHURU na Daily
News na mfanyakazi (Gazeti la NUTA). Gazeti huru la kwanza
lilikuwa Majira. Sasa tunachagua kusoma hili na kuliacha
lile. Radio pekee ilikuwa RTD (Radio Tanzania Dar Es
Salaam). Sasa karibu kila mkoa una vituo vitatu mpaka vine.
5) Usafiri wa kawaida kutoka mathalan Kijijini kwetu Bwanjai
kuja Bukoba mjini kilomita 25 usafiri ilikuwa ni kutembea
kwa mguu au baiskeri.
6) Mpaka 1977 Mtu ukipanda gari Tukuyu asubuhi ulikuwa
ukifika Dar Es Salaam kesho yake saa nne. Hapo mmetembea
mchana kutwa na usiku kucha.
7) Kuna tunaokumbuka wakati ule tunachagua kati ya Nyerere
na bure. Wabunge walikuwa wanatembea pamoja kwenye gari.
Wakifika kila mmoja anajieleza halafu wanaondoka wote. Mwaka
huu tunauamuzi kati ya watu wanane.
Hata kwa hayo machache; yasiyo na yaliyo ya msingi
nitamshangaa mtu anayewakubalia wanaosema Vyama
vilivyopigania uhuru havijafanya lolote. Sitavishangaa vyama
ila wanaovikubalia. Sitavishangaa vyama wala viongozi wake
Maana mkapa alishalimaliza siku ya ufunguzi wa kampeni.
Elisa Muhingo
0767 187 507



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email
ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email
ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment