Wednesday, 25 June 2014

[wanabidii] Re: TUNAPOSEMA WATANZANIA WAGAWIWE SEHEMU YA MAPATO.....

Today at 12:43 PM
Bwana Mtatiro,
Wazo ni jema sana, nakumbuka mbuka hata Rais Kikwetwe kwenye kambeini zake za kuwania awamu ya pili aslidokezea kuwa kuna haja ya kuanza kuwalipa kiinua mgogo watanzania wote wenye umria kuazia kiwango Fulani, sikumbuki kama kulitajwa pesa hiyo vyanzo vyake vingelikuwa ni nini.
Ilivyo kwa viongozi wa Kiafrika husema chochote wakati wa kuwania nafasi za uongozi alimradi kauli hizo zitakosha mioyo ya watu na kuwapa matumaini.
Mpango unaosema na mifano unayotoa inapendeza sana kusikia. Tatizo la watanzania, kama hutaweka mazingira ya kuwabana wale wenyewajibu wa kugawa huo ujira, pesa hiyo haitawafikia walengwa, mtakuja kushitukia nani katumia bilioni ngapi kufania nini kwa shughuli zake binafsi, ndipo tatizo jingine la kujari kunusuru hizo pesa zilizotumiwa vibaya litakapoa anza, ka mazingira tuliyo nayo wale walioiba pesa hizo wataambia kwa wakati wao wazirudishe (chukulia mfano wa pesa za EPA, waliozikwepua wameagizwa wazirudishe, na kuna taarifa zingine zimekwisha rudishwa, kunaukweli au laa ni Muumba pekee anafahamu hilo).
Kwanye mapendekezo ya rasmu ya katiba mpya kulikuwa na vifungu vinavyolenga kuwakaba makoo wafuja mali za umma, lakini ndiyo hivyo inaonekana kunadalili za kushindwa kupatikana kwa vifungu hivyo kisheria, na kama unavyofahamu UKAWA wameachia ngazi, na wale waliobaki kwenye msafara wanampango wa kurekebisha vifungu vya sheria ili wapate kupitisha katiba inayowafaa wao na siyo nchi na wananci kwa ujumla. Bwana Mtariro, hayo yote uliyoyazunguzia hayatabaki "ndoto ya mwenda wazimu?" Hili si tusi bali kuna kitabu che kichwa cha habari hiyo.
Ninachoombea ni ninyi ukawa kutorudi nyuma kukaa pamoja kitu ambacho mngelikuwa mmekifanya miaka mingi ya nyuma, leo hii tusingelikuwa hapa tulipo. Kusije kuwa na mtu roho wa kubabaishwa na vijisenti mkasahau wajibu wenu kwa wananchi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, hii ni sala inayosemwa na kila mmoja Waliowengi Bungeni na Wachache, sifahamu  ni nani kati yao anayetamka maneno haya kwa uchungu moyoni.

No comments:

Post a Comment