Wednesday, 27 May 2015

[wanabidii] wahariri wanapo hamisha njaa kutoka tumboni na kupeleka kichwani na kuharibu akili, wameshindwa hata kuhoji hizi laki sita sita za E L

KADA AFICHUA SIRI MBIO ZA LOWASA

Hata hivyo katika kundi hilo la wajumbe waliokwenda kwa Lowasa , mjumbe mmojawapo amezungumza na waandishi wa habari na kwenda  bayana kuwa hakuwa akijua kinachoendelea

"mimi  nilikuwa pale makao makuu, nikawakuta watu pale wapo na magari wanasema twendeni nikapanda gari nikaenda, nilipofika kule nikashangaa kuona  mambo yanayoendelea. Hata zile shilling laki sita (600,000) zilizotolewa na Mukasa wala hatukuchangishana, alizitoa mwenyewe mfukoni mwake" Jacqueline Ngonyani  mjumbe kutoka Ruvuma.

Chanzo Raia Tanzania
Toleo  no.  0338

0 comments:

Post a Comment