Monday, 4 August 2014

RE: [wanabidii] Re: MDAHALO KUJADILI UMUHIMU WA KUZINGATIA MAMBO YA MSINGI KATIKA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA, JUMATATU TAREHE 4 AGOSTI 2014

Dr. Kitila,
 
Nakubaliana na wewe, lakini bado mjadala huu ni muhimu sana kusikia kutoka kwa wale ambao walipewa jukumu la kukusanya maoni. Mengi yamesemwa kuhusu kazi yao na mapendekezo yao, itakuwa vyema tukisikia kwa upande wao nao wanasemaje. Kuna wanaohoji takwimu, kuna wanaosema kuwa maoni fulani yalitoka eneo fulani tu na pia wamesingiziwa mambo mengi sana. Itakuwa fursa nzuri sana nao kupaza sauti zao na kuweka record vizuri.
 
Siku mbili zilizopita JK amesema kuwa alikuwa akifanya mazungumzo nao lakini hayakuwa ya kina na hayakugusia nini kiwemo na nini kisiwemo!! mimi siamini kabisa katika hili, na wala sioni mantiki ya wao kukutana bila kumweleza bwana mkubwa kuwa upepo ni serikali tatu. Lakini, akaamua tu kuwasingizia na kuwazulia uongo. Wanaweza wasimjibu bwana mkubwa lakini ni vizuri kupata perspectives zao. Naamini utakuwa mjadala mzuri.
 
Aidha, ndugu yangu Dr. Kitila,  mjadala wa jana ulinishangaza kidogo na uliniacha na maswali mengi. Naona ulikuwa umepangwa strategically kuwapa forum chama fulani. Najiuliza kwa nini wachangiaji walikuwa wanaitwa kwa majina na Mwenyekiti wa Mdahalo, halafu wanapozungumza hoja zao zinafanana na chama fulani! Nakumbuka yule Mzee ambaye badala ya kujadili mada akaenda katika kumshambulia mzee Warioba. Kwa kweli yule mzee aliwadhalilisha wazee wenzake na wale wote waliopanga mkakati ule. Amejitia aibu yeye na familia yake.
 
 Pia kwa nini washiriki wengi hasa waliokaa pale chini walikuwa wanashangilia sana hoja ambazo zinaugwa mkono na chama fulani! kwa nini mahudhurio ya viongozi na mawaziri wa CCM yalikuwa ni mazuri sana kiasi kile! tofauti na midahalo mingine!!? kwa nini mdahalo ulifungwa na William Lukuvi!! badala ya watoa mada? na kwa nini Prof. Mpangala hakupewa nafasi ya kujibu maswali na hoja kutoka kwa washiriki?
 
Binafsi niliona ni mjadala wa ajabu kidogo na nilipata nilisikitika sana kuona kuwa hata wasomi wanatumika katika kueneza propaganda zenye hoja dhaifu sana.
 
Selemani Rehani.
 

Date: Mon, 4 Aug 2014 10:35:20 +0300
Subject: [wanabidii] Re: MDAHALO KUJADILI UMUHIMU WA KUZINGATIA MAMBO YA MSINGI KATIKA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA, JUMATATU TAREHE 4 AGOSTI 2014
From: kitilam00@gmail.com
To: mwandemanieddie@yahoo.com
CC: wanazuoni@yahoogroups.com; wanabidii@googlegroups.com; wanataaluma@googlegroups.com; lissubulali@yahoo.com; ulimwengu@jenerali.com; jenerali@gmail.com; kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com; phata@yahoogroups.com; issashivji@cats-net.com; mnyika@yahoo.com; info@policyforum.or.tz; info@tango.or.tz; tamwa@tamwa.org; dkibamba@tcib.or.tz; shivyawata@yahoo.com; makongo@gmail.com; usu.mallya@tgnp.org; ananilea_nkya@yahoo.com; wlac@raha.com; tawla_tawla@yahoo.com; humphreypolepole@yahoo.com; sungusia@gmail.com; jmkuchu@cssc.or.tz; mkulaba2000@yahoo.com

Tatizo la mdahalo huu wazungumzaji wakuu wote wana mlengo unaofanana. Hapo hapawezi kuwa na debate. Ili mdahalo uwe mdahalo kunahitajika kuwe na watoa mada wenye hoja kinzani. 






2014-08-03 18:18 GMT+03:00 EDGAR Atubonekisye <mwandemanieddie@yahoo.com>:
MDAHALO    MDAHALO   MDAHALO   MDAHALO
JUMATATU TAREHE 4 AGOSTI 2014, Blue Peal Hotel, Ubungo Plaza
kuanzia saa 9.00 mchana hadi 12.00 jioni


 
Taasisi ya Mwalimu Nyerere imeandaa mdahalo kujadili umuhimu  wa kuzingatia mambo ya msingi katika mchakato wa kupata Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 
Wazungumzaji katika mdahalo huu ni pamoja na waliokuwa Makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba: Jaji Joseph S. Warioba, Mwenyekiti wa Tume, Dr. Salim Ahmed Salim, Mzee Joseph W. Butiku, Bi Mwantumu Malale, Prof. Palamagamba Kabudi, Ndugu Awadh Ali  Saidi, na Ndugu Humphrey Polepole. 


Wananchi wa kawaida na viongozi kutoka taasisi na asasi mbalimbali. zinazowakilisha jamii ya Watanzania ambazo ni pamoja na asasi za kiraia (NGOs), vyama vya siasa, madhehebu ya dini, wasomi, vyombo vya habari, taasisi za kitaaluma, vyama vya ushirika vya wakulima na wafugaji, vyama vya wafanyakazi,  n.k nyote mnakaribishwa.


                                 Muda na Mahali: JUMATATU TAREHE 4 AGOSTI 2014, kuanzia saa 8.30 mchana hadi 12.00 jioni,                         
                                              Blue Peal Hotel, Ubungo Plaza.    
                                            
Mdahalo utarushwa moja kwa moja na television ya ITV.

NYOTE MNAKARIBISHWA.

Edgar Atubonekisye
Assistant Programmes Officer, The Mwalimu Nyerere Foundation
+255 754 988 946

 


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment