Thursday, 25 June 2015

Re: [wanabidii] Tuwaulize wawania urais maswali magumu

Ananilea dadangu mbona unasita kutamka kuwa anayetufaa kwa sasa ni warioba
SENT FROM ALCATEL ONETOUCH TABLET

'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

>Na zaidi tunahitaji Rais mwenye aliyeamua mwenyewe na kwa dhati kabisa anaona uongozi wake unaweza kutoa mchango mkubwa kwa nchi. Maana yake awe ni mtu mwenye maono, utashi, mchapa kazi, hekima, asiye mbinafsi na zaidi mwenye ujasiri wa kusimamia serikali yake iwajibike kwa wananchi na siyo kuwakandamiza na kuwaumiza kwa kutumia jeshi la polisi wanapodai haki ya afya, elimu, barabara na ajira yenye staha zinazotokana na utajiri wa nchi yetu na wala siyo kuomba omba kwa wafadhili ambao nao wanakwapua mali zatu.
>
>Mtu anaweza kuwa msafi lakini moga wa kupigania haki za wanyonge. Moga wa kufanya maamuzi mpaka amuulize aliyemsukuma kugombea hiyo nafasi. Si mnakumbuka Rais Kikwete awali alionekana kama vile alikuwa na dhamira kusimamia upatikanaji wa Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi lakini mwishoni alikosa ujasiri huo baada ya kuvutwa na chama chake maana Katiba ya wananchi ingeondoa ufisadi unaokinufaisha chama chake? Alikosa sifa moja tu--ujasiri akaitumbukiza nchi kwenye mpasuko na zaidi kachelewesha mabadiliko chanya --rasilimali za nchi kunufaisha wananchi.
>
>Hivyo mgombea anaweza kuonekana ana sifa ya usafi lakini akaogopa kubomoa mfumo unaofukarisha na kutesa wananchi walio wengi huku wakitajirika watawala wachache.
>
>Sidhani kwamba kwa wananchi hoja ni mtu anatoka Tanganyika au Zanzibar,Kusini au mashariki, maana hoja siyo upande wa nchi atokako mtu katika jamhuri yetu, bali ni mtu mweye uwezo na nia kiasi gani ya kujitoa kuongoza nchi ili wananchi wengi wanufaike na rasilimali za nchi na wasiwe wananyanyaswa na na kuteswa wanapodai uwajibikaji wa serikali. Kuendelea kufanya Ikulu kuwa sehemu ya majaribio ya uongozi kutaendelea kutaigharimu nchi na wananchi.
>Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
>
>--------------------------------------------
>On Thu, 6/25/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Subject: [wanabidii] Tuwaulize wawania urais maswali magumu
> To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Thursday, June 25, 2015, 12:15 PM
>
> Evarist Chahali
>
> Ninaomba pia kutumia fursa hii kuwatakia ndugu zangu
> Waislamu mfungo mwema wa mwezi Mtukukufu wa Ramadhan.
>
> Katika makala ya hii nitaendelea kuzungumzia
> kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
> baadaye mwaka huu. Na zaidi nitaelemea katika nafasi ya
> urais, hususan mchakato unaoendelea ndani ya chama tawala,
> CCM, ambapo hadi wakati ninaandaa makala hii, makada 37 wa
> chama hicho wameshajitokeza kuomba ridhaa ya chama hicho
> kuwapitisha kuwania nafasi hiyo.
>
> Lakini kabda sijaingia kwa undani, pengine ni muhimu
> tukumbushane kuwa wakati idadi ya makada 37 (ambayo huenda
> ikaongezeka) ni ya kihistoria, suala la kushtua zaidi ni
> ukweli kwamba miongoni mwao ni pamoja na Makamu wa Rais,
> Waziri Mkuu na mawaziri kamili saba, bila kujumuisha manaibu
> waziri.
>
> Nimekumbushia suala hili kwa sababu ni vigumu kufahamu
> serikali yetu muda huu inaendeshwaje, hasa ikizingatiwa kuwa
> Rais Jakaya Kikwete nae amekuwa katika safari za mara kwa
> mara nje ya nchi (wakati ninaandika makala hii yupo nchini
> India).
>
> Ukiondoa Makamu wa Rais, ambaye anakuwa kaimu Rais wakati
> Rais anapokuwa nje, licha ya majukumu ya kiwaziri, Waziri
> Mkuu na hao mawaziri wengine pia ni wabunge. Katika hili ni
> vigumu kufahamu wanamudu vipi kugawa muda wao kwa majukumu
> yao ya kiserikali, kiubunge na hayo ya kuwania kuteuliwa
> kuwania nafasi ya Urais.
>
> Hata hivyo, si vigumu kudhani kwamba kwa muda huu, akili na
> nguvu kubwa kwa makada wote waliotangaza nia zitakuwa
> zimeelekezwa kwenye kinyang'anyiro cha Urais. Kwa kiasi
> gani hilo linaathiri utumishi wao kwa umma, ni vigumu kwa
> sisi wengine kufahamu.
>
> Nikirejea kwenye suala la makada wa CCM kutangaza nia zao
> kuwania urais, jina lililosikika zaidi wiki iliyopita
> lilikuwa la Jaji Mkuu wa zamani, Augustino Ramadhan. Japo
> jina lake lilishawahi kutajwa huko nyuma kama mmoja wa watu
> 'wanaoweza kuokoa jahazi,' lakini kwa kiasi kikubwa
> habari zilizosikika huko nyuma zilionekana kama tetesi tu
> pasi uthibitisho.
>
> Angalau mara mbili, gazeti hili la Raia Mwema lilibeba
> habari zilizohusu uwezekano wa Jaji Ramadhani kugombea urais
> kwa tiketi ya CCM.
>
> Binafsi, kwanza ninaheshimu uamuzi wa Jaji Ramadhani kwani
> ni haki yake ya Kikatiba kuchukua uamuzi huo. Hata hivyo,
> tayari kuna baadhi ya wananchi walioshtushwa kumsikia Jaji
> huyo akielezea kuwa amekuwa mwanachama wa CCM tangu miaka ya
> sitini.
>
> Kwanza ninadhani alipitwa tu kutoa kauli hiyo kwa sababu CCM
> iliundwa mwaka 1977 baada ya TANU na ASP kuungana. Kwahiyo,
> hakukuwa na CCM miaka ya sitini.
> Jaji huyo alieleza kuwa alijiondoa CCM mwaka 1992 kufuatia
> mabadiliko ya sheria, ambapo mfumo wa vyama vingi
> uliruhusiwa na hiyo kupelekea watumishi wa umma kutoruhusiwa
> kuwa wanachama wa vyama vya siasa.
>
> Japo Jaji Ramadhan anasema alijiondoa CCM wakati huo, kuna
> wanaokwenda mbali zaidi na kutaka uthibitisho katika suala
> hilo. Sote tunaijua Tanzania yetu, na kwa hakika
> tunawafahamu vema viongozi na wanasiasa wetu. Ni kwa mantiki
> hiyo, kuna wanaotaka uthibitisho kuwa kweli Jaji huyo
> alijiondoa CCM na kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha
> siasa katika utumishi wake, ikiwa ni pamoja na Ujaji Mkuu.
>
> Na kauli hiyo ya uana-CCM wake, kwa namna flani, imerejesha
> tena suala la hukumu iliyotolewa na Jaji huyo kwa
> kushirikiana na majiji wengine dhidi ya kesi ya Mchungaji
> Christopher Mtikila aliyetaka mahakama itamke kuwa sheria
> inayozuwia mgombea binafsi ni kinyume cha Katiba.
> Pasi kuingiza kiundani katika kesi na hukumu hiyo, binafsi
> ninaichukulia hukumu hiyo kuwa moja ya hiba (legacies) kuu
> za utumishi wa Jaji Ramadhani.
>
> Kwa baadhi yetu tunadhani Jaji huyo angebaki shujaa kwa
> demokrasia kwa sababu mfumo wa sasa unaolazimisha wawania
> nafasi mbalimbali za uongozi ikiwa pamoja na urais kuwa
> wanachama wa vyama vya siasa unatupunja fursa ya kupata
> viongozi wa kisiasa wazalendo lakini wasiotaka kujihusisha
> na vyama vya siasa.
>
> Hata hivyo, ili kumtendea haki, ni muhimu kutambua kuwa
> hukumu hiyo haikuwa maamuzi binafsi ya Jaji Ramadhani bali
> licha ya kuwahusisha majaji wengine pia, ilikuwa ni ya
> kisheria na sio hisia binafsi.
> Lakini kwangu, licha ya dalili zinazoonekana wazi kuwa kana
> kwamba CCM imeshapata mgombea wake urais kufuatia uamuzi wa
> Jaji Ramdhan kutangaza nia, nina wasiwasi kidogo kuhusu
> ufanisi wake.
> Kubwa zaidi ni ukweli kwamba Idara ya Mahakama, ambayo licha
> ya Jaji Ramadhan kuitumikia muda mrefu bali pia aliwahi kuwa
> mkuu wake kwa maana ya ujaji mkuu, imeendelea kuwa moja ya
> taasisi sugu kwa rushwa.
>
> Takribani kila ripoti inayotolewa kuhusu tatizo la rushwa
> katika taasisi mbalimbali za serikali nchini mwetu, Idara ya
> Mahakama haikosekani, na tena ikishika nafasi za juu.
> Mara baada ya kuchukua fomu kuomba CCM imteue kuwania Urais,
> Jaji Ramadhan aliwaambia waandishi wa habari kuwa atatumia
> uzefu wake kupambana na ufisadi. Swali la msingi: uzoefu
> upi? Huohuo ulioshindwa ukiondoa Idara ya Mahakama katika
> orodha ya taasisi zinazoongoza kwa rushwa?
