Thursday, 25 June 2015

Re: [wanabidii] Tuwaulize wawania urais maswali magumu

Na zaidi tunahitaji Rais mwenye aliyeamua mwenyewe na kwa dhati kabisa anaona uongozi wake unaweza kutoa mchango mkubwa kwa nchi. Maana yake awe ni mtu mwenye maono, utashi, mchapa kazi, hekima, asiye mbinafsi na zaidi mwenye ujasiri wa kusimamia serikali yake iwajibike kwa wananchi na siyo kuwakandamiza na kuwaumiza kwa kutumia jeshi la polisi wanapodai haki ya afya, elimu, barabara na ajira yenye staha zinazotokana na utajiri wa nchi yetu na wala siyo kuomba omba kwa wafadhili ambao nao wanakwapua mali zatu.

Mtu anaweza kuwa msafi lakini moga wa kupigania haki za wanyonge. Moga wa kufanya maamuzi mpaka amuulize aliyemsukuma kugombea hiyo nafasi. Si mnakumbuka Rais Kikwete awali alionekana kama vile alikuwa na dhamira kusimamia upatikanaji wa Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi lakini mwishoni alikosa ujasiri huo baada ya kuvutwa na chama chake maana Katiba ya wananchi ingeondoa ufisadi unaokinufaisha chama chake? Alikosa sifa moja tu--ujasiri akaitumbukiza nchi kwenye mpasuko na zaidi kachelewesha mabadiliko chanya --rasilimali za nchi kunufaisha wananchi.

Hivyo mgombea anaweza kuonekana ana sifa ya usafi lakini akaogopa kubomoa mfumo unaofukarisha na kutesa wananchi walio wengi huku wakitajirika watawala wachache.

Sidhani kwamba kwa wananchi hoja ni mtu anatoka Tanganyika au Zanzibar,Kusini au mashariki, maana hoja siyo upande wa nchi atokako mtu katika jamhuri yetu, bali ni mtu mweye uwezo na nia kiasi gani ya kujitoa kuongoza nchi ili wananchi wengi wanufaike na rasilimali za nchi na wasiwe wananyanyaswa na na kuteswa wanapodai uwajibikaji wa serikali. Kuendelea kufanya Ikulu kuwa sehemu ya majaribio ya uongozi kutaendelea kutaigharimu nchi na wananchi.
Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 6/25/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Tuwaulize wawania urais maswali magumu
To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, June 25, 2015, 12:15 PM

Evarist Chahali

Ninaomba pia kutumia fursa hii kuwatakia ndugu zangu
Waislamu mfungo mwema wa mwezi Mtukukufu wa Ramadhan.

Katika makala ya hii nitaendelea kuzungumzia
kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
baadaye mwaka huu. Na zaidi nitaelemea katika nafasi ya
urais, hususan mchakato unaoendelea ndani ya chama tawala,
CCM, ambapo hadi wakati ninaandaa makala hii, makada 37 wa
chama hicho wameshajitokeza kuomba ridhaa ya chama hicho
kuwapitisha kuwania nafasi hiyo.

Lakini kabda sijaingia kwa undani, pengine ni muhimu
tukumbushane kuwa wakati idadi ya makada 37 (ambayo huenda
ikaongezeka) ni ya kihistoria, suala la kushtua zaidi ni
ukweli kwamba miongoni mwao ni pamoja na Makamu wa Rais,
Waziri Mkuu na mawaziri kamili saba, bila kujumuisha manaibu
waziri.

Nimekumbushia suala hili kwa sababu ni vigumu kufahamu
serikali yetu muda huu inaendeshwaje, hasa ikizingatiwa kuwa
Rais Jakaya Kikwete nae amekuwa katika safari za mara kwa
mara nje ya nchi (wakati ninaandika makala hii yupo nchini
India).

Ukiondoa Makamu wa Rais, ambaye anakuwa kaimu Rais wakati
Rais anapokuwa nje, licha ya majukumu ya kiwaziri, Waziri
Mkuu na hao mawaziri wengine pia ni wabunge. Katika hili ni
vigumu kufahamu wanamudu vipi kugawa muda wao kwa majukumu
yao ya kiserikali, kiubunge na hayo ya kuwania kuteuliwa
kuwania nafasi ya Urais.

Hata hivyo, si vigumu kudhani kwamba kwa muda huu, akili na
nguvu kubwa kwa makada wote waliotangaza nia zitakuwa
zimeelekezwa kwenye kinyang'anyiro cha Urais. Kwa kiasi
gani hilo linaathiri utumishi wao kwa umma, ni vigumu kwa
sisi wengine kufahamu.

Nikirejea kwenye suala la makada wa CCM kutangaza nia zao
kuwania urais, jina lililosikika zaidi wiki iliyopita
lilikuwa la Jaji Mkuu wa zamani, Augustino Ramadhan. Japo
jina lake lilishawahi kutajwa huko nyuma kama mmoja wa watu
'wanaoweza kuokoa jahazi,' lakini kwa kiasi kikubwa
habari zilizosikika huko nyuma zilionekana kama tetesi tu
pasi uthibitisho.

Angalau mara mbili, gazeti hili la Raia Mwema lilibeba
habari zilizohusu uwezekano wa Jaji Ramadhani kugombea urais
kwa tiketi ya CCM.

Binafsi, kwanza ninaheshimu uamuzi wa Jaji Ramadhani kwani
ni haki yake ya Kikatiba kuchukua uamuzi huo. Hata hivyo,
tayari kuna baadhi ya wananchi walioshtushwa kumsikia Jaji
huyo akielezea kuwa amekuwa mwanachama wa CCM tangu miaka ya
sitini.

Kwanza ninadhani alipitwa tu kutoa kauli hiyo kwa sababu CCM
iliundwa mwaka 1977 baada ya TANU na ASP kuungana. Kwahiyo,
hakukuwa na CCM miaka ya sitini.
Jaji huyo alieleza kuwa alijiondoa CCM mwaka 1992 kufuatia
mabadiliko ya sheria, ambapo mfumo wa vyama vingi
uliruhusiwa na hiyo kupelekea watumishi wa umma kutoruhusiwa
kuwa wanachama wa vyama vya siasa.

Japo Jaji Ramadhan anasema alijiondoa CCM wakati huo, kuna
wanaokwenda mbali zaidi na kutaka uthibitisho katika suala
hilo. Sote tunaijua Tanzania yetu, na kwa hakika
tunawafahamu vema viongozi na wanasiasa wetu. Ni kwa mantiki
hiyo, kuna wanaotaka uthibitisho kuwa kweli Jaji huyo
alijiondoa CCM na kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha
siasa katika utumishi wake, ikiwa ni pamoja na Ujaji Mkuu.

Na kauli hiyo ya uana-CCM wake, kwa namna flani, imerejesha
tena suala la hukumu iliyotolewa na Jaji huyo kwa
kushirikiana na majiji wengine dhidi ya kesi ya Mchungaji
Christopher Mtikila aliyetaka mahakama itamke kuwa sheria
inayozuwia mgombea binafsi ni kinyume cha Katiba.
Pasi kuingiza kiundani katika kesi na hukumu hiyo, binafsi
ninaichukulia hukumu hiyo kuwa moja ya hiba (legacies) kuu
za utumishi wa Jaji Ramadhani.

Kwa baadhi yetu tunadhani Jaji huyo angebaki shujaa kwa
demokrasia kwa sababu mfumo wa sasa unaolazimisha wawania
nafasi mbalimbali za uongozi ikiwa pamoja na urais kuwa
wanachama wa vyama vya siasa unatupunja fursa ya kupata
viongozi wa kisiasa wazalendo lakini wasiotaka kujihusisha
na vyama vya siasa.

Hata hivyo, ili kumtendea haki, ni muhimu kutambua kuwa
hukumu hiyo haikuwa maamuzi binafsi ya Jaji Ramadhani bali
licha ya kuwahusisha majaji wengine pia, ilikuwa ni ya
kisheria na sio hisia binafsi.
Lakini kwangu, licha ya dalili zinazoonekana wazi kuwa kana
kwamba CCM imeshapata mgombea wake urais kufuatia uamuzi wa
Jaji Ramdhan kutangaza nia, nina wasiwasi kidogo kuhusu
ufanisi wake.
Kubwa zaidi ni ukweli kwamba Idara ya Mahakama, ambayo licha
ya Jaji Ramadhan kuitumikia muda mrefu bali pia aliwahi kuwa
mkuu wake kwa maana ya ujaji mkuu, imeendelea kuwa moja ya
taasisi sugu kwa rushwa.

Takribani kila ripoti inayotolewa kuhusu tatizo la rushwa
katika taasisi mbalimbali za serikali nchini mwetu, Idara ya
Mahakama haikosekani, na tena ikishika nafasi za juu.
Mara baada ya kuchukua fomu kuomba CCM imteue kuwania Urais,
Jaji Ramadhan aliwaambia waandishi wa habari kuwa atatumia
uzefu wake kupambana na ufisadi. Swali la msingi: uzoefu
upi? Huohuo ulioshindwa ukiondoa Idara ya Mahakama katika
orodha ya taasisi zinazoongoza kwa rushwa?

Kwa upande mwingine, Jaji Ramadhan alikuwa mjumbe wa 'Tume
ya Warioba' iliyokusanya maoni kuhusu mabadiliko ya
Katiba. Sote twakumbuka yaliyomsibu Jaji Joseph Warioba na
baadhi ya wasaidizi wake kupigania sio tu kazi nzuri
iliyofanywa na tume yao bali pia mustakabali wa Katiba
mpya.
Kwanini Jaji Ramadhani amekuwa kimya sana katika suala hilo?
Je ukimya wake ulitokana na kufahamu kuwa siku moja angeomba
kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM?

Na katika hilohilo, kwa vile mapendekezo ya Tume hiyo
iliyomshirikisha Jaji Ramadhani yalikuwa muungano wenye
muundo wa serikali tatu, je kwa vile CCM ambayo jaji huyo
anaiomba ridhaa ya kumteua awe mgombea wake ina msimamo wa
serikali mbili kama ilivyo sasa, hilo si tatizo angalau
kimsimamo na kimtizamo?

Hadi muda huu, Jaji Ramadhani ni Rais wa Mahakama ya Afrika
kuhusu haki za binadamu. Sihitaji kuorodhesha matukio lukuki
ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania lakini
miongoni mwa matukio makubwa ni pamoja na ukatili unaofanywa
na Jeshi la Polisi na rushwa (naam, rushwa sio tu adui wa
haki bali pia inachangia ukiukwaji mkubwa wa haki za
binadamu).
Je Jaji Ramadhani amekuwa wapi wakati ukiukwaji wa haki za
binadamu ukiendelea kushamiri na kuwa kama umehalalishwa na
Katiba yetu? Ni nani anaweza kusimama hadharani na kuwaambia


Watanzania kuwa 'Urais wa Jaji Ramdhani katika Mahakama ya
Haki za Binadamu Afrika umechangia hili na lile katika
kutetea au kudumisha haki za binadamu nchini Tanzania'?
Niwe mkweli, binafsi ninamwona Jaji Ramadhani kama Rais
Kikwete alipojitambulisha mwaka 2005 kuwania urais na
hatimaye kushindwa nafasi hiyo.

Alionekana mtu mwadilifu, aliyeitumikia nchi kwa muda mrefu,
na pengine kubwa zaidi, msafi (asiye na kashfa). Sifa hizo
zinalingana na tunazosikia kuhusu Jaji Ramadhan. Je, kwa
mfano, kuwa msafi ni sawa na kuwa na uwezo wa kuongoza
nchi?

Lakini la mwisho kuhusu kada huyo ni taarifa za awali kuwa
amekuwa akiombwa na baadhi ya wana-CCM kuwania nafasi ya
urais (kuna wanaodai kuwa ndio mtu pekee anayeweza kumudu
'kumzuia' Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa asiingie
Ikulu, na wengine wanasema Jaji huyo ndio 'msafi zaidi'
kuliko makada wengine wanazowania nafasi hiyo).

Swali la msingi: je hao waliomwomba (kama ni kweli)
hawafanyi hivyo kwa maslahi yao binafsi? Na je, kumwomba
huko (kama ni kweli) hakutopelekea urais wa Jaji Ramadhan
(iwapo atashinda) ukaishia kuwa kama 'deni la kwa
wanamtandao' lilivyouandama utawala wa Rais Kikwete?
Nimalizie makala hii kwa kuwakumbusha tena Watanzania
wenzangu kuwa ni muhimu tujiulize na kuwauliza wawania urais
maswali magumu ili tusije kuishia kujiulaumu huko mbeleni.

Nchi yetu ipo katika wakati mgumu; umasini wa kupindukia
huku ufisadi ukizidi kuimarika, uhaba mkubwa wa uzalendo,
utovu mkubwa wa maadili ya uongozi ikiwa na pamoja na uhuni
katika matumizi ya fedha za umma, shilingi inayporomoka kama
ipo kwenye mashindano ya marathoni na kadhalika.

Tunahitaji rais ambaye si tu anajua matatizo yetu bali pia
ana uzalendo na uwezo wa kukabiliana nayo. Hatuhitaji Rais
msafi lakini mwoga wa kupambana na maharamia wanaoibomoa
nchi yetu kila kukicha.
Hatuhitaji mtu anayeahidi kupambana na rushwa ilhali hana
mfano japo mmoja wa jinsi alivyowahi kupambana na rushwa.

chanzo raia mwema

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment