Tuesday, 2 December 2014

Re: [wanabidii] offer, kiwanja 2m

Kiwanja cha aina hii kisichokuwa na maelekezo sahihi, si ajabu, kiko kwenye eneo linalokumbwa na mafuriko!

Kingine, Molel, tulishakushauri, kwa vile kazi hii inaonekana kama ndio ajira yako, basi, unapotoa taarifa, tulia, na andika kwa utulivu ili watu wakuelewe. Ndio, tunajua mwisho wa mwaka unakaribia na pilika zake ni nyingi, pamoja na mahitaji ya fedha ni mengi, lakini sio kwa staili hii.

Please, be serious with your work, specific, and to the point.

Maana kwa ujumbe wako, mtu anaweza akakufuata, kisha, kama walivyo madalali wengine, utamwambia, kabla sijakubeleka kwenye eneo husika, nipe ujira wangu au kamisheni yangu ya kukuonyesha au kama mnavyoita wenyewe, kifunga uchumba. Kumbe nyuma ya pazia kwa sababu ulizozijua mwenyewe, hukutaka kuziweka wazi, unenda na mteja wako kuona eneo husika, kumbe liko bondeni, kwenye mkondo wa maji, au halifikiki kwa barabara, au liko mbali, uswekeni kusikofikika kirahisi! Mteja, anakwazika, lakini, wewe unashangilia, maana umeshamvuna kifunga uchumba!

Yalishanikuta, na nimepitia kwa madalali kupata huduma msingi mji huu, na inauma ukiona mnavyotengeneza fedha kwa jasho jembamba na wakati mwingine mnalazimisha kupata fedha hata msizostahili. Nisiongee sana, ila, kuwa makini na kazi yako.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment