Muhingo nakubaliana na wewe hata siku moja haki haichanganyani batili ukawa tuliipenda lakini mafisadi wameipenda zaidi
On Jul 28, 2015 10:00 AM, "'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
-- anzania ina mascientist wa ajabu. aweza kujaribu kumhamisha Sangara kutoka ziwa kubwa kama Victoria na kumuweka katika bwawa la kuchimbwa na kutarajia humo aishi na kuzaa sana. Kuna wanaojua kuwa Sangara akishaona jua basi. haishi zaidi ya masaa. Sasa tusubiri tuone wanasayansi hawa. Waliambiwa Lowasa hawezi kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera yake kuwania urais. Wakabisha mpaka wengine kuapa kuwa asipoteuliwa wafe. Wengine wakasema wanaoona kichefuchefu wale limau. Ikatokea. Sasa wanadhani CCM iliyomkataa itamruhusu auchukue urahisi kupitia mabwawa ya kuchimbwa. Nani kasema. Toka lini moja kwon geza moja ikazaa sita? Hesabu nyingine mbona rahisi. Jamani Watanzania wamechoka kubahatisha. Wamebahatisha ndani ya CCM wakafika mahala wakaamua hawatabahatisha tena. Tumaini lilikuwa UKAWA. CCM ikaona hilo. Najua kuwa kama watanazania wakitaka kubahatisha tena watabahatisha ndani ya CCM inayoonekanas kujua watanzania wamechoka nini. Watanzania hawajaichoka
CCM. Wamezichoka sera zao za kuwavumilia mafisadi. Haiwezekani mafisadi wakakaribishwa UKAWA ikatarajia kuwa watanzania watasema sisi na ukawa. hapana. Wakati CCM inajipinda kuwatimua mafisadi UKAWA inadhani itaendelea kuwa UKAWA na mafisadi hao. Kifo cha UKAWA hakiwezi kuleta kishindo kama cha CCM. Hapana. Madereva tunajua. Ukikanyaga kuku wala gari haliyumbi. UKAWA inakufa
--------------------------------------------
On Sun, 7/26/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Lowassa apigwa shinikizo kali
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, July 26, 2015, 7:11 AM
Kwa
ufupi
Washirika wake wataka
maamuzi sasa, Mkewe, Rostam Aziz wadaiwa
kumzuia.
Shinikizo
dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, la kumtaka
akihame
Chama Cha Mapinduzi (CCM) linazidi kuongezeka na katika timu
yake ya
ndani ni watu wawili tu wanaonekana kumtaka abakie ndani ya
chama hicho.
Habari
za ndani ya vikao vya kujadili hatua za kuchukuliwa na
Lowassa baada ya
jina lake kukatwa kwenye mchakato wa kugombea urais kupitia
CCM,
zinasema kuwa wandani wake wanaamini kuwa hana atakachopata
kama
ataendelea kubaki kwenye chama hicho
tawala.
"Kaka
sikiliza, inavyoelekea shinikizo dhidi ya Lowassa ni kubwa
sana. Watu
wake wa ndani wanataka aondoke CCM. Wanaona kama
amedhalilishwa mno,"
kilisema chanzo chetu ndani ya vikao
hivyo.
Chanzo
hicho kilichoomba kutokutajwa jina kwa sasa, kilisema kuwa
watu wake wa
ndani wanaamini Lowassa akiendelea kubaki CCM atakuwa
amewavunja moyo
wale wote waliompigania, hasa vijana waliojaa matumaini ya
kumuona
akiongoza taifa hili.
Wandani
wa Lowassa wanaamini kuwa kama akiamua kujiunga na chama
chenye nguvu
cha upinzani anaweza kutimiza ndoto yake ya kuwatumikia
Watanzania kama
rais wa awamu ya tano.
Chanzo
chetu kinasema kuwa Lowassa mwenyewe amekwisha kuamua
kufanya uamuzi
mgumu, ila kuna msuguano juu ya namna ya kuondoka
CCM.
Taarifa
zaidi zinasema kuwa watu wawili katika timu ya ndani ya
Lowassa ndio
wanaelekea kuwa na mawazo tofauti. Hawa ni Rostam Aziz,
mwanasiasa na
mfanyabiashara mashuhuri nchini na mtu mwingine
anayetofautiana na
mkakati huu mpya wa kung'oka CCM ni mkewe, Mama Regina
Lowassa.
Chanzo
chetu kinasema kuwa wawili hao wanaamini mapigo ambayo
Lowassa
amekumbana nayo ni mengi na yanatosha, kwa maana hiyo
ingefaa tu
apumzike.
"Sijui
ni kwa nini RA (Rostam Aziz) anakuwa skeptical (shaka). Si
unakumbuka
ndiye aliyesema amechoshwa na siasa uchwara... sasa sijui
kwa nini
anapunguza makali," chanzo
kilisema.
Hata
hivyo, vyanzo vyetu vinaongeza kuwa pamoja na upinzani huo
Lowassa
anadaiwa kuwa amekwisha kuamua na kinachosubiriwa sasa ni
muda tu wa
kutamka anakokwenda.
Wakati
hali ikiwa hivyo ndani ya kambi ya Lowassa, kuna taarifa za
kuaminika
kuwa kumekuwa na mashauriano baina ya watu wake na viongozi
waandamizi
wa kambi ya upinzani juu ya mwelekeo wake wa
kisiasa.
Mwandani
mwingine katika kambi ya Lowassa alisema kimsingi yeye
(Lowassa)
amekwisha kuamua, anachofanya ni kuona kwamba watu wake wa
karibu
hawadhuriki na uamuzi wake huo.
Chanzo
hicho kiliiambia NIPASHE kuwa wenye msimamo mkali katika
kambi ya
Lowassa wanaamini utabiri wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
kuwa upinzani
utatoka ndani ya CCM utatimia mwaka
huu.
"Mnakumbuka ya Mrema
(Augustino) alipoondoka CCM siasa za Tanzania zilibadilika
mpaka leo? Sasa safari hii ni zaidi,"
alisema.
Takriban wiki mbili sasa,
Lowassa amekuwa na jambo kubwa moyoni analitaka kuwaambia
Watanzania.
Mara
ya kwanza alikuwa afanye mkutano na waandishi wa habari
Julai 13 mwaka
huu mjini Dodoma majira ya asubuhi, lakini mkutano huo
ukahamishiwa Dar
es Salaam ambako pia ukaahirishwa kwa muda
usiojulikana.
Tangu wakati huo kumekuwa
na tetesi kuwa alikuwa atangaze kujiondoa
CCM.
Lowassa
ni miongoni mwa makada 38 waliojitosa kuwania kuteuliwa
kuwa wagombea
wa nafasi ya urais wa CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika
Oktoba 25,
mwaka huu. Hata hivyo, jina lake halikuwamo katika orodha ya
makada
watano waliopitishwa kwenye vikao vya juu vya chama hicho
ambavyo
mwishowe vilimteua John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais
atakayekabiliana na wagombea wa upinzani katika uchaguzi
mkuu huo.
CHANZO:
NIPASHE
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment