TUNAPOSEMA WATANZANIA WAGAWIWE SEHEMU YA MAPATO YA GESI NA MAFUTA MOJA KWA MOJA MSITUBEZE;
"Utafiti unaonyesha wazi kuwa njia ya haraka ya kupunguza umaskini ni kuwagawia wananchi wenye kipato kidigo fedha taslimu. Mexico na Brazil wamefanikiwa kupunguza athari za umaskini kwa kuwagawia familia maskini fedha taslimu kwa masharti ya kuwapeleka watoto wao shule wapate elimu na kuwapeleka kwenye vituo vya afya wapate chanjo na tiba. Utafiti unaonyesha hata bila masharti familia maskini wanatumia ongezeko la kipato kuboresha lishe ya familia, kuwaelimisha watoto na kutunza afya zao. Kutumia mapato ya gesi na madini mengine kuwagawia wananchi kutaongeza kasi ya kuutokomeza umaskini".
"Mpango wa kugawa fedha za mali ya asili siyo nadharia tupu kwani tayari unatumiwa na baadhi ya serikali. Jimbo la Alaska, Marekani wana mfuko wa gesi na mafuta ambapo mapato ya mfuko huu yanagawiwa kwa wananchi. Mongolia wanatumia sehemu ya mapato yatokanayo na madini ya shaba na dhahabu kulipa ruzuku kwa watoto wote wa Mongolia. Bolivia inatumia sehemu ya mapato ya gesi kulipa pensheni kwa wazee wote".
"Watu wengi wenye uwezo na matumaini ya kuongoza serikali watapinga vikali wazo hili. Watadai kuwa fedha zibakie serikalini na zitumiwe kwenye miradi ya maendeleo. Nia halisi ni kutaka fedha hizo ziwe chini ya usimamizi wao waweze kuzipora kujitajirisha na kuzitumia kujiimarisha kwa kununua wapambe na wapiga kura. Fedha zikigawiwa kwa wananchi Serikali italazimika kuwa na mfumo mzuri wa kukusanya mapato na kutumia vizuri fedha za uma. Wananchi wenyewe kupitia asasi za kiraia watakuwa makini fedha zinazokatwa kuingia katika mfuko wa miundo mbinu na akiba ya taifa hazifujwi na kuibiwa".
Nukuu katika aya hizo tatu, nimeitoa katika hotuba ya Prof. Lipumba wakati akifungua mkutano mkuu wa SITA wa Chama Cha Wananchi CUF Jumatatu 23 Juni 2014. Mkutano huo Mkuu wa kila baada ya miaka mitano umekusanya wajumbe takribani 1000 kutoka nchi nzima na unafanyika kwa siku 5 hapa Dar Es Salaam.
Ajenda Kuu ni tatu;
1. Kupokea taarifa ya kazi za chama za miaka mitano, kuzijadili na kuzipitisha,
2. Kufanya Marekebisho makubwa katika katiba ya chama,
3. Kuchagua viongozi wa Chama ngazi ya Taifa.
HAKI SAWA KWA WOTE.
J. Mtatiro,

No comments:
Post a Comment