Tuesday, 24 June 2014

[wanabidii] Re: UTAFITI WA MAFUTA NA GESI ASILIA KATIKA MAENEO YA MOROGORO NA KILIMANJARO

TAARIFA KWA UMMA 
UTAFITI WA MAFUTA NA GESI ASILIA KATIKA MAENEO YA MOROGORO 
NA KILIMANJARO 
 
Katika toleo Na. 1734 la gazeti la Jambo Leo la tarehe 10 Juni, 2014 katika 
ukurasa wa tatu iliandikwa taarifa iliyokuwa na kichwa cha habari 
"Utafiti wa gesi kuinufaisha Morogoro, Kilimanjaro". Taarifa hiyo ilieleza kuwa 
wakaazi wa mikoa tajwa watanufaika na ugunduzi wa mafuta na gesi uliofanywa 
na Kampuni ya Swala katika maeneo hayo. 
 
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linapenda kuwafahamisha 
wananchi kuwa taarifa ya kwamba Kampuni ya Swala imegundua gesi na mafuta 
katika maeneo ya Morogoro na Kilimanjaro sio sahihi. Ugunduzi wa mafuta 
hufanyika tu baada ya kuchimba kisima cha utafiti na hatimaye mafuta au gesi 
iweze kutoka yenyewe kutoka ardhini. Hatua ya kuchimba kisima cha utafutaji 
hutokana na tafiti mbali mbali za awali za mitetemo ya ardhi na kubaini kama 
maeneo hayo yana uwezekano wa kuwa na mafuta au gesi ama la. Hata kama 
eneo linaonesha dalili nzuri za awali ni lazima sehemu hiyo ichimbwe na matokeo 
yake ni kuwa na ugunduzi au la. Vilevile ugunduzi huo lazima uonyeshe kutoa 
kiasi cha rasilimali ambacho kinaweza kuzalishwa kibiashara (economically 
viable). 
 
Kazi zilizofanyika mpaka sasa na Kampuni ya Swala katika maeneo ya Morogoro 
– Kilosa na Pangani - Kilimanjaro ni utafiti wa awali wa kukusanya takwimu za 
mitetemo na kubaini kama maeneo hayo yana kina (thickness) cha kutosha cha 
miamba tabaka ambayo utafiti wa mafuta na gesi unaweza kufanyika. Hivyo 
utafiti wa kina unaendelea ili kubaini kama kuna miamba mashapo (prospects) ya 
kutosha kwa ajili ya kuchimba kisima cha utafiti. Uchimbaji wa kisima hicho 
unaweza kutoa mafuta au/na gesi au maji matupu. Hatua ya uchimbaji visima 

bado haijaanza.Hivyo basi si sahihi kwa mtu yeyote kusema kuwa kuna 
ugunduzi uliofanyika. 
 
Utaratibu wa kutafuta mafuta nchini ni wa kugawana mapato kati ya Mwekezaji 
na Serikali kupitia Mikataba ya Kugawana Mapato (Production Sharing 
Agreement-PSA) kama mafuta au gesi ikigundulika. Kampuni isipogundua 
rasilimali yeyote, Serikali haimrudishii Mwekezaji fedha zake alizowekeza kwenye 
ufafiti huo, hivyo hasara hiyo ni kwa Mwekezaji mwenyewe. 
 
Shirika lina taarifa kuwa Kampuni ya Swala inauza Hisa zake katika soko la Hisa 
la Dar es Salaam ili Watanzania washiriki katika shughuli za utafutaji wa mafuta 
na gesi. Suala hili ni jema na Kampuni ya Swala inastahili kupongezwa kwa 
kuwawezesha Watanzania kushiriki kwenye sekta hii ambayo imeshika kasi katika 
miaka mitatu iliyopita. Aidha, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania 
linawashauri Wananchi wafanye maamuzi mazuri na kuwatumia washauri wao 
kuhusu ununuzi wa hisa hizo kwa kuzingatia mambo yaliyoelezwa hapo juu. 
 
Ikumbukwe kuwa Tanzania tumechimba visima vya utafiti wa mafuta vipatavyo 
78 na vyenye gesi ni asilimia 40% tu huko Mkuranga (Pwani), Songosongo 
(Lindi), Ntorya na Mnazi Bay (Mtwara) na Bahari ya kina kirefu. 
 
Taarifa kuwa katika mikoa ya Morogoro na Kilimanjaro kumefanyika ugunduzi wa 
mafuta na gesi haina ukweli wowote. Kama rasilimali ya mafuta au gesi asilia 
ikigundulika mwenye mamlaka ya kutangaza ugunduzi huo ni Mheshimiwa Waziri 
wa Nishati na Madini pekee. 
 
Kwa maelezo zaidi wasiliana na: - 
 
Mkurugenzi Mtendaji, 
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, 
BWM Tower A, 
S.L.P 2774, 
Dar es Salaam. 
Barua pepe: tpdcmd@tpdc-tz.com 

On Tuesday, June 24, 2014 12:43:27 PM UTC+3, Abdalah Hamis wrote:
TAARIFA KWA UMMA 
UTAFITI WA MAFUTA NA GESI ASILIA KATIKA MAENEO YA MOROGORO 
NA KILIMANJARO 
 
Katika toleo Na. 1734 la gazeti la Jambo Leo la tarehe 10 Juni, 2014 katika 
ukurasa wa tatu iliandikwa taarifa iliyokuwa na kichwa cha habari 
"Utafiti wa gesi kuinufaisha Morogoro, Kilimanjaro". Taarifa hiyo ilieleza kuwa 
wakaazi wa mikoa tajwa watanufaika na ugunduzi wa mafuta na gesi uliofanywa 
na Kampuni ya Swala katika maeneo hayo. 
 
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linapenda kuwafahamisha 
wananchi kuwa taarifa ya kwamba Kampuni ya Swala imegundua gesi na mafuta 
katika maeneo ya Morogoro na Kilimanjaro sio sahihi. Ugunduzi wa mafuta 
hufanyika tu baada ya kuchimba kisima cha utafiti na hatimaye mafuta au gesi 
iweze kutoka yenyewe kutoka ardhini. Hatua ya kuchimba kisima cha utafutaji 
hutokana na tafiti mbali mbali za awali za mitetemo ya ardhi na kubaini kama 
maeneo hayo yana uwezekano wa kuwa na mafuta au gesi ama la. Hata kama 
eneo linaonesha dalili nzuri za awali ni lazima sehemu hiyo ichimbwe na matokeo 
yake ni kuwa na ugunduzi au la. Vilevile ugunduzi huo lazima uonyeshe kutoa 
kiasi cha rasilimali ambacho kinaweza kuzalishwa kibiashara (economically 
viable). 
 
Kazi zilizofanyika mpaka sasa na Kampuni ya Swala katika maeneo ya Morogoro 
– Kilosa na Pangani - Kilimanjaro ni utafiti wa awali wa kukusanya takwimu za 
mitetemo na kubaini kama maeneo hayo yana kina (thickness) cha kutosha cha 
miamba tabaka ambayo utafiti wa mafuta na gesi unaweza kufanyika. Hivyo 
utafiti wa kina unaendelea ili kubaini kama kuna miamba mashapo (prospects) ya 
kutosha kwa ajili ya kuchimba kisima cha utafiti. Uchimbaji wa kisima hicho 
unaweza kutoa mafuta au/na gesi au maji matupu. Hatua ya uchimbaji visima 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

No comments:

Post a Comment