>
> Kwa upande mwingine, Jaji Ramadhan alikuwa mjumbe wa 'Tume
> ya Warioba' iliyokusanya maoni kuhusu mabadiliko ya
> Katiba. Sote twakumbuka yaliyomsibu Jaji Joseph Warioba na
> baadhi ya wasaidizi wake kupigania sio tu kazi nzuri
> iliyofanywa na tume yao bali pia mustakabali wa Katiba
> mpya.
> Kwanini Jaji Ramadhani amekuwa kimya sana katika suala hilo?
> Je ukimya wake ulitokana na kufahamu kuwa siku moja angeomba
> kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM?
>
> Na katika hilohilo, kwa vile mapendekezo ya Tume hiyo
> iliyomshirikisha Jaji Ramadhani yalikuwa muungano wenye
> muundo wa serikali tatu, je kwa vile CCM ambayo jaji huyo
> anaiomba ridhaa ya kumteua awe mgombea wake ina msimamo wa
> serikali mbili kama ilivyo sasa, hilo si tatizo angalau
> kimsimamo na kimtizamo?
>
> Hadi muda huu, Jaji Ramadhani ni Rais wa Mahakama ya Afrika
> kuhusu haki za binadamu. Sihitaji kuorodhesha matukio lukuki
> ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania lakini
> miongoni mwa matukio makubwa ni pamoja na ukatili unaofanywa
> na Jeshi la Polisi na rushwa (naam, rushwa sio tu adui wa
> haki bali pia inachangia ukiukwaji mkubwa wa haki za
> binadamu).
> Je Jaji Ramadhani amekuwa wapi wakati ukiukwaji wa haki za
> binadamu ukiendelea kushamiri na kuwa kama umehalalishwa na
> Katiba yetu? Ni nani anaweza kusimama hadharani na kuwaambia
>
>
> Watanzania kuwa 'Urais wa Jaji Ramdhani katika Mahakama ya
> Haki za Binadamu Afrika umechangia hili na lile katika
> kutetea au kudumisha haki za binadamu nchini Tanzania'?
> Niwe mkweli, binafsi ninamwona Jaji Ramadhani kama Rais
> Kikwete alipojitambulisha mwaka 2005 kuwania urais na
> hatimaye kushindwa nafasi hiyo.
>
> Alionekana mtu mwadilifu, aliyeitumikia nchi kwa muda mrefu,
> na pengine kubwa zaidi, msafi (asiye na kashfa). Sifa hizo
> zinalingana na tunazosikia kuhusu Jaji Ramadhan. Je, kwa
> mfano, kuwa msafi ni sawa na kuwa na uwezo wa kuongoza
> nchi?
>
> Lakini la mwisho kuhusu kada huyo ni taarifa za awali kuwa
> amekuwa akiombwa na baadhi ya wana-CCM kuwania nafasi ya
> urais (kuna wanaodai kuwa ndio mtu pekee anayeweza kumudu
> 'kumzuia' Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa asiingie
> Ikulu, na wengine wanasema Jaji huyo ndio 'msafi zaidi'
> kuliko makada wengine wanazowania nafasi hiyo).
>
> Swali la msingi: je hao waliomwomba (kama ni kweli)
> hawafanyi hivyo kwa maslahi yao binafsi? Na je, kumwomba
> huko (kama ni kweli) hakutopelekea urais wa Jaji Ramadhan
> (iwapo atashinda) ukaishia kuwa kama 'deni la kwa
> wanamtandao' lilivyouandama utawala wa Rais Kikwete?
> Nimalizie makala hii kwa kuwakumbusha tena Watanzania
> wenzangu kuwa ni muhimu tujiulize na kuwauliza wawania urais
> maswali magumu ili tusije kuishia kujiulaumu huko mbeleni.
>
> Nchi yetu ipo katika wakati mgumu; umasini wa kupindukia
> huku ufisadi ukizidi kuimarika, uhaba mkubwa wa uzalendo,
> utovu mkubwa wa maadili ya uongozi ikiwa na pamoja na uhuni
> katika matumizi ya fedha za umma, shilingi inayporomoka kama
> ipo kwenye mashindano ya marathoni na kadhalika.
>
> Tunahitaji rais ambaye si tu anajua matatizo yetu bali pia
> ana uzalendo na uwezo wa kukabiliana nayo. Hatuhitaji Rais
> msafi lakini mwoga wa kupambana na maharamia wanaoibomoa
> nchi yetu kila kukicha.
> Hatuhitaji mtu anayeahidi kupambana na rushwa ilhali hana
> mfano japo mmoja wa jinsi alivyowahi kupambana na rushwa.
>
> chanzo raia mwema
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit
> https://groups.google.com/d/optout.
>
>--
>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment