On Sunday, April 20, 2014 10:09:46 AM UTC-7, Abdalah Hamis wrote:
> JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
>
>
> WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
>
>
>
>
>
> Simu:022-2110146/2110150/2/211679 Faksi:022-2113271, Tovuti: www.moe.go.tz
>
> NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
>
>
>
>
> UTANGULIZI
>
>
> Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada ni wale wenye ufaulu mzuri katika mitihani ya kidato cha NNE na SITA. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi Daraja la Tatu tu.
>
>
> Aidha, kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa Sayansi na
> Hisabati wa takribani walimu 26,000 kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo Sayansi na Hisabati ili kuziba pengo hili. Nia ya Serikali ni kuwavutia wanafunzi wengi wa masomo ya Sayansi na Hisabati. Kuanzia mwaka huu wa masomo 2014/15 wanafunzi watakaojiunga na fani ya Ualimu kwa masomo ya Sayansi na Hisabati watagharimiwa na Serikali kupitia mfumo wa ruzuku na mkopo. Wanafunzi watakaokuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza watapatiwa Ruzuku na wale wenye Daraja la Pili na la Tatu watapewa mkopo ili kuwasaidia katika masomo yao. Watakaofaulu mafunzo ya ualimu katika masomo ya Sayansi/Hisabati watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za serikali.
>
>
> VIGEZO
> Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/15.
>
>
> 1: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA: MASOMO YA SAYANSI/HISABATI NA UFUNDI: MUDA MIAKA 2.
>
>
> (i) Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpapwa, Tukuyu, Songea , Butimba, Kleruu na Monduli
>
>
> Mwombaji awe amehitimu:
> Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa 'Principal Pass' mbili katika Masomo ya Sayansi na Hisabati.
>
>
> (ii) Ualimu wa ufundi katika chuo cha ualimu Kleruu
> Mwombaji awe amehitimu:
> a. Mafunzo ya FTC kati ya mwaka 2004 na 2010 kutoka Vyuo vya Ufundi, Au
> b. Mafunzo ya ufundi katika ngazi ya NTA Level 6 au sifa linganishi (equivalent qualification) kati ya mwaka 2007 na 2013 kutoka chuo chochote cha Ufundi kinachotambulika na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
>
>
> (iii) Ualimu wa Kilimo katika chuo cha ualimu Monduli
> Mwombaji awe amehitimu:
> Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu 'Principal Pass' mbili katika somo la 'Agricultural science' na 'Biology', 'Chemistry' au 'Food and Nutrition'.
>
>
>
>
> 2: MAFUNZO MAALUM YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA KWA KIDATO CHA NNE MASOMO YA SAYANSI/HISABATI NA ENGLISH: MUDA MIAKA 3
>
>
> Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati na English katika vyuo vya Butimba, Morogoro, Korogwe, Songea na Mpwapwa
>
>
> Mwombaji awe amehitimu:
> Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu, na Credit mbili (yaani A, B+, B au C) katika masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza.
>
>
> 3: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA: MUDA MIAKA 2.
> (i) Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu.
>
>
> Mwombaji awe:
> Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango cha 'Principal Pass' mbili
>
>
>
>
> (ii) Biashara katika vyuo vya Shinyanga na Kasulu
> Mwombaji awe:
> Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua 'Principal Pass' moja na 'Subsidiary' moja
>
>
> (iii) Sanaa za Ufundi, Sanaa za Maonyesho, Muziki na Michezo katika chuo cha Butimba.
> Mwombaji awe:
> Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua 'Principal Pass' moja na 'Subsidiary' moja
>
>
> Tanbihi: Masomo ya 'Economics', Basic Applied Mathematics', 'General Studies' na 'Divinity' hayatatumika kama kigezo cha kumchagua au kumdahili mwombaji.
>
>
> 4: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI STASHAHADA ELIMU YA MSINGI: MUDA MIAKA 3)
>
>
> Ualimu wa Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu
>
>
> Mwombaji awe:
> Amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 wenye ufaulu wa Daraja la I Daraja la Tatu katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.
>
>
> Tanbihi: Kipaumbele kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya 'Mathematics', 'Biology', 'Physics', 'Chemistry', 'Agriculture', 'Food and Nutrition', 'English' na Kiswahili na wahitimu wenye mahitaji maalumu.
>
>
>
>
> 5. MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA:- MUDA MIAKA 2
>
>
> Ualimu wa masomo ya Sayansi katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpapwa, Tukuyu, Songea , Butimba, Kleruu na Monduli
>
>
> Mwombaji awe amehitimu:
> Mwalimu wa Daraja 'A' aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua 'Principal Pass'moja na 'Subsidiary' moja katika Masomo ya Sayansi na Hisabati; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
>
>
>
>
> 6: MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA (SEKONDARI):- MUDA MIAKA 2.
>
>
> (i) Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa, Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu.
>
>
> Mwombaji awe:
> Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na mwenye ufaulu usiopungua 'Principal Pass' moja na 'Subsidiary' moja katika masomo ya 'Biology, 'Chemistry' na 'Food and Nutrition
>
>
> (ii) Ualimu wa masomo ya Biashara katika vyuo vya Shinyanga, Kasulu
>
>
> Mwombaji awe:
> Mwalimu wa Daraja 'A' aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua 'Principal Pass" moja na 'Subsidiary' moja; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
>
>
> (iii) Ualimu wa masomo ya Elimu Maalumu katika chuo cha Patandi
> Mwombaji awe:
>
>
> Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi; Au Sayansi ya Jamii na uzoefu wa kazi ya ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili, Au
>
>
> Mwalimu wa Daraja 'A' aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua 'Principal Pass' moja na 'Subsidiary' moja; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
>
>
> Tanbihi: Walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalum kama wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili, n.k. ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).
>
>
>
>
> 7: MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA ELIMU YA MSINGI: MUDA MIAKA 2:
>
>
> Ualimu wa Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu
> Mwombaji awe:
> Mwalimu wa Daraja 'A' mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
>
>
> MAELEZO MUHIMU
> (i) Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
> (ii) Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
> (iii) Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;<div style="font-family: Verdana, Geneva, sans-serif; font-size: 12px; line-height: 16.799999237060547px; color: rgb(46, 6...
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment