Na kwa maneno yako mwasa nashauri na ndugu Kaaya ili awee kwatuzima rtulifikiri ndipo alipo ausome ten ujumbe wa Dr Kigwa halafu aandike upya maoni yake. La sivyo watu watamfananisha na anayemuunga mkono.
--------------------------------------------
On Wed, 5/27/15, 'mwassa jingi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Nilichokisema jana kutokana na kauli ya Mhe. LOWASSA.
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, May 27, 2015, 10:40 AM
Hoja
za Mhe. Hamisi Kigwangala hata kama na yeye ni Mgombea ni za
maana sana kwa wana-CCM wanaomuunga mkono Mhe. Edward
Lowassa. Wana CCM wengi wanaamini Lowassa anauzika lakini
ipo kazi kubwa kumuuza kuliko hata wagombea wengine. Wana
CCM makini wanapaswa kuufanyia kazi ushauri wa bure wa
mheshimiwa Kigwangala.mwassa.
From:
'ekabwoto' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
To:
wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, May 26,
2015 9:31 PM
Subject: Re:
[wanabidii] Nilichokisema jana kutokana na kauli ya Mhe.
LOWASSA.
Kigwangala
toka hadharani.waambie wananchi haya
Sent from Samsung
Mobile
-------- Original message --------
From: 'mpombe mtalika' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
Date:
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Nilichokisema jana
kutokana na kauli ya Mhe. LOWASSA.
(Ndugiu hii nimecopy tu kama
ilivyoandikwa na mwenyewe)
Nilichokisema jana kutokana na kauli ya Mhe.
LOWASSA.
Mimi nilianza
kushiriki siasa toka nikiwa mdogo sana. Kuanzia Chipukizi,
Greenguard wa UVCCM na baadaye UVCCM. Miaka ya mwanzo ya 90
nilivutiwa sana na mijadala ya mfumo wa vyama vingi ama
kimoja. Nakumbuka, binafsi nilivutiwa zaidi na mfumo wa
kutanua demokrasia, nakumbuka nilichangia hoja zangu kwenye
mkutano wa tume pale Nzega mjini, viwanja vya parking
pembeni ya jukwaa.
Wengi
kwa hakika hawakuunga mkono mfumo wa vyama vingi. Waliamini
katika chama kimoja. Nilijiunga rasmi CCM mwaka 1994. Mwaka
2005, niligombea Ubunge wa Jimbo la Nzega, kura hazikutosha
kwenye mchakato wa maoni ndani ya CCM na vikao vilisema kuwa
wakati wangu bado.
Niliendelea kufuatilia kwa ukaribu sana
kilichokuwa kinaendelea kwenye duru za siasa. Mijadala ya
Bungeni ilikuwa ya moto sana, mara nyingine ikitutia simanzi
sisi vijana wa CCM haswa namna tulivyokuwa tukishuhudia
wabunge wachache sana wa upinzani wakiishambulia serikali
yetu ya CCM kuhusiana na wimbo mpya kwenye duru za siasa za
miaka hiyo, 'ufisadi'. Ufisadi ikiwa ni order of the
day.
Ufisadi ikiwa ni
mtaji na ajenda kuu ya wapinzani Bungeni, of-course pia
ajenda ya kikundi kidogo cha wabunge wa CCM
waliojitambulisha kama vinara wa kupinga ufisadi. Miaka hiyo
kila mtu akiuchukia ufisadi na mafisadi.
Mwaka 2008, mimi nikiwa kijana mwana mabadiliko
na ninayechukia ufisadi na mafisadi, kama walivyokuwa vijana
wenzangu wengi, kwenye duru za siasa na nje ya duru za
siasa, nilivutiwa na mijadala iliyokuwa Bungeni kutokana na
hoja iliyowasilishwa bungeni na Dr. Harrison George
Mwakyembe kuhusiana na mchakato wa kununua umeme wa dharura,
na zabuni hiyo kupewa kampuni ya Richmond Development
Company LLC ikidaiwa kuwa mchakato huo ulikuwa na ubatilifu
na mazingira ya rushwa ndani yake.
Nikiwa kama mwananchi mwenye strong affinity na
siasa, uongozi na namna nchi yetu inavyoendeshwa, nilivutiwa
sana na namna wabunge wengi wa CCM walivyoamka na kuonesha
kwa dhati ya mioyo yao namna walivyokerwa na ufisadi wa
Richmond. Nakumbuka Mbunge wangu Lucas Selelii alikuwa
kinara mmojawapo.
Mwanzoni
sikutarajia kama Waziri Mkuu niliyempenda sana na kumuamini,
niliyemtazama kama kiongozi wa mfano kwangu, aliyenivutia
sana kwa namna alivyokuwa akichapa kazi na akitoa kauli za
straight forward kwenye mambo mengi ya msingi, akikemea
uzembe, akiadhibu wabadhirifu bila soni wala huruma, akifika
kila kona ya nchi ambapo akitokea tu, basi wazembe na
wabadhirifu wanaangusha angusha karatasi hovyo, Mhe. Edward
Ngoyai Lowassa eti naye angehusishwa kwa namna yoyote ile!
Sikuamini. Lakini sikuamini zaidi niliposikia
anajiuzulu...tena eti kwa sababu ya Richmond.
Nakumbuka sana kwenye duru za
siasa yeye na Mjomba wangu Mhe.Jakaya Kikwete walipochukua
fomu za kuwania Urais mwaka 1995, wakiwa na ujana ujana
mwingi na sisi tukiwashangilia na kuwapenda kama
inspirational figures wetu. Na ilipotokea mwaka 2005
alipoingia Mjomba, nilijua wazi kabisa kuwa Waziri Mkuu
angekuwa Mhe. Lowassa, na tulitabiri kipindi kile kuwa Mhe.
Lowassa angekuwa Rais baada ya kumaliza kipindi cha Uwaziri
Mkuu, yaani 2015.
Nilisimamisha kagari kangu maeneo ya Biafra na kukimbia
kwenye Pub moja pale jirani kutazama televisheni iliyokuwa
inarusha kutoka Bungeni, nakumbuka watu walijaa kwa wingi
sana na wengi wakishangilia kuonesha kufurahishwa kwao namna
serikali ilivyokuwa ikiwajibika Bungeni. Sikuamini. Serikali
imeanguka! Lowassa out. Sikuamini kabisa.
Jana nikapata habari kuwa Mhe.
Edward Lowassa amezungumza na wahariri wa vyombo vya habari
nchini - amekana kuhusika kwake na Richmond. Nikashtushwa
sana na hili.
Nikajiuliza hivi ni nini
kinataka kutokea kwenye siasa za nchi yangu? Mjadala wa
Richmond ulifungwa Bungeni miaka 7 iliyopita, je inabidi
ufunguliwe upya, na watu wapya tutafakari upya? Maana kuna
minong'ono kuwa Mhe. Lowassa anataka kuwania Urais mwaka
2015, na ana mpango wa kutangaza nia muda si mrefu.
Nikajiuliza, ni kwa nini imemchukua Mhe. Lowassa zaidi ya
miaka saba kujibu hadharani kuwa hakuhusika na Richmond?
Kwa nini anatamka maneno haya
leo na kwa nini hakujitetea Bungeni siku ile alipojiuzulu?
Nakumbuka siku ile alisema tatizo ni uWaziri Mkuu, kwa nini
hakufafanua na alikuwa na fursa hiyo kama 'primus inter
pares (first among equals)?' Kipindi fulani alisemekana
kuwa ni 'gamba' na lingepaswa kuvuliwa...likaishia
kiunoni! Ni kwa nini halikuvuka? Maswali haya sijawahi
kuyapatia majibu.
Hivi
ilikuwaje Rais wa Nchi, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, Kamati
ya Wabunge Wote wa CCM Bungeni, na mamlaka zote za
kiserikali kushindwa kumlinda Waziri Mkuu wake dhidi ya
tuhuma za kuhusika kwake kwenye Richmond mwaka 2008?
Maana kwenye siasa za mabunge
yanayofuata mfumo wa Westminster, Waziri Mkuu ni 'primus
inter pares', kwamba ana fursa ya kwanza ya kuzungumza
kwenye mijadala Bungeni na ana-enjoy nguvu ya kuwa na
majority bungeni kuendesha mambo ya serikali na kutawala
mijadala na maamuzi.
Ilikuwaje Chama kilimuacha Waziri Mkuu wake akaanguka?
Ilikuwaje? Maswali: je kulikuwa na ukweli dhidi yake
kuhusiana na tuhuma za Kamati? Ama Kamati ilitumika vibaya
na mahasimu wake? Yeye amekana, sasa wanakamati inabidi
wamjibu watuweke wazi, na wamjibu kwa uwazi bila kuficha,
maana kama alionewa ijulikane na sisi tuliohuzunishwa ama
kufurahishwa na Bunge wakati ule tuujue ukweli. Yeye anasema
hakuhusika na ndiyo maana Kamati ya Mwakyembe haikuona haja
ya kumwita kumhoji. Ukweli tunauhitaji sana leo kuliko jana.
Ukweli huu ni haki yetu.
Kama Kamati ilimuonea, basi imuombe radhi na
ituombe radhi watanzania wote. Kama kweli Mhe. Lowassa
atagombea Urais Twentyfifteen, itakuwaje kwenye mijadala ya
uchaguzi na CCM itasimamaje (kama itampitisha kuwa mgombea)
kumuombea kura wakati ilimuangusha Bungeni kutoka kwenye
nafasi nyeti ya Uwaziri Mkuu? CCM itatoa majibu gani kuhusu
kwa nini ilimuita 'gamba' na ikatangaza hadharani
kuanza mchakato wa kuvua magamba (ambao haukukamilika).
Nilisema jana, Mhe. Lowassa
amefungua pandora box, na kama atatangaza kweli kuwania
Urais, inabidi haya mambo yawekwe wazi, yamalizwe, maana
hauwezi jua ya kesho - ikitokea akawa mgombea wetu,
tutaanzia wapi kumnadi na kusema ni mtu safi, muadilifu,
anayechukia rushwa na ubadhirifu na kwamba anafaa kuwa Rais,
wakati juzi tulisema hafai kuwa Waziri Mkuu na tukamtoa?
Nilisema jana kuwa , CCM
haipaswi ku-risk kuteua wagombea wenye mambo mengi ya
kutolea maelezo kwa wananchi, ikifanya hivyo itaangushwa
asubuhi ya saa nne. Watanzania wa leo siyo wa juzi
Imeandikwa na HKigwangalla
--
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment