Tuesday, 26 May 2015

RE: [wanabidii] MKUTANO WA EDWARD LOWASSA NA WAHARIRI

Ukweli ikiwa Edo ataupata uraisi itakuwa ni janga la kitaifa .  Kwa nini (1) Lazima hao marafiki zake waliomchangia watataka kurudisha hela zao na yeye pia atataka kurudisha fedha zake alizotumia kwani kila mtu anajua jinsi alivyomwaga fedha kununua kuungwa mkono.  Wote tunajua hakuna atakayetoa hela yake bure bila kujua atazirudisha vipi kwani kama ungekuwa ni msaada basi hata hao watoa msaada wangeweza kunipa mimi nipeleke kanisani na msikitini lakini hawakufanya hvyo kwani walikuwa wanajua wanachokitafuta kupitia kwa Edo. Uraisi wake utakuwa wa kununua na si vinginevyo. Angalia tangazo la kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe ya leo 26/5 ni tangazo la bei mbaya. Kizuri kinajiuza kibaya kinajitangaza. (2) Uraisi wake utaongeza mpasuko ndani ya chama cha mapinduzi na serikalini hasa kwenye vyombo vya usalama na kutakuwa na kulipiza visasi na kuhujumiana sana kuonyesha kila upande ulivyo na uwezo mdogo wa utendaji jambo litakaloongeza gharama za uendeshaji na matumizi mabaya wa taasisi za serikali (3) Kutokana na mambo hayo mawili ufanisi wa serikali na vyombo vyake utakuwa mdogo sana hivyo uchumi utayumba, rushwa itaongezeka sana na itatuumiza, kutakuwa na Serikali ya kulazimishana na kutokana na hilo vyama vya upinzania vitapata nguvu sana  (4) Kuongezeka kwa nguvu ya vyama vya upinzania kutafanya Serikali izidi kuwa ya kigandamizi kuua kabisa haki za msingi za kiraia. Hivyo fedha nyingi sana na nchi zitatumika kwa ajili ya kugandamiza haki za binadamu badala kulipia gharama za maendeleo.

Kitendo cha kusema eti kama angeendelea kuwa Waziri Mkuu hii nchi ingekuwa na maendeleo zaidi ni kitendo cha kuiponda Chama Chake na Serikali iliyoko madarakani ambayo ni kitu kibaya sana kwa mshikamano wa Chama na Serikali.  Sidhani kitu hicho kitavumiliwa na Watanzania wenye nia njema na nchi hii.  Vile vile kule kusema kuwa eti walimvizia Mkurugenzi wa Kampuni ya Maji ili wamfukuze kabla hajaenda mahakamani kupata zuio la kimahakama inaonyesha kabisa akipata Urais atakuwa Rais wa namna gani.  Kila mtu awe mtanzania au sio ana haki ya kupata haki yake kupitia mahakami na hairuhusiwi Serikali wala mtu yeyote kuzuia haki kwa sababu yeyote.

Ninaomba Watanzania watafakari hilo.

Herment A. Mrema

Date: Tue, 26 May 2015 11:42:39 +0300
Subject: Re: [wanabidii] MKUTANO WA EDWARD LOWASSA NA WAHARIRI
From: danielstephen688@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Fadhil kwani wewe ukisahaulika kuna ubaya gani??

2015-05-26 11:41 GMT+03:00 fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>:
ndio maana wamasai huwa jeuri sana kwao kuingiza mifugo shamabani na kutafuna mazao yote kwao si tatizo, morogoro kuna watu mpaka leo wanashindwa kulima kwa ajili ya hawa jamaa, ninachokiiona hapa kuwa huyu jamaa akipa urais wakulima imekula kwetu, ndio tutasahaulika kabisa hatuta kuwa na wakutumbuka,

2015-05-26 10:53 GMT+03:00 Jacob Ruvilo <ruvilo2010@gmail.com>:

Mi najua nilivyomuelewa Rais Mtarajiwa nikwamba kila jambo liwe lina anza na elimu ya kutosha, kama ni kilimo watu wapate elimu ya kutosha kuhusu jambo hilo ukiachilia mvali elimu ya jumla

On May 26, 2015 10:49 AM, "fadhil fadhil" <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:
Lengo kuu atakaloanza nalo ni Elimu na sio Kilimo kwanza cha serikali ya JK. Amesema serikali ya JK ilikosea kuanza na kilimo na kuweka kando elimu. Ametangaza kuwa sera yake ni Elimu Kwanza

kwa kauli hii hata kama utapita ccm, hutapata kura yangu, Lowasa huoni aibu kuongopa kwa watanzania kuwa JK,alikosea alitakiwa kuanza na elimu elimu kwanza badala ya kilimo kwanza.

Lowasa kweli unautaka urais lakini hebu jaribu kuwa mkweli, umesahau kipindi Jk anaingia madarakani na wewe ukiwa warizi mkuu wake nchi ilikuwa na ukame, kiasi ambacho ilisababisha zaidi mifugo laki 2 kupoteza maisha maisha?

umesahau kuwa hali ya chakula nchini ilikuwa mbaya wakati wewe ukiwa waziri mkuu, mpaka ukaenda thailand na kuwaleta watengeneza mvua. lakin zoezi hilo lilikufa baada ya kujiuzulu kwako,

lowasa unataka kutwambia uluikuwa hujui njaa ilivyokuwa nchini mpaka watoto walikuwa wanakosa kwenda shule na wafugaji walilazimika kuuza mazao yao ili kununua chakula.

leo hii Jk kafanya jambo la maana kufanya uhamasishaji wa kilimo kwanza ingawa bado kuna changamoto za hapa na pale nchi imejaa chakula kila kona na maghara ya ya chakula ya serikali yamejaa mpaka tunafikia hatua ya kutoa misaada kwa nchi zenye njaa kama somalia

Lowasa  kuhusu elimu, Jk amefanya mapinduzi makubwa katika elimu kuanzia elimu ya msingi sekondary na elimu ya juu hayo nayo unavaa miwani ya mbao?

Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita tumeweza kupiga hatua kubwa katika sekta ya elimu nchini. mafanikio tuliyoyapata ambayo ni matokeo ya kuongezeka kwa shule, idadi ya wanafunzi, idadi ya walimu, vitabu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Katika kipindi hicho, Shule za msingi zimeongezeka kutoka shule 14,257 mwaka 2005 hadi kufikia shule 16,343 mwaka 2014.  Hii imefanya idadi ya wanafunzi kuongezeka kutoka milioni 7.54 hadi kufikia milioni 8.23. Kwa upande wa shule za sekondari, idadi yake imeongezeka kutoka shule 1,745 mwaka 2005 hadi kufikia shule 4,576 mwaka 2014. Hali kadhalika, idadi ya wanafunzi wa shule za sekondari imeongezeka kutoka wanafunzi 524,325 mwaka 2005 hadi kufikia wanafunzi 1,804,056 mwaka 2014.
Jumla ya walimu wote wa msingi na sekondari idadi imeongezeka kutoka 153,767 mwaka 2005 hadi 301,960 mwaka 2015. Katika kipindi hicho, vyuo vya ufundi vimeongezeka kutoka 184 mwaka 2005 hadi 744 mwaka 2015. Wanafunzi wa elimu ya ufundi nao wameongezeka kutoka 40,059 mwaka 2005 hadi 145,511 mwaka 2015. Kwa upande wa elimu ya juu, wanafunzi wa vyuo vikuu wameongezeka kutoka 40,719 mwaka 2005 hadi 200,986 mwaka 2014.
Hii ni kutokana na kuongezeka kwa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki vimeongezeka kutoka 26 mwaka 2005 hadi 52 mwaka 2015. Upanuzi huu mkubwa katika udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu umewezekana kutokana na kuongezeka kwa bajeti ya Bodi ya Mikopo ya wanafunzi na kuruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu vya binafsi navyo wapatiwe mikopo. Bajeti iliongezwa kutoka shilingi bilioni 56.1 mwaka 2005 hadi shilingi bilioni 345 mwaka 2015 na kunufaisha wanafunzi 98,000 mpaka sasa.
Mafanikio haya ni matokeo ya kutoa kipaumbele cha kwanza kwa elimu katika bajeti ya serikali. Leo hii bajeti ya sekta ya elimu ndiyo kubwa kuliko zote nchini ambayo sasa imefikia shilingi trilioni 3.4 ikilinganishwa na shilingi bilioni 669.5 mwaka 2005.
Kweli kabisa Lowasa unautaka urais lakini kuwa mkweli, katika elimu awamu ya nne imejitahidi na atakae kuja anapaswa kuendeleza pale palipofikiwa lakini si kubeza kama unavyofanya wewe,

On Mon, May 25, 2015 at 5:07 PM, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:
" Hayo ni kwa ufupi. Wahariri wakuu katika media zote kupitia Jukwaa la Wahariri walikuwepo, na Absalom Kibanda (New Habari) na Nevil Meena (Free Media) ndio walikuwa waratibu wakuu wa mkutano huu."
teh teh teh tehhhh mbio zimeanza pale, kipenga kinalia watazamaji wenzangu.....

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment