Wengi walio bungeni wanatamka Mungu ibariki Tanzania kwa maneno lakini moyoni ni Mungu nibariki peke yangu niendelee kuushika utamu. Na ndiyo maana kinara wao alidokeza kwamba wabunge kuwa na ukomo wa kugombea haikubaliki. Liliandikwa na Mtatoro linawezekana sana kwani wao wanaoweza wana nini na sisi tusiweze tunakosa nini? Ukikiambia kichwa kwamba hili haliwezekani kweli halitawezekana milele
2014-06-25 14:43 GMT+03:00 'Mike Zunzu' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Bwana Mtatiro,Wazo ni jema sana, nakumbuka mbuka hata Rais Kikwetwe kwenye kambeini zake za kuwania awamu ya pili aslidokezea kuwa kuna haja ya kuanza kuwalipa kiinua mgogo watanzania wote wenye umria kuazia kiwango Fulani, sikumbuki kama kulitajwa pesa hiyo vyanzo vyake vingelikuwa ni nini.Ilivyo kwa viongozi wa Kiafrika husema chochote wakati wa kuwania nafasi za uongozi alimradi kauli hizo zitakosha mioyo ya watu na kuwapa matumaini.Mpango unaosema na mifano unayotoa inapendeza sana kusikia. Tatizo la watanzania, kama hutaweka mazingira ya kuwabana wale wenyewajibu wa kugawa huo ujira, pesa hiyo haitawafikia walengwa, mtakuja kushitukia nani katumia bilioni ngapi kufania nini kwa shughuli zake binafsi, ndipo tatizo jingine la kujari kunusuru hizo pesa zilizotumiwa vibaya litakapoa anza, ka mazingira tuliyo nayo wale walioiba pesa hizo wataambia kwa wakati wao wazirudishe (chukulia mfano wa pesa za EPA, waliozikwepua wameagizwa wazirudishe, na kuna taarifa zingine zimekwisha rudishwa, kunaukweli au laa ni Muumba pekee anafahamu hilo).Kwanye mapendekezo ya rasmu ya katiba mpya kulikuwa na vifungu vinavyolenga kuwakaba makoo wafuja mali za umma, lakini ndiyo hivyo inaonekana kunadalili za kushindwa kupatikana kwa vifungu hivyo kisheria, na kama unavyofahamu UKAWA wameachia ngazi, na wale waliobaki kwenye msafara wanampango wa kurekebisha vifungu vya sheria ili wapate kupitisha katiba inayowafaa wao na siyo nchi na wananci kwa ujumla. Bwana Mtariro, hayo yote uliyoyazunguzia hayatabaki "ndoto ya mwenda wazimu?" Hili si tusi bali kuna kitabu che kichwa cha habari hiyo.Ninachoombea ni ninyi ukawa kutorudi nyuma kukaa pamoja kitu ambacho mngelikuwa mmekifanya miaka mingi ya nyuma, leo hii tusingelikuwa hapa tulipo. Kusije kuwa na mtu roho wa kubabaishwa na vijisenti mkasahau wajibu wenu kwa wananchi.MUNGU IBARIKI TANZANIA, hii ni sala inayosemwa na kila mmoja Waliowengi Bungeni na Wachache, sifahamu ni nani kati yao anayetamka maneno haya kwa uchungu moyoni.On Wednesday, 25 June 2014, 10:06, 'julius mtatiro' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
--TUNAPOSEMA WATANZANIA WAGAWIWE SEHEMU YA MAPATO YA GESI NA MAFUTA MOJA KWA MOJA MSITUBEZE;
"Utafiti unaonyesha wazi kuwa njia ya haraka ya kupunguza umaskini ni kuwagawia wananchi wenye kipato kidigo fedha taslimu. Mexico na Brazil wamefanikiwa kupunguza athari za umaskini kwa kuwagawia familia maskini fedha taslimu kwa masharti ya kuwapeleka watoto wao shule wapate elimu na kuwapeleka kwenye vituo vya afya wapate chanjo na tiba. Utafiti unaonyesha hata bila masharti familia maskini wanatumia ongezeko la kipato kuboresha lishe ya familia, kuwaelimisha watoto na kutunza afya zao. Kutumia mapato ya gesi na madini mengine kuwagawia wananchi kutaongeza kasi ya kuutokomeza umaskini".
"Mpango wa kugawa fedha za mali ya asili siyo nadharia tupu kwani tayari unatumiwa na baadhi ya serikali. Jimbo la Alaska, Marekani wana mfuko wa gesi na mafuta ambapo mapato ya mfuko huu yanagawiwa kwa wananchi. Mongolia wanatumia sehemu ya mapato yatokanayo na madini ya shaba na dhahabu kulipa ruzuku kwa watoto wote wa Mongolia. Bolivia inatumia sehemu ya mapato ya gesi kulipa pensheni kwa wazee wote".
"Watu wengi wenye uwezo na matumaini ya kuongoza serikali watapinga vikali wazo hili. Watadai kuwa fedha zibakie serikalini na zitumiwe kwenye miradi ya maendeleo. Nia halisi ni kutaka fedha hizo ziwe chini ya usimamizi wao waweze kuzipora kujitajirisha na kuzitumia kujiimarisha kwa kununua wapambe na wapiga kura. Fedha zikigawiwa kwa wananchi Serikali italazimika kuwa na mfumo mzuri wa kukusanya mapato na kutumia vizuri fedha za uma. Wananchi wenyewe kupitia asasi za kiraia watakuwa makini fedha zinazokatwa kuingia katika mfuko wa miundo mbinu na akiba ya taifa hazifujwi na kuibiwa".
Nukuu katika aya hizo tatu, nimeitoa katika hotuba ya Prof. Lipumba wakati akifungua mkutano mkuu wa SITA wa Chama Cha Wananchi CUF Jumatatu 23 Juni 2014. Mkutano huo Mkuu wa kila baada ya miaka mitano umekusanya wajumbe takribani 1000 kutoka nchi nzima na unafanyika kwa siku 5 hapa Dar Es Salaam.
Ajenda Kuu ni tatu;
1. Kupokea taarifa ya kazi za chama za miaka mitano, kuzijadili na kuzipitisha,
2. Kufanya Marekebisho makubwa katika katiba ya chama,
3. Kuchagua viongozi wa Chama ngazi ya Taifa.
HAKI SAWA KWA WOTE.
J. Mtatiro,
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.--

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:
Post a Comment