Thursday, 25 June 2015

Re: [wanabidii] CCM imethibisha kuwa mgombea wake ndiye Rais wa Tanzania na hakuna mtu maarufu zaidi ndani ya chama hicho

Margeryalex;
Je sisi sio sehemu ya umma wa Watanzania?
Hapa tunajalibu kujadili na kuwekana sawa kwaajili ya mustakabali wa umma wote.
Kwani wengine tunahitaji kuwajua zaidi hawa jamaa wenye nia ya kuongoza Taifa,sasa tusipobadilishana mawazo na uzoefu sijui kama itakuwa ni afya kwa Taifa.
 
Reuben



On Wednesday, June 24, 2015 11:08 PM, 'margeryalex' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Mnajitahidi sana, hongereni. Maamuzi ni ya umma wa Watanzania tu.

A M

'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

>KWA zaidi ya mwezi mmoja sasa, macho na masikio ya Watanzania yamekuwa yakielekezwa kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambako pazia la uchaguzi wa ndani ya Chama wa kumsaka mgombea urais lilifunguliwa. Hadi sasa wagombea wasiopungua 38wamejitokeza, baadhi wametangaza nia na wengine wamechukua fomu bila kutangaza nia hadharani kama wengine.
>
>Mwitikio wa wananchi na vyombo vya habari umekuwa mkubwa sana kiasi kwamba wananchi na vyombo vya habari ni kama wamesahau kuwa kuna matukio mengine yanaendelea nchini, ikiwamo Bunge la Bajeti mjini Dodoma, ambalo kwa kawaida, huvuta msisimko kuliko tukio lolote lingine la kitaifa.
>
>Somo kubwa ninaloliona ni ule ukweli kuwa pamoja na mawaa yake, bado Watanzania wengi, wenye vyama na wasio na vyama, wanaitazama na kuitumainia CCM kwa uongozi wa nchi. Ukweli huu unaakisi ile nasaha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa "Rais wa nchi yetu anaweza kutoka Chama chochote cha siasa, lakini Rais bora wa Tanzania atatoka CCM".
>
>Hadi sasa, CCM ni chama pekee ambacho kimeweza kubeba haiba na taswira ya utaifa na Chama chenye hazina ya viongozi, demokrasia pana na mifumo. Pengine ndio sababu wananchi na vyombo vya habari hawaonyeshi shauku hiyo hiyo kwa michakato inayoendelea ndani ya vyama vya upinzani ikiwemo vile vinavyounda Ukawa, maana vina wigo finyu wa demokrasia ya ndani ya vyama hivyo na isitoshe wagombea wake ni wale wale wa siku zote. Na wengine wanapoonesha nia huundiwa zengwe na kufukuzwa.
>
>Jambo ambalo halina mjadala ni kuwa Watanzania wanahitaji mabadiliko ambayo yatawatoa katika lindi la umasikini na ufisadi. Pamekuwepo na chambuzi mbalimbali hapo nyuma zikihitimisha kwamba kiu hiyo ya Watanzania ya mabadiliko ilimaanisha kuchoshwa na CCM, ama kuitoa CCM madarakani. Tofauti na chambuzi hizo, tunachokishuhudia ni wananchi kuendelea kuamini mabadiliko haya yanaweza tu kutokea na kuletwa na CCM na si nje ya CCM.
>
>Matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba mwaka jana yanatupa fundisho kubwa. Kwa matarajio ya wapinzani, kufanyika kwa uchaguzi ule baada ya Bunge la Katiba kukamilisha Katiba Inayopendekezwa tuliyoambiwa imechukiza wananchi, na kufuatiwa na mjadala wa Bunge wa sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, CCM ingeanguka katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Pamoja na yote hayo, CCM ilipata asilimia 84 ya kura ikilinganishwa na wapinzani waliopata 16.
>
>Ukiachana na picha ya jumla inayoonyesha kuwa asilimia za ushindi kwa wapinzani zilipanda kutoka asilimia nne mwaka 2009 hadi 16 mwaka 2014, ukifanya uchambuzi wa kina wa maeneo waliyoshinda wapinzani, utaona kwa kiasi kikubwa, pale wapinzani walipoongeza viti, ushindi wao ni matokeo zaidi ya hujuma zilizosababiswa na teuzi za ndani za CCM kuliko jitihada na mkakati wa ushindi wa upinzani.
> Ndio sababu kuna mtawanyiko wa viti walivyoshinda wapinzani ndani ya kata, wilaya na mikoa ambao ukiujumlisha haukupi uhakika wa kusema kata, jimbo au wilaya fulani imechukuliwa na upinzani. Kwa kifupi, ushindi wa upinzani hauonekani kuwa ushindi wa kimkakati.
>
>Kabla ya CCM kutangaza ratiba yake ya uchaguzi, kulikuwepo na manung'uniko na lawama kutoka kwa wananchi tena wengi wasio wanachama wa CCM kuhusu kuchelewa kutangazwa kwa ratiba ya uchaguzi wa CCM. Binafsi, haikunishangaza sana kutokana na ukweli kuwa, kwa ukubwa wake na dhamana yake, CCM si ya wana CCM peke yao bali inamhusu kila Mtanzania.
>Ndio kusema, yale maneno ya Baba wa Taifa ya mwaka 1995 kuwa CCM ikishatangaza mgombea ni kama imeshatangaza Rais wa nchi yetu bado yangali mujarabu hadi sasa.
>Katika uhai wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alishauri kutokana na ule uhalisia kwamba upinzani wetu bado ni dhaifu, na kusababisha mgombea wa CCM ndiye awe Rais, ni muhimu kwa mgombea urais CCM akajulikana mapema zaidi, ikiwezekana mwaka mmoja.
> Aliamini kwa kufanya hivyo, wananchi wote, hasa wale walio nje ya CCM watapata pia muda wa kutosha kumjua na kumpima, maana ndiye mwenye uwezekano mkubwa wa kuwa Rais wao. Utamaduni huu wa Chama kutangaza mgombea wake mwaka mmoja hutumika pia na jirani zetu wa Msumbiji.
>
>Utaratibu huo wa kumtangaza mgombea wa Chama mapema zaidi unasaidia kukilazimu Chama kuchagua mgombea muadilifu maana, wananchi wanakuwa na muda mrefu wa kumjua tofauti na utaratibu wa sasa ambapo hutangazwa muda mfupi na kuingia katika Uchaguzi Mkuu. Salama pekee katika utaratibu wa sasa uko katika uthabiti wa mifumo na vikao vya Chama katika kuhakiki, kuchuja na kuchagua mgombea. Kwa lugha nyepesi, tumewekeza matumaini na imani yetu kwa wajumbe wa CCM wasiozidi 2,300 kutuchagulia Rais wa Tanzania, na sisi kubaki na jukumu la kumthibitisha tu.
>
>Katika zama hizi ambazo tunasikia kuwa wajumbe wa vikao hivyo hupata nafasi hizo kwa fedha, na hivyo pia kununulika na wagombea kwa fedha, kuna shaka kuwa wale wasio waadilifu wanaweza kununua njia yao ya kwenda Ikulu. Maana unachotakiwa kufanya ni kuwanunua wajumbe wasiopungua 1,500 tu. Ni kwa s

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment